JUMAPILI:
03 AUGUST 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Mdudu aitwae Panzi |
Imeandikwa katika HESABU 13:33….. [Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo
Baba SNP Dr. Godson Issa Zacharia akihubiri somo la "Kuivunja Roho ya Mapanzi, katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro, leo 03 /08 / 2014. |
Mwanadamu anazo sehemu kuu tatu: mwili ambao
ulitolewa udongoni, roho ambayo asili yake ni mbinguni ilikotoka, na nafsi
ambayo ni muunganiko wa mwili na roho. Nafsi ni bora kuliko mwili, na roho ni
bora kuliko vyote (mwili na nafsi). Asili ya nafsi ni hapa hapa duniani.
MWANZO
2:7…[Bwana Mungu
akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa
nafsi hai.]… Neno
nafsi linaanza kuonekana kwa mara ya kwanza hapa. Miili yetu imetokea kwenye
udongo. Tofauti yake na udongo wa kawaida ni kuwa, udongo uliopo kwenye mwili uliwahi kuguswa na mikono ya Mungu.
LUKA
9:24… [Kwa
kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi
yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.]… Tamaa na kiburi ni matunda ya
nafsi, kwa sababu ilitoka hapa hapa duniani.
1
JOHN 2:15… [Msiipende dunia,
wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo
ndani yake.].. Nafsi ya mtu ikiharibika na huyo mtu anaharibikiwa kwa sababu nafsi ni muunganiko. Utu wa mtu (personality)
inatokana na nafsi. Nafsi ndiyo utambulisho wa mtu, na kiini cha utu wa mtu.
Huwezi kuvuna roho. Kwa Wazungu hawasemi wanavuna
roho, bali nafsi “soul winining”.
Ukitaka kuibadilki tabia ya mtu lazima kwanza uanze na nafsi yake. Mtu anapokufa,
nafsi nayo hutoweka. Hayupo mtu ambaye ni
profesa ambaye pindi akifa
ataendelea kuwa professa huko mbinguni,kwa sababu kinachoenda mbinguni siyo
mwili na nafsi bali ni roho. Ijulikane kuwa, ndani ya nafsi ya mtu ndimo elimu, hukaa.
Ndani ya nafsi zipo idara tatu:-
Nafsi ina idara ya kwanza inayoitwa NIA.
Ni idara ya fikra (Deprtment of mind / thoughts). Ndiyo idara
inayoruhusu mtu kufikiria, kufanya
mipango mbali mbali (mfano: Mwaka huu nisome, nilime, nioe /niolewe n.k.). hii
idara haipitishi mambo ovyo ovyo. Endapo
mashetani wataivamia nia yako, hapo
ndipo panapoleta shida‼!. Ndiyo maana imeandikwa katika WARUMI 12:2..[Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. ]...
Idara ya pili ndani ya nafsi huitwa UTASHI (Will).
Hii idara hufanya maamuzi. Ndiyo maana Mungu ametupa uhuru wa kufanya maamuzi
ya mtu kuokoka au la‼
YASHUA
15:24…[Nanyi kama
mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni
miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya
wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu
tutamtumikia Bwana.]…
Idara ya tatu katika nafsi huitwa HISIA (Emotions). Ni idara ambayo nafsi ya mtu
hujidhihirisha. Hapa mtu hhuwa na majonzi au furaha. Unamuona mtu anakuwa na jazba kali sana hata
kwa mambo madogo. Mtu aweza kufanya maamuzi ghafla na baada ya muda hujishangaa
imekuwa je hata nikafanya maamuzi ya aina hii.
HESABU
13:33….. [Kisha, huko
tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi
zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.]… Hapa ni
kwamba kila mmoja wao alijiona kama panzi. Jambo la ajabu ni kuwa pamoja na
kuona uzuri wa ile nchi na mazoa yake, lakini hawa wapelelezi wa Israeli walizileta taarifa mbaya (HESABU 13:1-33).
Biblia haijasema wale wakazi wa ile nchi waliwaona
wapelelezi kama mapanzi, bali wapelelezi hawa kwanza walijiona mapanzi, na wale
wenyeji hawakuwahi kusema kuwa wapelelzi walikuwa kama mapanzi. Jinsi unavyojiona wewe ndivyo
ambavyo wengine nao watakavyokuona.
ROHO
YA MAPANZI INAPATIKANA JE?
Shetani ni roho
na anao mashetani wenzake wa
kuweza kupanda hizi roho. Shetani hupanda roho ya kukufanya ujione huwezi chochote.
Kwa lugha nyingine huitwa kifungo cha nafsi. Shetani huweza kupanda ndani
ya nafsi yako pepo moja la kukufanya UJIONE huwezi chochote au hufai
kwa jambo lolote, na ukawa hujikubali hata kidogo.
Wapo watu huwaendea waganga wa kienyeji ili wawape
dawa ya kuinamisha wengine wajione hawafai kwa kuwaingizia roho ya mapanzi. Ndiyo
maana unaweza kumkaribisha mtu ndani ya nyumba yako lakini badala ya kukaa
kwenye kiti/kochi, mtu huyo hauomba akae chini kwenye mkeka!!!. Kuna mtu hataki
kabisa kupanga nyumba mitaa mizuri, mjini lakini hupendelea kutafuta vyumba maeneo ya
Manzese au Uswahilini kwa sababu ya roho hizi za mapanzi.
MAOMBI: Katika Jina la Yesu, naifuta
roho ya mapanzi ndani yako. Ugeuzwe kuanzia leo kwa Jina la Yesu.
ISAYA
43:4...[Kwa kuwa ulikuwa
wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo
nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.]….
Mungu ametufanya kuwa wa thamani. Wapo watu
ambao hata sura zao huzikataa kwa sababu
tu ya roho za mapanzi. Wapo watu wengine hata biashara hawawezi kuzifanya, na
kutokana na roho za mapanzi huleta kisingizio
tu kwamba aina hii ya biashara huwafaa watu wa kabila fulani.
JE
ROHO YA MAPANZI ITANG’OLEWA JE?
HESABU
14:1-9 …..[
Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi
usiku ule. 2 Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni;
mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri,
au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3 Mbona Bwana anatuleta
mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa
mateka; je! Si afadhali turudi Misri? 4 Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe
akida, tukarudi Misri. 5 Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya
mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli. 6 Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu
mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo
zao; 7 wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile
tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 8 Ikiwa Bwana
anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye
wingi wa maziwa na asali. 9 Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji
wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye
Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.]… Walikuwepo wanaume wawili wasiokuwa na roho ya
mapanzi (Yoshua na Kalebu). Kuna namna ya kuiondoa roho hii
ya mapanzi nayo ni kubadilishwa jina. Wapo watu walishakuita majina: Mfano; wewe ni
mgonjwa, taabu, asiyeweza, maskini, kilema, asiyefaa, .... n.k.
YOSHUA mwana wa Nuni, kabla ya kutumwa na Musa
alikuwa akiitwa HOSHEA (Maana yake; Yahwe ni mwokozi wangu. Imeandikwa YOSHUA
13:16…[Hayo
ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo
Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.]…Musa alimbadilisha
Jina Ili Roho ya Mapanzi isiwe ndani yake.
Jina kubadilishwa hufanywa pale mtu anapohama kwa kuookolewa na kuondolewa
kwenye ufalme wa ibilisi.
HESABU
14:6-9…[Na Yoshua mwana
wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza
nchi, wakararua nguo zao; 7 wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli
wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya
ajabu. 8 Ikiwa Bwana anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu,
nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. 9 Lakini msimwasi Bwana, wala
msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu
yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.]…Ukiivua
roho ya mapanzi, waliokuteka watarudisha vitu vyako vyote kwa Jina la
Yesu. Unatakiwa kubadilishwa Jina na
Kuhama kwa Jina la Yesu. Roho hii ya mapanzi imefanya baadhi ya watu kushindwa
kuthubutu kufanya hata maendeleo yao binafsi.
Leo ni siku ya kuwaponda wote waliokuonea kwa Jina
la Yesu. Kumbuka kuwa, yalikuwepo makabila 12 kuwakilisha upelelezi wa ile nchi
ya ahadi, lakini ni Yoshua na Kalebu tu (makabila mawili) waliyoweza kuikataa
roho ya mapanzi na hivyo kuokoka na wasifie jangwani. Wale wapelelzi wengine wote
walioasi walifia jangwani kutokana na
roho hii ya mapanzi.
MAOMBI: Katika Jina la Yesu, leo ninakataa roho ya mapanzi iliyopandwa ndani yangu. Imeandikwa “kila pando asiloopanda baba wa mbinguni litango’oloewa” , Nami nayang’oa mapando yote ya adui shetani niliyopandiwa kwa Jina la Yesu. Leo ninasimama kinyume na roho ya mapanzi waliiyoniwekea ndani yangu kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo, nionekane vile vile kama ambavyo Bwana alikusudia kwa Jina la Yesu.
MAOMBI: Katika Jina la Yesu, leo ninakataa roho ya mapanzi iliyopandwa ndani yangu. Imeandikwa “kila pando asiloopanda baba wa mbinguni litango’oloewa” , Nami nayang’oa mapando yote ya adui shetani niliyopandiwa kwa Jina la Yesu. Leo ninasimama kinyume na roho ya mapanzi waliiyoniwekea ndani yangu kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo, nionekane vile vile kama ambavyo Bwana alikusudia kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==