JUMAPILI: 22 FEBRUARY
2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Jumapili ya leo 22/02/2015 Somo letu linaitwa “Amenitokea Ana Sura Nyingine”. Yesu ana sura nyingi sana, na hutokea watu kwa sura tofauti. Ndiyo maana Yesu alivyokutokea mwaka jana, siyo kama atakavyokutokea mwaka huu. Au jinsi Yesu alivyokutokoea mwezi jana sivyo ambavyo alivyokutokea mwezi huu.
UFUNUO 1:9-20….[Mimi ni Alfa na Omega,
mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja,
Mwenyezi. 9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika
mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho
Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. 10 Nalikuwa katika
Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa
saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na
Laodikia. 12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona
vinara vya taa saba vya dhahabu; 13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu
mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa
dhahabu matitini. 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu
nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; 15 na miguu yake kama
shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake
kama sauti ya maji mengi. 16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa
kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na
uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake. 17 Nami nilipomwona, nalianguka
miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu,
akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami
nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo
za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo
yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. 20 Siri ya zile nyota saba
ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu.
Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni
makanisa saba.]… Yesu
katika wale wanafunzi 12, alikuwa na wanafunzi watatu aliokuwa anawapenda sana:
Yakobo, Petro na Yohana. Kila mwanafunzi mmoja anazo sifa zake za utambuzi: Yohana akiwa na hekima za
kufundisha wengine kuhusu UPENDO,
ikidhihirishwa na zile nyaraka alizoandika. Yakobo alikuwa ni mwalimu wa TUMAINI, na hata kwa mtu aliyekata tamaa, ilikuwa ni
rahisi kufarijika. Petro alikuwa mzuri sana katika kufundisha mambo ya IMANI.
Yesu aliwahi kusema kuwa mmoja
wa wanafunzi wake hatokufa kabisa, naye ni YOHANA,ambaye walimtesa sana,
wakamtupa katika mafuta ya moto, lakini hata hivyo hakufa. Ndiposa walipomtupa katika kisiwa vha Patmo, ambapo alikaa upweke na wanyama wakali wakiwemo dubu.
Yesu alimtokea Yohana akiwa na sura na umbo tofauti kabisa.
Wanafunzi watatu wa Yesu aliowawapenda zaidi walikuwa na kawaida ya kuegama
katika kifua chake. Hata hivyo, Yohana
alijishangaa mara hii kuona Yule Yule aliyekuwa anaegama kifuani mwake mbona leo inakuwa ngumu hata kumtambua?
'Naomba kupokea upako mara mbili'... Bila shaka ni AP Amos akimsihi RP Adriano hapo Jumapili 22/2/2015 katika Bonde la Maono Morogoro |
'Na mimi sikuachi, hadi unibariki'.... Maneno ya AP Steven Nampunju kwa RP Adriano wakati wa ibada Jumapili 22/2/2015 katika Bonde la Maono Morogoro. |
MARKO 16:12-13…[Baada ya hayo
akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika
njia kwenda shamba. 13 Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala
hao hawakuwasadiki. ]…. Hapa tunajifunza kuwa, wale wanaoenda
shamba, shule, kazini, hospitalini,n.k Bwana huwa anaweza kuwatokea na ktana na hitaji lao kwa kuwa Yesu hana
ubaguzi.
LUKA 24:13 …[ Na tazama, siku ile
ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau,
kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. 14 Nao walikuwa
wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. 15 Ikawa katika
kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. 16
Macho yao yakafumbwa wasimtambue. 17 Akawaambia, Ni maneno gani haya
mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. 18 Akajibu
mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika
Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? 19 Akawauliza, Mambo gani?
Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo
katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; 20 tena jinsi wakuu wa
makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. 21
Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya
hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; 22 tena,
wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi
na mapema, 23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na
malaika waliosema kwamba yu hai. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda
kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye
hawakumwona. 25 Akawaambia, Enyi
msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26 Je!
Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27 Akaanza
kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu
yeye mwenyewe. 28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya
kama anataka kuendelea mbele. 29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa
kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. 30 Ikawa
alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32
Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi
njiani, na kutufunulia maandiko? 33 Wakaondoka saa ile ile, wakarejea
Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa
pamoja nao, 34 wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni. 35
Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao
katika kuumega mkate.]…
Ukeshakuwa unasemezana na wengine habari za Yesu, Yesu
huja na kuambatana nanyi. Yesu huungana nasi tunapozungumzia habari
zake. Tunapolifunua neno la Mungu leo, Yesu naye afunuliwe kwetu. Baada ya Yesu
kuumega mkate, wale watu walifunguliwa macho yao.
LENGO LA SOMO LA LEO
1. Yesu ana uwezo wa kugeuka sura
2. Yesu ana uwezo wa kukutokea akiwa na sura
nyingine (maana yake, alivyokutokeea jana sivyo atakavyokutokea kesho).
Sehemu ya umati wa majeshi ya Bwana waliokuwepo wakati wa ibada Jumapili 22/2/2015 katika Bonde la Maono Morogoro |
YOHANA 1:9…[ 11 Alikuja
kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;]…..Yesu anawazungumzia Wayahudi, ambao hata baada ya kutokea wao hawakumpokea.
Ni kwa sababu, Wayahudi walitarajia masiya atazaliwa kwenye familia ya
kitajiri, lakini badala yake akazaliwa katika hori
la kulia ng’ombe, hali ya umaskini kabisa.
KUTOKA 6:2-3…[Kisha Mungu akasema na
Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na
Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.]…. Ina maana kuwa, ni wepesi zaidi kwa Musa kumfahamu Mungu kuliko
baba zake. Kwamba baba zake Musa hawakuwahi kumjua Mungu kwa jina la Yehova.
Ndiyo maana hata sasa, wapo wengi wasioelewa maana ya Ufufuo na Uzima. Maana
yake, Mungu ni Yule Yule mmoja lakini
huvijia vizazi kwa namna tofauti.
UKIRI
Bwana Yesu, Ninaomba
unipe akili ya kujua waweza kunitokea kwamba waweza kunitokea katika sura
nyingine, ninaomba unipe imani, unipe
ujasiri na nuru yako ya kujjifunza maneno ya uzima, kwa Jina la Yesu. Amen
|
Shetani ambaye ni mungu wa dunia hiii, hupofusha fikra za watu
ili wasiijue kweli. Imeandikwa katika 2KORINTHO
4:4….[Lakini ikiwa injili yetu imesitirika,
imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha
fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye
sura yake Mungu.]…. Maana
yake, nuru ya injili yenye kuondoa giza haiwezi kuwazukia waliopo chini ya
shetani. Ikumbukwe kuwa mwanadamu ana
sehemu tatu: mwili, nafsi na roho. Tunajua je haya?
Imeandikwa katika 1
THESALONIKE 5:23…[ 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa;
nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama,
wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.]….
Imeandikwa katika MWANZO
1:25….[Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya
ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.]….Maana yake mwili na roho huifanya
nafsi. Muunganiko huu wa mwili na roho
ukitengana, nafsi nayo hutoweka.
NAFSI nayo imeundwa na viitu vitatu: NIA, HISIA na UTASHI. Nafsi
ni sawa na masjala ambayo hufanya usajili,ni kama ghala ambalo hutunza vitu. Mtu anapokosa kumbu kumbu zake,
ni kuwa ndani ya nafsi yake taarifa hizi
zimepotea. Nia ni idara ya fikra (2KORINTHO 4:4). Nia ya mtu ndipo
anapofikiri mtu. Mungu hakuwahi kumuumba mwanadamu akiwa na mapungufu.
Ndiyo maana baada tu ya Mungu kumaliza
uumbaji alisema kila kitu alichoumba
kilikuwa chema. Hakuna aliyeumbwa akiwa mbumbumbu. Mungu aliviumba vyote vikiwa
vikamilifu. Ni vyema kukataa kuitwa majina kama vile vile: ‘Mama wa nyumbani’, kwa sababu Mungu
hajwahi kumuumba mwanamke awe wa kukaa nyumbani.
UKIRI
Kwa Jina la Yesu, Baba wangu wa mbinguni,ninaomba fikra zangu
zilizokamatwa na kutiwa giza na mashetani ziachiliwe,
nanyunyiza Damu ya Yesu, kwa
kila anayetumia nia yangu nakuamuru achia nia yangu kwa Damu ya Yesu.
Baba yangu wa mbinguni najua ulimuumba mtu ukamwekea pumzi ya
uhai, mtu akawa nafsi hai, leo naidai
nafsi yangu hai kwa Jina la Yesu. Eneo la mawazo leo naondoa vifungo vya
mashetani kwa Jina la Yesu. Naiondoa laana iliyo katika fikra zangu kwa Jina
la Yesu. Naondoa uzito kwenye nia yangu, na kwenye akili yangu, nafyatua kwa
Jina la Yesu. Achia nia yangu kwa Jina la Yesu. Amen
|
Showers of Glroy wakicheza na kuimba mbele za Bwana wa Mabwana wakati wa ibada Jumapili 22/2/2015 katika Bonde la Maono Morogoro. |
SHETANI HUPOFUSHAJE FIKRA ZA MTU?
MATHAYO 28:11-15…[Nao wale walipokuwa
wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa
makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee,
wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 wakisema, Semeni, ya kwamba
wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno
hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea
wasiwasi. 15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na
neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo. ]… Askari walipewa fedha nyingi ili waseme
uwongo. Hapa ni kuwa Wayahudi walipofushwa fikra zao hadi leo kuhusiana na
ufufuo wa Yesu. Shetani hutumia aina hii ya mfumo kupindisha ukweli. Yapo pia
mafundisho ya kishetani ambayo nyakati kadha kadhaa watu
wakiyasikiliza basi hugeuka na kuwa sababu ya upofu wa fikra zao, kwa sababu imani huja kwa
kusikia.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778