JUMAPILI: 29 MARCH 2015 -
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Jumapili ya leo 29/3/2015, Somo letu
linaitwa “NJIA”. Unapotaka kwenda mahali
popote, sharti uijue njia. Kila iitwapo leo, mwanadamu anakuwa amepiga hatua fulani ya njia ya safari ya maisha yake, na kuna mahali huyu mtu anaelekea, aidha
uzimani au motoni. Zipo pia safari ambazo njia zipo lakini usafiri haupo. Kilichowafanya wana wa Israeli
waliotoka Misri wasifike Kanaani, nchi
ya Ahadi ni njia. Ni kwa sababu njia
waliyopitia ilikuwa na changamoto nyingi, na majaribu mengi. Njia ndiyo yenye
uhakika wa kukufikisha unakokwenda. Kwenye
njia ndipo shetani alipoweka makao, na kuwakamata watu na kuwafanya wajisahau.
Children Ministry wakiimba na kucheza mbele za Bwana katia ibada ya Jumapili 29//2015 Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro (Bonde la Maono) |
AYUBU 38:18-20…[Umeyafahamu mapana ya dunia?
Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi? 20 Upate
kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa
na mapito ya kuiendea nyumba yake?]… Ukielewa hiyo njia
inakufanya ujue unapaswa kufanya nini kwa wakati gani. Zipo njia mbili,kwa mujibu wa Ayubu,moja ya nuru na ingine ya giza. Shetani
yupo kwa ajili ya kupinga na kuzuia. Yapomakao yako ambayo Mungu alikuandalia uwepo pale. Jinsi ya
kwenda kwenye hayo makao, inakupasa uijue hiyo njia.
Usiogope vita kwa
sababu hata Samweli alizaliwa kutokana
na Penina kumsumbua Hanna. Vita inapoinuka kazini kwako, kwenye nyumba ya
kupanga n.k. ni sababu ya kukupeleka wewe kwenye hatima njema zaidi. Imeandikwa
kuwa, ‘Mungu wetu ni mtu wa vita, Bwana ni Jina lake’.
HESABU 24:21 …[Kisha akamwangalia Mkeni, akatunga mithali yake, akasema, Makao
yako yana nguvu, Na kitundu chako kimewekwa katika jabali.]…
Wao wanaweka mitego ili wakuzuie na kukuonea, lakini Yesu Krsito ameshakuwekea
njia katikati ya jabali. Ndiyo maana
Yesu alisema katika YOHANA 14:6… [“mimi ndimi njia, kweli na uzima”]… Katika
dunia yote tokea uumbaji, hayupo nabii aliyewahi kutamka maneno kama haya ya
Yesu. Eliya pamoja na kushusha moto, hakuwahi kusema ni njia. Elisha pamoja na
kufufua wafu, hakuwahi kusema ni njia. Musa pamoja na kutenda miujiza yote,
hakuwahi kusema ni njia. YESU KRISTO ndiye pekee ambaye ni NJIA. Yupo adui
anayezuia njia yako, katika ndoa yako, kazi yako n.k. lakini hakuna atakayeweza
kukuzuia.
Huwezi kumzuia mtu aliyetumwa.
Kama kweli unaweza, kampigie simu Musa kumuuliza je, waliokuzuia walifanikiwa? La
sivyo mpigie simu Farao, je ulipowazuia Israeli, ulifanikiwa? Waliinuka mitume
na manabii na wachungaji wengi, lakini
hayupo wa kufananishwa na Yesu Kristo.
RP Bryson akiombeawatu waliamua kuma Yesu Kristo maisha yao kwa Kuokoka, Jumapili 29/3/2015 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Yusufu aliuzwa na
ndugu zake, wakidhani wamempoteza, kumbe
wamempeleka kwenye eneo la kumiliki
kwake. Endapo ndugu zake hawa wasingemuuza Yusufu, asingetawala. Leo hii
tunalitaja jina la Yusufu kwa sababu ya
hao ndugu zake kumuuza. Kile kikao wanachokaa maadui zako, Mungu yupokaatikati
yao na najua mpango wao. Mungu anaweza kusababisha uondoke, lakini ukirudi
unarudi kwa nguvu mpya na mamlaka mapya. Wasikutishe wale wanoinuka. Ukiona wanga
au wachawi wanakuwangia usiku, yapasa ujisifu sana, kwa sababu umeweza
kuwafanya watu wasilale usiku huo kwa ajili yako tu. Ukiona unatengenezewa zengwe kazini kwako,
maana yake wewe ni mtu wa hatari sana,
na unapaswa kupandishwa cheo. Ni ushahidi kuwa ndani yako ipo nguvu inayowatisha.
Showers of Glory wakati wakiimba na kumsifu Bwana Yesu Jumapili 29/3/2015 Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. |
MITHALI 24:15….[Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;]…
Yupo aliyegusa makao yangu, lazima leo nimshughulikie.
ZABURI 55:15…[Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai,
Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.]…. Wote wanaokuzia
kwenye mipango yako, ni saa ya kuwaondoa kwa Jina la Yesu.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778