Saturday, April 6, 2019

AMEZUILIWA ASIENDE KWENYE HATIMA YAKE

SIKU YA TANO YA SEMINA YA NENO LA MUNGU
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
ALHAMISI TAR O4 APRIL, 2019
MUHUBIRI: PASTOR PAUL JOSHUA (SNP KIGOMA)

Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia.

Mchungaji Kiongozi Paul Joshua (SNP KIGOMA)

UTAMGULIZI
Kwenye maisha yeyote mtu unayemuona yupo juu kuna mtu alimsaidia kumvusha ili aweze kwenda kwenye hatima yake. Wewe peke yako huwezi kwenda kwenye hatima yako hata kama umesoma, unaakili, unahela huwezi peke yako unahitaji mtu akuvushe. Hata Daudi kuwa mfalme alimuhitaji Samweli ampake mafuta ndipo awe mfalme. Pia Samweli ili awe nabii alimuhitaji Eli ampake mafuta hivyo katika maisha unamuhitaji mtu ili akusaidie kusonga mbele.
Kila mtu ana hatima yake yaani ana sehemu ambayo Mungu amempangia kwenda, kila aliyeokoka kuna sehemu ya maisha yake ambako anaelekea. Unaweza kuanzia chini kabisa lakini kuna sehemu Mungu anakupeleka na wakati Mungu anakupeleka huwezi kujua kama kuna sehemu unaenda lakini utaona mabadiliko katika maisha yako. Unaweza kuzaliwa kwenye nyumba ya majani lakini ukaishia kwenye ghorofa unachotakiwa kujua ni kwamba unapoanzia sio utakapo ishia. Sauli alianza na Mungu kama mtu aliyepoteza punda wa baba yake lakini katika kutafuta tafuta akaishia kwenye ufalme, Daudi alianza kwenye kuchunga kondoo wa baba yake lakini katika kuchunga kondoo akachaguliwa na Bwana kumuua Goriath na kisha akawa mfalme, ndugu yangu usidharau mambo madogo Mungu huwa anaanza na mambo madogo lakini baadae yanakuwa makubwa.
Jioni ya leo hii tamka ya kwamba hujafika yaabi hujafika mahali ambako unatakiwa kwenda ili umiliki hatima yako, hata maisha uliyonayo bado hujafika na ndio maana unaona shida, mateso, magonjwa na taabu, unaona kila ukijaribu kufanya biashara hufanikiwi kabisa kuna mtu umekwama sehemu ili usiende mbele lakini nataka kukwambia kuwa leo hii lazima uende kule ambako Mungu anataka uende. Wachawi wanaweza kuona unakoelekea, wanaweza kuona ndoa inapoelekea wanaweza kukuona kwamba huyu baba au mama leo kaanza kidogo lakini baada ya miaka mitatu minne utakuwa mtu fulani, unaanza kuonekana tangu ukiwa mdogo.
“Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.” (Mathayo 2:1-2)
Watu walifunga safari kwenda kumtazama Yesu Mfalme wa wayaudi maana yake mtu anaweza kuonekana kwamba atakuja kuwa tajiri, kuwa kiongozi, kuolewa na mtu fulani mkubwa hivyo wachawi wakiona tu wanaamua kukuzuia. Shetani anafanya kila njia kupindisha hatima yako yaani ulikuwa na mikono ya fedha, ulikuwa na mambo mazuri, lakini leo hii umekwama unaona biashara haiendi kama zamani, unaona mambo hayaendi kabisa unajiuliza ni kwanini mbona zamani yalikuwa yanaenda lakini kumbe kuna wachawi wamekaa wakachungulia hatima yako na kuamua kukufunga ili kwamba usifanikiwe usiende kwenye mafanikio yako.
Kuna mtu mwingine kafungiwa kwenye nyumba ya majani ili kwamba asiende kwenye nyumba nzuri. Hakuna vita vikubwa kama mtu kuwa na kwake yaani vita vya ardhi au vita vya kumiliki ardhi. Kuna watu mpaka wanakufa hawajawahi kumiliki ardhi na ndio maana watu wanapigana kwa sababu ya ardhi huwezi kuwa tajiri kama huna ardhi, huwezi kumiliki kama huna arhi, utajiri wote umo ndani ya ardhi, madini, mazao, nyumba pamoja na vitu vizuri vyote vimo ndani ya ardhi.
Kuna watu wengi wamezuiliwa sana ili wasiweze kumiliki ardhi lakini leo hii ninatangaza kwenye ulimwengu wa roho mashetani wote waliokaa ili kukuzuia wewe usiende unapotakiwa kwenda leo hii ninawafyeka kwa jina la Yesu Kristo na ninafungua hatua zako tena umiliki kile ardhi tena na kujenga nyumba nzuri kwa jina la Yesu Kristo.
Kuna watu wanatakiwa kwenda kwenye nyumba zao lakini wamefungwa wasiende, mwingine hata ramani unayo kabisa lakini umefungwa miguu ili usiende kumiliki nyumba. Mwingine unaweza kuota ndoto kwamba miguu yako imekuwa mizito sana, mwingine unaota ndoto unatembea lakini miguu ni mizito sana yaani haufiki kule unapoelekea, mwingine unaota ndoto unapanda mlima lakini miguu yako ni mizito sana ukiona hivyo jua kuwa miguu yako imelogwa yaani umefungwa sehemu ili ushindwe kwenda kwenye hatima yako. Kuna kamba za wachawi, waganga, na mashetani zimekufunga ili usikimbie na ndio maana unaona mambo yako yanaenda polepole biashara inaenda taratibu unaweza kuona kuwa unaanza biashara na mtu mnaanza na mtaji sawa, mnaanza siku sawa lakini biashara yako ikawa inasuasua na ya mwenzako inaenda vizuri ni kwa sababu miguu yako imefungwa ili usiende.
Wachawi wanaweza kuona nyota yako, wanaweza kuona je hii nyota ni ya wapi, je ataishia wapi. Hata kwenye kazi ya Mungu kuna sehemu ya kufika ambayo Mungu amekuandalia ili ufike kama mtumishi wa Mungu Jehovah, aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo hata mimi naona kuwa bado sijafika naona mbele kuna baraka zangu, mbele kuna mafanikio yangu, naiona huduma yangu mbele yangu inakwenda kustawi. Hata wewe katika maisha yako ifike wakati uanze kuona mabo mazuri yaliyo mbele yako, inatakiwa ifikie wakati uanze kuwa baraka kwa wengine yaani uwe na mali mpaka utoe kwa wengine, ifikie wakati uwe unamiliki nyumba mpaka unawabariki wengine, uwe na magari mengi mpaka mengine unatoa kwa watu, ifikie wakati uwe na vyakula vingi mpaka vingine unaamua kusaidia watu wengine.
Kila mtu anayo njia ya maisha yake ambayo Mungu amemuandalia ambayo kwa hiyo inakuongoza kuelekea kwenye hatima yako njema inaweza kuwa kwenye biashara yako, kazi yako, ndoa yako, kazi yako n.k. Siku moja nilimwomba Mungu anionyeshe njia ya maisha yangu nikafunga na kuomba mara ya kwanza nikaona magogo na miti mikubwa imezuia njia yangu, nikaomba sana tena kwa mara ya pili nikaona kwenye njia yangu kubwa kuna mtu mmoja mkubwa amekaa kwenye njia yangu mkubwa anatisha sana anasema kuwa huku huendi unaenda wapi mbona kwenye familia yako hakuna mtu aliyeenda huku kisha nikaona kamba zimenifunga miguuni nikasema kwa jina la Yesu kamba zikakatika katika miguu. Wakati huu nilikuwa katika maombi ya mfungo ndugu yangu nataka nikwambie kuna mambo mengine hayatoki bila kufunga na kuomba ukishinda kwenye kipengele cha kufunga yaani kuto kula pamoja na usingizi yaani kuamua kuto kulala ili uombe na ndipo mambo yako yatakapo kwenda sawa.
Kanisa likimtafuta Mungu hata mchungaji anapata unafuu wa kufungua kanisa, jifunze kuamka usiku anza kuomba mtafute Mungfu asipojibu leo atajibu kesho omba yafanye maombi kuwa sehemu ya maisha yako omba omba mpaka unazeeka mpaka unakufa omba mpaka unakata roho.
Kuna mtu leo hiii anatamani kujenga lakini hawezi ni kwa sababu katika ulimwengu war oho ame3fungiwa kwenye nyumba ya majani yaani anaishi kwenye kibanda kilichoezekwa kwa majani na ndio maana huna nyumba na huta weza kujenga kwa sababu ardhi imeambiw kuwa utangetange kwenye nyumba za kupanga mpaka ufekwa sababu kwenye adhi kuna mtawala. Wakati mwingine unaweza kufanikiwa kujenga nyumba lakini usikae kwenye hiyo nyumba aidha unaweza kufa au unaweza kukaa kwenye hiyo nyumba lakini ukawa hulali kila unapol,ala unaona kama nyumba inapanda juu na kushuka inakuwa ni mateso makubwa kwa sababu umezuiliwa ili usimiliki ardhi.


Baadhi ya makutano waliohudhuria semina ya Neno la Mungu lililofundishwa na Mchungaji Paul Joshua kutoka Kigoma.
Kuna watu ambao wanatakiwa kwenda kwenye hatima zao lakini wachawi wamewafunga miguu yao. miguu inaisha ray a kumiliki (Joshua 1: 3)… kila mahali mabako nyayo za miguu zikikanyaga tu panakuwa ni petu haijarishi amejenga nani, anakaa nani, kuna siri ya kumiliki mali za adui, kila kitu ambacho unakitafuta kuna mtu yupo hakuna kipya, unatamani uwe bosi ofisi Fulani tayari kuna bosi hivyo inatakiwa kusukumana tu yaani kumuondoa mtuj ili u7kae wewe, kuna mtu amekushikia gari lako, kiwanja chako, ofisi yako kinachotakiwa tu ni kumuondoa na kumiliki vitu vyako na leo hii nakufungfua miguu yako uende ukamiliki kazi yako, ndoa yako, ardhi yako n.k. nenda kwa jina la Yesu Kristo.
Kila sehemu ambayo uliwahi kuota ndoto kuwa umeenda lazima ufike ikiwa utapambana kumuondoa azuiaye kwa maana tayari umesha pamiliki mahali pale, mguu wako wa ndani amekwisha kufika imebaki tu wewe kwenda kimwili unatakiwa kupambana ili uende kwa jina la Yesu Kristo. Usikubali kufia jangwani kwa jina la Yesu Kristo.
Kuna wengine baraka zako zimo ndani ya wito; yaani ukiacha wito umeziacha baraka kuna mwingune unasikia kusaidia watu, kumtumikia Mungu n.k. ambacho Mungu amekuitia ndani yake kuna baraka yako, kuna kazi yako, ndoa yako, biashara yako n.k. ukitaka kuishinda vita kwa wepesi basi mtumikie Mungu ukimtumikia Mungu hata kama unadeki kanisa unaitwa ni mpaka mafuta wa Bwana, hata kama ni showers unakuwa ni masihi wa Mungu, hata kama ni muimbaji, muhubiri, au mpokea wageni kanisani unakuwa ni mpakwa mafuta wa Bwana hivyo mtu akikugusa anakuwa amegusa mboni ya jicho la Bwana hivyo anapondwa kabisa na wewe unakuwa huru.
Kuna watu ambao wanatamani sana kwenda kwenye hatima zao lakini wanashindwa kwenda mwingine miguu yao imefungwa na nyoka kabisa; nyoka amewafunga ili wasiende. Yaani unatamani kwenda mbali kimasomo lakini huwezi kwa sababu kuna kamba ambazo zimekufunga ili usiende, unaweza ukaona kuwa umempamtu mtaji.
Kuna wengine miguu yao ina mavazi ambayo imevikwa. Kuna mavazi ya kitajiri, maskini, kikuhani, vazi la heshima, vazi takatifu n.k. mwingine anatembea lakini rohoni hana nguo kabisa wamekwisha kunyang’anya vazi lako lakini njioni ya leo vazi lako litaonekana tena Yesu mwenyewe alivaa vazi ambalo lilikuwa na jina Mfalme wa wafalme kumbe kwenye vazi kuna jina. Kuna wengine hawana vazi la rohoni lakini leo hii Yesu anakwenda kukurudishia vazi lako kwa jina la Yesu Kristo.
Kuna vitu umepoteza yaani vitu vya rohoni umepoteza kama vazi, viatu vyako vya kiroho. Ukipoteza hivi unakuwa ni wakawaida kabisa yani hata hutishi wachawi hawakuogopi kabisa kwa sababu huna vazi na viatu vya rohoni. Viatu vya rohoni vinakusaidia wewe uweze kumiliki biashara, utajiri, afya, ardhi, viatu vinakusaidia umiliki huduma n.k. leo hii naifungua miguu yako iliyofungwa kwa jina la Yesu Kristo.
Kamba za kichawi zinaweza kumfunga mtu yaani anaweza kuanza biashara akafanya wewe lakini baadae ikafa kwa sababu miguu yake ya rohoni imefungwa ili asiende kwenye mafanikio. Mwingine kafungwa miguu yake yaani miguu imelogwa asiende mbali. Kuna mtu alitegewa uchawi njiani ukakanyaga na shida ikaingia kwenye maisha yako.
“Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu” (Ayubu 13:27)
Miguu inaweza kufungwa na mikatare; hii ni aina ya kamba ngumu sana ambayo ikikufunga huwezi kupiga hatua kabisa. huwezi kupiga hatua kuelekea kwenye ushindi wako, utajiri wako lakini leo nakufungua na uwe huru kabisa kwa jina la Yesu.
DALILI ZA MTU ALIYEFUNGWA MIGUU YAKE ILI ASIENDE KWENYE HATIMA YAKE.
1. Miguu kuwaka moto
2. Miguu kuwasha
3. Miguu kuvimba; unaweza kuwaza ama ni presha au nini na miguu hii inavimba kwa muda fulani tu ambapo unatakiwa kwenda kwenye mafanikio yako. ukitaka kuanza biashara inavimba na ukisema kuwa basi naamua kukaa nyumbani basi miguu inapona kabisa. lakini leo hii ninaamuru kwenye ulimwengu wa roho kila kamba zilizoka kufunga miguu yako ili usiende leo hii ninazikata kwa jina la Yesu Kristo.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
FIKA KANISANI,
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MKUNDI MINARA MITATU MOROGORO
AU WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia


TEL: +255 719 798 778
Share:
Powered by Blogger.

Pages