Sunday, March 4, 2018

KWA NINI WAKRISTO WASIOTOA ZAKA HUWA MASKINI


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 4 MACHI, 2018
MCHUNGAJI, DR. HAPPINESS GODSON (RP)


Mchungaji Dr. Happiness Godson akifundisha somo kwa nini wakristo wasiotoa zaka huwa masikini.

Utangulizi:
Mara nyingi tumejifunza mambo mengi ya rohoni lakini sio mambo ya sadaka. Lakini biblia inatufundisha utii kwa habari ya kutoa zaka. Zaka ni agizo la Mungu kumtolea. Wakristo maana yake ni watu wanaomfuata Yesu, wenye tabia za Kristo na wanaoenenda na tabia za Kristo. Mtume Paulo anatusihi tuwe na nia kama iliyokuwa ndani ya Kristo. Imeandikwa, ‘Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;’  Wafilipi 2:5-7

Yesu alikuwa Mungu lakini akaamua kuiacha mbingu ilia je duniani kutuokoa. Yesu alitii mamlaka ya Mungu na akakubali yote. Lakini Yesu aliazimishwa, aliinuliwa baada ya kutii mpaka mauti ya msalaba. Watumishi wa Mungu wanapofundisha kwa habari za utoaji watu huwaona kama vile wanampango wa kuwataka watu wawape pesa kwa ajili ya mahitaji yao. Mungu aliwai kumwambia Ezekieli kuwa naona watu wako wanafurahi kuyasikia maneno ya uzima lakini hawayatendi. Anasema watu wamemwona Mungu kama wimbo mzuri maana wanayasikia maneno yako lakini hawawezi kuyatendea kazi. Tupone leo ili tuyatendee kazi maneno ya uzima.
Imeandikwa,  ‘Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.’  Ezekieli 33:31
Ni sadaka maalaum tofauti na sadaka nyingine. Hii ni moja ya kumi ya  sehemu ya mapato yako kama mwanadamu. Imeandikwa,  ‘Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.’ Mambo ya Walawi 27:30
Sadaka ya Zaka pengine inaitwa Kodi ya Mungu. Kama serikali za wanadamu wanaweza kuchukua kodo kwa nguvu zote, Mungu je si zaidi ya wanadamu. Imeandikwa, ‘Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea Bwana kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani. Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha.’ 2 Nyakati 24: 9-10

SABABU ZA UMASIKINI WA WATU WASIOTOA ZAKA 

·         HAWANA CHA KUVUNA.
Mungu anasema kwa Yule asiyetoa zaka hawezi kupanda na akavuna. Kwa yeyote asiyetoa zaka kila atakachokipanda hakiwezi kuzaa kwa sababu hukuwai kupanda kwa Mungu. Mungu anasema kwa kutokutoa zaka ni dhahili mtu anakuwa amaejitenga na kanuni ya kupanda na kuvuna. Hii ndio inasababisha kila unachofanya hakiwezi kuendelea wala kuongezeka. Kuna miradi umeanza lakini hakuna matunda. Tufani huwa ina nguvu kuliko upepo wa kawaida. Tufani ni mbaya zaidi maana inaambatana na uharibifu wa hali ya juu sana.
Imeandikwa, ‘Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.’ Hosea 8:7

·         HAWAVUTI BARAKA ZA MUNGU KWENYE MAISHA YAO.
Kwa kutoa zaka kamili unakuwa unavuta Baraka maana unakuwa umeitimiza sharia ya Mungu. Kwa kutokutoa zaka unakuwa unajiweka mbali na Baraka za Mungu. Kwa kutoa zaka unakuwa unafungua madirisha ya mbinguni ili Baraka zije juu yako.
Malaki 3:10
Hapa duniani tunaishi maishe yenye ugumu na zimejaa taabu. Na tuko chini ya laana ya dhambi ya Adamu kwa sababu wote tu wanadamu. Sasa ukichukua dlaana ya Adamu na laana ya Zaka, huwezi kupata Baraka juu ya maisha yako. Kumbe kwa kutokutoa zaka huwa tunafunga madirisha ya mbinguni ili Baraka zisiachiliwe juu yangu. Unaweza kujaribu kila biashara lakini hakuna hata biashara moja iliyowai kukufanya ufurahi. Kwa kumtolea Mungu unakuwa unaweka mvuto wa Baraka kutoka mbinguni zije juu ya maisha yako.  Imeandikwa, ‘Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi? Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.’ Mwanzo 47:8-9

Kama madirisha ya mbinguni yamefungwa jua nchi unayoishi haiwezi kuzaa kwa ajili yako. Kila unachokifanya hakiwezi kuongezeka kwa sababu hakuna mkono wa Mungu. Imeandikwa, ‘Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.’ Kumbukumbu la Torati 28:23

·         WAKO CHINI YA LAANA.
Laana ni mbaya sana maana kwa asili palipo na alaana hakuna kufanikiwa. Mungu amesema mnaniibia kwa zaka na dhabihu. Usipotoa zaka unakuwa umejiweka chini ya laana ya Mungu mwenyewe. Laaana zingine unaweza kuziondoa kwa kuomba na kushindana na shetani na ukashinda. Lakini laana ya zaka haiondoki kwa kushindana bali kwa KUTUBU NA KUTII NENO. Mtu akiwa chini laana ya zaka anasababisha laana ndani ya kanisa. Mungu anatutaka tututbu na kumtii yeye.  Laana hii inasababisha mtu kukosa amani ya moyoni. Na mtu anakosa ujasiri wa kumwendea Mungu wakati wa maombi.
Imeandikwa, ‘Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.’ Malaki 3:8-9
Platform team wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu wakati wa Ibada ya leo.
·         WAHARABU HULA MAZAO WAKATI WOTE.
Baraka za Mungu kwa mtu anayetoa zaka ni hakika. Neno la Mungu linasema Mungu atatuma malaika ili awapige wale wanaoharibu mazao. Yule anayekula matunda ya kazi ya mikono yako, kazi na miradi yako. Hata kwenye nchi kuna laana kwa sababu nchi na viongozi wake hawamtolei Mungu zake kama sharia ya Mungu inavyomtaka kila mwanadamu. Kuna nchi ni ndogo lakini uchumi wao uko vizuri. Unakuwa na matobo kwenye mifuko yako na kila unachopata huwa unapoteza. Umasikini huu wa leo ni kwa sababu ya laaana ya zaka. Imeandikwa, ‘Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.’ Malaki 3:11

·         MATUNDA YA MASHAMBA YAO HUARIBIWA WAKATI WOTE
Kila unachofanya huwa kinaharibika. Ukilima huwezi kuvuna kwa sababu hakuna ulinzi juu ya kazi za mikono yako. Kuna matukio ya kutisha kwa sababu ya kutokutoa fungu la Kumi. Watu wanamatukio kwenye familia zao kwa sababu hawana ulinzi wa Mungu. Malaki 3:11
MATUNDA YANAPOTEA KABLA YA KUVUNA.
Hapa utaona hakuna uwiano wa mapato na kile ulichokiwekeza. Mtaji uloweka unaisha kabla ya kuzalisha kitu chochote. Kuna watu wanafanya kazi masaa mengi lakini malipo yao ni kidogo sana. Wengine kila wakifanya kazi wazulumiwa na kuonewa sana. Kila ukilima huwezi kuvuna kwa sababu yupo Yule mwarabu. Kuna mambo yanakupata kwa sababu ya laana ya kutomtolea sadaka. Kila unachoaanza kinaishia njiani. Malaki 3:11
Kumbe Mungu anaangalia moyo wetu wa kutii ili atubariki kwa kila tunachofanya. Faida   ya kutii ni kusababisha upenyo kwenye njia zako. Hakika mafanikio yako yanategemea sana moyo wako wa Utii. Imeandikwa, ‘Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;’ Isaya 1:19
Kwa nini wachungaji wakifundisha kuhusu sadaka watu hawaachangamki sana? Ni kwa sababu mioyo yao iko mbali na sharia ya Bwana. Mungu anamwambia Ezekieli watu wangu wamekuwa wanakuja kwako wanasikiliza neno langu lakini hawayatendi yaani wewe umekuwa kama wimbo mzuri. Mungu atuponye leo kwa jina la Yesu sisi tuyasikie na kuyatenda maneno yake. “Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi.” Ezekieli 33:31-32
Makutano wakimimina Roho zao mbele za BWANA ili wasamehewe dhambi ya kumwibia Mungu Zaka. ulikuwa wakati mwema sana kwa ajili kubadilisha maisha yetu. Hakika Mungu amesamehe.

MAANA HALISI YA KUMWIBIA MUNGU
Ø  Sisi kama wakristo tunauelewa gani kama tunamwibia Mungu; Mungu anasema 10% ni mali yake, vitu vyote ulivyonavy ya mapato yako, ya mifugo na kila kitu ni mali ya Mungu. Mfano una maguni 10 ya mpunga, gunia 1 ni la Mungu. Hii si zawadi, si chagizo balimali ya Mungu, hii unatoa kwanza halafu matumizi mengine yanaendelea. Ukimtolea Mungu sadaka bila kutoa zaka, Mungu anaona kuwa ni zile pesa zake ulizoiba na kumpelekea kanisani. Mfano ni kama umeniibia pesa zangu halafu ile hela unanunua keki unaniletea. Usichukue fungu la 10 ukamnunulia mchungaji zawadi. Kwa sababu biblia haijasema kuhusu kumwibia mchungaji bali ni kumwibia Mungu. Fungu la 10 si zawadi.

Ø  Mungu ametoa Onyo kali sana kwa wezi Imeandikwa, “bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;” Mathayo 6:20

Ø  Kuiba fungu la 10 kunaharibu ushirika wako na Mungu, Mara nyingi si salama sana kuishi karibu na mwizi. Mfano katika jamii anayeiba anawekwa jela ili akae mbali na jamii. Kwa hiyo usipotoa fungu la 10 unaharibu mahusianao yako na Mungu. “Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu.” Hosea 4:1-2.

Ø  Kuiba fungu la 10 unasababisha kanisa lisifanye matumizi yake kawaida. Kwa kuiba maana yake hupendi mikutano ya injili, hupendi kiwepo chakula kiwepo nyumbani mwa Bwana. Kanisa linatembea kwenye laana, kanisa linakosa mvuto.

Ø  Kuiba kunaleta hasira ya Mungu iwke juu yako, “Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang'anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki. Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.Ezekieli 22:29-31, Mungu amekuacha uende katika njia zako mwenye kwa sababu umekataa kukubali na kutii. Wewe kama unamwibia Mungu unataka Mungu akufanye nini.

MATATIZO YA KIROHO KWA WATU WASIOTOA ZAKA
§  Watu wasitoa zaka ni kwa sababu hawatii mamlaka kuu/mamlaka iliyopo, hamtii Mungu, mchungaji hawalipendi kanisa. “Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.” Yohana 12:4-6 Yuda alikuwa hamtii Yesu, lakini Yuda alipoona yule mama anapomimina yale mafuta anapoteza hela, lakini alionekana anawahurumia maskini na yale mafuta yangeuzwa angefaidika kwa sababu alikuwa mtunza mkoba.
§  Uasi mtu asiyetoa zaka ni muasi, “Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana?  Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.1 Samweli 15:21-23,  unatakiwa utafakari kama umemuasi Mungu kwa kutotoa zaka
§  Wachoyo;  watu wanatamani kupitiliza, wnatamani vitu visivyokuwa vya kwao, zaka ni mali ya Mungu, “Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka.  19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.” Mithali 1:13, 19 watu wanauwawa kwa kutoyoa zaka kwa sababu injili haiwafikii.
§  Watu hawaenendi kwa roho; Kama huenende kwa roho ni vigumu kuenenda kwa roho. Kama Roho mtakatifu yupo atakusukuma utoe na utapata amani.
Imeandikwa “Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.” Warumi 8:6
§  Wamerudi nyuma, watu wsiotoa zaka wanarudi nyuma, yupo kanisani kama mshirika wa jengo lakini si mshirika wa MUngu, ukitengeneza vizuri na Mungu utaona nguvu. “Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.” Luka 16:13
§  Unampenda Mungu kwa kiwango kidogo sana; Ni vigumu sana kwa mtu anayempenda Mungu kwa kiwango kidogo kumpenda Mungu kwa mali zake na vitu vyake vyote “Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, naitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;” 1 Nyakati 29:3  
§  Watu wasiotoa zaka wanawaza wanamwadhibu mchungaji; mtu anawaza kwamba anamwadhibu mchungaji, kama mchungaji anataka kufanya kitu atumie fedha zake. Ukiwaza hivyo ni mawazo ya kiumaskini na uukiendelea hivyo hutaon aBaraka za Mungu.

Mchungaji Dr. Godson Issa Zacharia akiongoza maombi ya Toba wakati wa Ibada ya leo.
MAWAZO MABAYA YA WASIOTOA ZAKA/WANA SABABU ZAO
o   Napata kidogo sana hivyo siwezi kutoa zaka, mtu anakuwa maskini ni kwa sababu anawaza kinyume na maandiko, “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.  Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.” Mithali 23:7, usipowaza mawazo chanya, ukiwaza ndivyo ulivyo na ndiyo yatakayokupata.  Mtu akiwaza kuwa ana kidogo hii ni dalili ya wizi, na mawzo ya mwizi ni kwamba hupata kidogo sana. Katika habariya utoaji hakuna habari ya kidogo au kingi.
o   Napata sana siwezi kutoa zaka; “Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.” 1 Nyakati 29:14, Unakuta kuna mtu amepata milioni 20, na 10% ya milioni 20 ambayo ni milioni mbili, anaona ni kubwa sana anawaza hiyo hela angefungua kamradi kingine. Lakini anasahau huo uwezo wa kutafuta milioni 20 ameupata kwa Mungu. Hutakiwi kumlinganisha Mungu na vitu vyako.
o   Pesa amepata kwa shida, hivyo hawezi kumtolea Mungu zaka; “Bwana, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.” Zaburi 131:1 unatakiwa ujue myoni mwako unamtolea yeye na usitake kujua matumizi ya pesa/zaka hiyo.
o   Wachungaji wanatumia pesa zake kwa anasa; watu wengine wanawaza pesa zinatumiwa na wachungaji kwa anasa/kwa faida zao, unatakiwa uwaze hiyo zaka unafaidika mwenyewe. Hataki kumwona kiongozi wake amefanikiwa au amepiga hatua. Huyu mtu anatamani mchungaji amevaa viatu vimetoboka na ndipo ataona pesa zake zinatumika vizuri.
o   Wachungaji wote ni matapeli na wezi; mtu mwenye mawazo mabaya anaona wachungaji ni wezi, hutakiwi kuwasulubisha wema na waovu. Maandiko yanatupa maonyo ya kuwaza huyu ni mwema na kumbe ni mwovu, wewe unatakiwa umtii Mungu. Hukumu unatakiwa kumwachia Mungu, wewe unatakiwa utoe zakakwa ajili yakufungua madirisha ya mbinguni. Kwa habari ya kwamba mchungaji anaiba mwachie Mungu. Imeandikwa,“Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!” Isaya 5:20.  
o   Fungu la kumi ni kubwa sana siwezi kutoa; kuna mtu anawaza 10% ni kubwa sana anaanza kutoa 5% au 1% na akiona ni kubwa anazidi kupunguza. Lakini serikalini tunalipa kodi 18%. Pia waza kama Mungu akaruhusu kiwanda unachofanya kazi kikifungwa utapata wapi mapato. Utalala kanisani uombe Mungu atende, na maombi ya mwenye dhami ni kelele mbele za Mungu.
o   Najenga nyumba yangu hivyo siwezi kutoa zakazangu; lakini Mungu hajawi kutanguliza tujenge nyumb zetu kabla yak wake. “Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?” Hagai 1:3-4. Unaweza ukawa unajenga nyumba na ukawa unaibiwa na mafundi.
o   Nina msiba/sherehe ya kuchangia hivyo siwezi kutoa zaka; lakini serikali huwezi kuiambia serikali wasikate kodi kwa sababu una msiba.
o   Nina madeni mengi sana hivyo siwezi kutoa zaka; unawaza una mkopo CRDB, VICOBAna Mchezo, na kwa nini usiache kuchangia ili utoe zaka.
o   Mimi ni mjane hivyo siwezi kutoa zaka; wajane wanatakiwa kuhurumiwa kabisa, Biblia inasema tusiwaonee wajane. Tunajifunza hata Eliya alienda kwa mjane na alitaka kujua kama huyu mtu kama atatii. Mama Yule alipofanya mkate Eliya akamwambia akakusanye vyombo. Maana yake muujiza wake ulikuwa tayari baada ya utii. Hapa tunajifunza kila mtu anaweza kumtolea kawa nafasi bila kujalisha hali aliyonayo. “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;” Marko 12:41-43, 
Baadhi ya makutano walioamua kumpa Yesu maisha yao ili waondokane na laana ya sadaka ya Zaka.
o   Mimi ni mwanafunzi siwezi kutoa zaka Wanafunzi wengi wanamwibia Mungu kwa kujiteteta hawana kipato, ili hela unayopewa ya matumizi unatakiwa utoe 10% maana ni sehemu ya Mungu. Neno la Mungu halijaweka matabaka bali linawataka watu wote kumtolea Mungu zaka. Imeandikwa, “Mheshimu Bwana kwa mali yako,  Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.” Mithali 3: 9.  
o   Sijaajiriwa siwezi kutoa; hata ukiajiriwa huwezi kutoa kwa sababu umekosa utii. ukikosa uaminifu ukiwa haujaajiriwa na hata ukiajiriwa hautakuwa mwaminifu. “Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida.” Luka 9:10.  
o   Nimestaafu niko kwenye pensheni siwezi kutoa zaka; kuna wastaafu wengine wanapesa nyingi kuliko walioajiriwa. Hatutoi zaka kwa sababu ya wingi wa pesa bali tunatoa kwa sababu ni agizo la Mungu.
o   Nasaidia maskini, nafanya miradi hivyo siwezi kutoa zaka, kusaidia maskini ni jambo zuri lakini hakuzuii wewe kutoa zaka, ili kuvunja umaskini katikati ya wakristo lazima tujifunze kutoa zaka. Kuwa mtii wa sharia za Ufalme wa Mungu.
Showers of Glory Morogoro wakimsifu Mungu baada ya maombi ya toba wakati wa ibada ya leo.
 KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.co  m/


Share:
Powered by Blogger.

Pages