Baba (SNP) Dr. Godson Issa Zacharia akiomba leo 11-05-2014 (Jumapili), Ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Utangulizi: Somo letu ni “Ushindi kwa Nguvu ya Msalaba”. I KORINTHO 6:18…[Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali
kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.]… Nguvu ni uweza wa kutenda jambo Fulani. Nguvu ya Mungu inahitajika kuifanya kazi ya Mungu. Biblia
inasema hatuwezi lolote kama hatuna nguvu ya Mungu. Yesu Kristo aliwaambia
wanafunzi wake wakae Jerusalemu waisubiri nguvu….. MATENDO 1:4….[Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke
Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;]…..
Katika mstari wa 8 ahadi hii imezungumzwa: “ Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho
Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi
wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Kwa hiyo ukiongelea
Ukristo, unaongelea nguvu ya Mungu.
Endapo Ukristo hauna nguvu, basi huo hautatofautiana
na dini zingenezo zote duniani.
1 KORINTHO 2:4…[Na neno langu na
kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu,
bali kwa dalili za Roho na za nguvu,]…. Nguvu hii ikiwepo
kwako, utatofautishwa na imani nyingine zote.
2 KORINTHO 4:20…. [20 Maana ufalme
wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.]…. Mtu anaweza
kushawishi wengine sana, lakini endapo maneno yake hayana nguvu ya Mungu,basi
hayana maana.
1 THESALONIKE 1:5….[ya kwamba injili
yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho
Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia
zetu kwenu, kwa ajili yenu.]…. Nguvu ya Bwana Yesu inatutofautisha na watu wengine.
Mtu amjuaye Yesu kristo lazima nguvu ya Mungu ikae kwake: Nguvu ya uponyaji, kutoa mapepo, kufufua wafu
n.k. WAEFESO 3:20…[Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno
kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani
yetu; 21 naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote
vya milele na milele. Amina.]…
LUKA
4:18…[Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa
maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu
kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,]…. Huu ni utambulisho wa Yesu
Kristo na kazi aliyoijia. Baada ya kuifanya kazi hii kwa miaka 3 na nusu,
alikamatwa, akateswa na kusulubishwa msalabani…. YOHANA19:28…[Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote
yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.].
MATUKIO YA MSALABA
- Jua lilipoteza NURU
na dunia ilikuwa giza. LUKA 23:44-…..[Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya
nchi yote hata saa kenda, 45 jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu
likapasuka katikati.]…. Jua lilisalimu amri. Utukufu wa jua ni
kuwaka na kuichoma nchi. Jua likinyamaza maana yake kwenye msalaba, vitu
ambavyo kihistoria haviondoki kamwe, vinaweza kutiishwa na kuondoka. Endpo
tutautazama msalaba ina maana, magonjwa yatainama, vilivyopotea vitarudi
kwa Jina la Yesu. Kila kilichopotea kinapatikana pale msalabani. Je, unalo
jambo umelipoteza katika maisha yako? Msalaba ni kama mtambo ambao vitu
vilivyopotea: mfano, Kazi/mke/mume/watoto/elimu n.k vilivyopotea vinarudi upya katika
Jina la Yesu. Msalaba sio mti kama ambavyo wengine wanawaza na hata kuchonga miti yenye mfano wa msalaba na na
kupeleka majumbani kwao.
- Pazia la hekalu likapasuka toka juu hadi chini…. Leo
ndugu yangu unatakiwa ubebe nguvu ya msalaba na kisha utembee nayo, ili utakapofanya mambo yafanikiwe katika Jina la
Yesu. Wakati wa Agano la Kale, Mungu aliwahi kuwaagiza wana wa Israeli kutengeneza Hema la Kukutania, lenye
maeneo matatu:-
·
Nyuani
mwa Bwana
·
Patakatifu
·
Patakatifu
pa Patakatifu
KUTOKA
26:31-33 …. [Nawe
fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi
nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa
makerubi, kazi ya fundi stadi; 32 kisha litungike katika nguzo nne za mti wa
mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika matako
ya fedha manne. 33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete
lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia
litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.]…..Mahali
pale palipowekwa Sanduku la Agano palitengwa kwa pazia, maana hapa ni
Patakatifu pa Patatkatifu. Pazia liliwakilisha kuwatenga wasiostahili
kuingia mahali hapa Patakatifu pa Patakatifu. YESU alivunja vizuizi vyote vya
kumuona Mungu, ili kila mmoja aende kwa
Mungu endapo ataukimbilia Msalaba. Nguvu
ya msalaba inatupa nguvu ya kumuendea Mungu moja kwa moja. Ukiona umeshindwa na
dhambi, siyo wakati tena wa kusema “Mtakatifu Petro uniombee/ au Mtakaatifu X uniombee”…
Msalaba wa Yesu ulipasua kizuizi hicho, na sasa tunamwendea Mungu moja kwa moja
kwa njia ya Msalaba. Kumbuka kuwa Patakatifu pa patakatifu pana Utukufu.
MAOMBI: Pazia lolote lililozuia maisha yako leo nalipasua kwa Jina la Yesu. Ee pazia la kunizuia nisikutane na Baraka zangu,kwa nguvu ya msalaba pasuka…………Kwa Jina la Yesu.
Lipo pazia ambalo ndugu yangu haulioni. Ndiyo maana watu wengine mnaota ndoto za kukutana na wazuiao maishani mwenu. Unaweza kuwa umeomba kwa muda mrefu kumpata mume/mewnza wa maisha yako, lakini zuio linatokea kwa mmoja wa wazazi wako akisema “Huwezi kuolewa na mtu wa kabila hilo”.
- Dunia ikatetemeka, dunia ikatikisika:.. MATHAYO
27:51… [51
Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini;
nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;]… Ukiibeba nguvu ya
msalaba, mtaa/kata/ukoo/nchi/mkoan.k. vinaweza kutikisika. Uwezo wa
msalaba ni zaidi ya matikisiko haya ya kidunia kama vile tsunami, kwani
haya yote hutokea eneo mojatu la dunia lakini upande mwingine
halitoke.lakini msalaba wa Yesu
ulikitisika maeneo yote,ndiyo maan Biblia inasema nchi ikatisika.
MAOMBI: Natikisa magonjwa,
taabu, dhiki, kuharibu mimba, kukosa
kazi…..Tikisika, kwa Jina la Yesu.
- Miamba ikapasuka: Ule mtikiso ulizaa tukio hili la nne la msalaba. Miamba ni
vitu vigumu sana. kuna miamba ya
maisha yako ambayo unaona ngumu
sana kuondoka maishani mwako. Yesu ni
mwamba.imeandikwa Yesu ni jiwe la pembeni.
MAOMBI: Miamba ya maisha
yako, tunaipelekea nguvu ya msalaba ukaisagesage na kupasuka pasuka yote kwa
Jinala Yesu.
- Makaburi yakafunuka: Msalaba unayo nguvu ya kupasua na
kufunua. Kibinadamu, kaburi
likeshafunikwa inakuwa ni mwisho wa maisha ya binadamu, na hakuna awezaye
kufanya lolote (siyo mbunge, rais au ndugu yeyote yule awezaye). Makaburi yana
tabia ya kuficha ilivyovishikilia.
MAOMBI: Leo naileta
nguvu ya msalaba kwenye kata/wilaya/ukoo/ popote ambapo wachawi wameniweka kwenye makaburi yao, name nayapasua yote kwa
Jina la Yesu.
- Miili mingi ya waliolala ikainuka….. Hapa inamaanisha
ni wale watu wailiokuwa wamekufa siku nyingi. MATHAYO 27:52…. [52 makaburi
yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;]…. Kwenye
msalaba ipo nguvu ya kufufua vitu vilivyokufa. Nguvu ya msalaba inao uwezo
huo wa kuleta hai tena kwa Jina la Yesu. Miradi iliyokufa inafufuliwa, ndoa iliyokufa na kuzikwa inafufuliwa n.k kwa Jina la Yesu.
MAOMBI: Naagiza nguvu
ya msalaba kwa damu ya mwanakondoo, kazi
iliyokufa ifufuke, mitaji iliyokufa
ifufuke, ndoa zilizokufa zifufuke kwa
Jina la Yesu. Aliyekuzika ukiwa hai, majeneza yapasuke na kukuachia kwa Jina la Yesu.
- Akida wa kikosi cha kumsulubisha Yesu akasema mwenyewe “Hakika
huyu ni Mwana wa Mungu”…. MATHAYO 27:54…[ Basi yule akida, na hao waliokuwa
pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo
yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa
Mungu.]…. Kwenye msalaba pana nguvu ya kujua /kugundua vitu
ambavyo ulikuwa hujui )it is the centre for discovery). Yamkini yapo mambo
ambayo familia, ofisi, au mamlaka Fulani yameshindwa kujua uwezo ulio ulioko ndani yako wewe. Hii ni kwa
sababbu umefichwa. Iponguvu katika malaba wa Yesu ukiuendea, na baada ya hapo watu wataanza kuuona uwezo huo.
MAOMBI: Bwana Yesu kwa
nguvu ya msalaba, vile vitu vyote ndani yangu ambavyo wengine hawajavigundua, kwa nguvu ya msalaba wako
wavigundue mapema kwa Jina la Yesu. Isiwepo kuchelewa kama Akida kwa Jina la
Yesu.
Akida alichelewa
sana kugundua nguvu ya msalaba (late discovery). Unaweza kuwa Mkristo kabisa na matumaini
yako yakiendelea. Pindi utakapofikia
miaka 80 pengine ndiyo watu wengine wataanza kushtukia uwezo wako.
MAOMBI: Nakataa
kutoonekana, kutotambulika kwa Jina la Yesu. Naagiza kuanzia sasa, watu wote ambao wanapaswa kuniona,wagundue leo
mapema kwa Jina la Yesu. Uwezo wangu uonekane kwa nguvu ya msalaba. Nakataa kufunikwa na kutoonekana kwa Jina la
Yesu. Nami binafsi weze kugundua mapema vitu vile vinavyonihusu kuvifanya kwa
Jina la Yesu.
Ipo nguvu
katika msalaba ya kugeuza mioyo ya watu. Wale waliokuwazia vibaya, wanapaswa
kugeuza mioyo yao kwa nguvu ya msalaba. Waliokupinga siku zote,watafika wakati
wa kubadili mawazo yao juu yako kwa nguvu ya msalaba kama yule Akida. Waliokuwa
wamekukataa kabisa wataanza kukupigia debe. Mkristo mwenye msalaba anayo nguvu
hii ya msalaba.
MAOMBI: Nageuza mioyo ya waliokukataa ikugeukie kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==