JUMAPILI: 08 FEBRUARY
2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
'Wachawi wanaweza kukulaza madhabahuni kwao'... RP Adriano, hapo 8/2/2015 akiwa Morogoro alipokuwa akifundisha kwenye ibada katika Bonde la Maono |
Utangulizi: Jumapili ya leo 08/02/2015 Somo letu linaitwa “Kulazwa madhabahuni”. Kuna watu wanakuwa wamelazwa madhabahuni,
na hasa zile za wachawi na hawaamki. Mtu anaweza kulazwa, kusimamishwa au kuketishwa. Ulimwengu wa sasa
mtu hawezi kufanya jambo lolote bila
kujenga madhabahu. Mwanadamu (mtu) ni roho yenye nafsi, inayokaa kwenye nyumba na hiyo nyumba ni
mwili. Mwanadamu anaweza kuwa nje ya mwili
au ndani ya mwili. Je, yawezekana je mtu yupo kanisani lakini wakati huo
huo awe amelazwa kwenye madhabhu?
Imeandikwa katika 2
KORINTHO 12:2-4….[Namjua
mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa
katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo
alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu
huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;
Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika,
ambayo haijuzu mwanadamu ayanene..]…. Kwa hiyo, mtu anaweza kutolewa ndani ya mwili wake na kwenda kulazwa kwenye madhabahu
mahali fulani. Mtu anaweza kutolewa nje
ya mwili wake na kulazwa kwenye madhabahu na ndiyo maana mambo ya mtu huyo hayawezi
kufanikiwa wala hawezi kusifiwa na mtu mwingine yeote hata pale atakapofanya vyema. Kwamba mtu anaweza kutolewa kwenye mwili na kupelekwa mahali, akalishwa au kuvishwa huko
alikoenda.
MIFANO MICHACHE YA WATU AMBAO WALIZIFANYA
MADHABAHU KATIKA BIBLIA
1.
IBRAHIMU
MWANZO 22:9-10…[Wakafika mahali pale
alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni,
kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. 10
Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.]…. Isaka alijua kanuni ya madhabahu,
kwamba lazima iwepo kafara ya madhabahu na ndiyo maana akmuuliza baba yake
kujua yupo wapi kondoo wa kafara kwenye hiyo madhabahu. Biblia inaonesha kuwa Isaka alilazwa kwenye
madhabahu hii.
2.
ELIYA
WAFALME 18:17-31….[ Ikawa, Ahabu
alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli? 18
Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba
yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali. 19 Basi sasa
upeleke watu, unikusanyie jamii ya Israeli katika mlima wa Karmeli, na wale
manabii wa Baali mia nne na hamsini, na wale manabii wa Ashera mia nne, walao
chakula mezani pa Yezebeli. 20 Basi, Ahabu akapeleka watu kwa wana wa Israeli
wote, akawakusanya manabii pamoja katika mlima wa Karmeli. 21 Naye Eliya
akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata
lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya!
Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno. 22 Ndipo Eliya akawaambia watu, Mimi
nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia
nne na hamsini. 23 Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie
ng'ombe mmoja, wamkatekate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami
nitamtengeza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto
chini. 24 Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana;
na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu. Watu wote wakajibu
wakasema, Maneno haya ni mazuri. 25 Eliya akawaambia manabii wa Baali,
Jichagulieni ng'ombe mmoja, mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi;
mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng'ombe
waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri,
wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao
wakarukaruka juu ya madhabahu waliyoifanya. 27 Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya
akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda
anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe.
28 Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao,
hata damu ikawachuruzika. 29 Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, walitabiri
hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala
aliyejibu, wala aliyeangalia. 30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni
mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya Bwana iliyovunjika. 31
Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo,
aliyejiliwa na neno la Bwana na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. 32 Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo
katika jina la Bwana; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu,
ukiizunguka madhabahu. 33 Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng'ombe
vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji,
mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni.]… ELiya aliijenga madhabahu ya Bwana
iliyobomoka. Kwa kuwa madhabahu ni daraja,
kuna vitu vya muhimu kuwekwa katika
madhabahu, na ndiyo maana Eliya aliamuru mawe 12 kuwakilisha makabila 12
wa Israel. Hii ina maanisha kuwa kabila
zote 12 za wana wa Israelin (Yakobo) zililalzwa madhabahuni.
3.
MUSA
Musa aliijenga madhabahu ya vita dhidi ya kizazi cha Waamaleki. KUTOKA 17:15…[Musa
akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi* (Yehova-nisi maana yake ni
Bwana ni bendera yangu); akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na
Amaleki kizazi baada ya kizazi.]… Kwamba endapoWaamaleki watajitokeza kupigana na Israeli,
lazima watapigwa tu. Yamkini hapo kale
kuna mtu alijenga madhabahu kinyume na familia au ukoo/
kabila lako ili watu wake waende
kwa ugumu, wasifanikiwe,wasipate maendeleo. Wengine
UKIRI
Katika Jina la Yesu, ninaomba Bwana Yesu, kama nimelazwa kwenye
madhabahu yeyote ili niwe jinsi nilivyo,leo nawapiga wanaonishikilia huko
kwa Jina la Yesu. Nazikamata kila madhabahu na
kuzinagusha zote kwa Jina la Yesu. Amen
|
Majeshi ya Bwana ya Morogoro - Bonde la Maono wakiomba ili kujitoa katika madhabahu za kichawi zinazolaza watu ili wasifanikiwe kama inavyowapasa, hapo 8/2/2015 |
Katika madhabahu wapo MAKUHANI
kwa ajili ya kuhudumia madhabahu na
kuchochea moto wa madhabahu.
Upande wa Mungu Jeshovah, makuhani wa madhabahu ni wachungaji, mitume, manabii,
walimu na wainjilisti. Upande wa
Shetani, wachawi na waganga wa kienyeji ndio makuhani wa madhabahu za mashetani.
1 KORINTHO 10:1-4…[Kwa maana, ndugu
zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu;
wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na
katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa
kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata;
na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.]…. Kuna vyakula vya kulishwa rohoni wakati umelala. Unapoota ndoto zakula vyakula kwenye ndoto,
ujue unakula chakula cha roho. Itategemea ni vyakula vya upande gani umelishwa.
Wachawi nao wanamtindo wa kufanya sherehe zao na kuwalisha watu wengine vyakula
vyao vya kichawi ili kupunguza nguvu a watu.
UFUNUO 6:9…[Na alipoifungua muhuri
ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la
Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.]….
UFUNUO 14:18….[Na malaika mwingine akatoka katika ile
madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule
mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya
mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.]…
UFUNUO 16:7….[Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana
Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.]…
1 KORINTHO 10:14-18...[Kwa ajili ya hayo,
wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili;
lifikirini ninyi ninenalo. 16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si
ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi
sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni hao Waisraeli
walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na
madhabahu?]… Chakula
alishwachomtu kinakuwa kimeungamanishwa na nguvu ya madhabahu fulani. Mtu
anaweza kuwa na ushirika na madhabahu fulani bila kujua. Ni utaratibu kuwa
katika ufalme wa Nebukadneza vyakula
vilikuwa vinasomewa dua kabla ya kuliwa ili watakaovila wawe shirika na miungu
yake, na ndiyo maana Danieli na wenzake walikataa kula aina ile ya vyakula. Hata sasa, kuna watu wamekula
vyakula vya msibani na kuwa chanzo cha
shida inayowakabili. Siyo kila msiba unakuwa na mambo ya aina hii, lakini kumbuka kuwa
siyo kila anayeenda kwenye msiba ana kusudi jema na waliohuduhuira msiba huo.
UKIRI
Ninataa leo kukamatwa, chochote nilicho nacho, ninawasha moto wa
Damu ya Yesu, kwa Jina la Yesu. Amen.
|
Showers of Glory wa Bonde la Maono Morogoro wakiimba na kumchezea Bwana Yesu hapo Jumapili 8/2/2014 |
Mungu ameweka vitu vyote kwa wakati na majira yake, na endapo mtu
amelazwa kwenye madhabahu,wakati wa Mungu ukiwadia mtu huyo anakosa kupata vile
vya Mungu maishani mwake. ….MHUBIRI
3:1-8….[ Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2
Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;
Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; 3 Wakati wa kuua,
na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa,
na wakati wa kujenga; 4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; 5
Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa
kutokumbatia; 6 Wakati wa kutafuta, na
wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na
wakati wa kutupa; 7 Wakati wa kurarua,
na wakati wa kushona; Wakati wa
kunyamaza, na wakati wa kunena; 8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.]…..
GALATIA 4:4…..[Hata ulipowadia
utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke,
amezaliwa chini ya sheria,]…… Kila mtu amewekewa
utimilifu na Mungu. Yapo mambo ambayo Mungu alikusudia uyapate kwa wakati wake
mwaka huu 2015. Hata hivyo, wakati huo ukeshapita ndipo unapogutuka kuwa
ulikuwa wapi…… Kutokutambua majira ya kujiliwa kwao, kulisababisha Yesu
awalilie watu wa Yerusalemu… LUKA
19:41-44…..[Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42
akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini
sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako
watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44
watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya
jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.]….
WARUMI 13:11…[Naam, tukiujua wakati,
kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu
wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini]….. Adui amewalaza kwenye madhabahu ili
wasizione fursa.
ISAYA 6:9-10…[Naye akaniambia,
Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni
kutazama, lakini msione. 10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio
yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio
yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.]… Nabii Isaya anapewa maelekezo kuwa watu
watakuwa wanasikia lakini wasifahamu. Hapa nabii Isaya anatumwa akawatie uzito
masikio ya hao watu. Zipo madhabhau za kutia uzito, masikio ya rohoni, vinywa
vya rohoni (kuongea kwa namna ya rohoni), miguu ya rohoni (kuweza kukanyaga na
kumiliki), mikono ya rohoni (ili baraka za Mungu zionekane kwa kila unachotia
mikono yako kufanya). Musa alipokuwa akipigana na Waamaleki, aliinyoosha mikono
yake juu na kufanya Joshua na jeshi lake kushinda, na pale mikono ya Musa
ilipochoka hata akaishusha chini, Joshua na jeshi lake walipigwa na Waamaleki.
Joshua kwa upande wake, alikuwa na barakaa za Mungu kupitia miguu yake.
Mungu alimuandaa Mfalme Koreshi wa Uajemi ili kuijenga upya nyumba
ya Bwana iliyopo Yerusalemu: 2 NYAKATI 36:22-23…[Ikawa
katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana
alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake
Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote,
akaiandika pia, akisema, 23 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Bwana, Mungu
wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba
katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake,
Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.]….. Leo
ni siku ya kuiamsha roho yako ili
yale uliyopaswa kuyafanya mwaka huu
yatimie kwa Jina la Yesu. Kama Bwana
aliweza kuiamsha roho ya Koreshi, ni dhahiri kuwa roho (ambayo ndiyo mtu)
yaweza kulazwa.
EZRA 1:1-2…[Ikawa katika mwaka wa
kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa
kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme
wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;
Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza
nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda.]…
Majeshi ya Bwana ya Bonde la Maono Morogoro wakipaaza sauti zao juu wakiomba kinyume na nguvu zote za giza zinazowalaza watu kwenye madhabahu hapo Jumapili 8/2/2015 |
Mungu alilazimika kuziamsha roho za watu mabli mbali katika
Biblia. HAGAI 1:14…. [14 Bwana
akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya
Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda,
wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao; ]……
Kwa nini Mungu anaamsha roho za watu na siyo miili yao? Ni kwa sababu roho
ndizo zimepewa majukumu ya kufanya. Mafanikio ya mtu huanzia rohoni, na baadae
kudhihirika mwilini. Hata kushindwa kwa mtu huanzia rohoni na kudhihirika
mwilini (3 YOHANA 3:2.…[Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako
ifanikiwavyo.])…
UFUNUO 9:13-14…[Malaika wa sita
akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu
ya dhahabu iliyo mbele za Mungu, 14. ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na
baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.]…. Malaika ni roho lakini wanaweza
kufungwa mahali ili wasilifanye kusudi walilotumwa kulifanya. Ina maana endapo
hata malaika wanaweza kufungwa, hata wewe pia roho yako inaweza kufungwa na
wachawi kwenye mito, milima n.k. ili usiweze kufanya yale makusudio ya Mungu
maishani mwako.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778