JUMAPILI: 28 JUNE 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:
Shetani
ana uwezo wa kugeuka na kubadilika, na kutumia maumbo au vitu tofauti kwa lengo
la kuwakamata watu ili wasifikie hatima zao. Shetani ana uwezo wa kugeuka na kufanana na
jiwe (ingawa yeye siyo jiwe) lakini kwa macho ya kawaida unaliona ‘jiwe’ kumbe
katika ulimwengu ule wa roho yeye siyo jiwe, amejigeuza tu. Anachofahamu
shetani ni kwamba, akija na kukaa ndani yako, atatolewa mara moja pale
unapoombewa ila akikaa ndani ya maumbo hayo au katika mavazi (nguo) wewe siyo
rahisi umbaini.
Shetani huwa na uwezo wa kujificha hata katika
mavazi bila wewe kujua. Unaweza kuwa unavaa nguo fulani na mara zote uzivaapo tatizo
huanzia pale. Katika kitabu cha MWANZO Mungu alishuka toka mbinguni
kuja duniani kwa lengo la kumshonea Adamu na Eva mavazi kupitia ngozi ya
kondoo aliyemchinja kwa ajili hiyo.
Mungu angeweza kumwambia Adamu afanye hiyo kazi, lakini unajua kwa nini
alifanya mwenyewe? Mungu pia alimwambia Musa amtengenezee Haruni mavazi
matakatifu. Kumbe mavazi yaweza kuwa matakatifu au kinyume chake.
Endapo maduka ya mavazi yapo mijini kote na wauzaji wake
wanawasha ubani kwa lengo la kuyalisha
mashetani chakula, kipi kinatokea uyanunuapo vazi la aina hiyo? Maana yake, wewe unaweza kulinunua vazi la aina hiyo bila kujua kuwa nguo hiyo ilikuwa inapuliziwa chakula cha majini na ukaona ni nguo nzuri tu, kumbe
haina uzuri wowote. Nyoka alipomuonesha Eva lile tunda, Eva kwa mara ya kwanza
alilitamani akasema linavutia na lafaa kula. Lakini hebu jiulize, kwani Eva
alikuwa mara zote halioni hilo tunda hapo bustanini?
Kwenye Biblia, Mavazi yaliponya watu. Yule mwanamke
aliyekuwa anatokwa damu, alilishika pindo la vazi la Yesu.
Kilichomponya siyo lile vazi, bali nguvu ya Yesu ilitoka kwake na kuingia kwenye
lile vazi. Bartmayo kipofu wakati wa uponywaji wake, alilitupa lile vazi mara
moja na papo hapo akapata uponyaji wake. Kumbe pengine lile vazi ndiyo lilificha shetani wa upofu wake
ule. Pale msalabani, nguo za Yesu
zilipigiwa kura, na siyo viatu vyake. Kwa
nini iwe hivyo? Tunaona katika Biblia watu wanatumia leso za mitume kama akina
Paulo na papo hapo wanapata uponyaji.
Nitajitoa je mimi nisivae hayo mavazi ya kishetani?
Kwanza utambue kuwa Shetani anaweza kutumia vitu unavyonunua madukani. Pili inabidi
ujue namna ya kuepuka au kufanyia
maombi vitu hivyo kabla ya kuvitumia.
Kila nguo unayoinunua kuanzia leo
hii inenee maneno ya Bwana. Weka neno la
Mungu katika hiyo nguo kabla hujaanza kuivaa. Kumbuka tunayo mamlaka kuliko wao. Imeandikwa “tumempewa mamlka
ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za Yule adui, wala hazitatudhuru”. Weka
maneno ya Mungu kwenye hizo nguo
unazonunua ili kwamba kila wakati utakapozivaa nguo hizo neno
la Mungu litangazwe.
Imeandikwa katika 2
KORINTHO 2:11…[ Shetani asije akapata kutushinda; kwa
maana hatukosi kuzijua fikira zake.]….Katika maisha yako
ya kila siku yapo mawazo ya shetani. Anaowaza shetani, hupanga pia mipango ya jinsi ya
kukukamata. Njia atakazotumia shetani
kukukamata wewe siyo hizo atakazotumia kumkamata mwingine.
AYUBU
1:6-10…[Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda
kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7 Bwana
akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema,
Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 8
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa
kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha
Mungu na kuepukana na uovu. 9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo
Ayubu yuamcha Bwana bure? 10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na
nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo
mali yake imeongezeka katika nchi.]… Shetani ni mtu wa
kufuatilia vitu na kuwaza jinsi ya kuwafunga watu. Mungu alitaka kujua kama
shetani amemuona Ayubu lakini majibu ya shetani na mawazo yake ni kuwa, ‘ee
Mungu ondoa ulinzi uliomwekea Ayubu’.
Shetani anajua uliinzi wa Mungu ukiondoka, mwanadamu hana chochote.
Inapaswa kujua kuwa, yapo mawazo ya shetani
yaliyo kinyume na wewe kila iitwapo leo. Saa imefika na saa ni hii, kila
wazo la kishetani kwenye maisha yangu,
kwenye ndoa yangu, kwenye kazi yangu au uzao wangu liteketezwe kwa Jina la
Yesu. Unaweza kuwa kwenye amani, ukiwaza kuwa upo salama lakini kile usichokijua ni kuwa lipo wazo baya la kishetani ambalo
linasogelea maisha yako au vitu vyako.
UFUNUO
2:24…[
Lakini nawaambia ninyi
wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za
Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.]….
Zipo fumbo za shetani. Shetani huwaletea watu vitu vinavoitwa ‘fumbo’. Ukiona
fumbo ujue aliyelitengeneza ni mtu mwenye akili sana. Mtu wa kufumbua fumbo
naye ni lazima awe na akili sana kumpita
aliyetengeneza fumbo. Shetani anapotengeneza
fumbo lake, anajua akilileta kwako siyo rahisi ulifumbue. Katika ndoa unaweza
kuona mambo usiyoyaelewa, lakini wewe bila kujua unaanza kuwawazia majirani au
marafiki lakini kumbe lile ni fumbo na hao unaowawazia siyo wahusika
wakuu. Ndiyo maana wengi
hukimbilia kwenye kutibu matunda ya tatizo badala ya chanzo cha matatizo
hayo. Mfano: Mtu anapotaka aombewe
kupata kazi, akidhani kukosa kazi ndiyo tatizo. Lahasha‼. Kukosa kazi siyo
tatizo ila ni tunda tu. Kipo chanzo cha
hiyo kukosa kazi ambacho inabodi kishughulikiwe.
Hebu jiulize, je shetani ananiwazia nini mwaka huu?
Vile vitu unavoviwaza kuvifanya mwaka
huu vimekaa je? Shetani katika hivyo vitu unavyowaza kwa mwaka huu amekuwazia
nini? Usipoweza kufahamu mawazo ya huyo
shetani juu yako, hata yale uliyopanga hayatatokea. Unaopopigwa na mawimbi makali, ni wakati wa kwenda kumuamsha Bwana ili
asimamishe mawimbi. Yupo aliyeleta mawimbi. Petro alijaribu njia zote kwa kuwa
alikuwa mtaalamu wa uvuvi na hivyo kwa yale mawimbi alivyoyaona, akasema hapana, huu ni wakati wa kumuamsha
Bwana na ndiye wa kuweza kuyanyamazisha. Mawimbi yanappokuja siyo kwa ajili ya
kukuangamiza, lakini uyaonapo, ni budi kutafuta alipokaa Bwana Yesu ili aje na
kuyanyamazisha mawimbi ili uende ng’ambo.
2
TIMOTHEO 2:26…[ wapate tena fahamu zao, na kutoka
katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.]…
Paulo haongelei mambo ya imani hapa.
Anaongelea mambo ya ufahamu. Mtu
akitengeneza mpango, inahitaji
mtu mwenye ufahamu na akili kugundua huu
ni mtego wa ibilisi. Kipo kifungo ammbacho kinahitaji tu akili
zako. Ukirudi kwenye ufahamu wako, utaenda kwa Yesu Kristo na kumweleza shida
yako ili tatizo lililopo litoweke kwa
Jina la Yesu. Wenye ufahamu wa dunia hawawezi kukupa akili ya kufanikiwa, ila
yupo mmoja tu mwenye uwezo huo, naye ni Yesu Kristo
1
YOHANA 5:18-20…[Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi
dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 19
Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. 20
Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba
tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani,
ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.]…
Dunia yote imekaa chini ya muovu lakini tumepewa akili za kuweza kuwatawala hao
waovu. Shetani anatamba kwa kukusumbua pale ambapo unakuwa hujitambui. Kile
usichokijua ni kuwa, hata boss wako anayekusumbua ofisini mwako unao uwezo wa
kumfunga nyumbani kwako na kumwambia ‘nyamaza kimya’. Cha kufanya ni kuyatiisha mapepo yaliyo ndani
mwake na kuyaamrisha ‘kuazia leo mnyamaze kimya’na lazima
yatakutii . Paulo kwa kujitambua, alimwambia Elima yulee mchawi maneno haya: MATENDO 13:11‘Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu
yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na
giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.’.Kila
adui yangu kazini au katika uzao wangu au katika maisha yangu napaswa kumuambia
‘uwe
kipofu’. Sifa kuu ya kipofu ni
kuwa hakioni kinachoendelea.
Ninayo pia mawazo ya Mungu, zaidi ya yale mabaya
anayoniwazia shetani. Imeandikwa katika YEREMIA
29:11…[Maana
nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya
mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.]…. Mungu
anakuwazia mema lakini adui anawaza
mabaya. Uonapo vurugu katika ndoa ujue siyo mawazo ya Mungu bali ni shetani.
Haya maovu ya shetani anayoniwazia,
ndiyo yanayonifanya niwe katika hali ngumu nisiyoitaka. Kiwanda
kikiungua zile bidhaa hazitengenezwi tena. Kiwanda kinachotengeneza vurugu,
shida na magonjwa ni cha mashetani. Leo
tunaingia kwenye hicho kiwanda na kukifunga kwa Jina la Yesu.
Leo ni siku ya kupiga X vibanda vyote ambavyo
mashetani wamevijenga kwenye njia yako ya ushindi na baada ya hapo kuwaagiza
malaika kazi ya kuchoma vibanda vyote vya adui zangu walivyojenga kwenye njia
zangu za mafanikio. Kama vile malaika alivyopita Misri usiku ule na kuua
wazaliwa wa kwanza wote wa Misri ambao alama ya damu ya mwanakondoo
haikuonekana kwenye milango yao, hata
sasa itakuwa vivyo hivyo kwa adui zako,
na kila kibanda walichojenga kwenye barabara yako, leo ni siku ya kupita na
kuweka alama ya X na malaika wa Bwana atafanya usafi kwa kuviondoa vibanda vyote vya adui kwa Jina
la Yesu.
Imendikwa “Kila pando
asilolipanda Baba wa Mbinguni litang’olewa” nami naamuru kwa Jina la Yesu, kila pando la
magonjwa, pando la umaskini, pando la
matatizo na mikosi lazima yatoke kwa Jina la Yesu. Gideoni alipoliona tatizo ni nyumba ya miungu aliibomoa, na watu
walipomfuata baba yake mzazi ili kutaka
kumwajibisha, Yoashi babaye aliwajibu yafuatayo: WAAAMUZI 6:31…[Yoashi akawaambia
watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi?
Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi
yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake..]…. Kama
shetani anaweza kujitetea na ajitetee.
Leo tutabomoa madhabahu za kishetani na vibanda alivyojenga kuziba
mafanikio yetu na kama shetani anaweza kujitetea na ajitetee.
UKIRI
Kila wazo la kishetani lililokaa kunionea leo nalishambulia kwa Jina la Yesu. Shetani
aachia maisha yangu kwa ina la Yesu.
Wote wananifuatilia na mawazo ya giza leo nawashambulia kwa Jina la
Yesu. Amen
|
Kuokoka kwa kumpokea Yesu Kristo maishani mwako kuwa
Bwana na Mwokozi wako ni hatua ya kwanza
ili kuweza kupokea kibali cha Bwana na kuwashinda adui zako wote ambao leo tunawashughulikia.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church inMorogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545