SNP Dr. Godson |
Na Mwandishi wetu| Morogoro| Jumapili| 17/11/2013.
Jumapili ya leo imeitwa jumapili ya furaha ni kutokana na matukio mbalimbali ambayo yaliipamba siku hii mpaka kuonekana kuwa jumapili iliyojaa furaha kwa kila mtu aliyehudhuria ibada ya jumapili ndani nyumba ya ufufuo na uzima morogoro.
Awali ya yote ibada ilianza kwa watoto wa showers of Glory walipoanza kumsifu Mungu kwa wimbo uliojaa Shukrani mbele za MUNGU unaoitwa Tunakushukuru kwa kuwa u mwema, kwa maana Fadhiri zako ni za milele. Wimbo huu ulitoa unabii wa jinsi ambavyo fadhiri za Mungu zilivyo kuu mno ambazo baadae zikaja kuonekana kuwa wazi kwa watu wote
showers of Glory wakimsifu Mungu leo katika ibada |
Mtoto wa kwanza alikuwa ni Evelyne ambaye baba yake alishuhudia umati uliohudhuria ibada kuwa Yeye alikuwa hataki kabisa kusikia habari ya kanisa la ufufuo na uzima, hasa ukiangalia linavyoonekana, lina mabati, halina kuta, halina feni, wala halijasakafiwa chini, lakini kutokana na ukweli kuwa alikuwa akihitaji motto alishauriwa na mkewe kuja kanisa hilo hilo ambapo alipokuja aliongozwa sara ya toba na baadae mkewe kupata uja uzito ambao ulikuwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na mama kupitiliza tarehe zake za matazamio ya kujifungua, na mwishowe alivyoenda hospitali aliambiwa kuwa atazaa kwa kupasuliwa. mara baada ya kuambiwa hivyo mumewe alienda kwa mchungaji kiongozi dr Godson na alipowaombea aliwapa uhakika kuwa mkewe hatazaa kwa kupasuliwa bali atazaa kawaida. wakati akiwa ameandaliwa kupelekwa chumba cha upasuaji akatokea mgonjwa wa dharura yeye akaachwa na mpaka akajifungua kwa njia ya kawaida.
mtoto Evelyne akiwa amebebwa na Mch wa watoto Mp Ombeni |
Evelyne akiombewa na mchungaji kiongozi Dr Godson, Mama Mch Happiness na RP Mwandambo |