Picha 1. Asha akionesha machungu ya kuteswa na Mkoba, Usiku wa Mkesha wa Ijumaa 18/07/2014 |
Kwa nini afanye hivyo? Kipi kilimsibu? Fuatilia Ushuhuda huu wa ajabu, kweli na wa kusisimua.
Asha Mohamed (36) Alipatwa na matatizo ya magonjwa kwa muda mrefu. Alikuwa na kazi ya hotelini, na kila akienda kazini, mambo yake hayaendi kama alivyotarajia. Ilifikia kipindi fulani boss wake akamfukuza kazi. Ndiposa alianza biashara ya kuuza kuku sokoni Buguruni Dar es Salaam. Biashara ilikuwa nzuri sana ila mwishowe kila akihesabu fedha yake anapata pungufu. Nyakati nyingine akajikuta hata mtaji wake unazidi kupungua siku hadi siku na kuku wa biashara akiwa nao, mathalani 300 hivi, wanaokufa ni zaidi ya 30. Kipindi hiki alikuwa na mume Muislamu baada ya kuachana na mumewe Mkristo, ambaye kwa maelezo yake walipendana sana ila ndugu zake Asha walilazimisha wawili hawa waachane ili aolewe na Muislam mwenzake.
Kwani ilikuwa je hata mara hii aolewe na Muislamu? Asha anadokeza kuwa alifunga ndoa mwaka 2010, na hakujua ndoa hii ilianza je!!. Anasema Majini ndiyo yalimuotesha ndotoni usiku juu ya mume huyu mpya wa kiislamu atakayekuja kumuoa. Alirudi kwake nyumbani mara tu baada ya kupigiwa simu na kijana ambaye wala hakutarajia kuolewa naye. Walifanya taratibu zote na wakaoana. Ingawa mume huyu naye ni wa pale kijijini Kipera, lakini Asha anasema alimpa sharti huyu mwanaume, kuwa hajazoea maisha ya kijijini hivyo baada ya ndoa itabidi warudi Dar es Salaam. Hata hivyo, ugomvi haukupungua nyumbani. Tokea akiwa na mwezi mmoja tu wa ujauzito, Asha alianza kuumwa mfululizo na madaktari wasiweze kumpatia tiba. Siku zilipokaribia kujifungua, Asha alipelekwa Zahanati ya Mzumbe, lakini madaktari wakasema apelekwe Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwani wataalamu wa hali kama ile watapatikana. Hata hivyo, alipofikishwa Hospitali Kuu ya Morogoro, madaktari bila hata kumpima, walimuingiza Chumba cha Upasuaji, na wakamtoa mtoto. Bahati mbaya, mtoto yule aliishi muda mfupi tu, na siku ya 3 kichanga hiki kikafariki dunia. Matatizo ya magonjwa kwa Asha yakaendelea kushika kasi.
Ndipo wakahamia TIBA MBADALA!!! Mmoja wa waganga wa kienyeji alikowahi kupelekwa kutibiwa alimwambia Asha kuwa anapaswa akakabidhiwe MKOBA. Mama mzazi naye alimshawishi Asha apokee huo mkoba ili kuumwa kwake kuishe.
Akakubali kupokea mkoba huo Oktoba 2011.
Je kuna gharama yoyote kupata mkoba kama huu? Ndiyo. Asha anasema ni gharama sana kupata mkoba, na alilipia Sh. 150,000 (Laki na Hamsini elfu) kupatiwa mkoba huu. Mganga wa kienyeji aitwae Sefu anayeishi Kipera (hadi sasa) ndiye alimkabidhi mkoba huo. Kazi ilianza rasmi ya kuagua. Akawa anatibia wateja wengine wenye shida mbalimbali, ikiwemo maradhi na kusuluhisha ndoa zao lakini yeye binafsi akabakia kuwa ni mgonjwa na hawezi kujitibia. Ndiyo maana, pamoja na uganga wake, Asha alikuwa akienda kwa waganga wengine maeneo mbali mbali Tanzania kama Tanga, Sumbawanga n.k ili kujipatia tiba bila mafanikio.
Je kuna gharama yoyote kupata mkoba kama huu? Ndiyo. Asha anasema ni gharama sana kupata mkoba, na alilipia Sh. 150,000 (Laki na Hamsini elfu) kupatiwa mkoba huu. Mganga wa kienyeji aitwae Sefu anayeishi Kipera (hadi sasa) ndiye alimkabidhi mkoba huo. Kazi ilianza rasmi ya kuagua. Akawa anatibia wateja wengine wenye shida mbalimbali, ikiwemo maradhi na kusuluhisha ndoa zao lakini yeye binafsi akabakia kuwa ni mgonjwa na hawezi kujitibia. Ndiyo maana, pamoja na uganga wake, Asha alikuwa akienda kwa waganga wengine maeneo mbali mbali Tanzania kama Tanga, Sumbawanga n.k ili kujipatia tiba bila mafanikio.
Jumanne wiki jana (15/07/201) Asha alipelekwa kwa mganga
mwingine, na ambaye ndiye wa mwisho kabla ya kuokoka na kuachana na ushirikina. Mganga huyu alimchinja jogoo na kumpika, kisha ile sahani yenye nyama za hiki chakula ikawekwa juu ya kichwa cha mama huyu. Baadae watoto 7 walitafutwa hapo mtaani wakaitwa ili kula hiki chakula juu ya kichwa cha Asha. Watoto hawa walipewa masharti kuwa, ni marufuku kutafuna mifupa ya huyo jogoo. Mumewe alipewa masalia ya mifupa ile na kwa kuwa Morogoro hakuna bahari, aliagizwa akaitupe kwenye mto mmoja hivi huko Mlali ambao maji yake yametulia na hayaendi haraka. Alifanya hivyo, lakini pamoja na hayo, waliporudi nyumbani matatizo ya Asha yalimrudia upya.
Yapi madhara ya ule mkoba? Kwa mujibu wa Asha, Mkoba ule haukumruhusu aoge, wala kufua, wala kupiga mswaki. Siku nzima alikuwa
ni mama wa kulala kitandani tu. Mumewe ndiye alikuwa akifanya kazi za kufua nguo, kupika chakula n.k. kiasi kwamba ndugu za mwanaume walianza kufikiria kuwa mama huyu amemwekea 'limbwata" mume wake. Hata wateja wake walianza kupungua na akimpata mteja wa sh. 5,000 ilikuwa ni bahati.
Picha 2: Baadhi ya Shehena ya vifaa vya uganga (Mkoba) ambao Asha alikabidhi kanisani kabla ya kuteketezwa kwa moto Ijumaa 18/07/2014 |
Ikawa je hata akautupa mkoba na kipi kilitokea? Ndiposa Asha akamkumbuka Shangazi yake ambaye huko zamani aliwahi kumwambia Asha aokoke lakini nduguze (na hasa mama mzazi na bibi yake) wakamkataza. Asha akaazimia moyoni kipi cha kufanya. Mama huyu mwishowe kwa ujasiri mkubwa alimwambia mume wake, "Pamoja na kuwa mimi ni mwislamu, ninakwenda kanisani. Sina faida na huu mkoba, na hatujawahi kununua chochcote hapa ndani zaidi ya kupeleka pesa zetu kwa waganga wa kienyeji. Ninayeumia ni mimi, kama ni kufa ni mimi. Imetosha". Msimamo huu wa Asha ulipata upinzani mkubwa kutoka kwa mumewe, ambaye haraka alikimbilia kwa mama mzazi wa Asha ili amzuie mwanaae abadili nia lakini akawa amechelewa. Mume huyu bila mafanikio alimshawishi sana Asha eti asiende kanisani, kwa sababu wateja wa mkoba watakosa mtu wa kuwahudumia. Aliendelea kumdanganya Asha kuwa magonjwa yale yanayomsibu yatapatiwa tiba huko huko kwa waganga wa kienyeji tu na wala siyo kanisani!!!!!.
Picha 3: Majeshi ya Bwana Yesu yakishuhudia Mkoba wa Asha ukichomwa na kuteketea Usiku wa Mkesha wa Ijumaa 18/07/2014 |
Kanisani ikawa je? Ilipofika Ijumaa 18/07/2014, Asha aliongoza watenda kazi wa Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro kwenda nyumbani kwake na kukusanya furushi kubwa sana lenye vifaa vya kufanikisha uganga wake liitwalo MKOBA. Mongoni mwa vitu hivyo ndani yake, ni vibuyu, hirizi, sanda, kaniki, kigoda, vibakuli, mnyama mfu (kalungu yeye), kapu, mtwangio, kinu, chupa, kisu n.k (kama zinavyoonekana katika picha namba 2). Vitu vyote hivi vilichomwa moto kwenye Mkesha wa Usiku wa Ijumaa 18/07/2014. Asha aliombewa na kuokoka kwa kumpa Yesu Kristo maisha yake, na kuachana na utumwa wa shetani uliomtesa kwa muda mrefu.
====MWISHO WA USHUHUDA====