Monday, March 2, 2015

SOMO: KIFUNGO CHA NAFSI-Na: ADRIANO MAKAZI (RP)


JUMAPILI:  01 MARCH 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

Bwana na Bi Adriano Makazi (RP) wakati wa utambulisho kwenye
Ibada ya Jumapili 1/3/2015 Bonde la Maono Morogoro.

 
Utangulizi: Jumapili ya leo,ya kwanzakwa Mwezi March, Somo letu linaitwa Kifungo cha Nafsi”. Mwanadamu ana sehemu tatu ambazo ni MWILI, NAFSI na ROHO. Kazi ya Nafsi ni kuunganisha Mwili na Roho. Biblia inaongelea kuhusu uumbaji uliofanywa na Mungu kama ilivyoandikwa katika MWANZO 2:7….[Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.]…. Ndiyo maana kila mwanadamu alifinyangwa kutoka kwenye  mavumbi ya ardhi, na kitendo cha Mungu kumpulizia pumzi huyu mwanadamu, maana yake Mungu alimwekea ROHO. ‘Mtu akawa nafsi hai’ na hivyo Biblia haisemi ‘Mtu akawa roho hai’  bali ‘nafsi hai’. Kama nafsi yaweza kuwa hai, maana yake nafsi pia yaweza kufa.

 

Kuna mtu  wa mbinguni na kuna mtu wa duniani. Imeandikwa 1KORINTHO 15:45…[Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.]…. Maana yake mbinguni hautoki  udongo,  bali roho. Mtu  wa  kwanza ni udongo,  namtu wa pili ni  roho.

 

ZABURI 142:7…[Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.]… Nafsi yaweza kuwekwa kifungoni. Ndani ya nafsi ndipo kunakowekezwa aina zote zaelimu na ujuzi. Daudi alijua kuwa nafsi ikiwa salama mambo  mengine yote yanakuwa vizuri. Unapoona mtu ambaye hajisikii  raha akiwa ndani  ya Yesu,  ujue mtu huyo nafsi yake tayari ipo kifungoni.

 

HESABU 30:10-13….[Tena kama aliweka nadhiri nyumbani mwa mumewe, au kama aliifunga nafsi yake kwa kifungo pamoja na kiapo, 11 na mumewe alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichojifungia kitathibitika. 12 Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na Bwana atamsamehe. 13 Kila nadhiri, na kila kiapo kifungacho, ili kuitaabisha nafsi ya mwanamke mumewe aweza kuthibitisha, au mumewe aweza kutangua.]….Nadhiri ni kifungo cha ahadi. Nadhiri hufunguliwa tu pale ambapo ile ahadi ikeshatimizwa.  Kifungo cha nafsi hutaabisha nafsi (maana yake usisikie raha).

 

Ninaamuru mahali popote nafsi yangu ilipofungwa na kutaabishawa, leo nasimamam kinyume na kifungo chchote cha nafsi yangu kwa Jina la Yesu. Amen

 
Media na Information Ministries wakiwa kazini, katika ibada ya Jumapili 1/3/2015
Bonde la Maono Morogoro iliyoongozwa na RP Adriano Makazi

AYUBU 33:18…[Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,  Na uhai wake usiangamie kwa upanga.]….maana yake ni kuwa nafsi yaweza kuzuiliwa.

 

AYUBU 33:22….[Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi.]…. Yaani bado  kidogo tu kukaribia kuingia shimoni. Kuna watu ambao nafsi zao hazimo  mashimoni,  lakini zinakaribia kuingia huko.

 

AYUBU 33:28….[Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,  Na uhai wangu utautazama mwanga.]…. Baada ya nafsi yake kukombolewa,  haikuenda shimoni.

 

ZABURI 35:7…[Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.]…. Yaani wavu huu ni kama mtego uliofichwa kwa ajili ya nafsi ya mtu ili iingie shimoni, na huu wavu umefichwa. Shetani ana mbinu nyingi sana za kuwakamaata watu na kuwaweka mashimoni, na mbinu  hizi ndizo huitwa nyavu. Ndiyo maana Biblia inasema ipo njia ionekanayo njema machoni mwa mtu lakini mwisho wake ni uharibifu (MITHALI 14:12…[Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,  Lakini mwisho wake ni njia za mauti.]….

 

Shetani anazo akili sana. Je akili uliyo nayo ni ya nani? Imeandikwa MITHALI 3:4-5…[Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,  Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;]…. Endapo kuna akili njema ujue kuwa ipo akili mbaya. Akili zauovu au za kuangamiza wengine zinatoka kuzimu. Kuna watu ambao hawaanzi na Bwana katika mambo yao, lakini mambo yakeshaharibika huleta mambo yao  makanisani wakitaka ushauri na kutaka wengine wamtie nguvu.

 

UKIRI
Kwa Jina la Yesu, Ninaomba Bwana Yesu unipe akili ya  kukutumaini wewe,nifumbue fumbo za iblisi anazonijia nazo ili kunitega kwa Jina la Yesu.  Leo natuma malaika,  nakata nyavu zote, na lile shimoa alilochimba adumbukie mwenyewe kwa Jina la Yesu. Amen
 

 
Showers  of Glory wakiimba na kumchezea Bwana Yesu wakati wa ibada Jumapili 1/3/2015
Bonde la Maono Morogoro. Wimbo walioimba unasema  "Ninakushukuru kwa kuwa u mwema"
 

ZABURI 86:13…[Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.]….Waweza kuonekana upo duniani lakinni kumbe nafsi yako inatumikishwa kuzimu. 

 

MITHALI 23:13-14…[ 13 Usimnyime mtoto wako mapigo;  Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.  14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.]…. Endapo  nafsi ipo ndni ya mtoto yaweza je kwenda kuzimu? Unapoona watu wanasema mtu fulani hana utu maana yake nafsi yake imeingiliwa na kuwekwa uuaji, wizi, tabia mbaya n.k.  Nafsi haiendi mbinguni,  na ndiyo maana hata kama mtu ni daktari, hayo  yote yanaishia hapa  duniani.  Mbinguni hakuna wembamba au wanene,  matajiri au maskini.

 

UKWELI KUHUSU NAFSI YA MWANADAMU

1.      Nafsi ya mtu ndiyo chanzo cha utu wa mtu:

Kila kitu lazima kiwe na chanzo. Ni Chanzo cha uhai, uzuri, ubaya n.k.

2.      Tabia ya mtu hukaa katika nafsi

Tabia ya kudharau wengine, tabia ya kupenda fedha, tabia ya wizi, n.k.


LUKA 9:23-24…[Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.]… Kwamba hata kumfuata Yesu ni lazima mtu  ujikane nafsi yako. Nafsi ni  lazima iangamizwe lakinikwa ajili  ya Yesu.

 

YOHANA 12:25….[Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.]….Kuia nafsi yako  maana yake usiiche itumiwe na mtu mwingine bali  itumiwe na Yesu Kristo peke yake.

 

GALATIA 2:20…[Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.]... mtu anapojitoa kwa asilimia 1%, Mungu naye hukutumiakwa asilima1%.ukijitoa kwa asilimia 100% ujue mungu naye hukutumia kwa kkiwango hicho hicho.

 

Nafsi yaweza kuwa kifunogini. Mtu anapoikamata nafsi,  ankuwa amekamata utu wako. Nafsi ya mtu  ikeshageuzwa,  huweza kukosa utu kabisa na kufanya mambo ambayo siyo ya kawaida kufanywa na wanadamu wa kawaida (mfano mauaji,  kukata wengine vichwa/mikono n.k).

 

Nafsi ni masjala ya kusajili vitu vya kimungu au vya kishetani. Nafsi ya mtu inazoidara kuu tatu: Nia,Hisia na Utashi.

(a)  NIA:

WARUMI 12:2….[ Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.]….. Chochote unahokiona leo hii kinakuwa na mkono wa Lusifa. Kama makanisani, hata wachawi wanaingia, je si zaidi sana huko Bungeni au Baraza la Madiwani? Kumbe nia yaweza kugeuzwa.

 

UKIRI
Baba Mungu, katika Jina la Yesu, Ninakwenda kinyume leo na mawakala wa kuzimu, waliokamata nafsi yangu na kuichimbia shimo, leo nakataahuzuni, nakataa hofu kwa Jina la Yesu, enyi mashetani mlioniwekea hofu na huzuni,  leo naamuru achi nafsi yangu kwa Jina la Yesu,  leo naitoa nafsi yangu kwa ajili ya Bwana katika Jina la Yesu. Amen
 

 
 

1SAMWELI 2:30-35 …[ 30 Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. 31 Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. 31 Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. 32 Nawe utalitazama teso la maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. 33 Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa watu wazima. 34 Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; watakufa wote wawili katika siku moja. 35 Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.]…. Maana yake ndani ya nia ya Mungu ameweka mambo ya kufanya.

 

(b)  UTASHI: Ndani ya nafsi pia kuna utashi

 

(c)  HISIA: Ni ile hali ya  mtu kusdhisi kitu. Wakati mwingine humfanya mtu kuhisi.

Leo ni  siku ya kufanya vita kwa ajili  ya kuikomboa nafsi zilizokamatwa vifungoni. Lazima tushindane kwa sababu kule zinapokamatwa, nafsi hizi huzingirwa na majeshi ya mpepo wachafu huko kifungoni. Lazima tuyashambulie hayo mashetani, ili yale magumu yaliyokuwa mbele yetu yaanze kufanyika kwa wepesi.

 

Nafsi yaweza kushibishwa:

 

ZABURI 119:11….[Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.]…. Kwa hiyo maneno  huweza kuwekwa moyoni

 

KUTOKA 15:19…[Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara, Nafsi yangu itashibishwa na wao; Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.]…. Nafsi inaweza kushibishwa.

 

 

ZABURI 123:4…[Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.]…. Nafsi ni kama ghala la kuwekea vitu. 

 

 

Njia zinazotumika kufanya usajili wa nafsini au ubongini ni kama vile KUONA (kwa njia ya macho), KUNUSA (kwa njia ya pua), KUONJA (kwa njia ya ulimi), KUSIKIA (kwa njia ya masikio).

 

 

 

UKIRI
Leo ninakwenda kukatas vifungo vyote vya  nafsi yangu, leo natumia mamlaka ya Damu  ya Yesu, nawaamuru enyi mashetani wa ian ya  mizimu, aniaya majoka, ewe uliyekamata nia ya nafsi yangu ukapofusha fikra zangu,  uzito  mlioniwekea,leo nauondoa kw Damu ya Yesu, ewe kuzimu achia nafsi yangu kwa Damu ya Yesu, ewe mwenye kutaabisha nafsi  yangu,achia nafsi yangu, naamuru yeyote aliyejiungamanisha na nafsi yangu loe najitenga naye kwa Jina la Yesu,  ewe joka,ewe jini, leo ninakuamuru achia nia, achia hisia, achia utashi wangu kwa Jina la Yesu. Idara ya mashetani waletao giza, waletao fikra mbaya leo nawapiga kwa Damu ya Yesu. enyi mliojenga kwenye nafsi yangu,magonjwa yaliyosajiliwa nayafuta, kwa Damu ya Yesu. Amen

 

 

 

© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

 
Share:
Powered by Blogger.

Pages