JUMAPILI: 12 APRILI 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Shetani anao uwezo wa kuingia ndani ya
mtu kama ‘maelekezo’. Ukumbuke kuwa Mwanadamu ana akili, lakini mwandamu siyo akili. Sasa mwanadamu ni
kitu gani?
Mwanadamu ni roho
yenye nafsi, inayokaa katika nyumba na hiyo nyumba inaitwa mwili. Mwanadamu Anazo
sehemu kuu tatu: nafsi, mwili na roho. Pia taarifa za mbalimbali za huyu
mwandamu zinahifadhiwa ndani ya moyo (siyo huu wa moyo nyama, lahasha‼). Kila taarifa ninayoiona au
kuisikia hukaa moyoni.
Shetani
anafahamu kuwa hawezi kukamata kwa
kukutia tu pepo, bali hukukamata kwa kukuingizia taarifa. Yesu alisema, “manaeno niwaambiayo ni roho, tena
ni uzima”.
Ina maana maneno ya Yesu Krsito yamebeba roho ya uzima. Kuna roho inaingia
ndani ya mtu, kwa jinsi anavyokuwa anakaa na wenzake na kusikiliza maneno yao.
Inategemea maneno hayo ni ya kimungu au
ya kishetani.
1 NYAKATI 21:1… [Tena shetani akasimama juu
ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.]…
Daudi aliletewa taarifa na shetani naye akakubaliana naye, huku akijua Mungu
alishakataza Israeli kuhesabiwa. Kwa nini Daudi ahesabu watu wake? Ni kwa
sababu alikuwa akishinda kataika kila vita aliyopigana, akadhani ushiindi wake
unatokana na ukubwa wa jeshi alilo nalo. Kinachomfanya Daudi amkosee Mungu ni
ile taarifa iliyoingia moyoni mwake. Shetani
anao uwezo wa kumpumbaza mwanadamu.
MATHAYO 13:15…[Maana mioyo ya watu hawa
imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba;
Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo
yao, Wakaongoka, nikawaponya.]…Ndiyo maana wapo watu ingawa hawapendi kufanya
uovu, lakini kutokana na taarifa
walizojaza mioyoni mwao,basi hutenda
uovu.
2KORINTHO 4:4..[].. Mioyo ya watu inakuwa inefungwa
ili wasiamini.
WARUMI 1:21…[kwa sababu, walipomjua
Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika
uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.]…Shetani
anajua kwenye moyo wako, ndiyo kitovu
cha kukupatia taarifa.
MATENDO 28:27…[Kwa maana mioyo ya watu
hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa
macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili
nia zao, nikawaponya.]….
Ushindi wa mwanadamu
upo moyoni. Yafaa ujifunze ni nani umsikilize na nani usimsikilize. Kila unachosikiliza
ni roho, na unapobaki peke yako yale
maneno yanaanza kukusemesha. Maneno ya kuzimu yakeshaingia ndani yako, yanaweza kukupeleka usipotaka.
Moyo wa mwanadamu ni kama sumaku. Kinachomfanya
mtu awepo kanisani na siyo disko ni kwa sababu mtunhuyo hana taarifa za disko.
Haiwezekani kusikiliza nyimbo za Bongo flavor tokea asubuhi halafu unatarajia uwe mchungaji wa kanisani. Taarifa
ndiyo maarifa, pasipo taarifa hakuna
maarifa.
Ukimuona mtu aliyefanikiwa, ni kwa sababu alitumia taarifa
iliyokuwepo moyoni mwake.
JOSHUA 14:17…[Mimi nilikuwa mtu wa miaka
arobaini umri wangu, hapo Musa mtumishi wa Bwana aliponituma niende kutoka
Kadeshbarnea ili kuipeleleza hiyo nchi; nami nilimletea habari tena, kama
ilivyokuwa ndani ya moyo wangu.]…. Haya ni maneno ya
Kalebu, akikumbushia kuwa alitoa taarifa sawasawa na moyo wake. Maana yake
nikuwa, pamoja na kuyaona yale majitu,
lakini hayakumtisha bali taarifa zao
hakuziweka moyoni mwake, bali aliazimia kuiweka taarifa ya Mungu Baba
aliyewavusha toka Misri kupitia Bahari ya Shamu. Taarifa unayoiweka ndani ya moyo
wako,yaweza kukufanya uingie Kanaani au la. Ndiyo maana Daudi alisema, “Bwana
nimeliweka neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi”.
Hayupo wa kukuzuia
kwa sababu Yesu ni kila kitu katika
vyote. Silaha kubwa ya shetani ni hofu. Je, wewe umeweka taarifa gani
moyoni mwako? Tunaye Mungu aliye mkuu kuliko miungu yote. Ufufuo na Uzima ni Yesu mwenyewe. Muweke
Mungu Mkuu katika moyo wako. Huyu
ni Yule aliyewingia katika msiba wenye
huzuni akabadilisha taarifa yao ya msiba ikawa taarifa ya furaha. Hayupo mtu wa
kuizuia Ufufuo na Uzima hapa duniani, kwa sababu Ufufuo na Uzima ni Yesu
mwenyewe. Taarifa nzuri ni za Yesu
Kristo. Kalebu akamwambia Joshua, “sikuaangalia
yale majitu, bali nilitoa taarifa
kulingana na moyo wangu”.
Neno la Mungu ni taa
ya miguu yako.ukiona inafikia mahali
unakata tama, unakuwa na wasi wasi, na maswali ya aina hiyo ujue moyoni
mwako kuna kitu ambachohakipo. Kila vita
inapoinuka, Mungu huibeba silaha iliyoko
moyoni mwako ili kukushindia. Vita unayotaka uipiga inategemeasilaha ulizo
nazomoyoni mwako. Wakatiwa amani,nsiyo wakati wa kutengeneza silaha. Wakati wa
vita ni wa kuchukua silaha ulizo nazo ghalani na kuzitumia. Badhi ya Wakristo
hupigiga simu wachungaji wakitaka maombi nyakati zile mambo yanapowakwamia.
EFESO 6:11…[Kwa maana kushindana kwetu
sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa
giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa
sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu,
na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.]…. Kuna siku ya uovu,
ambayo mashetani wanakuwa wameweka kituo, kuwa leo ni kawa ajili ya ndoa ya
mtu fulanii. Hiyo ndiyo siku ya uovu.
Inabidi ufahamu kuwa, shetani
anakufuatilia usiku na mchana.
Nchi na nchi zinapopigana,majeshi yao huanza kwa kushambulia maghala ya
silaha. Ili adui asikushinde, weka vizuri ghala lakola silaha moyoni mwako. Usisubiri vita iibuke kazinimwakoau
katika ndoa yako. Maneno ya Mungu mkuu yawepo mioyoni mwetu. Weka silaha ya
moto ndani ya moyo wako, achana na
silaha ya mwaka jana ambayo tayari ina kutu.
Wokovu tulio nao siyo
wa mazoea. Samsoni alijidanganya, hata baada ya kunyolewa,aliendelea kudhani
kuwa nguvu zake zitamrudia kwa kujinyoosha tu. Mbinu anazotumia shetani ni mpya
kila siku. Yale ya jana
hayatakusaidia leo, kwa sababu leo ni siku mpya na ya tofauti. Kuna tofauti ya
chakula cha jana kilicho kwenye frijina chakula kilichoivishwa leo. Silaha
iliyopo moyoni,ukiweza kuinoa vizuri,
inakuwa na makali yale yale.
Njia nzuri ya kuweza
kuwa na silaha moyoni mwako ni yaw ewe kuokoka na kumkabidhi Yesu Kristo maisha
yako.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778