JUMAPILI:
27 JULY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Walionichimbia Shimo Wametumbukia
Wenyewe”.
ZABURI 35:7… [Maana bila
sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.]…
Maana yake ni kuwa waliochimba hayo mashimo ni watu na siyo vinginevyo. Mashimo
tunayoongelea hapa, siyo yanayochimbwa
karibu na mlango wa nyumba yako kiasi
kwamba uweze kuona. Ni mashimo yanaochimbwa na watu kwa ajili ya watu wengine katika ulimwengun wa roho.
ZABURI
119:85…. [Wenye kiburi
wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria yako.]…. Kumbe
kuna uwezekano wa mtu kuchimbiwa shimo wakati mtu huyo yu hai. Anayekuchimbia shimo
huwezi kuliona kwa macho lakini yapo. Mashimo haya kwa lugha nyingine huitwa KUZIMU (bottomless pit). Mashimo haya yapo hapa hapa duniani. Yanaandaliwa kwa
utofauti tofauti. Mkuu wa mashimo haya
ni shetani. Mashimo haya yana majina
tofauti, mfano: Shimo la kukosa kazi, shimo la
kuchukua akili za watu, shimo la
kukataliwa, shimo la kuharibu mimba,
n.k. Kibinadamu, katika mashimo ya dhahabu, huwezi kupata aina nyingine ya
madini zaidi ya hayo madini. Mashimo haya ya rohoni ni mabaya sana.
Shetani hukumu yake ipo tayari.
Yeye kwa kuwa yupo shimoni,
anatamani kupata watu wa kukaa naye
huko kuzimu.
ISAYA
5:14…[Kwa hiyo kuzimu
kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na
wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia
humo.]… Unaona kuwa
kuzimu ina kinywa kinachofunika na
hakina kipimo. Watu waovu ni wale wanaopatikana katika kitabu cha Yeremia
sura ya 5. Hawa ni wale wanaochimba mashimo
ya kutopendwa na mtu yeyote, shimo la kukosa kazi, shimo la umaskini.
YEREMIA
5:26… [Maana katika
watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega
mtego, na kunasa watu. 27 Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao
zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. 28 Wamewanda sana,
wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili
wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. 29 Je! Nisiwapatilize kwa
mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa
la namna hii?]… Wanaochimba mashimo wanafanya hivyo kama hifadhi
ya eneo la kuzitunza roho za watu waliopaswa kuishi. Wanaziua roho za watu
ambao hawakupaswakufa. Kuzimu siyo
Jehanamu.
Kuna mauti za aina mbili:-
Mauti
ya kwanza – pale ambapo mwili unakosa uhai
kwa kuondokewa na roho yake.shetani anao uwezo wa kuua mwili tu. Ndiyo maana
Biblia inasemausiogope wanaoua mwili, bali uogope wale wanaoua roho na mwili.
MIKA
3:2-3…[Ninyi
mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na
nyama mifupani mwao. 3 Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi
zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa
chunguni, na kama nyama sufuriani.]…
HESABU
16:30-33…[Lakini Bwana
akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na
wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu
hawa wamemdharau Bwana 31 Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya
yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; 32 nchi ikafunua kinywa chake, na
kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao
vyote. 33 Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo
nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.]…Mashimo haya ni ya rohoni.kwa hiyo mchana wa leo tunaenda kuwarushia mawe ya
rohoni, ili udhihirisho utokezee katika
miili yao katika Jina la Yesu. Shimo la hasara likimweka mtu, hata kama huyo
mtu atapewa kitu gani atabaki na hasara
tu maishani mwake kote.
MAOMBI: Ewe Mchawi mwanamke, mchawi mwanaume, nakufuata
huko ulikoniweka kwaa Jina la Yesu. Yeyote aliyebeba nafsi na kuifungia kwenye
shiimo, mashimo ya familia, mashimo ya baharini, mashimo ya
mashuleni, mahali popote mlipo, najiungamanisha na Yesu, nakataa kubaki
mashimoni, Achia, Kwa Jina la Yesu. Roho yangu, nafsi yangu, mwili
wangu unapotumika, leo nakuamuru Achia kwa Jina la Yesu.
Hawa wanaochukua watu mashimoni ni waatu, na hufanya hivyo kwa sababu ya wivu tu. Biblia
inasema, ‘Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu’….YOHANA
6:63. Mungu alipokuumba alikuwekea vitu muhimu sana vya thamini na ambavyo
ndivyo wachawi huviwinda.
Anayetaka kukuchukua wewe ana kazi na wewe. Mashimo yana tamaa, yamechukua watoto, na Bwana Yesu anataka kukutoa huko leo. Kama yupo mtu ambaye hujaokoka, ni nafasi yako leo kumpa Yesu maisha yako ili utolewe kwenye hayo mashimo walikokufungia.
MAOMBI:
Imeandikwa, ‘‘Achimbaye shimo, atatumbukia mwenyewe’’. Leo ninasababisha
aliyeandaa madhara juu ya kichwa changu yampate mwenyewe kwa Jina la Yesu. Kwa
damu ya Yesu, ninaagiza kama Bwana
aishivyo, yeyote aliyenitegea hila, malaika wa Bwana nawaamuru mumkamate aingie
mwenyewe. Mimi mwenyewe natoroka, kwenye mashimo ya kuharibu mimba, mashimo ya umaskini,
mashimo ya uharibifu, natoroka kwa Jina la Yesu. Wajumbe wa kuzimu leo warudi
huko wenyewe, kwa Jina la Yesu. Amen.
==Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==