Sunday, June 10, 2018

SOMO: NINAKATAA UDHAIFU NA MAGONJWA YA KISHETANI


GROLY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA -MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA

JUMAPILI 10 JUNE, 2018

“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani?, Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka”
Zaburi 27:1-2

UTANGULIZI;
Magonjwa na udhaifu wowote unao ufahamu na usioujua hautokani na Mungu,. Asili ya magonjwa na udhaifu ni ulimwengu wa roho (yaani mashetani). Kuna watu wanawaza magonjwa, shida na udhaifu ni mambo ya kibaolojia, si kweli! Ukijua vizuri na kumpiga anayaeleta udhaifu na magonjwa utakuwa salama.
Kupitia SOMO hili utajifunza namna shetani anavyoleta udhaifu kwenye maisha ya watu na jinsi ya kuyakataa ili uwe huru kwa jina la Yesu.

Ninaposema magonjwa na udhaifu simaanishi magonjwa na udhaifu wa mwilini tu, bali magonjwa na udhaifu wa vitu mbalimbali mfano udhaifu kwenye mambo ya fedha, akili, tabia, mambo ya ndoa n.k;
Mfano; mtu anaweza kuwa na udhaifu wa kihisia, akipanda kwenye daladala nilazima amtongoze jirani yake hata kama hajuhi ni mke wa mtu au ni mgonjwa. Mwingine anaweza kuwa mdhaifu kwenye pombe, akisikia harufu ya pombe anakosa amani. Udhaifu huu unatengenezwa na mashetani ili wewe uachwe, usipige hatua, leo Bwana anataka useme kwa kinywa chako kuwa NAKATAA magonjwa, NAKATAA udhaifu wa kishetani kwa jina la Yesu.
Kuna nguvu katika kukataa, Raila Odinga alikataa kukubali matokeo ya uraisi, na alilopokataa akawekwa pamoja na raisi madarakani. Ulipoumbwa Mungu hakukuumba uwe mlevi, mchoyo au kilema, shetani ameandaa udhaifu na magonjwa ili afya, kazi, ndoa iharibike. Kama shetani alikuwa ameandaa udhaifu wewe ukianza kukataa udhaifu, magonjwa mara kwa mara mletaji anayabeba na kuyapeleka mahali pengine.
Ikiwa Bwana ni nuru ya wokovu wetu, je twaweza kuwaogopa wachawi, wasoma nyota, waganga? Hapana! Ikiwa watenda mabaya wamekuja kukutesa, wakiwa wamebeba magonjwa na udhaifu wa kila aina ya mateso, waje kula nyama yako, kukuangamiza wewe USIOGOPE!! kwa maana Mungu tunayemtumikia yu ndani yetu. Mungu yuko kila mahala, kazini, porini, ukiamini haya kuwa yeye ni mwokozi na mtetezi wetu hutaogopa maisha ni mwako.
“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.” Zaburi 27:1-5
Duniani kuna mashetani ambao kazi yao ni kukukaribia ili wale nyama yako, kula ndoa yako, elimu yako n.k. Wakotayari kukutia udhaifu, wale mnofu wa biashara yako lakini Biblia inasema hata kama watakuja kukukaribia ukiwa na Yesu wao watajikwaa, kwa maana Yesu anaitwa jiwe likwazalo.
Shetani akimwona mtu ana mafanikio anatuma majeshi yake, akiona ameshindwa, anatuma wenye mamlaka kwenye ulimwengu wa roho, akishindwa analeta wakuu wa giza (Waefeso 6:12), anajipanga na majeshi aje akudhuru, wakati anaandaa jeshi ili kukudhuru Mungu naye anaandaa jeshi la kukulinda. Yawezekana yapo majeshi ya kishetani yamejiandaa kukuua wewe na maisha yako lakini leo naamuru jeshi la Bwana likae, likulinde wewe na familia yako kwa jina la Yesu.
Hii ndio siri tunayoijua sisi tunaomjua Bwana, mashetani wanafanya kazi pasipo kujulikana, kwa akili ya mbinguni tunafahamu kuna waanao taka kula nyama, hivyo wanajipanga kukuharibu. Tunalo jeshi la Bwana linatulinda, unaweza kutumiwa jeshi ili kuangamiza kazi yako, waue ndoa yako n.k. Mashetani wakimtia mtu udhaifu wao wanachukua wanacho kitaka kutoka kwake.

Asili ya magonjwa na udhaifu unaousikia duniani chanzo chake ni mashetani, katika ulimwengu wa roho. Baadhi ya watu wanawaza hivi magonjwa, shida na udhaifu ni mambo ya kibaologia si kweli wanasema mtu anaugua kansa kwa maana kuna wadudu fulani wameingia. Lakini tabu, shida na magonjwa vyote huanzia kwenye ulimwengu wa roho. Na si tatizo la kibailojia tukijua vizuri na kumpiga anayaeleta tutakuwa salama.
Lakini ikiwa huamini hivyo, ukiumwa kitu ukasema niende kwa daktari yeye atakata vidole vyako kwa sababu ya kansa, ni kweli madakarii wanafanya kazi lakini wewe kabla hujaenda kwa daktari omba kwanza. Ukiomba Yesu akikaa ndani yako wanapokukabiria wanijikwaa wanashindwa kuleta hayo magonjwa na udhaifu.
Mfano shetani anaweza kwenda kwa mtu kuweka udhaifu wa kichwa, mtu anaanza kuugua presha, anakunywa kila dawa lakini maumivu yako palepale, akidhoofika anakuja mwingine mla nyama, wanambeba wanamchukua msukule wengine wanajua kuwa amefariki kumbe amemchukuliwa na chanzo kimeanza rohoni ndo maana limeshindwa kutibika.
Mtu anaweza kuugua kansa lakini nyuma yake kukawa na roho ya kichawi, Dr. Robert Galo mwanasayansi wa Marekani, aliyetengeneza virusi vya UKIMWI alipomaliza akasema, “I have created HIV Aids in order to depopulate black people” nimetengeneza virus vya ukimwi ili kuwapunguza waafrika. Lakini wengine wanaita ugonjwa wa kisasa. Wachawi wanaweza kutengeneza udhaifu ili wapigane na wewe ili ushindwe, ushindwe kuanza kazi, ushindwe kuomba ndio maana lazima ukatae kwa jina la Yesu.
Magonjwa na udhaifu wote hautokani na Mungu, ukiona unaharisha, mgonjwa au mdhaifu hayo yote hayatokani na Mungu. Raisi wa Zambia alipoona kuna shida ya kipindupindu nchini mwake aliita watu wote waombe hadi kipindupindu kiishe. Magonjwa hayatokana na Mungu wala Mungu hawezi kukuwekea magonjwa au udhaifu ili akujaribu wewe. Ikiwa yatokana na Mungu kwa nini asikujaribu kwa kukupa fedha kuona kama utatoa sadaka au zaka, wengine wanasema ni mitihani ya Mungu, je nani anasahihisha mitihani hiyo?.
Magonjwa au udhaifu vinatokana na shetani, moyo wa Mungu hapendi kumtesa au kumuhuzunisha mwadamu. Mtu yoyote mwenye udhaifu na magonjwa hana furaha na Mungu amesema hapendi kumuhuzunisha mwanadamu, Yule mwanamke aliyetokwa na damu alikuwa na huzuni nyingi na kuteseka, na Mungu ameahidi kutomuuzunisha mwanadamu hivyo mateso yanatokana na shetani.
“Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha.” Maombolezo 3:32-33
Vipo vitu vinaleta huzuni, kuna mambo ulikuwa unafanya lakini hufanyi tena, kazi ulikuwa unafanya lakini hufanyi tena, husomi, huwezi kutembea n.k. Ndio maana Yesu alipokuja duniani alisema alikuja kuleta uzima na kuchukua huzuni zetu yeye akiona husomi, huzai, hufanyi kazi anapata huzuni ili akupe furaha, huzuni si sehemu ya Mungu kabisa.
“Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.” Isaya 53:3
Kwa Mungu ukionekana una matatizo ni huzuni, lakini kwa shetani ukionekana una udhaifu na huzuni nyingi kwakwe ni furaha, cha ajabu watu wakimwona mtu anaukimwi au kisukali, au kansa wanasema ni mapenzi ya Mungu.
Je, umeteseka? Je, una huzuni ? Je, una huzuni? Ikiwa una hali kama hizo ujue ni shetani amekuletea hali hiyo, Mponyaji Mungu hawezi kutia magonjwa, hakuna mahala aliposema kuwa yeye ni Mungu wa kutia udhaifu.
"akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. " Kutoka 15:26
Wakati mwingine shetani anakuletea magonjwa na udhaifu kwa njia ya akili sana, anaweza kukuletea udhaifu kama zawadi, kama chakula, kama pongezi , ni wakati wako sasa kukataa, ukisema kabisa nakataa udhaifu, nakataa balaa, vinaondoka kwa jina la Yesu.
Siku moja shetani alienda mbele za Mungu, Mungu akamuuliza shetani unatoka wapi?, akasema natoka kuzunguka huku na huku (sawa na kusema nilikuwa kugawa vifurishi vya udhaifu dunia, lakini kuna kajamaa kamoja kanaitwa Ayubu kamekataa kupokea kifurushi cha udhaifu). Baada ya shetani kuharibu vitu vyake akawa anamtafuta yeye, ndipo akampiga Ayubu kwa majipu mwili mzima.
“Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.” Ayubu 2:2-7
Shetani akikutembelea anakuja na kifurushi cha kuua, kuiba na kuharibu. (Yohana 10:10) akikuta huna wigo wa kimungu anakurushia kifurushi cha magonjwa, cha udhaifu, na aikisha kutia udhifu anakula nyama yako, anakuchukua mzima mzima, anachukua ndoa yako, kazi yako na kila ulicho nacho. Unapoona mwanzo ulikuwa sawa lakini gafla huko vibaya ujue kuna kifurushi cha udhaifu kimeletwa juu yako na shetani.
Ikiwa umezingirwa na wigo wa Mungu shetani hawezi kukudhuru kwa jambo lolote, atakapojaribu kula nyama yako anakuta umezingirwa wewe na mambo yako anashindwa kukuingilia. Ukimwona mume wako amepatwa na shida usimkimbie kama alivyofanya mke wa Ayubu mara nyingine ni shetani. Leo Bwana akuwekee ulinzi wa kimungu kwenye afya yako, kazi, watoto na mali yako na kila ulichonacho kwa jina la Yesu.
Kabla hujaenda hospitali omba kwanza, kuna magonjwa mengine ambayo njia za kidaktari hayawezi kutibika kwamaana chanzo cha magonjwa hayo ni rohoni yaani ya kichawi hayatokani na kibailogia kama watu wanavyo waza. Ndio maana Yesu Kristo alikuja kuleta uzima, yeye ambaye ni mfalme, aliyekuwako na Mungu akapigwa mijeredi ,ili kwakupigwa kwake sisi tupate uzima.
“Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.” Isaya 53:4
Ikiwa umeamini kwamba Bwana hawezi kukukuhuzinisha ni rahisi kwako kukataa magonjwa na udhaifu wa kichawi. Biblia inasema Yesu alinyenyekea hata mauti , na kwakuwa alinyeyekea Mungu alimkilimia jina lipitalo majina yote ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwa la vitu vya duniani na mbinguni. Jina la Yesu ni zaidi ya ukimwi, ni zaidi ya kansa, ni zaidi ya kifua kikuu. Ukiliamini jina la Yesu unashinda udhaifu wowote,
Shetani anaweza kuweka udhaifu kwenye kazi, ndoa, biashara yako na wewe ukaridhika. Biblia inasema lifanyeni kila jambo kwa jina la Bwana. Ukitumia jina la Yesu lenye nguvu, kwa jina la Yesu mashetani, udhaifu, magonjwa, kuzimu, inapiga magoti.
Injili ya Kristo inazungumza kwamba Yesu alifanya kazi kubwa ya kuwaondoa mapepo kwamaana kuna mahusiano kati ya mapepo na udhaifu na magonjwa, alishughurikia vitu vya rohoni ingawa alikuwa katika mwili, hakuja kutengeneza hospitali ya kansa, au kufungua hospitali ya watoto, au ya moyo, au benki ya fedha kwa maana alijuakuwa haya matatizo waliokuwa nayo wanadamu yanasababishwa na mambo ya kiroho
Siku moja alikwenda nyumbani kwa Petro akamkuta mkwe wa Petro hajiwezi kwakuwa alikuwa na homa, ndipo Yesu akamgusa mkono na homa ikamwacha akamtumikia. Wapo watu wamepata homa za kichawi na wamekuwa hawawezi, hawawezi kufanya kazi, hawawezi kusoma n.k lakini kwa jina la Yesu homa zinatoka na hao wanakuwa wanaweza tena kwa jina la Yesu.
“Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.” Matahayo 8:14-15
Kuna vitu vinaweza kukufunga kisha ukawa dahifu, huwezi.. Unaweza kupatwa na homa ya kishetani ukawa huwezi, unaweza kukaliwa na pepo miguu ukawa huwezi kutembea, unaweza kufungwa mikono kichawi ukawa huwezi kushika, unaweza kufungwa mwili na kugeuzwa kila kitu chako na ukawa huwezi. Lakini pepo huyo akiondolewa unaweza tena kwa jina la Yesu. Ndio maana homa nyingine zina majina ya ajabu kama vile homa ya manjano, homa ya kuku, homa mafua,n.k kumbe ni pepo kazi yake ni kumfanya mtu asiweze.
Mambo tunayo yafanya katika dunia ya kawaida ni ya kibinadamu, kuna namana nyingine tumijiita majina mengi kama vile, siwezi kula, siwezi kusoma, siwezi kuona n.k. Neno hili limekuja baada shetani kutawala, limekuja baada shetani kuweka udhaifu kwenye maisha ya wanadamu. Yesu alikuja kuwaaondoa mashetani ya kutoweza
Injili ya Yesu inasema yeye alikuja kuwaondoa mapepo hili watu waweze, wazae, wafanye kazi, wafanye biashara wawe na afya njema. Wapo watu hawawezi kukaa na mke au mume pamoja kumbe ni mapepo yametengeneza kitu kwenye familia hata wanaonana kama mtu na dada, yakiingia mtu hatamani kufanya kazi tena, hawezi kujishughuisha kabisa.
Yesu alitembea mahala pote hata Galilaya akiwatoa watu mapepo na kuwaponya. Shetani amepanda vitu kwenye maisha ya watu lakini yeye alikuja kuvitoa, alipita kila mtaa na miji, ili aondoe udhaifu huo. Ndio maana kila pando lisilopandawa na Baba wa mbinguni litangolewa.
“Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.” Mathayo 4:23-24
Kuna mtu amewekewa udhaifu kwamba hawezi kujibidiisha, hawezi kutafuta kazi, hawezi wala kufanya kazi, tangu asubuhi ameshinda anaangalia Tv kwamaana amewekewa roho ya kutoweza, kuna watu hata kusema nakupenda kwa mke wake ni mwiko, unatakiwa sasa uondoe hali ya kutoweza maisha mwako kwa njia ya kukataa kwa jina la Yesu,
Mungu amekuweka juu ya mataifa na falme ili kung’oa mapando ya kishetani ili uwe huru kwa jina la Yesu. Yesu alaitembea miji na vijiji akifundisha na kuwatoa watu mapepo kuwatoa katika hali ya kutoweza, na baada ya kazi yake aliwatuma wanafunzi kuifanya kazi yake aliyoianzisha, wewe unaye mwamini Yesu unaweza kuponya magonjwa na udhaifu wa kila namna.
“Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Mathayo 10:1
Wachawi, mapepo, waganga kazi yao kubwa ni kuleta udhaifu na magonjwa kwenye maisha ya wanadamu. Yakitolewa mtu anakuwa salama kwa jina la Yesu. Siku moja Yesu aliletewa mtu mwenye kifafa, aliyekuwa anamwangusha kwenye moto, kwenye maji, Kuna mahusiano makubwa kati ya mapepo na kuanguka kwa Yule kijana, na mapepo yalipo mtoka akawa salama.
“Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.” Marko 9:25-27
Ni sawa na wewe uliyetembea kila mahala na kuingia kila hospitali lakini ujapata nafuu, ni wakati wako sasaa kuja kwa Yesu kugusa pindo la vazi lake ili upate uponyaji, ukigusa pindo la vazi la Yesu unapata uzima, udhaifu unaondoka, nawe unakuwa huru kwa jina la Yesu.
Jifunze kuomba, protokali za kidunia ziache ziende lakini mtu anaye mtumikia Mungu lazima uombe, unakataa magonjwa, unakataa udhaifu wako na wafamilia yako, ukikataa kwa maombi udhaifu wowote ule unaondoka kwa jina la Yesu. Nivizuri ujifunze kuomba (Tafuta kitabu cha KUOMBA KWA BIDII KILICHOANDIKWA NA PASTOR, DR. GODSON ISSA ZACHARIA, kwa msaada wa kujifunza kuomba) ukiwa ni mtu wa maombi shetani hawezi kukushinda.
Ukitaka kutoa tatizo maishani usishughurike na matawi ya tatizo lako, bali shughurika na chanzo cha tatizo lako, ikiwa mizizi ya tatizo lako ikiisha unakuwa salama, Yesu aliletewa shida ya kifafa lakin chanzo cha shida hiyo ilikuwa ni mapepo
Pepo anaweza kumfanya mtu atokwe na povu, asage meno, lazima utumie mamlaka na uwezo wa kutoa mapepo hayo. Nguvu hizi zinatokana na kumpokea Yesu, lazima umkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wake, na kumwamini moyoni mwake utaokoka. Kuoka si baadaye, au hakupo, wokovu ni sasa.
Mungu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea akikuokoa wewe anakuokoa wewe na mambo yako yote, kukiri kunasababisha mtu kufanyika mtoto wa Mungu, ukifanya hivyo unahama ufalme kutoka ufalme wa giza kuingia wa ufalme wa nuru, ndio sasa unapata uwezo wa kumshinda adui shetani kwa jina la Yesu.
“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Warumi 10:9-10

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
FIKA KANISANI,
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MKUNDI MINARA MITATU MOROGORO
AU WASILIANA NASI KUPITIA 
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro
Share:
Powered by Blogger.

Pages