Sunday, June 1, 2014

SOMO: VIKAO VYA MAPATANO YA KUZIMU - Na: Pastor Godson Issa Zacharia (Snp)

JUMAPILI: 01 JUNE 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

SOMO: VIKAO VYA MAPATANO YA KUZIMU

Utangulizi: Somo letu  linaitwa “Vikao vya Mapatano ya Kuzimu”. Ukisoma kitabu cha Ufunuo 20 utafahamu maana ya kuzimu  ni kitu gani. Kuzimu iko chini hapa duniani, haiko mbinguni. 

UFUNUO 20:1-3 [Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.]… Kuzimu ni makao makuu ya shetani hapa duniani,  wala siyo mbinguni. Ndiyo maana mtu aliktolewa msukuleni huweza kuelezea mahali amabapo  alikuwemo, ikiwemo mashimoni.

UFUNUO 12:7…. [Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;]… Malaika alio  nao joka ni  mashetani tu. Shetani  na wasaidizi wake hawa wanayo kazi maalumu ya kuleta uharibifu. 

YOHANA 10:10 …[Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.]...

Shetani anapopanda kutoka mashimoni, hufanya kazi zake 3 ambazo Bibilia inazizungumzia katika Yohana 10:10. 

Kazi ya kwanza ya Shetani ni kuiba. Huiba  kazi ya mtu, afya,  furaha, ndoa,  n.k. Je, endapo shetani ni roho, iweje aweze kuniibia?  Ni kweli kuwa shetani ni roho,  lakini kwa habari ya wizi huwatumia mawakala wake hapa duniani. Mfano, unakuta faili la mtu halionekani popote ofisini kwa sababu mawakala  wa uharibifu walitumika kulipoteza  ili mtu huyo asipandishwe cheo kazini.

Kazi ya  2 ya shetani ni  kuchinja. Huwezi kula nyama ya ngo’mbe bila kumchinja. Ndiyo maana shetani huchinja kazi, furaha, afya, ndoa  n.k.  watu  wanapotaka kumchinja mnyama,  hawampi taarifa. Humvizia  na kumuotea.  Ndivyo shetani anavyofanya kazi hata leo maishani mwa watu.

Kazi ya 3 ya shetani  ni kuharibu. Shetani hufanya uharibifu katika ndoa, maisha, afya, kibali n.k. hata hivyo, Bwana Yesu  anao uwezo wa kuleta uhai hata kama shetani alishafanya uharibifu. Lazaro aliwahi kukumbwa na mambo haya. Shetani alimletea mauti Lazaro. Hata hivyo, Baada ya siku 4 Yesu alisogea kaburini mwa Lazaro ambaye alishaoza,  na akamfufua.

Kuzimu huachilia taabu, dhiki, uharibifu, uzinzi, mitindo ya uvaaji na unyoaji nywele n.k. Yapo mapepo maalumu  ya kusimamia tabia hizi. Ndiyo maana makondakta wa mabasi waliopo Morogoro, DSM, Kigoma n.k. pamoja na kwamba hawakai vikao vya kujadiliana juu ya kazi zao, lakini  ukichunguza utaona kuwa tabia zao zinafanana:- Mfano, Kuvaa nguo chafu,  kauli  mbovu kwa abiria, kuvaa suruali chini  ya kiuno n.k.

Vikao  vya Kuzimu hufanyika kuzimu. Mungu naye alishapanga kikao juu  ya kila mwanadamu na kumpangia mambo mazuri, mfano: Utakuwa hivi na hivi,watoto wako watazaliwa wengine wakurugenzi mahali Fulani n.k. Hii  ni kwa sababu imeandikwa Mungu hapendi  kumhuzunisha mwanadamu. Mtawala wa kuzimu  naye hupanga vikao vya uharibifu na wanadamu.

ISAYA 28:14-…. [Basi, lisikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu. 15 Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;]… Kwa nini Agano lifanyike na mauti? Ni kwa sababu mauti ni  roho  tu, lakini kuzimu ni ofisi ndiyo maana Mapatano yakafanyika. Unapofanya mapatano, yapo makubaliano  ambayo mnaandikiana. Hayapo  mapatano ya  upande mmoja tu, sharti  yawepo  makubaliano ya pande mbili au zaidi.  Wachawi, waganga wa kienyeji ndio wanaofanya mapatano kuzimu ya aina hii.

MAOMBI: Kwa jina la Yesu, Leo nakataa mapatano yoyote yaliyofanyika juu yangu kwa jina la Yesu.

Mashetani wanapotaka kupatana wanakuwa na vikao. Ijulikane kuwa katika mapatano yoyote yale,  lazima watu wakae chini na kujadiliana nani afanye nini,  au yupi afaidi nini‼ Ndani ya kikao hutolewa maamuzi. Isaya aliona jinsi ambavyo watu wamefanya mapatano  na kuzimu. Baada ya vikao vya aina hii, huandaliwa HATI YA MASHTAKA. Ndani ya hati hii  yaweza kuandikwa, “tumekubaliana kuwa kuanzia leo mtu XX asikamate kabisa hela mkononi mwake……” Mashetani ya kusimamia hati hii hutumwa kutekeleza kazi yao.

MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, nakataa matokeo ya vikao vyovyote vya mapatano na kuzimu, vilivyofanyika kwa ajili yangu. Kuaniza leo vikao vya mashetani, na wachawi na wasoma nyota, nakataa kwa Jina la Yesu. Kila mapatano ya wachawi na kuzimu ili kwamba nisisome,  nisizae, nisipate kazi, nakataa. mapepo wote waliotumwa kusimamia mapatano na kuzimu nawafyeka, kwa Jina la Yesu.

LUKA 22:1-6….[Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka. 2 Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu. 3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5 Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. 6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.]…. Kabla ya Yesu kuuawa, miongoni mwa wanafunzi wa Yesu ni  Yuda Iskariote. Watu wakubwa wa dini  walikuwepo. wakaona cha kufanya ni kumtumia Yuda Isakariote kama silaha yao ya kutokea ndani. Mapepo  yakatumwa kwa Yuda Isakariote na yalipomuingia wakaweza kupatana nao, hata wakafurahi sana. mmoja hapa anapata pesa,  na mwingine anamtoa mtu (Yesu). Hiki ni  kikao kilichokaa ili  kwamba Yesu afe.

Mambo matatu muhimu  kutokana na kikao hiki cha Uharibifu kumhusu Yesu ni:-
  1. Mabadilishano yapo, mmoja anapaata fedha, mwingine anakufa. Wapo watu wanaokaa vikao na hutoa fedha ili wewe uuawe, au ndoa yako  ife, au biashara/kazi n.k ife.
  2. Makuhani ambao ni viongozi wa dini wakafanya maamuzi ya kikao.walishabaini  kuwa huduma ya Yesu iinatishia imani zao. Katika maisha yako, wapo wanokuona wewe kama tishio  lao ili kuwa uondoke ili wao wawe na furaha. Pengine katika ndoa yako umekuwa tishio.  Jinsi  unavyopanda cheo osisini mwako umekuwa tishio.
  3. Sababu ya wivu. Makuhani waliona wivu kuwa,  mbona huyu Yesu ni mdogo sana lakini anakubalika, na anakuwa na wafuasi wengi  sana? mbona anaongezeka sana? ndivyo inavyokuwa hatsa leo katikamaisha yako. Maadui zakosasa hukaa vikao vya kukujadili hufanyika ili weweufunikwe. Shetani huitwa ni kerubi  afunnikaye. Utaanza kushangaa mbona siku  hizi bosi hanitumi tena safari za nje? Utajjibiwa ni  utaratibu wa ofisi. Wakati wewe umelala usingizi, maadaui zako wamakuwa kwenye vikao vya uharibifu.

YOHANA 11:38-44.. [38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.]… Unaweza kusema umeokoka, lakini kumbe kuna sanda za kiroho bado zinakung’ang’ania miguuni  mwako, mikononi mwako na kwenye uso wako.

1.     Sanda za miguuni siyo rahisi kuziona, lakini kwa sababu ya kufungwa sanda miguuni huwezi kutembeza biashara yako kama zamani katika baadhi ya maeneo ili usipate maendeleo. Miguu nidyo hupiga hatua. Endapo hatua zako  zimefungwa, utajikuta biashara unayoifanya inabakia pale pale miaka nenda miaka rudi. Je, ndoa yako  inaenda mbele? Biashara yakoje?

2.      Ukiwa umefungwa sanda mikono huwezi kufanya lolote. Mungu alitupa mikono miwili kwa makusudi mazuri tu.  Kazi inapotangazwa huwezi hata kuandika barua ya maombi ya kazi endapo  mikono imefungwa sanda. Vyombo vya ndani  unakuwa mtu wa kuvidondosha na kuvivunja tu. Ukifanya mitihani kwa mikono hiyo wewe unakuwa mtu wa kufeli tu.

MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Sanda yoyote niliyofungawa kwa sababu ya mapatano ya kuzimu, leo ninaikata kwa jina la Yesu.

3.      Leso pia iliwekwa kwenye uso wa Lazaro. Leso ni kifuniko. Kupitia leso hii, anayetaka kukusaidia hawezi  kukuona.  Wachawi hupatana kwenye vikao vya kuzimu ili kwamba wakuwekee sanda ya usoni ili mtu  huyo asionekane. Kuna mwingine unakuwa umeolewa lakini ukifika nyumbani mumeo anakuona kituko. Sanda hizi  hazionekani kwenye macho ya mwilimni bali kwa kuwa mtu ni  roho, sanda za aina hii huonekana katika roho.

MAOMBI:  Kwa jina la Yesu, sanda waliyokuwekea ili usionekane,  naikatakata katika Jina la Yesu. Ewee sanda unayetesa maisha ya mtu huyu nakukaanga leo kwa Jina la Yesu. Nauwasha moto kukiunguza kitambaa hicho kwa Jina  la Yesu.

==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
Share:
Powered by Blogger.

Pages