Utangulizi: Ukristo haufananishwi na dini zingine
zozote. Hii ni kwa sababu, mwanzilishi wa imani hii zaidi ya miaka 2,000 iliyopita alikufa na
baada ya siku 3 akafufuka, na kaburi lake liko
wazi hadi leo hii. Alfajiri ya siku kama ya leo, Yesu Krsito aliishinda
mauti, akainuka tena. Hata sasa, tatizo
ulilo nalo si kitu tena,
kwa sababu aliyeko ndani yako
ameinuka tena kwa nguvu.
UFUNUO
5:5…[Na
mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya
Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile
muhuri zake saba.]…. Hii siyo saa ya kulia tena, bali ni ya ushindi. Yule Yesu
Krsito waliyetaka kumzimisha, huwa haondoki moja kwa moja, bali anapoondoka huweka ‘appointment’ ya kurudi
tena. Yesu tunayemtuaminia sisi huwa hakai makaburini kama waanzilishi wa dini
zingine ambao wapo makaburini hadi leo
hii.
KUTOKA 22:23..[ Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi,
hakika yangu nitasikia kilio chao,]… Wao walikaa ili wewe
uteseke/ au uangamie/ au upotee, lakini Yesu Krsito aliiweka saa kama hii ili
kuitikisa malango ya giza. Yesu Krsito alikuja ili watu wawe na uzima, tena
wawe nao tele. Kumbe basi, Yesu Kristo alikuwa akinipitisha katika mafunzo ya
kupokea ushindi wangu. Kwa kufufuka kwake, Yesu Kristo leo amenitangazia
ushindi.
YEREMIA 31:16-17…[Bwana asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako
yasitoke machozi; Maana kazi yako
itapata thawabu, nao watakuja tena toka
nchi ya adui; Ndivyo asemavyo Bwana. 17 Tena liko tumaini kwa siku zako za
mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe.]…
Yesu Kristo amesimama ili kuwaangusha waliokupinga na kukalia njia yako. Wao
wamejipanga ili maisha yako yawe ya huzuni, lakini Yesu Krsito asubuhi na mapema leo, ameinuka tena na kutoka kwenye lile shimo
walilomchimbia. Yesu anapofufuka, hatoki hivyo hivyo, bali hutoka huko na ‘funguo’
za kukutoa wewe kwenye lile tatizo lako.
Yesu Kristo anazo funguo za maisha yangu na kazi yangu. Wao walijipanga kinyume
nami lakini yeye alipofufuka alikuja na
funguo akijua kuwa lile tatizo lako lina mahali lilipofungiwa, na atazitumia
hizi funguo kulifungua.
Yesu Krsito huonekana
kwenye kilio. Usitarajie kumuona Yesu Krsito katika vicheko vyako. Wana wa Israeli
walipokaa Misri kwa miaka 430,hatimaye Yesu Kristo alishuka baada ya kukisikia
kilio chao ili kuwatoa katika hali ya vilio. Yesu Ksrito amesema atayafuta
machozi yako. Kwa sababu hiyo, hata mipango yangu iliyokuwa inaelekea kwenye
mauti,imefufuka tena.
Yesu Kristo baada ya
kufufuka alipewa JINA lipitalo majina
yote. Kwa sababu Yesu yu hai, huzuni yangu imekwisha. Hawezi mtu kuuzuia Ukristo usienee hapa duniani.
Hawezi mtu kuzuia Ufufuo na Uzima kuenea
duniani,kwa sababu aliyetupa hii kazi ni Yesu Kristo mwenyewe. Hayupo wa kunizuia, kwa sababu
aliyeigwa Bahari ya Shamu yu ndani yangu,
aliyemwangusha Mfalme wa Bashani yu ndani yangu, aliyewatoa wana
waIsraeli Misri kwa mkono wenye ngubu yu
ndani yangu, aliewalisha wana wa Israeli mana jangawani yu ndani yangu.
ZABURI 23:4…[ 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la
uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na
fimbo yako vyanifariji.]… Usikate tama kamwe kwa sababu yote unayoyaona katika maisha yako
siyo mauti, bali ni uvuli wa mauti tu.
ZABURI 23:5…[Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka
mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.]…
Unapoona madui zako wamekuzunguka, jua
kuwa katikati pana mafanikio yako.
Usiuzuie upanga wako kuwaangamiza,
kwa sababu umwonapo adui ujue kuna ushindi wako. Adui hakai kwenye
nyumba za manyasi au udongo.n umwonapo mlinzi ujue ndani ya hili jumba
pana mali na vitu vya thamani. Kwenye
nyumba Za nyasi hapaka walinzi. Hapo hapo penye ulizni mkali, pana kitu
unapaswa kuking’ang’ania. Kama hamna kitu, kwani nini kunuzuia? Hata wewe uwaonapo watu wakizuia, ujue kuna kitu. Goliath aliinuka kipindi cha
Daudi na siyo cha Sulemani kwa sababu Daudi ndiye saizi yake. Sauli aliinuka
wakati wa Daudi, hakuinuka wakati wa Sulemani kwa sababu Sulemani asingemweza.
Ahabu anamtaka mtu jeuri kama Eliya. Kila adui na mbambe wake. Hata wapiganaji
masumbwi, hupimwa ili wapambanishwe kwa uzito sawa. Ukiona adui ameinuka huyo
ni saizi yako.
Daudi aliinuliwa kwa
ajili ya Wafilisti. Sauli kuona vile akampa kazi ya kumpatia Wafilisti 50, naye Daudi aksema hiyo si taabu, nitakuletea.
Kila jaribu ulionalo maishani mwako ujue lina mlango wa kutokea. Imeandikwa, ‘mimi ni silaha ya Bwana ya vita’, na ndiyo maana Mungu amekuweka kwenye hili tatizo
ulilo nalo, na kwamba utumike sawasawa
kumuangamiza huyo adui wako.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778