JUMAPILI: 12 JULY 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:
Hivi
kiapo ni kitu gani? Na kwa nini watu wanaapa? Kwa muhtasari, kama kiapo hakina
mahusiano yoyote na Mungu au na wanadamu, hakuna ambaye angekifanya. Mungu naye
huapa, na wanadamu vivyo hivyo. Imeandikwa katika EBRANIA 6:16-17…[Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na
kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. 17 Katika
neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri
yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;]….Maana
yake, mtu aapo anaweka rehani uhai wake. Ni kuyaweka
maisha yako katika kile unachokiapia.
Kumbuka kuwa uhai wa mwanadamu ndicho kitu cha thamani kuliko vyote alivyo navyo. Ndiyo kusema kwamba, endapo mwanadamu hana uhai ni sawa na ‘takataka’ tu.
Tunasema hivyo kwa sababu ukeshachimbia shimo kitu na kukiweka huko, maana yake
kile ulichokiweka huko ni takataka tu.
Kiapo ni njia ya mwisho kuliko zote aitumiayo mwanadamu
kuondoa mabishano. Mtu umkutapo anaapa, huapa kwa jina la wazazi wake au jina
la miungu yake. Kwa nini iwe hivyo: ni
kwa sababu wazazi ndio walio wakuu kuliko wote kwa maisha ya huyo mtu. Endapo
mtu ataapa kwa jina la Mungu, nayo itategemea, je huyu mtu ameapa kwa Mungu wa herufi ndogo
(mungu, ambaye pia ni shetani) au MUNGU wa
Herufi Kubwa (yaani Jehovah).
Katika ulimwengu wa roho kiapo ni kitu cha thmani
sana. Unaposema ninaapa, maana yake unajiweka kwenye nafasi ya hicho kitu. Tunaona
kuwa Mtu anapodhamiria kuapa anayaweka maisha yake rehani. Mtu afanyapo kiapo, atahakikisha kuwa maisha yake yule aliyemdhamiria katika hicho kiapo hayatakaa
sawa hata kidogo.
Imeandikwa hivi katika MARKO 5:2-7 ..[ Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu,
ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale
makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;
4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile
minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za
kumshinda. 5 Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani,
akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa mbali,
alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini
nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.]….
Ukisoma maandiko, Huyo ndiyo pepo pekee aliyehojiana na Yesu Kristo. Pia ndiye
pepo pekee ambaye Yesu Kristo alimuuliza jina lake ni nani? Kilichomfanya atoe
ruhusa ya hao pepo kuwaingia wale nguruwe ni kwa sababu alimwapisha Yesu Kristo
kwa Mungu. Pepo hili lilijua ‘nguvu ya kiapo’. Washirikiana nao
wanaijua hii nguvu ya kiapo, na ndiyo maana huifanya afya ya mtu isiwe nzuri,
au maisha yake kwa sababu kuna watu walioweka
kiapo mahali fulani. Kumbuka kuwa, kiapo
kinapofanywa, walinzi wa kiapo nao huwekwa ili kusimamia hicho kiapo.
Kafara ya kiapo hutofautiana kulingana na ukubwa wa
kile kilichotolewa. Kafara ni kama
sadaka ambayo hchinjwa (kuku,
kondooo,mbuzi, ng’ombe au ikizidi sana mwanadamu). Damu ya hizi kafara
zikiwamwagika, huongea zikiwa ardhini. Ndiyo maana Biblia inasema ‘Damu ya Yesu hunena mema juu
yetu’. Hata Pilato alipokuwa akimhukumu Yesu Kristo, alinawa
mikono yake na kusema ‘Damu ya mtu huyu hainihusu’. Leo hii tupo huru kutokana na kafara ya
Kalvari ya Damu ya Yesu Krsito. Endapo hii Damu
ya Yesu hadi leo inanena mema juu yetu, je, hizi kafara za waganga wa
kienyeji na wachawi wanazotoa kwa ajili
yako zinanena kitu gani?
Wakati mwingine maisha yetu hayaendi vizuri kwa
sababu ya kukamatwa na viapo. JOSHUA
6:26…[Naye
Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu
yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa
kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa
kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.]…. Joshua aliweka
kiapo hiki kwa Jina la Bwana, Mungu aliye mkuu kuliko wote. Ni kitu gani kilitokea kwa wale walioinuka kuujenga huu
ukuta baada ya muda mrefu sana kupita tokea kuwekwa kwa hiki kiapo? Imeandikwa
katika 1WAFALME 16:34 ….[Katika siku zake,
Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu
mzaliwa wake wa kwanza na kuyaweka
malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana
alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.]…
Kile kiapo kilikuwa hai, ingawa wale
waliokuwepo wakati Joshua anaapisha wale watu walikuwa walishakufa. Kiapo
chaweza kuwa hai, na kufuatilia maisha ya mtu wakati wowote ule. Katika familia
zetu za Kiafrika, mambo mengi hayaendi kwa sababu vipo viapo ambavyo mababu zetu walivifanya, na usipokuwa
makini kujitoa humo, utaendelea na aina
hiyo ya maisha magumu.
Zipo koo
ambazo mapatano yalifanyika zamani sana
bila wewe kujua. Inawezekana kweli hujawahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, lakini unajua je kama babu au bibi
yako hakuwahi kwenda kwa hao waganga wa kienyeji? Pengine
babu yako aliweka mapatano hayo enzi
hizo na waganga wa kienyeji, na kwa
sababu hiyo familia yako inaendelea kufuatiliwa. Chale zifanywazo na waganga wa
kienyeji ni mojawapo ya aina za viapo.
Ni kwa sababu damu ni uhai (kwa mujibu wa Biblia). Kila damu ina vinasaba
(DNA), na pale waganga wakizichanganya, hufanya watu wa aina hii kupitia maisha
yasiyokuwa yao.
Katika familia zetu kuna uwezekano wa mmoja wapo kuunganisha
hiyo familia na kuzimu. Katika wale 12 wanafanuzi wa Yesu Kristo, mmojawao alikuwa ni shetani. Watu
wanaweza kuweka mapatano na kuzimu.
Pengine afanyaye hayo yote atakuwa tayari kukusaidia kwa kila jambo, ili
usimgundue. Miili yetu hii ni sawa
na majumba tu. Kumbuka ukiwa na nyumba
unaweza kuwa ndani ya hiyo nyumba au ukawa nje ya hiyo nyumba. Katika ulimwengu
tuliopo sasa, usiamini mwanadamu wa nje,
ila muhimu ni ile roho ndani mwake, kwa sababu mtu ni roho na siyo mwili.
Kipo kiapo ambacho mababu zangu au baba yangu
alikifanya, leo ni saa ya kuvivunja
hivyo viapo vyao kwa Jina la Yesu. Sikuja hapa duniani hivi hivi, na hata mimi
ninacho kiapo changu. Imeandikwa katika 1WAFALME 2:43…[Mbona basi hukukishika kiapo cha Bwana,
na amri niliyokuagiza?]… Kumbe basi kipo KIAPO CHA BWANA. Kama wao walienda kwa mizimu na kuapa, hata mimi
ninao uwezo wa kuweka kiapo na Bwana, kwa sababu kiapo huondoa mabishano. Ni
wakati wa kuondoa ubishani. Kiapo cha Bwana kitakomesha kila balaa ndani ya
maisha yangu. Kumbuka kuwa, Mungu wetu anapoapa huapa kwa nafsi yake mwenyewe. Siyo kama miungu ya dini zingine
ambayo huapa kwa vitu vilivyoumbwa.
Uonapo dada yako ana matatizo yanayofanana na wewe,
jiulize kwa nini iwe hivyo wakati ninyi
wawili mpo tofauti? Unapomuona kaka yako ana matatizo yanayofanana na wewe,
jiulize kwa nini iwe hivyo wakati ninyi
wawili mpo tofauti? Haya yote yametokea kwa sababu kuna kiapo mahali fulani na
wapo waliokaa kwenye hico kikao cha kiapo na kusababisha hayo uyaonayo yaendele
kutokea. Ni saa ya kukata kila mnyororo wa kiapo kwenye familia yako. Ni saa
ya kutoa kiapo na kuweka kiapo.
WAEBRANIA
7:20….[
Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,]….
Hakuna kitu kilichofanyika pasipo kiapo.
Na ndiyo maana ili Mungu atende jambo, aliapa. Maana yake, mambo yangu pia
hayafanikiwi kwa sababu hakuna kiapo.
Endapo hakuna kiapo, maisha yako yanakuwa na matatizo. Ndiyo maana hata
shetani alishindwa kumgusa Ayubu kwa sababu kati ya Mungu na Ayubu palikuwepo na KIAPO. Cha wewe kufanya ni kuamua yafuatayo:- Sina msamaha na mchawi anayeniwangia usiku. Biblia
inasema, “usimwache
mwanamke mchawi kuishi”. Kumbuka
Mungu huyuhuyu ni Yule aliyesema “usiue”, lakini kwa habari ya wachawi na washirikina Mungu ameruhusu
wasiishi, maana yake wauawe.
Israeli waliongozwa usiku na mchana, bila hata adui
mmoja kuwasogelea wakati wanaenda zao nchi ya Ahadi. Lile wingu lililowaongoza
mchana, kwa sababu ya kile kiapo cha
Mungu na Ibrahimu kwamba uzao
wake atawapa hiyo nchi. Hata kwa sasa, kinachowafanya Israeli wakae salama
ni kwa sababu ya kile kiapo walichokifanya, kwa kusema “Damu yake (Yesu) iwe juu yetu na juu ya kizazi chetu”.
Ingawa hawakujua wasemacho, hata sasa Damu ya Yesu inazidi kunena mema juu yao. Daudi alikosea kwa kuwahesabu Israeli
yote, na adhabu ambayo Mungu alimpatia
achague mojawapo ya hizi zilivyoandikwa katika 2SAMWELI 24:13-14 … [ Basi Gadi
akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie
katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku
wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa,
ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.14 Naye Daudi akamwambia
Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa
Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa
wanadamu.]… Maana yake ni kuwa, nchi yote ya Israeli ilikuwa iadhibiwe
kutokana na kosa la Daudi kama kiongozi
wao. Endapo vipo “Viapo vya Kishetani” vilivyowekwa na viongozi wa serikali yetu leo
lazima tuvivunje kwa Jina la Yesu. Viapo vya kishetani vilivyowekwa na Serikali
ya Awamu ya Kwanza, au Awamu ya Pili au Awamu ya Tatu au ya Nne lazima
tuvivunje kwa Jina la Yesu.
Je, umemwamini
Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako? Huwezi kuweka kiapo na Mungu
ambaye hujapatana naye. Unapoamua kuokoka unakuwa kwenye nafasi nzuri ya
kuvunja viapo vyote vivlvyowekwa kinyume nawe, na utaweza kuweka kiapo na Bwana
Mungu, aliye Mungu Mkuu kuliko
miungu yote, kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Kuanzia sasa kila kiapo cha giza
niachie, wote walioshika afya yangu, au maisha yangu leo nawasambaratisha kwa Jina la Yesu. Viapo
vyote vilivyofanyawa juu ya maisha yangu naviharibu kwa Damu ya Mwanakondoo. Amen
|
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545