Sunday, July 13, 2014

SOMO: NYOTA YA MTU NA MAISHA ALIYO NAYO - Pastor Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 13 JULY 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Utangulizi: Somo la leo  linaitwa “Nyota Ya Mtu  na Maisha Aliyo Nayo”. Nyota ni kiwakilishi cha mtu /au kipawa/ au hatima/ au lengo la mtu fulani kuwekwa hapa duniani. Kwa wengine ni ule umahiri ambao Mungu aliuweka ndani ya mtu huyo.

Ukisoma MATHAYO 2:1-12....Nyota inayooneshwa hapa siyo sawa na zile za Waandishi wa Habari kama nge,  cobra, mbuzi n.k. Nyota ni aina ya ubunifu/kibali toka kwa Mungu alichompatia mtu akitumie na kisha anufaike. Haya ndiyo yale ambayo Mamajusi waliyaona toka kwa Yesu na hata wakaamua kusafiri umbali  wote huo  ili waje kumuona Yesu.

MATHAYO 2:1-12….[ Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli. 7 Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.8 Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. 9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10 Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. 12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.]… Bethlehemu ipo  Mashariki ya Kati, lakini Mamajusi walitokea Mashariki ya Mbali, nchi kama vile Japan, China,  Korea n.k.


MHUBIRI 9:11 ….[Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.]… Ndiyo maana kwa leo hii si ajabu kumuona mtu aliyemaliza darasa la saba ana mafanikio makubwa kifedha na kimaendeleo kuliko Profesa wa Chuo  Kikuu. Haya yanatokana na nyota aliyopewa na Mungu maishani mwake.


YEREMIA 1:4-7...[Neno la Bwana lilinijia, kusema, 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. 7 Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. 8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. 9 Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako; 10 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.]… Mungu anayaona mambo yasiyokuwepo kana kwamba yamekuwepo. Ndicho wanachokifanya wachawi leo hii. Wakiiona nyota yako hata ukiwa mtoto mdogo, wanaivizia na kuiiba ili huyo  mtoto asije kufikia malengo aliyokusudia Mungu katika maisha yake.

SIFA ZA NYOTA MAISHANI MWA MTU  NI ZIPI?

1.0.                       Nyota humfanya mtu awe mahiri. Wanaweza wakawepo mafundi kadhaa ambao wana cheti cha aina moja, lakini kati yao anaweza kuwepo ambaye kazi yake akiifanya imenyooka na watu wanaisifia, lakini wenzake wanakuwa kazi zao zina migogoro na lawama. Nyota ikiwepo na ubunifu unakuwepo. Ndiyo  maana wengi wa watu huigilizia  wanapoona mtu ameanzisha kioski, nao wanaiga kufanya hivyo hivyo. Wanafunzi mashuleni vivyo hivyo, wanafanya mitihani kwa kuigilizia wenzake majibu ya mitihani. Pikipiki nyingi zinatumika kwa kazi ya kubeba abiria tu, baada ya kukosekana kwa ubunifu wa kutumia pikipiki kwa kazi zingine za kuleta maendeleo. Majumbani vivyo hivyo ubunufu unapokosekana utamkuta mama anapika ugali-tembele  au wali-maharage kuanzia Jumatatu hadi Jumapili, na matokeo yake waume wengine huingia mahotelini ili kubadilisha milo yao.

MAOMBI: Kwa Jina leo, ninarudisha ubunifu wangu kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo, ninaita ubunifu wangu njooooo, kwa Jina la Yesu.


2.0 Nyota huleta ufanisi, kwa habari ya ndoa, kazi, biashara n.k. Ufanisi huletwa sawa sawa na Bwana. Nyota ya mtu huleta mvuto kwa watu. Unaona Yesu alivyozaliwa, mamajusi walitoka mashariki ya mbali kuja na kuleta zawadi. Nyota ikiwepo, hata kama mtu hakujui wanavutika kuja na kukuletea zawadi popote unapokuwa. Mamajusi kibiblia ni wachawi. Hata hivyo kwa utukufu wa Yesu hawakuja kumdhuru bali  kumletea zawadi. Ukiona mtu anakuambia “Nyota yako kali sana” usifanye masihara, ni kwamba laishaona mambo yako  yanaenda kunyooka.

MAOMBI: Nyota yako ionekane katika  Jina la Yesu.

3.0.                       Nyota huleta mwelekeo. Mtu asiye na mwelekeo hawezi kueeka mambo yake sawa kwa ajili ya kesho yake.

4.0.                       Nyota ikionekana huweza kufunikwa. MATHAYO 2:2- …[]… Mfalme Herode aliposikia habari za nyota ya Yesu, alianza kupanga mbinu za kumuangamaiza huyu mtoto. MfalmeHerode sawa na wachawi wa leo hii, hufadhaika wanapoona mwenye mafanikio anatokezea. Mtu aliyefadhaika hawezi kuleta zawadi.


MATHAYO 2:16….[Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.]… Wachawi wanawinda watoto wanaozaliwa, kiasi kwamba wapo tayari kuua watoto wengi kwa wakati mmoja kwa kumuwinda mmoja tu mwenye nyota ya mafanikio katika kipindi  husika. Ni  vizuri  nyumba yako iisionekane katika ulimwengu wa wachawi kwa Jina la Yesu. 

5.0.                       Nyota huweza kuchukuliwa au kufunikwa kabisa. Endapo itachukuliwa, maana yake, mvuto wako/ufanisi wako/umahiri wako/ vyote vimechukuliwa. Kuna watu wanakuwa wanashindana na wewe bila wewe kujua. Yamkini unalima shamba, mahindi yako yanazaa sana tofauti na ya watu wengine, na ndiyo maana hupeleka mashtaka kwa mkuu wao (shetani) kutaka uadhibiwe.  Ndiyo maana utakuta wapo watu wanaotumika kupaatanisha mataifa yanapokuwa kwenye vita. Uteuzi wa watu kama hao huendana na nyota zao jinsi zinavoonesha kwamba wapo na umahiri wa kupatanisha wengine.  

6.0.                       Nyota ikiibiwa, mtu aliyekuwa mfanyabiashara maarufu huisihia kuwa na majibu ya kuelezea historia ya zamani zake, jinsi mambo yualivyokuwa. Lakini hawezi  tena kufurukuta kufanya biashara.  Shetani huitwa ni “Kerubi afunikaye”. Nyota ikeshaibiwa hutokea ugumu wa kufanya jambo  lolote. Ndiyo maana baadhi ya Waimbaji wenye majina makubwa, ingawa nyimbo zao wakati mwingine hazina maana sana lakini utakuta zinapata washabiki wengi kila kona.


UFUNUO 18:9-13…[Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; 10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. 11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.]…


MAOMBI: Kwa jina la Yesu, ewe mchawi, ewe mtu mfanyabiashara,  unayetumia nyota yangu naifuata,  kwa Jina la Yesu.


MAMBO YA KUFANYA ILI NYOTA UYAKO IKIRUDIE

1.0.                       Kumfuata Bwana Yesu kwa kuokoka. Maana ya kuokoka ni  kukaa mahali pa usalama,  kama ambavyo Yesu alikaa mahali pa usalama wakati ule Herode alipoangamiza watoto wadogo wote katika Bethlehemu.

2.0.                       Ukeshaokoka, Yesu anakupa mamlaka ya kupigana. Imeandikwa, "umemeza mali nyingi,  nawe utayatapika yote". Umeenda kwa ugumu lakini leo Bwana anataka akurudishie vile vibali vyako vya upendeleo kwa Jina la Yesu.

MAOMBI: Kwa jina la Yesu, leo nyota yangu popote inapotumika, duka si langu lakini aliyeniibia mafanikio yangu tofauti na mimi. Ninaamuru ilete nyota yangu kwa Jina la Yesu. Nataka nyota yangu, nataka mwelekeo wangu, leo nataka umahiri/kibali/kipawa  changu kwa Jina la Yesu. Amen.

==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713 45 95 45)==
Share:
Powered by Blogger.

Pages