JUMAPILI: 07 SEPTEMBER 2014 - UFUFUO NA
UZIMA MOROGORO
Baba (SNP Dr. Godson) akifundisha somola "Laana ya Wachawi" katika ibada Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro 07/09/2014. |
Utangulizi: Somo
la Jumapili ya leo linaitwa “Laana ya Wachawi”. Laana
ni jambo linaloagizwa lifanyike kwa mtu
kwa kumletea huyo mtu mambo mabaya. Ukiona
laana inamfuata mtu, ujue ni jambo litakaloleta mambo mabaya kama vile, magonjwa, ajali, kufukuzwa kazi n.k. Hakuna mtu anayemlaani mwingine ili huyo alaaniwaye apate gari. Kusudi la laana ni kuona mambo mabaya yakitokea. Laana
inasababisha mtu mambo yake yamuendee vibaya. Wakala wa laana ni ibilisi.
Zipo laana za aina mbalimbali. Zipo laana za wazazi,
laana za wanadamu, laana za wachawi, laana zitokanazo na dhambi, laana ya kutolipa fungu la kumi, laana za ukoo n.k. Laana ya wachawi ni laana inayotolewa na wachawi
wenyewe. Wachawi ni wanadamu ambao wamekubali kutimiza makusudi ya shetani hapa
duniani. Shetani ni takataka kutoka kuzimu.
MAOMBI: Takataka za shimoni zibaki
shimoni. Ninakataa kuingiliwa ndani ya
mwili wangu na takataka kutoka shimoni, Kwa jina la Yesu.
Majeshi ya Bwana Morogoro wakisikiliza kwa makini somo la "Vifo vya Kichawi" katika ibada ya Jumapili 07/09/2014. |
Shetani hushirikiana na wachawi hapa duniani, na kujenga madhabahu za uharibifu. Ili Mungu
aseme na wewe, hutumia binadamu kwenye
madhabahu za Mungu. Vivyo hivyo, hata
shetani hutumia wachawi katika madhabahu
zake za uharibifu. Zipo laana
zinazoandaliwa na wachawi. Hata hivyo imeandikwa, “usimwache mwanamke mchawi
kuishi”.
HESABU 22:1-3 ….[Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. 2 Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. 3 Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli.]..Unapoanza kufanikiwa katika maisha yako, au nyota yako ikaanza kung’aa, wanakuwepo watu ambao wanajisikia vibaya. Na hapo ndipo watu wa aina hii huwatafuta wachawi ili kulaani.
HESABU 22:4-6..[ Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. 5 Basi Balaki akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. 6 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.]…. Kumbe wachawi wanavyo vitu vyao, na sisi tunao uwezo wa kuagiza vitu hivyo vilambwe kwa Jina la Yesu. Mtu unapookoka ni sawa na Israeli walipotoka Misri. Ndiyo maana unapookoka, na mambo yako yakaanza kunyooka, wachawi hutafuta namna ya kukulaani ili mafanikio haya yako yasiwepo.
Balaam alikuwa nabii aliyepakwa mafuta na Bwana, na alikuwa akitamka kitu kinakuwa. Hata hivyo,kutokana na tamaa yake, alianza kufanya kazi ya uganga, na kupata ujira wa uganga kama ilivyoandikwa katika HESABU 22:7…[Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.]
Uwaogope sana watu ambao wanaopenda sana kuombea watu na kudai fedha kama malipo. MATHAYO 10:8….[Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.]….. Endapo ukikumbana na watu au viongozi wa dini wakihimiza utoaji wa fedha ili wakufanyie maombi ya tatizo lako, unapaswa kuwakimbia mara moja kwa sababu siyo wa kweli.
HESABU 22: -20…[ 8 Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama Bwana atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu. 9 Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe? 10 Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, 11 Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza. 12 Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa. 13 Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana Bwana amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi. 14 Wakuu wakaondoka wakaenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi. 15 Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza. 16 Wakamfikilia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lo lote lisikuzuie usinijie; 17 maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lo lote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa. 18 Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza. 19 Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua Bwana atakaloniambia zaidi. 20 Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.]… Hata Danieli mwenyewe, baada ya wale washtaki wake kuona haipo njia ya kumkamata Danieli kupitia utendaji wake wa kazi, waliamua kutunga sheria yenye kupingana na imani yake kwa Mungu wake. Watu wengi wanapoona unafanikiwa zaidi, hudhani kuwa wewe una mganga wako anayekusaidia. Wapo watu wenye vinywa vya kutamka mambo nayo yakawa. Wapo wachawi ambao vinywa vyao ni maalum kutamka laana na laana hizo zikatimia.
MAOMBI: Kwa jina la Yesu leo ninakataa laana yoyote iliyotamkwa kwenye madhabahu za kichawi, ili mimi nipate madhara, nakataa kwa Jina la Yesu. Laana za kichawi, ninazifuta kwa jina la Yesu.
Endapo mchawi wa aina hii akatumiwa kutamka laana za kichawi kwenye madhabahu zao, mashetani hulinda zile damu za kafara walizomwaga. Wajumbe wa utekelezaji huamriwa kwenda na kusababisha ule uharibifu uliotamkwa kwenye zile madhabahu za kichawi.
Wapo watu wanaotamka laana za uharibifu usiku na
mchana. Mashetani yakeshapokea ile
sadaka hutekeleza laana husika mara moja. Biblia inasema “Laana isiyo na sababu haimpigi mtu”.
Hata hivyo, laana ya kichawi haihitaji sababu yoyote kumpata mtu. Shetani
hahitaji ruhusa kufanya uharibifu. Imeandikwa
“Achimbye shimo atadumbukia mwenyewe”. Kuna mtu ametoa milioni moja mahali ili wewe ufukuzwe kazi ingawa hujui hilo. Leo kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo,tutamchakaza huyo mtu
kwa Jina la Yesu.
ISAYA
54:17…[Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi
utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa
watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.]…
Kumbe kuna ndimi zinazoinuka dhidi yako.
MAOMBI: Laana ya Uchawi iliyoleta matatizo
juu yangu, naifuta kwa Jina la Yesu. Maneno
yoyote yaliyotamkwa kwenye madhabahu za wachawi, nayafuta kwa Damu ya Yesu. Shetani
na malaika wote mliotumwa mkae kichwani mwangu, mkae kwenye familia yangu, ili mtekeleze laana za wachawi, mtekelezaji wa laana jini, leo nawafyeka kwa Jina la Yesu. Mtekelezaji
wa laana, mtekelezaji mwanaume au mwanamke,
ng’ooka kwa Jina la Yesu. Amen.
Maneno uliyotamkiwa wewe nayafuta kwa Jina la Yesu. Msalaba wa Yesu Kristo ulifuta laana zote. Laana humfanya mtu mambo yake yasimwendee vizuri. Laana yaweza kuing’oa milango ya mafanikio yako. Kumbuka maneno huumba, na hata Yesu aliumbwa kwa neno la Mungu. Bwana aligeuza kinywa cha Balaam kutamka Baraka kwa Wana wa Israeli badala ya laana.
Hata ndugu zako wanaweza kukodi waganga wa kienyeji ili wewe uharibikiwe. Wanapotamka uharibifu ule, mashetani hunyweshwa hiyo damu ya sadaka na kukimbia mara moja kutekeleza huo uharibifu.madhabahu zingine hujjengwa ndani yako mwenyewe, kwa kuweka “kiti cha enzi” ndani yako ili kufuatilia hatua kwa hatua maisha yako. Mtu wa aina hii, endapo atakuja mwenza/mchumba akitaka amuoe, mara huanza kukataa mwenyewe kuolewa. Au endapo mtu huyo anapata kazi, maadamu kituo kile kimo ndani mwake, huanza kujisikia kutoipenda hiyo kazi, na kutaka kuacha. Wasimamizi hufanya kituo. Na wanapokuwa wanatamka laana, wasimamizi wa laana huteuliwa kusimamia hiyo laana.
MAOMBI: Ewe kiti cha enzi cha Ibilisi, nakupiga kwa Jina la Yesu.leo mwili wangu naugeuza kuwa mwali wa moto kwa Jina la Yesu. Wageni wa baharini, wageni wa shimoni nawfyeaka kwa Jina la Yesu. Amen.
Leo ni siku ya kuyafuta maneno yoe yaliyowahi kutamkwa kwenye madhabahu za uchawi. Maneno ya wachawi ndiyo yaliyokufikisha kwenye taabu uliyo nayo leo hii. Yapo mambo yanayokupata, kutokana na maneno yaliyotamkwa zamani na wazazi au wachawi wa eneo lako. Leo tunavuruga damu za kishetani, kisha tuwarudishie wao kwa Jina la Yesu.
Dhambi ni sehemu mojwapo ambayo huwafanya wachawi waweze kukuona katika madhabahu
zao. Wote waliokimbilia msalaba wa Yesu walipata heri. Ni vyema leo ufanye
maamuzi ya kumfuata Yesu na kuzishinda
nguvu za wachawi kwa Jina la Yesu.
==Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==