JUMAPILI:
20 JULY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP Dr. Godson Issa Zacharia katika Mahubiri tarehe 20/07/2014 Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro |
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Wawindao Roho za Watu”. Wawindao roho za watu wanaitwa wawindaji,
siyo wale wanaowinda nguruwe au wanyama wa pori; la hasha. Wawindaji kazi yao
ni kujificha mahaali na kasha kutegesha mtego wake. Hata wanyama huwinda wanyama
wenzao.
YEREMIA
5: 26-27…[Maana katika
watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega
mtego, na kunasa watu. 27 Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao
zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. 29
Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je!
Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?.].. Katika maandiko haya,
anayetega ni mtu na anayetegwa ni mtu. Hawa
ni wachawi na waganga wa kienyeji,
walioamua kumtumikia shetani. Hawa huiba akili za watu, ndoa, furaha,
nyota za watu n.k. Husababisha vifo vya ghafla, vya kutatanisha.
EZEKIELI
13:18-21…. [useme, Bwana
MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote
vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu;
je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19
Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na
vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi
hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu
wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha
hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa
katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama
ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono
yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa
mimi ndimi Bwana.]… Wawindaji wapo wakiwinda roho za watu ili hao
watu wawindwao wasiishi tena.
MAOMBI…Kwa jina la Yesu, jeshi lolote,
lijapojipinga kupiga nami, moyo wangu hautaogopa. Ninaamuru mahali popote
nilipofungiwa, ninapaagiza pafunguke kwa
Jina la Yesu. Mchawi yeyote, aliyeshona
hirizi ili aniwinde, ninakuamuru achia, kwa Jina la Yesu. Roho yangu popote
ilipo nakuita njooooo kwa Jina la Yesu.
Ewe hirizi uliyetega roho, nipo kinyume
na wewe. Kitambaa cha kichawi uliyenifunika,
achia, kwa Jina la Yesu.
ISAYA
42:22… [Lakini watu hawa
ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.]… Wachawi wanapoiiba roho, huenda na kuitumi
kufanyia kazi ile ile ambayo Mungu
aliikusudia hapo awali. Mathalani Mungu alikusudia mtu awe mwimbaji wa
Nyimbo za Injili, na pale wachawi wanapoiba roho yake, huenda kuitumia kuimba
nyimbo za shetani.
MAOMBI:
Bwana
asema hivi, yupo kinyume na hirizi zenu.
Kwa jina la Yesu.
==Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==