Sunday, March 11, 2018

MUHULA WA KUANGAMIZA MASHETANI WANAOKUTESA


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 10 MACHI, 2018
  
Mchungaji Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha somo la Mhula wa kuangamiza Mashetani Wanaokutesa.
Utangulizi:
Neno muhula lina maana ya muda au wakati uliokubalika kwa ajili ya jambo Fulani kufanyika. Ni majira yaliyokubalika kwa ajili ya kitu Fulani kufany ika. Linaweza kuwa jambo jema au baya lakini haya yote yana muhula wake. Muda huu ukifika kama ni wakati wa kucheka au kulia lazima mtu ama alie au acheke. Muhula wa jambo Fulani huwezi kushindana nao. Kama kuna vitu mtu hatakiwi kushindana nao ni muhula wa jambo Fulani kwenye maisha ya mtu. Hata neno la Mungu linazungumza kwa habari ya muhula wa mtu.

Mungu alimwambia Ibrahimu kwa hakuna neno gumu la kumshinda Bwana. Aliambiwa kwa sababu mke wake alikuwa hapati mtoto. Malaika akamwambia kwa muhula wake atazaa mtoto. Mama huyu alikuwa hajapata mtoto kwa sababu muhula wake ulikuwa haujafika. Mama huyu muhula wake ulipotimia alizaa mtoto wa kiume katika uzee wake. “Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.” (MWANZO 18:14)

Mhula ukifika unapata kile ambacho amekuahidi Mungu ukipate, biblia inasema Sara alipata mtoto kwa muhula ule ule aliopangiwa na Mungu.

“Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.” (MWANZO 21:2)


Sara alikuwa hana watoto lakini muhula ulipotimia alipata mtoto. Anna alikuwa hana mtoto na akasumbuliwa sana na Penina. Mama huyu akaliitia jina la Bwana mpaka akapata mtoto. Mtoto Samweli akazaliwa na mafuta ya Unabii. Kinachozaliwa kwenye muhula huwa kinastawi sana.
 
Platform team wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu wakati wa Ibada.
Mungu anatufundisha kwa habari ya muhula ili tuyatambue majira. Kuna wakati wa kila kusudi chini ya nchi. Mungu akamwambia Mhubiri kuna wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa. Kuna wakati wa kucheka, kulia, kucheka, kufurahi, kukataliwa na kutumikishwa. Yako majira mengi nay a kutisha lakini yuko Bwana wa kuokoa. Anasema kuna wakati wa kung’oa yale Bwana hakuyapanda kwenye maisha yako. Kuna mapando yaliyopandwa kwenye kazi, biashara, ndoa na uchumi wako, lazima yote yang’olewe kwa jina la Yesu.
“Kwa kila jambo kuna majira yake,  Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;  Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza;  Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka;  Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;  Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe;  Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;  Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;  Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona;  Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia;  Wakati wa vita, na wakati wa amani.” (MHUBIRI 3:1-8)

Kuna wakati Yesu alikuwa anasema na kuwauliza wale waliokuwa wanakuja kwake; je unaamini? Wakijibu ndiyo anawaambia pokea sawasawa na ulivyo amini.  Pokea leo kibali, uwezo,utajiri sawasawa na ulivyo amini kwa jina la Yesu. Bwana Yesu aliwahi kutoa mfano mmoja kuhusu mpandaji. Mkulima alipanda ngano na alipo lala usingizi adui akaja akapanda magugu ndani yake. Wafanya kazi wakenda kwa bosi kumweleza kilichotoke hivyo akawaambia wayaache magugu na ngano pamoja ili ukifika wakati wa kuvuna atayatenganisha magugu na ngano. Shetani ukiwa umelala anaweza kukupandia mabaya na uhuribifu kwenye maisha yako; atapanda shida taabu, dhiki, mikosi na balaa, lakini haya ni mapando ya kishetani ambayo ni lazima kuyang’oa kwa jina la Yesu.
Kuna wakati na muhula wa kuwaangamiza mashetani na wote wanao tesa maisha yetu. Siku moja Yesu alipovuka ng’ambo alipita katika njia akakutana na watu wawili waliokuwa na mapepo, wakali mno waliokuwa wanawazuia watu kupita njia hiyo. Yalitamba kwa namna nyingi sana lakini Kristo alipofika yaliona nguvu yake hata wakapiga kelele wakisema wataka kutuangamiza kabla ya muhula wetu.

“Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?” (MATHAYO 8:28-29)
Kwa habari ya wagerasi na mashetani yaliyo tesa watu huko yalikuwa na muhula wa kuangamizwa na aliipofika Yesu yakaondolewa. Vilevile mashetani wanaolinda hatima yako, wanaotesa maisha yako, wanao haribu kazi yako na kusumbua ndoa yako hata hakuna furha tena. Bwana ameleta muhula maalumu wa kuwaondoa wale walio kutesa  maishani mwako kwa jina la Yesu. Shetani kwa asili ni muonezi; mawakala wake yani majoka, mizimu na wachawi, waganga na wasoma nyota wamewaonea watu kwa mda mrefu, amewachukua watu misukule, anaanawazui katika mipango ya maisha, analeta mgonjwa, anazuia watu wapate kazi, wasisome na kila wanalotaka kulifanya.

“habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.” (MATENDO YA MITUME 10:38)
 
Baadhi ya Makutano wakisikiliza  mafundisho kuhusu muhula wa Kuangamiza mashetani wanaokutesa.
Shetani akifunga watu huwa hataki kuwaruhusu  kupiga hatua katika maisha yao. Anawaweka katika kifungo na kuwahusuru humo na kuwajengea ngome, anaweka ulinzi mkali wasitoke, hataki wapate msaada. Lakini leo Bwana amekuja kuwafungua watu kutoka katika vifungo mbalimbali, amekuja kufungua biashara yako, haki yako, elimu yako, biashara yako, pokea vyote kwa jina la Yesu.

“Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ” (ISAYA 14:17)

Biblia imeweka wazi kwa habari ya uonevu wa shetani kwa wanadamu. Naye Mungu amechungulia katika ulimwengu wa roho ameona jinsi wanadamu walichukuliwa na wachawi, walivyowekwa katika vifungo na kuwaingiza katika balaa na magonjwa. wengine anawasomba na kuwaweka shimoni, nyumba za kufungwa.

Basi sasa nafanya nini hapa asema Bwana ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawasla wanapiga yowe asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.’  (ISAYA 52:5)

Uonevu wa shetani ni kila mahali; matatizo yote unayo yaona leo yanasababishwa na shetani, japokuwa matatizo yana tofautiana. Mfano mzuri, ukiamka tu asubuhi kichwa kinaanza kuuma unashindwa kufanya mambo ya msingi hatimaye mambo yako yanakwama. Unapata pesa kwa ajili ya kufanya mambo muhimu yeye anakuletea mikosi, magonjwa na dhiki hata hufanikishi lile ulilo kusudia kulifanya kwa pesa zako. Anapoteza malengo na kupindisha hatima za watu kwa uonevu wake.

“Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.”  (ISAYA 5:13)
Baadhi ya makutano wakifuatilia kwa makini Mchungaji akifundisha

Vita kati ya watakatifu na shetani ilisha isha tangu mbinguni.Malaika watakatifu walimwondoa mbinguni na kumtupa shimoni, kama vile shetani alivyotupwa toka mbinguni tunao uwezo wa kumtupa nje ya maisha yetu kwa jina la Yesu. Biblia inasema wakamshinda shetani kwa damu ya Kristo tunao uwezo wa kumshinda shetani. Inuka leo mshinde anaye haribu mipango yako, anayekula ndoa yako, anayeharibu watoto wako kwa jina la Yesu.

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.  Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.” (UFUNUO12:7-12)
Yesu alikuja duniani kwaajili ya kuwaokoa wale walionewa na kuwafungua waliofungwa; kazi kubwa aliyokuja kufanya dunia ilikuwa ni kuzivunja kazi za shetani dunia, kuwakomboa walio na taabu, shida na matatizo kadha wa kadha.  Alikuja kutupatia vile ambavyo shetani kimsingi alivizuia tusivipate maishani mwetu, tulipangiwa utajiri lakini tu maskini. Alikuja ili wewe utoke katika uonezi wa shetani kwa jina la Yesu.
“atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi”.(1YOHANA3:8)

Hujafikia kiwango kizuri cha maisha kwa maana amekuzuia mahali.  Ulipangiwa uwe mmliki wa kiwanda kikubwa leo ni mfugaji wa kuku, ulipangiwa kuwa mwanasiasa mkubwa leo ni fundi viatu. Ukiona hayo jua shetani anakaa mbele yako na kuweka mipango ili ufukuzwe kazi, ili usisaidiwe lakini Bwana amekuja ili utoke kifungoni katika jina la Yesu.
Shetani anaweza akakaa ndani ya mtu akakuzuia katika mipango yako. Anaweza kuwa kaka,   rafiki, shangazi au ndugu wa karibu au mtu yoyote. Biblia inasema wafanyakazi wenzake na Danieli walimchongea ili Danieli afe, lakini yeye alimtii Mungu akawa anamwomba kwa bidii mara tatu kwa siku. Kwa sheria ya waajemi alikuwa amevunja sheria nao wakamtupa katika tundu la simba lakini Bwana akamwokoa na midomo ya simba kwa jina la Yesu. Kuna watu wameonewa sana na watu walio waonea hawajaguswa bado; mwingine ameshindwa kusoma laikini yule alimzuia kusoma bado hajaguswa. Kuna mwingine ameonewa katika matatizo, afya ,kazi maendeleo na wale walikuonea bado hawajaguswa kwakuwa muhula wao ulikuwa bado. Leo muhula wao umefika na wataangushwa kwa jina la Yesu.

Mashetani wanatetemeka mbele za Mungu:
Shetani anajua uwezo wake na mamlaka yake, hawawezi kukaa palipo na nguvu ya Mungu. Mashetani yakimwona Yesu yana ogopa. Tumia jina la Yesu kumshinda shetani na ataondoka maisha ni mwako, kwa maana kwa nguvu za Mungu shetani ameshindwa kwa jina la Yesu.

“Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.”  (YAKOBO 2:19)

Ndugu mmoja aliyekuwa na mapepo walipomwona Yesu kwa mbali alipiga mbio akapiga magoti mbele za Yesu, kuashiria kuwa alikuwa amesalimu amri mbele ya nguvu ya Mfalme Yesu. Kila mwenye pepo husalimu chini ya mamlaka ya Kristo , je mwanadamu aliye umbwa na Mungu? Leo upate hofu unyenyekee chini ya mkono wa Mungu kwa jina la Yesu. Kwa unyenyekevu wako mashetani watawekwa mbali na wewe kwa jina la Yesu.

“Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.” ( MARKO 5:6-7)
Mtu akifunguliwa kutoka muhula wa mateso aliyokuwa amewekewa na mashetani.

Shetani ni mwoga sana akishajua muhula wake wakumwangamiza umefika anaanzisha lugha za kujitetea tetea, anaanza kufanya mambo fulani ya kujionesha kuwa mtakatifu. Lakini Bwana hakuruhusu shetani azungumze mbele yake. Pokea  uwezo wa kumwangamiza mashetani kwa jina la Yesu.

 “akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.” (MARKO 1:24-26)
Ukimwamini Yesu, Yesu anakaa ndani yako. Mashetani wakija kukuangalia wanamwona Yesu. Ili kumwangamiza shetani na mapepo wabaya lazima uwe na nguvu ya Mungu ndani yako kwa maana kile aliye na Yesu ananguvu ya Mungu ndani yake. Leo upokee nguvu ya Mungu ndani yako ukafukuze mapepo kwa jina la Yesu.

“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” (YOHANA 15:5)

Tunayo amri au kibali cha kuwaondoa mapepo maishani mwetu. Kwa kumpokea Yesu tunao uwezo wa kufukuza mashetani yanayotutesa kwa jina la Yesu. Alipowaita wanafunzi wake akwapa amri ya kuwatoa mapepo na kushinda nguvu zote za adui na hakuna kila litakalo wadhuru. Hivyo ukiwa na amri ya Kristo hakuna nguvu ya shetani itakayo kudhuru kwa jina la Yesu.
“Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.”(MATHAYO 10:1)
Children Ministry wakiimba na kucheza mbele za Bwana wakati wa Ibada ya Leo.

Ukisha kuwa na mamlaka ya Mungu ndani yako Roho yake inakaa ndani yako nawe unakuwa na mamlaka ya kuangusha nguvu zote za shetani na kutoa mateka wote. Sisi tuliokoka tunayo nguvu ya Mungu ndani yetu na Yesu anafanya kazi yake kupitia sisi, kwa nguvu hiyo tutaangusha maadui wote wanao tuzuia kuingia na wanotutesa kwenye muhula wetu kwa jina la Yesu
“Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;” (ISAYA 61:1-2)

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/




Share:
Powered by Blogger.

Pages