Sunday, August 31, 2014

SOMO: VIFO VYA KICHAWI - Na: Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 31 AUGUST 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwa “Vifo vya kichawi”. Vifo vya kichawi ni vifo vya kutatanisha au ghafla. Ni vifo vinavyosababishwa au kutengenezwa na mawakala wa mauti, na siyo  mapenzi ya Mungu. Ufufuo na Uzima hatukatai kuwa watu  wanakufa, ila tunachokataa ni vifo vya kichawi,  vya ghafla na vya kutengenezwa. Iweje,  wodini watoto 20 wazaliwe lakini  katika hao, 8 wazaliwe mfu? Mbaya zaidi, wapo watu/viongozi wa dini wanaendesha ibada za vifo  vya vichanga kama hivi na kuishia kusema “Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe”.  Hili jambo siyo sahihi kabisa,  kwa sababu Mungu si dhalimu, na hawezi kuruhusu vifo vya aina hii vitokee.


Baba (SNP Dr. Godson) akitambulisha Somo  la Wiki Hii,
"Vifo vya Kichawi"
Katika maisha ya mwanadamu, ndani yake kuna wakala wa aina mbili: Wakala wa Uzima na Wakala wa Mauti. Wote wawili kazi yao ni kusambaza kile walichotumwa wafanye. Kwa mfano, unapomuona wakala wa vocha za Tigo  hapaswi kamwe kuuza vocha za Voda kwa kuwa hakuwekwa kuwa wakala wake.

YOHANA 10:10…[Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.]… Maneno haya yanazungumzia mawakala wawili.  Aliyeyazungumza ni YESU mwenyewe, na imeandikwa katika YOHANA 10:7… [Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.]… Yesu ni wakala wa uzima, na alisema kilichomleta duniani ni kuleta uzima tele. Maana yake ni  kuwa,  endapo  ulikuwa mgonjwa wa tumbo, kichwa na miguu, basi endapo YESU anakuponya unakuwa mzima tele.  Siyo kwamba Yesu atakuponesha tumbo lakini miguu bado inauma‼! La hasha. Utakuwa na uzima tele.


Samson Mollel (Kulia) akitoa ushuhuda wa
mambo makuu ambayo Bwana ametendea
familia yake.  Kushoto ni Baba (SNP Dr.Godson)
Wapo ambao wamepata uzima katika eneo la  biashara lakini ndoa zao bado hazina uzima!. Yesu haleti uzima kidogo  kidogo. Anatoa uzima tele, kwenye biashara, elimu, uchumba, ndoa, n.k. unapoona leo unapata “A” kwenye masomo na kesho unapata "F" ujue hauna uzima tele  kwenye masomo yako. Unapoona leo una uzima na baaada ya wiki moja unakuwa mgonjwa ujue hauna uzima tele kwenye afya yako.




MAOMBI: Kwa jina la Yesu,  imenadkiwa "mimi  nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele", Bwana Yesu nakuomba niwe na uzima tena niwe nao tele. Amen

Majeshi ya Bwana ya Nyumba ya Ufufuo na  Uzima Morogoro
yakifuatilia kwa makini,neno kwa  neno lihusulo "Vifo vya
Kichawi" kutoka kwa Baba (SNP Dr. Godon).
Wakala wa pili ni SHETANI ambaye ni  wa kuleta 'mauti au kifo na uharibifu', naye pia hutaka kuleta hivi vyote tele. ISAYA 42:22..[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.].. . Shetani husambaza mauti zake katika kazi,  ndoa,  biashara, masomo n.k. na huletwa na wakala wa mauti.



KUTOKA 23:25-27…[Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. 25 Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.]….Katika Biblia siku zetu za kushi zimetajwa kuwa siyo chini ya 70. Wakala wa mauti anao uwezo wa
·        kuua watu kabla au wakati wa kuzaliwa.
·        Kuua watu  waliokwsiha kuzali kwenye maisha yao.





Baba (SNP Dr.Godson) akimwombea mmoja wa watu wenye
kusumbuliwa na wakala wa mauti Jumapili 31/08/2014.
Kabla au wakati wa kuzaliwa
Kwa kuongeza ufalme wao,  kuongeza umaarufu wao, au  kudiidmiza familia husika.

KUTOKA 1:8-22….[ 8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.  15 Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. 17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. 18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? 19 Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. 20 Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. 21 Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. 22 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.  ]…. Kama Mfalme huyu (Farao) ambaye ni kiongozi  mkuu kabisa wa nchi ya Misri,  ujue kuwa hata sasa endapo wapo  watu wenye nyota nzuri maishani  mwao watakuwa wanawindwa. Mfalme huyu alisema “watenddeeni kwa akili”, ilitoa majibu yafuatayo:
·        Azaliwapo  mtoto mwanaume auawe.


Wachawi vivyo hivyo, wanapoiona nyota ya mtu kabla ya kuzaliwa kwake, hufanya kama ambavyo Farao alikusudia. Wakunga wale wa kipindi cha Farao walikuwa mawakala wa Uzima, na ndiyo  maana hawakutii amri ya Mfalme (Farao) ya kuua wale watoto kwa sababu walikuwa wakimtii Mungu (17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.). Endapo hawa wazalishaji wasingekuwa wacha Mungu, watoto wengi wa kiume wangeuliwa na watu wangeishia kusema maneno haya “Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.” Hili halikubaliki.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Ninakataa kukutana na mawakala wa mauti mahali popote ninapokwenda, iwe ni kazini, iwe wodini, iwe barabarani, ninakataa kukutana na mawakala hao wa mauti kwa Jina la Yesu. Amen


Kumbe kuna umuhimu wa kuwa hodari. Yamkini kuna mcha Mungu katika mahali ambapo mwanao amezaliwa  hai, na sasa wachawi wamekuwa wakimfuatilia ili wamwangamize baada ya kuzaliwa hai. Ni vyema kulinda vile uvipatavyo kwa Damu ya Yesu.


Unapoanza safari yako kwa kitu chochote ni sawa na safari ya mama mjamzito  kuanzia first trimester hadi third trimester ya ujauzito wake. Iwe unafanya biashara au masomo, ipo safarai sawa na ile  ya mama mjamzito.


MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Ninakataa kifo cha kichawi kilichopangwa juu ya familia yangu, juu ya masomo yangu, juu ya biashara yangu, nakataa kwa Jina la Yesu.  

Hata siku moja usikubali kuona watu wanaokuzungusha kwenye hitaji lako katika ofisi  yake, na wewe ukakaa kimya bila kuomba. Ukiona hayo yanatokea, usibishane,  nenda nyumbani anza kuomba na kusambaratisha hao mawakala wa mauti. Mama wa Musa alichukua jukumu  la kumwepusha Musa na mauti kwa kumficha kwa miezi mitatu,  kabla ya kumtengenenezea safina ndogo na kumweka mwenye mto.


Ukiona uchumba unavurugika siku ile ya utambulisho, ujue ni kifo au mauti ya kabla ya kuzaliwa. Endapo siku ya harusi inakaribia na papo hapo kifo cha ghafla kinatokea kwa mwenza wake,  ujue hicho ni kifo cha kabla au wakati wa kuzaliwa.


Yapo mambo yanatakiwa yaanze katika maisha yako. Wakati mwingine unakuwa umeandaa mazingira Fulani  lakini ghafla mtu anaahirisha mipango ile. Mwingine  anapooza miguu mara tu baada ya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa mahali Fulani.

Leo tunaenda kuivipinga vifo vyote vya aina hii kwa JIna la Yesu.

MAOMBI: Mauti yoyote iliyopangwa kunipata kabla au wakati wa kuzaliwa  ndoa yangu, Mauti yoyote iliyopangwa kunipata kabla au wakati wa kuzaliwa  ndoa yangu uchumba, Mauti yoyote iliyopangwa kunipata kabla au wakati wa kuzaliwa  ndoa yangu nyumbayangu -  Leo  kwa Jina la Yesu nakufyeka,  kwa Jina la Yesu. Mauti yoyote iliyochioorwa lwenye maisha yangu, nakufyeka. Ewe mauti uliyotengenezwa kwenye maisha yangu, ndoa yangu, kwenye uzima wangu nakufyeka. Imeandikwa

Kifo ni  roho. Zipo mauti zinazompata mtu kabla au wakati wa kuzaliwa  kwa mambo yake. Hata hivyo, Kuna mauti nyingine zinazompata  mtu baada ya kuzaliwa, ni mauti inayoua ambavyo tayari vimeshazaliwa.


MATHAYO 2:16-18…[Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. 17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, 18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.]… Hapa ni mfano mmojawapo katika Biblia inavyoonesha mango wa kusababisha mauti baada ya mtu kuwa ameshazaliwa. Kaatika mauti ya aina hii,  unakuwa umeshaanza shamba unalima, umeshaanza nyumba unajenga,  umeshaanza kazi unafanya, umeshaanza elimu unasoma,  umeanza kitu tayari,  kisha wachawi wanapeleleza na kumtauma Herode wa maisha yako ili kuviua. Kuna vitu ulishaanza, lakini  Herode anaingilia  katikati na kuleta mauti. Herode alikuwa anamuwinda Yesu pale, hata akaangamiza waoto wote wa kiume. Aliposhindwa kumpata  Yesu, aliamaua kuua ovyo ovyo (random killing). Utaona jinsi ambavyo Yusufu alikuwa anawindwa,hata mama yake mzazi (Raheli) aliyekuwa amechumbiwa, wakafanya mauzauaza ili yeye pamoja na   kuwa ndiye chaguo la Yakobo, ili asioliwe bali aolewe mwingine (Leah) badala yake.


Majeshi ya Bwana yakiwa makini kufahamu 'Vifo vya Kichawi',
somo ambalo lilihubiriwa na Baba (SNP Dr. Godon) katika
Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro 31/08/2014
MAOMBI: Mauti ya vitu vyangu vilivyowahi  kuwepo, naifuta kwa Jina la Yesu. Ewew mauti,  roho ya ajali,  roho ya magonjwa ili nife, toweka kwa Jina la Yesu. Roho ya mauti, katika masomo yangu,  katika kazi yangu, niachie kwa Jina la Yesu. Roho ya kuachwa, roho ya kukimbiwa,  roho ya watoto kuharibika,  roho yoyote iliyopandwa ndani yangu niachie kwa Jina la Yesu. Amen.






Wapo wanaosababisha mauti baada ya kuzaliwa kwa mtu/ kitu. Mfano, imeandikwa EZEKIELI 13:18-21… [19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.]… Wapo wanaoua miradi isitakiwa kufa.  Wanaua ndoa isiyopaswa kufa, wanaua biashara isiyopaswa kufa. Hawa ndio wanaoua kichawi.  Hawa huleta magonjwa ili hayo magonjwa yaonekane ndiyo ndiyo sababu ya kifo husika, kumbe ni kifo tu cha kutengeneza.


MAOMBI: Ewe kifo kilichotengenezwa na washona hirizi, roho ya kifo iliyopandwa ndani yangu,  naishambulia kwa Jina la Yesu.

==Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713 45 95 45)==



Share:
Powered by Blogger.

Pages