JUMAPILI: 22 MARCH 2015 -
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Jumapili ya leo 22/3/2015, Somo letu
linaitwa “Jinsi Mtu Achukuliwavyo Msukule”. Huwezi kulikuta neno ‘msukule’
katika Biblia, na hii imewafanya watu wengi wanavyolikosa katika Biblia
wasikubaliane na mafundisho hayo wakidhani
ni imani potofu. Hata hivyo kutokuwepo kwa neno hili katika Biblia
hakumfanyi shetani asiwachukue watu katika msukule. Biblia hata hivyo inatukumbusha kwamba yapo
mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya lakini katika Biblia hayapo kwani
hayakuandikwa.
YOHANA 21:25….[Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja
moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.]….Kumbe
ni mengi sana yale ambayo hayajaandikwa
katika Biblia, ikiwemo mambo ya “msukule”. YOHANA
20:30….[Basi
kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake,
zisizoandikwa katika kitabu hiki.]…. Maana yake ni kuwa,
yapo mengine ambayo hayajaandikwa, lakini haimaanishi kuwa kutoandikwa hayawezi
kutuathiri leo hii. Mathalani, hata kama
Yesu aliwaweka huru misukule, na haijaandikwa katika Biblia, si kigezo cha
kubisha na kusema misukule haipo.
Maneno kama vile
upako, nayo hayapo katika Biblia, ila ni neno linalotaokana na ‘mpakwa mafuta’.
Wamiminiwa mafuta katika Biblia ni kama vile Wafalme na Manabii, vyombo
vya Bwana kwa ajili ya matumizi ya Bwana.
1WAFALME 19:15-16 … [Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia
ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. 16 Na
Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa
Shafati wa AbelMehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.]….
Wachungaji wa Bonde la Maono Morogro (APs) wakifuatilia maandiko kwenye Biblia zao, Kutoka Kushoto ni AP Gideon, AP Gwamaka, AP Steven na Ap Amos |
Mtu aweza kuchukuliwa
msukule mzima mzima,au kwa kuchukuliwa
mikonoyake,au miguu yake, au macho n.k. mikono kama imechukuliwa
huwezikufanikiwa,kwani Mungu amesema atabariki kazi zamikono yako.
Endapo wachawi wamekuwekea mikono yap aka,si rahisi
ubarikiwe kwani mikono hiyo si yako.
Kichwa endapo kimeibiwa,
na pengine mtu huyo kawekewa kichwa cha paka au cha kuku, si rahisi kusonga mbele kwa mafanikio. Leo lazima turudishe kichwa chako kwa Jina la
Yesu.
Mwingine anakuwa
amewekewa tumbo la bandia, matokeo yake tumbo la aina hiyo lililopaswalizae
marais, au mawaziri linashindwa kuzaa. Kila mara uvimbe
unatokea tumboni.leo ni siku ya kuamuru matumbo
yote yaliyochukuliwa yarudi kwa Jina la
Yesu.
UKIRI
Kila
mchawi anayetumia tumbo,
miguu,mikono, kichwa changu,
nawaponda wachawi,kwa kuwa imeandikwa usimuache mwanamke mchawi kwa Jina la
Yesu, nawaponda wachawi owte,kwa kuwaimeandikwa mimimni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita. Leo navua uso bandia, navua tumbo
bandia kwa Jina la Yesu. Amen
|
Majeshi ya Bwana ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Bonde la Maono Morogoro, wakati wa Ibada ya Jumapili 22/3/2015 - iliyoongozwa na RP Adriano. |
Mtu anaweza kuwekewa
sura bandia. Katika mashindano ya Miss
Tanzania au Miss University, unaweza
kushangaa kuwa anayechaguliwa kama mshindi wala si Yule aliyetarajiwa, na wala
hafananii kupata nafasi kama hiyo.
AINA ZA MISUKULE
Msukule ni mtu aliyekufa au aliyechomolewa ndani ya
mwili wake na kwenda kutunzwa mahali pengine bila ridhaa yake. Lipo shimo kubwa sana la kuzimu ambalo ndiko makao
makuu kwa shetani. Wachawi nao wametengeneza mashimo yao madogomadogo ya kuhifadhia watu humo ndani. Mashimo kama
vile ‘gambushi’ ni mfano mmojawapo.
Zipo biashara za miili ya watu. UFUNUO
18:11-2…[ 11 Nao
wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye
bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na
lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo
nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti
wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na
mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya
mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari,
na miili na roho za wanadamu.]… Baada ya malikia wa
mbingu kupigwa, wafanyabiashara wa nchi walilia na kumuombolezea. Miili na Roho za wanadamu ni
miongoni mwa bidhaa hizi zilizokosa wateja. Katika Biblia,wana wa Yakobo
walimuuza ndugu yao kwa Waishmaeli, naye akapelekwa hadi kwa nyumba ya Potifa.
MWAZO 37:27…[ 27 Haya, na tumwuze kwa hawa
Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu.
Ndugu zake wakakubali. 28 Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa
Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa
vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.]….
Waishmaeli ni Waarabu, na baada ya kumnunua Yusufu walienda na kumuuza tena. Tama ya mali inaweza
kumfanya mtu kumuuza mwingine. Yesu naye
aliuzwa na mwanafunzi wake, Yuda Iskariote.
MWANZO 39:1…[Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao,
mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta
huko.]… Inawezekana hata wewe hapo ulipo ulishauzwa na hauna habari.
Wanachosubiri ni ule mtego wao wa kugonngwa na bodaoda, ili mwishowe madktanri
waseme kwa ajali hii damu imevunja sana huwezi kupona. Endapo mtu hana Yesu, atakuwa na shetani wake
anayemtegemea. Si vyema kkutamani vitu au aina ya maisha ya mtu fulanii kwa
sababu kwa kufanya hivyo utamtamani ha ta
Yule aliyempa. Ni kweli kuwa shetani
anaweza kumpatia mtu vitu, fedha, utajiri, na ndiyo maana shetani katika kumjaribu
Yesu, alimwambia ‘endapo
utanisujudia nitakupa vitu vyote hivi kwa sababu vipo mikononi mwangu’.
UKIRI
Bwana Yesu, Ninaomba leo unipe neema ya kutoka kwa Jina la Yesu. Ninakataa kukaa utumwani, ninakataa kuonewa mimi kwa Jina la Yesu, Ninaamuru leo mikono yangu kama imeibiwa na inatumiak na mtu yeyote namnyang’anya leo kwa Jina la Yesu. leo macho yangu kama yameibiwa na inatumika na mtu yeyote namnyang’anya leo kwa Jina la Yesu. Amen |
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778