JUMAPILI: 15 FEBRUARY
2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Jumapili ya leo 15/02/2015 Somo letu linaitwa “Mamlaka ya Rohoni”. Mamlaka huweza kumfanya mtu afanikiwe
au asifanikiwe. Zipo mamlaka za rohoni upande wa Mungu na zipo
nyingine za rohoni upande wa shetani. Kuna enzi au
mamlaka zinazowashikilia watu kiasi kwamba wanapotaka kwenda au kupiga
hatua, wanakuwa wamenaswa na kushikiliwa
wasiondoke kiasi kwamba hawawezi kamwe kujikwamua.
RP Adriano akitafakari maandiko katika ibada Jumapili 15/2/2015 Bonde la Maono - Morogoro. |
Imeandikwa WARUMI 13:1-7…[Kila mtu na aitii
mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo
umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la
Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao hawatishi watu
kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka
usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye
ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa;
kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye
kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa
sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena
mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.
7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye
hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.]…
Tena imeandikwa YOHANA 19:8-11…[Basi Pilato aliposikia
neno hilo, akazidi kuogopa. 9. Akaingia tena ndani ya ile Praitorio,
akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10 Basi
Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua,
nami nina mamlaka ya kukusulibisha? 11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka
yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia
mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.]…. Pilato alitaka kujiridhisha kwa
kumuuliza Yesu maswali kadhaa kadhaa ili aweze kutoa hukumu. Yesu aliamua
kumpa majibu rahisi, kwa kumwambia Pilato kuwa mamlaka aliyo nayo Pilato imetoka kwa
Baba yake aliye mbinguni. Kwa hiyo aliye kwenye mamlaka anaweza kumfunga mtu au
kumfungua, na anao uwezo wa kumuachia
mtu huru au kumsulubisha. Kwa mujibu wa Yesu, shetani ndiye aliyemtia mikononi
mwa Pilato, kwa kuwa ndiye aliyemuingia Yuda Iskariote. Kama Yesu alimwambia
Pilato mamlaka aliyo nayo imetoka juu
(mbingunni) ujue kuwa zipo mamlaka ambazo zinatoka chini (kuzimu).
MITHALI 8:15…[Kwa msaada wangu
wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki.]… Ndiyo maana wana wa Israeli
walipomlilia Mungu ili awape mfalme sawa na mataifa mengine, Mungu alimwambia
SAMWELI, hawajakukataa wewe bali wamenikataa
mimi (Mungu).
1 SAMWELI
10:1- …[1 Ndipo
Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu,
akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe
utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa
ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake. 2
Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la
Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao
uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari
za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?]…. Sauli kabla ya kuwa mfalme
alimiminiwa mafuta na nabii wa Bwana (Samweli) ili aweze kuwaongozana kuwatawala
watu wa Mungu. Kumiminiwa mafuta kwa kipindi cha Agano la Kale ni sawa na kujazwa Roho Mtakatifu) katika Agano
Jipya).
Sauli alipewa maelekezo ya kipi kitakachotokea baada ya kumiminiwa
yale mafuta:
1 SAMWELI 10:3-9…[Kisha utakwenda mbele
kutoka hapo, na kufika kwa mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana
nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wanambuzi watatu,
na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai; 4
nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. 5 Baada
ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha
itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka
mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao
watakuwa wakitabiri; 6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri
pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 7 Basi, hapo ishara hizi
zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 8 Nawe
utatelemka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakutelemkia huko, ili
kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja,
hata nitakapokujia, na kukuonyesha yatakayokupasa kuyafanya. 9 Ikawa,
alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu akambadilisha moyo; nazo ishara zile zote
zikatukia siku ile ile.]….
Ipo mamlaka ya rohoni ambayo mtu
hupokea na baada ya hapo angeuzwa nakuwa kitu cha tofauti kuliko hapo awali. Ndiyo
maana hata Petro hakuwa ana ujasiri wa kuongea mbele za watu, lakini baada ya
kujazwa Roho Mtakatifu, aliwaeza kusimama kwa ujasiri na kuwahubiria maelfu ya
watu juu ya Yesu Kristo.
LUKA 20:20….[Wakamviziavizia,
wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno
yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali.]…Biblia inawazungumzia watu waviziao. Yamkini
hata wewe wapo wapelelezi wamekuja kwako wakijifianya watu wa haki (wapendwa,
walokole, wakristo n.k) kwa namna ya kutaka kukunasa, na wewe hujui.
Wakati fulani Herode aliwahi kumchinja Yakobo na jambo kama hilo
likawafurahisha sana Wayahudi, na kipindi hiki kanisa lilikuwa limelala,
hawaombi. Hata hivyo majira yale yale,
Herode alitaka pia kumchinja Petro, hapo ndipo kanisa lilipoingia katika maombi,
na malaika wa Bwana akaja kumfungua Petro, na na vile vikosi vinne vya maaskari
wanne wanne waliokuw wakimlinda hawakuweza kumzuia Petro. Hata wewe, yale ambayo kwako yamekuwa magumu,
kifungo kisicho na mlango kitakavyokuachia, na hatimaye uone kama vile ni maono.
MWANZO 1:3…[Mungu akasema, Iwe
nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru
na giza.]… Kila
anachosema mtu yeyote kinakuwa na unakiona baadae. Hii haijalishi itapita muda gani,kwa kuwa hii ni sheria
katika ulimwengu wa roho. Pengine umesema vingi na kwamba hujaona matokeo yake, lakini ukumbuke kuwa
ipo siku yakuviona vile ulivyowahi
kuvisema.
MWANZO 1:31….[Mungu akaona kila kitu
alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya
sita.]… Hitimisho la
yale ambayo Mungu alivisema, ni pale ambapo Mungu aliona kila kitu
alichokifanya kuwa ni chema. Kabla Mungu hajafanya huwa anasema sema kwanza. Vivyo
hivyo, chochote asemacho mtu kinakuwa
kama alivyosema.
MITHALI 18:20-21...[Tumbo la mtu litajazwa
matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao
ya midomo yake. 21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. ]…. Kumbe uweza wa uzima na mauti vimo
kwenye kinywa chako mwenyewe. Shetani huitumia mbinu hii ya ulimi/kinywa cha mtu ili kumnasa, hasa
pale amabppo ameshindwa kukukamata kwenye mambo mengine.
LUKA 20:1…[Ikawa siku moja,
alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa
makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula;]…. Lengo la hawa watu kuja kwa ghafla kwa Yesu, lilikuwa kujua ni
kitu gani Yesu anafundisha,ili wamnase
kwa maneno ya kinywa chake. Imeandikwa ISAYA
42:22….[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na
kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,wamefichwa katika magereza; wamekuwa
mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]… Kumbe hata maneno anayotamka mtu
yaweza kumfanya akafukuzwa kazi,
kuachika katika ndoa n.k. Wapo watu ambao kutokana na maneno waliyowahi kuyatamka,
walijikuta wamenaswa kwa maneno ya vinywa vyao.
1 WAFALME 22:7-8….[Lakini Yehoshafati
akasema, Je! Hayupo hapa nabii wa Bwana tena, ili tumwulize yeye? 8 Mfalme wa
Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza
Bwana kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla; lakini namchukia; kwa sababu
hanibashirii mema, ila mabaya. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.]….
Unaweza kumchukia mtu ambaye ndiye
mwenye muujiza wako. Mtu yeyote
ambaye akionywa huchukia,ujue huyo mtu hayupo vizuri.
1 WAFALME 22:9-13 ….[Ndipo mfalme wa Israeli
akamwita akida, akamwambia, mlete hima Mikaya mwana wa Imla. 10 Basi mfalme wa
Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wakikaa kila mtu katika kiti
chake cha enzi, wamevaa mavazi yao, katika sakafu langoni pa Samaria; na
manabii wote wakafanya unabii mbele yao. 11 Na Zedekia mwana wa Kenaana
akajifanyia pembe za chuma, akasema, Bwana asema hivi, Kwa hizo utawasukuma
Washami, hata waharibike. 12 Na manabii wote wakasema hivyo kwa unabii,
wakisema, Kwea RamothGileadi, ukafanikiwe; kwa kuwa Bwana atautia mkononi mwa
mfalme. 13 Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema,
Angalia sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja husema mema kwa mfalme; neno
lako na liwe, nakusihi, kama neno la mmojawapo wao, ukaseme mema.]….. Wapo manabii wenye mbwembwe kama Zedekia
mwana wa Kenaana, hata kwa kuvaa pembe za chuma, ili kufuata mkumbo.
1 WAFALME 22:14-16…..[Mikaya akasema, Kama
Bwana aishivyo, neno lile Bwana aniambialo, ndilo nitakalolinena. 15 Na
alipokuja kwa mfalme, mfalme alimwambia, Je! Mikaya, tuende RamothGileadi
kupiga vita, au tunyamaze? Akamwambia, Kwea, ufanikiwe; kwa kuwa Bwana atautia
mkononi mwa mfalme. 16 Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno
ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana?]….Maana yake yapo majira ya kkupigana vita na majira ya
kutopigana vita. Daudi kabla ya kwenda vitani alikuwa anamuuliza Bwana kwanza. Ukitaka
kufanya biashara, muulize Bwana kwanza.
1 WAFALME 22:17-24…[Akasema, Naliwaona
Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. Bwana
akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. 18
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema,
ila mabaya? 19 Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana
ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande
wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 Bwana akasema, Ni nani
atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema
hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi
nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa
pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na
kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa
uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako. 24
Ndipo akakaribia Zedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu,
akasema, Roho ya Bwana alitokaje kwangu ili aseme na wewe?]…. Alichokifanya Zedekia, mwana wa
Kenaana ni sawa na yale yanayofanyika
kwa baadhi ya watumishi wa Mungu kwa kuwasema watumishi wengine kwenye madhabahu zao.
Chikdren Ministry Bonde la Maono Morogoro wakimlazimisha shetani arudi kuzimu makao yake makuu wakati wa Ibada ya Jumapili tarehe 15/2/2015. |
1 WAFALME 22:25-28…[Mikaya akamwambia,
Angalia, utaona siku ile utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche. 26
Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya, mkamrudishe kwa Amoni mkuu wa mji
na kwa Yoashi mwana wa mfalme; 27 mkaseme, Mfalme asema hivi, Mtieni mtu huyu
gerezani, mkamlishe kwa chakula cha shida, na maji ya shida, hata nitakaporudi
kwa amani. 28 Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana hakusema kwa
mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.]…. Ahabu aliitumia mamlaka yake vibaya, kwa kuwaachia
huru wasiostahili na kuwafunga wasiostahili kufungwa. Ndiyo maana hata wewe
hupati unachotaka kupata kutoka kwa Bwana, ni
kwa sababu ipo mamlaka rohoni yenye kuwafanya watu wapate, na wale
wasiostahilikupata wapate. Mikaya anagandamizwa kwa kutenda haki. Hupaswi kuridhika na hali uliyo
nayo.
Hata kama baba na babu yako hawakuwahi kumiliki hata
baiskeli, lakini yale yalitokea kwa
sababu ya vifungo walivyovopitia. Wewe unapaswa
kujitoa humo kifungoni na kumimliki,kutiisha na kutawala sawa sawa na mapenzi
ya Bwana kwa Jina la Yesu. Shetani hana chochote alichowahi kukifanya au
kuumba, bali hata yeye aliumbwa. Mwanadamu ndiye aliyepewa vitu vyote avimiliki
hapa duniani,na shetania akaja kwa ujanjaunjanja akamwibia mwanadamu ile
mamlaka. Je, utaweza je kumnyang’anya shetani vile alivyokuibia? Ni kwa kupigana. Leo tunawafuata mawakala wa
shetani (wachawi na waganga wa kienyeji) huko huko waliko, na kuwapiga mbele ya
familia zao kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Bwana Yesu naomba leo iwe siku
ya ufumbuzi wa shida yangu. Kwa dama yamwanakondoo, ninaamuru kila
mamlaka katika taifa, na ukoo wangu zinzonishikilia ili niwe maskini, nasema
achia ufahamu wangu, achia akili yangu
kwa Jina la Yesu. naharibu mamlaka zote za giza zinazofanya kazi kwenye
maisha yangu, kwa damu ya mwanakondoo.
|
Showers of Glory wakicheza na kumwimbia Bwana wa Mabawana katika Bonde la Maono Morogoro wakati wa ibada ya Jumapili ya tarehe 15/2/2015 |
LUKA 20:20….[Wakamviziavizia,
wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno
yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya liwali.]…. Waviziaji hawaji moja kwa moja kukukabili.
Mikaya hakuwa amekosea kwa maneno yake, na Ahabu mfalme alimtia gerezani nakupewa
chakula cha shida. Ina maana hata wewe, yamkini ipo shida inayokukabili kutokana
na mwenye mamlaka ambaye aliamua kufanya hayo yatokee. Yamkini wapo watu
wanaofuatilia maisha yako,ili wakunase kw amaneno yako. Ndiyo maana Biblia
inasema, maneno yako yawe ndiyo ndiiyo
na siyo siyo. Usiwe mtu wa kusitasita. Shetani na mawakala zake (wachawai na wahanaga wa kienyeji) hawachoki
kumfuatilia mtu. Endapo leo hii wamekukosa,bado wataendelea kukufuatilia hadi
wakunase.
Samsoni ni mfano mwingine wa watu waliokuwa wakiviziwa viziwa sana
katika Biblia. Ndugu zake walipomfunga kwa kamba na kumkabidhi kwa Wafilisti ili kujiokoa,
Samsoni alijitoa kwa kuzikakata kamba na kuwapigakwa taya la punda zaidi ya
watu 2,000 na kuwashinda wote. Ukipigana na kushinda rohoni unatumia pia akili
za mwilini.
WAAMUZI 16:1-5…[Samsoni akaenda Gaza,
akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, ya
kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye
lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko,
ndipo tutamwua. 3 Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati
ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa
pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima
ule unaokabili Hebroni. 4 Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika
bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. 5 Nao wakuu wa Wafilisti
wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate
kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.]….. Hapa ni kuwa, Wafilisti walijua ili
kuweza kumpata Samsoni, njia rahisi ni ya kujua siri na asili ya nguvu zake.
WAAMUZI 16:15-19…[Mwanamke akamwambia,
Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara
hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu
zako nyingi. 16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na
kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 17 Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa
moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu
tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami
nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 18 Delila alipoona ya kuwa
amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti,
akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake.
Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. 19
Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile
vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake
zikamtoka.]….Delila
alifanya kazi ya kumtega Samsoni kwa maneno ya kinywa chake. Kuanzia mara ya
kwanza hadi ya tatu, Delila alimwambia
Samsoni asimdanganye kama kweli
anampenda, kwani kama anampenda asingemficha siri ya nguvu zake. Delila alimlaza
Samsoni magotini, na kumnyoa nywele zote hasa baada yakujua siri ya nguvu za Samsoni. Wapo
watu waliolazwa magotini mwa Delila hata
leo. Wachawi wamekunyoa nywele zako. Ni wakati
wa kujua kanuni ya kuzifanya nywele ziote tena. Leo hii Samsoni anasaga ngano
ya Wafilisti. Adui zako wakeshakunasa kwa maneno ya kinywa chako wanakutoboa
macho na kukufanya usage ngano zao. Kiu yako ya kumtumikia Bwana inakuwa
imetoweka. Hata hivyo, bado lipo tumaini,
kwa sababu nywele za Samsoni zilianza kuota tena. Wale waliokutesa ni wakati wa kujiliipizia kisasi kwa Jina la Yesu.
Maombi maalumu kwa ajili ya kurudisha akili za wanafunzi (toka chekechea hadi vyuo vikuu), yaliyofanyika katika Bonde la Maono Morogoro Jumpili tarehe 15/2/2015. |
LUKA 4:5-6…[Akampandisha juu,
akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia,
Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami
humpa ye yote kama nipendavyo.]… Yesu alikuwa anaongea na shetani kabla hajaenda
msalabani. Yesu aliyeenda msalabani ni
tofauti na wakati ambao alikuwa bado hajaenda msalabani.
UFUNUO 1:17…[Nami nilipomwona,
nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu
yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,]….
Maana yake, ile mamlaka ya kuwafungulia watu waliokuwa magerezani ipo mikononi
mwa Yesu. MATHAYO 28:18…[Yesu
akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.]…. Yesu anayo ‘mamlaka yote’ duniani
hapahapa na mbinguni. Hata kama ipo shida kubwa sana maishani mwako, mpelekee
Yesu kwa sababu mamlaka ya kuiondoa ipo mikononi mwa Yesu baada ya kufufuka.
Maombi maalumu kwa ajili ya watu wenye maono ya kufanya mambo makubwa lakini bado hawajachukua hatua, yaliyofanyika Jumapili 15/2/2015 katika Bonde la Maono Morogoro. |
UKIRI
Bwana Yesu, biashara yangu iliyofungwa leo ifunguliwekatika Jina
la Yesu. nipe ufahamu Bwana wa jinsi ya kuendesha biashara yangu kuanzia leokwa Jina la Yesu. Amen
|
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778