JUMAPILI:
18 MAY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo letu ni “Mashujaa wa Daudi”. Duniani kumejaa
matatizo mengi sana yanayohitaji
mashujaa. Kawaida ya shujaa ni
mtu asiyeogopa kitu chochote. Mashujaa huweza kukatiza katikati ya matatizo na kuleta ushindi. 1 SAMWELI 22:1-2…
[Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na
ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo,
wakamwendea huko. 2 Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu
aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika
kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu
mia nne.]… Daudi baada ya kumuua Goliath, alikimbizwa na mfalme Sauli
hata akaenda kujificha pangoni. Wapo watu
waliomfuata kwenda kukaa naye wakiamini kuwa Daudi anao uwezo wa kuwahamisha kutoka hatua moja hadi
nyingine na kuwaletea ushindi. Wafuasi wake hawa ni watu wenye dhiki, madeni kukataliwa, uchungu
mioyoni mwao, wapata watu 400, naye
Daudi akawa Jemedari wao. Hili ni jambo
la ajabu sana.
Swali
hapa ni je, Kwa nini waatu hawa wamfuate Daudi? Jibu ni kwamba, Watu hawa waligundua kuwa, pamoja na
udogo wa Daudi, lakini ndani yake kipo kibali cha kuwaondolea watu dhiki zao,
madeni yao, tabu zao, uchungu wao n.k. Hapo ndipo watu walipoifahamu neema
iliyoko ndani ya Daudi, hata wakaziacha
nyumba zao nzuri mijini na wakaenda kukaa na Daudi maporini. Kwa hiyo Daudi
akaanza kuwaondolea watu dhiki zao, madeni
yao, uchungu wao, n.k. na hata wakawa mashujaa. Mashujaa wa Daudi
waliweza kukaa na kusimama na Daudi hata nyakati za magumu.ni kwa sababu
alianza nao wakati wana madeni, dhiki, tabu, umaskini, uchungu n.k. kitendo
hiki cha Daudi kukaa nao wakati wa matatizo yao, kiliwafanya hawa watu wazidi
kuambatana na Daudi. Mungu naye alifungua milango ya kuwaondolea wale watu
dhiki zao, matatizo yao, uchungu,
umaskini n.k.
Baba (SNP) Dr. Godson Issa Zacharia, akiomba leo tarehe 18-05-2014 ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Morogoro |
Ndugu yangu,
wewe bila kujua umeingia ndani ya Nyumba
ya Ufufuo na Umaskini ukiwa na dhiki zako, umaskini, shida n.k. na Roho wa
Bwana aliye juu yangu ni sawasawa na ule
uliokuwa juu ya Daudi ili baadae uwe Shujaa wa Daudi. Kwenye pango pana majibu
ya dhiki zako, umaskini wako, uchungu, tabu n.k. zinazokukabili.
Ipo siri
iliyomfanya Daudi akae muda mrefu sana madarakani. Siri kuu hapa ni kiutendo
cha Daudi kukaa na watu pangoni wenye uchungu, taabu, misiba, dhiki na walikataliwa sana na
kuwachukua. Akaanza kufanya nao kazi.
SIFA ZA MASHUJAA WA DAUDI ---- (C.V ZA MASHUJAA WA DAUDI):
1.
YASHOBEAMU, ELEAZARI NA SHAMA: ….. 2 SAMWELI 23:8-14…[Haya
ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, mkuu wa
maakida; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja. 9 Na
baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale
mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa
wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 10
huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake
ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu
wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. 11 Na baada yake kulikuwa na Shama,
mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi,
palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; 12 ila
huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye
Bwana akafanya wokovu mkuu.13 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini
waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la
Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la
Warefai.14 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti
wakati ule walikuwako Bethlehemu.]…
- ABISHAI
….. 2 SAMWELI 23:18…. [Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu
wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua,
akawa na jina kati ya wale watatu.]…
- BENAYA…..
2SAMWELI 23:20-22… [Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli
aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, k
pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji; 21 huyo
naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi;
lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake,
akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 22 Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana
wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu.]…
Kawaida
ya mashujaa wa Daudi, siyo watu matajiri. Daudi huanza na wale wenye taabu
ili baadae wakikumbuka walikotoka, basi kuambatana kunakuwa kukubwa zaidi.
MAOMBI: Bwana Yesu, Nimekanyaga katika pango mahali
hapa, ambako hapana uzuri wowote, lakini Bwana Yesu umenipatia Daudi wa Kizazi
hiki ili kuniondolea dhiki, taabu, kukataliwa,
madeni na umaskini ulionisonga kwa Jina la Yesu.
Leo ikiwa
ndiyo siku ya kumalizia mfungo wa siku 21, tumuendee Bwana ili atuondolee zile
dhiki na matatizo ya maisha yetu katika Jina la Yesu.
MAOMBI: Bwana Yesu, leo hii nimnyang'anye adui silaha zake, nimchinje
kwa silaha yake mwenyewe.
Shujaa
hupigana kwanza ili kupigania kile kitu
anachokitaka. Mtu yeyote anayetaka kitu bila kukifanyia kazi ni mwizi.
Leo ikiwa
ni siku ya 21 ya maombi yetu ya kufunga
na kuomba, tungependa kukuona wewe mtu uliyekuwa nasi kwa kipindi hiki cha Mfungo, Bwana
akakufanye shujaa kama wale mashujaa wa Daudi katika Jina la Yesu. Yesu anaenda
kukutengeneza na kukuondolea zile dhiki zako, uchungu wako, umaskini, tabu,
misiba yako n.k. kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==