JUMAPILI: 05 JULY 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:
Wale
wanaokuonea na kuyasumbua maisha yako
huitwa “watu wa ulimwengu huu”.
Ukumbuke kuwa huu ulimwengu upo chini ya yule adui yetu shetani. GALATIA 1:4…[ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya
dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda
Mungu, Baba yetu.]… Je, dunia ndiyo mbaya au wakaao duniani ndio
wabaya? Je, Mungu aliumba kitu au vitu vibovu. Mungu ndiye aliiumba hii dunia. MWANZO 1:1-31, uumbaji wa Mungu
unaonekana, na kila alichokiumba Mungu alisema ni kizuri, tena kinachopendeza. Kwa kawaida kitu kizuri kinachopendeza hata
siku moja siwezi kukiita kibovu. Mungu aliiacha dunia ikiwa inapendeza. Kipo
kitu kilichotokea na kuifanya dunia iwe mbovu.
1YOHANA
1:4-5…[Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 5
Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu
ni Mwana wa Mungu?]… Mtu aliyeushinda ulimwengu ni yule aliyemkiri
Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
Imeandikwa 1YOHANA
5:19…[Twajua
ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.]…
Hapa tunagundua kuwa dunia hii inatawaliwa na shetani. Na mimi ambaye
nimeokoka, sipo upande wa hii dunia. Kama dunia haipo upande wangu, ina
maana ya kwamba shetani anaweza
kuwatumia wale wote wasiomwamini Yesu (ambao wapo duniani) ili kunipinga. Ndiyo maana Yesu Kristo aliniokoa mimi na
wewe kama mbegu ya kuzitikisa falme za hii dunia ili zote ziwe falme za
mwanakondoo. Watu wa ulimwengu wanakupinga lakini Baba wa mbinguni alikujua na
kukuandaa ili kuushinda ulimwengu na hiyo balaa iliyokuja mbele zako.
Sikuzaliwa chini ya utumwa, bali nina kazi maalumu kwa ajili ya ushindi
niliyopewa na Baba wa Mbinguni. Huyo adui anayekupinga hana kitu kwako, kwa
sababu unayo mamlaka ya ushindi. Kabla ya vita yako, mshindi ameshatangazwa.
Tatizo ni kuwa adui anayakamata mawazo na akili zako ili ujione kuwa uwezo wako
ni huo kumbe siyo. Mamlaka na uwezo na nguvu ulizo nazo vyote ni vya Mungu, na
kama Mungu hawezi na mimi siwezi. Ila kama Mungu anaweza na mimi naweza. Ndiyo
maaana imeandikwa “waliozaliwa
na Mungu huushinda ulimwengu”. Yawezekana siyo leo au kesho
lakini ninachokijua ni kuwa sitaondoka hapa kama aliyeshindwa bali kama
mshindi.
Biblia inasema ujapopita katika bonde la uvuli wa
mauti, sitaogopa mabaya. Kwa kuangalia kwa macho unaona mauti, lakini mbele za
Baba anona hayo mapito kama ‘uvuli wa mauti’. Acha kulia na kusema maisha ni magumu. Kumbuka
kuwa kati ya nuru na giza, chenye nguvu zaidi ya kingine ni nuru kwa sababu
mahali penye giza ikiwekwa nuru giza hukimbia.
Kwa kuwa wewe umeokoka, ujue kuwa wewe ni nuru na wote walio gizani lazima
wakimbie mbele zako. MATHAYO 5:13-16…[Ninyi ni chumvi ya
dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena
kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu.
Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na
kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo
nyumbani. 16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona
matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.]… Wanaokupinga wakikuangalia wanaona
kitu kinang’aa na ndipo hutafuta namna ya kuifunika nuru yako. Wasichokijua ni
kuwa hiyo nuru yako haijatoka kwa wanadamu. Giza haliwezi kuiondoa nuru mahali popote. Fahamu kuwa
waganga wa kienyeji ni giza. Ukiona giza linakufuatia ujue kuwa kuna
mahali ambapo taa yako imezimika.
Inapaswa kuiwasha taa yako ili kuifukuza
giza mbele yako.
Kiu ya shetani ni kunizua nisitoke. Hata hivyo,
sikuja kupata mafanikio kupitia watu ila mafanikio yangu yanatoka kwa Baba wa
Mbinguni. Mtu unayemuona leo ni wa leo, ila usichokiona ni kesho yake mtu huyu.
Fahamu kuwa kazi ya shetani ni kukupinga na kukufunga.
Imeandikwa katika ISAYA 14:17…[Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake;
Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ]… Mpango wa shetani na
mawakala wake ni kuwafunga watu wasiweze kwenda kwenye ushindi wao. Hupaswi
kuwaza juu ya mamlaka aliyo nayo wakala wa shetani (adui). Mamlaka uliyo nayo
ni makubwa kuliko ya adui zako. Haipaswi kukaa ndani ya kanisa ambalo watu wake
wanamtegemea tu Mchungaji wao kuwaombea kila wakati. Unapaswa kukaa kanisani
ambapo unapata maarifa ya kuomba mwenyewe,
kwa sababu hata huyo mchungaji
wako anakuwa na mambo yake binafsi ya kuombea, na hawezi kuanza kukuombea wewe
kabla ya yale ya kwake.
Andiko mojawapo la kukutia nguvu lipo katika YOHANA 14:30…[Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena,
kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.]….
Ina maana kwamba, huyo mkuu wa ulimwengu
hata kwako hana uwezo katika maisha yako. Kushindana watashindana nami, lakini
hawatanishinda. Kuwepo katikati ya mapambano siyo tatizo, kwa sababu hata mimi
ni mmojawapo wa wanaopigana. Vita vikiwa mbele yako havipo kwa ajili ya
kukuangamiza, bali kwa ajili ya wewe kushinda.
Msogelee adui
wa maisha yako, ndoa yako, biashara yako
n.k. siyo kwa sababu nyingine bali ni kwa Jina la Bwana wa majeshi. Usihesabu
matatizo uliyo nayo bali hesabu ushindi ulio nao ndani ya
Kristo. Imeandikwa “mateso ya mwenye haki ni mengi lakini Bwana humponuya
nayo yote”.
MHUBIRI
9:11…[Nikarudi, na kuona chini ya jua,
ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari
washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu
wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati
huwapata wote.]… Kuna wakati wa kila jambo ndani ya maisha
yangu. Maisha yako hayatakaa katika
ugumu wakati wote. Ndege akipita
juu ya kichwa changu siyo tatizo lakini
tatizo ni huyo ndege kutengeneza kiota chake juu ya kichwa changu. Ukiona mambo yanazidi kuwa magumu, jua kuwa
ushindi nao unakaribia.
Wanaokupiga vita wanakusaidia kwenda kutawala. Yuda Iskariote
kwa kumuuza Yesu Kristo alisababisha Yesu afe na baada ya siku ya tatu YESU akafufuka na kupewa JINA LIPITALO MAJINA YOTE. Siyo wakati
wa kumlaumu Penina, kwa sababu bila Penina hakuna Samweli. Hanna alimimina
maombi yake mbele za Bwana kwa sababu ya Penina kumchokoza. Eli hakuwahi kumuona Hanna akiomboleza, lakini baada ya kuinuka Penina ndiposa Eli
akakutana na Hanna na kumwambia “Bwana na akupatie haja ya moyo wako”. Nipo
kanisani kwa sababu ya Penina wa maisha yangu. Ni saa ya kukutana na Eli na
kumwambia Eli shida ya maisha yako.
Je ,umempokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa
maisha yako? Kama upo na hujaokoka, ni
saa yako kuanza upya kwa kuzaliwa upya .
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church inMorogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545