JUMAPILI: 02 AUGUST 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Na:
BRYSON LEMA (RP) &
Dr. GODSON I. ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Wapo
Wafilisti waliomuonea Samsoni, kwa kuwa tu walishazoea sana kuwaonea wana wa
Israeli, wakiwaona ni wanyonge na wa kawaida, na hivyo wakawafanya wanavyotaka.
Kwa kipindi kirefu hali hii iliendelea,
na wana wa Israeli wakaizoea. Hatimaye Mungu
alimweka shujaa mmoja wa familia ya Manoa, ili aje kuwaokoa watu wake Israeli.
Imeandikwa katika WAAMUZI 15:9-11 kwamba...[Basi Wafilisti wakapanda
wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. 10 Watu wa Yuda
wakasema, Mbona mmekuja kupigana nasi? Wakasema, Tumepanda ili kumfunga
Samsoni, kumtenda yeye kama alivyotutenda sisi. 11 Ndipo watu elfu tatu wa Yuda
wakatelemka hata ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya
kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia,
Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao.]…
Wafilisti wanaonekana kuijua kanuni hii muhimu: “ Ukitendewa na wewe lazima
uwatende”. Ndiyo maana watu wa Yuda walimfuata Samsoni kumuuliza kwa nini
amefanya vile alivyofanya, kwa sababu wanajua kuwa na wao watafanyiwa vivyo
hivyo‼. Hata wewe hapo ulipo siyo mpango
wa Mungu kupitia kile unachopitia katika maisha yako. Siyo kwamba Mungu alitaka
uishi jinsi unavyoishi. Hata vile ulivyo
navyo usiridhike ukadhani ndivyo alivyokusudia Mungu uwe navyo, la hasha‼!
Shetani
ndiye aliyekuja na kukunyang’anya ile hati miliki yako, ili upitie yale
unayopitia leo hii au umiliki vile uvimilikivyo
leo hii.
Kwa siku ya Leo hatujaja kanisani kwa ajili ya
kusali, kama yupo mtu mwenye fikra hizo amekosea‼!. Leo tumekuja kanisani ili
kuwatenda wale waliotutenda maishani kwetu. Unapoiona ndoa yako haiko sawa,
siyo kwamba mumeo au mkeo ndiye mbaya.
Kuna kitu‼! Unapomuona mwanao hafanyi vizuri darasani pamoja na kumpeleka
tuition siku zote, ujue kuna kitu‼! Adui ndiye amekuingizia kitu hicho, na
usikubali kusema eti hiki ni kitu cha kawaida katika familia au ukoo wako. Kila
kitu kina chanzo na mwanzo wake. Hakuna ugonjwa
ambao utamwelezea daktari halafu aseme eti ni ugonjwa mgeni usio kuwa na
chanzo chake.
Kila unachopambana nacho sasa hivi ujue kina mwanzo
wake. Wana wa Israeli walifahamu kabisa
wapo watu wanaopambana nao kila wakati. Ndiyo maana wakamuuliza Mungu swali,
kuwa kwa kuwa Yoshua amekufa, ni nani atakayewaongoza kwa ajili ya kupambana na adui zao? Imeandikwa WAAMUZI
1:1…[Ikawa baada ya
kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani
atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?]…
Cha msingi hapa ni kwamba wana wa
Israeli walitambua kuwa wana adui na adui
yao ni nani‼ Hata wewe na mimi, kama Mkristo inabidi ufahamu kuwa katika maisha ya kila siku, lazima uwe tayari
kupigana na pia kumjua adui yako ni nani unayepigana naye.
Sihitaji kumtafuta adui yangu ni nani‼ Ninachotakiwa
kufanya ni kulipiga tatizo, na nikimuona yupo anayelia papo hapo nitafahamu kuwa ndiye chanzo cha
tatizo langu. Hii ni kwa sababu, ya ile
kanuni kuwa ‘ukienda kumfungua punda
aliyefungwa, atakayekuja kukuuliza kwa nini unamfungua ujue ndiye mwenye punda’. Hatuhitaji kuwa kama wapiga ramli. Sisi
kazi yetu ni kupiga tatizo na
atakayefungua mdomo kulia tutajua ndiye alikuwa mmiliki wa lile tatizo‼!
Pamoja na shida iliyosimama mbele yangu, Kanaani
tunaingia. Pamoja na ugonjwa uliosimama mbele yangu, Kanaani nitaaingia. Pamoja na Bahari ya Shamu iliyosimama mbele
yangu, Kanaani tunaingia…. Tumechoka kwenda makanisani na kuagwa kwa kuambiwa “Amani ya Bwana iwe nanyi”…. Lakini hata
hivyo, ukutanapo njiani na mganga wa kienyeji atakuwa anakucheka. Kwa nini? Kwa
sababu huyo mganga wa kienyeji amefanikiwa kukuchezea usiku kucha, na hivyo
amani uliyopewa kanisani hauna. Je, ni nani
mbabe kati yenu wawili? Ni dhahiri mbabe ni huyo mganga wa kienyeji.
Inafaa ifike wakati ambapo hata mganga wa kienyeji awe anakiri mbele za watu
kuwa “Mungu unayemtumikia siyoMungu wa kawaida‼” Leo ni siku ya
kupambana na wale waliotutenda, nasi tuwatende vivyo hivyo.
Leo tumejipanga kupambana na adui yetu katika maeneo
matatu:
1. Kwanza
ni AFYA,
kwa kuwa adui anajua kuwa mwili wako
ukiwa mgonjwa, hauwezi kupigana. Magonjwa siyo mpango wa Mungu. Kila ugonjwa
umetengenezwa na shetani kuzimu. Lazima umnyang’anye shetani afya yako
asiimiliki. Wapo wanaopata mishahara yao tena mikubwa tu, lakini yote huishia kwenye matibabu ya watu wa nyumbani mwao. Unaposikia CHUMA
ULETE, siyo rahisi kuelezea kwa jinsi
ambavyo magonjwa ya kutengenezwa yanapotokea, na kusababsiha fedha iishie
kwenye matibabu‼‼. Shetani hana mamlaka ya kufunga kule mbinguni, ila uwezo
wake ni wa kukufunga hapa duniani tu. Hata hivyo wewe unayo mamlaka ya kufunga mambo yote ya shetani hapa duniani
na hata mbinguni yawe yamefungwa vivyo
hivyo. Imeandikwa katika 2WAKORINTHO 10:4-5…
[(maana silaha za vita vyetu si za
mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo
na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara
kila fikira ipate kumtii Kristo;]… Tunayo mamlaka ya kuangusha
kila kazi za kishetani zipate kumtii Kristo.
UKIRI
Kila kiwanda cha kutengeneza magonjwa, leo nakiunguza kwa Damu Ya Yesu. Kila adui anayetaka kurudisha kiwanda hiki
namtangazia kifo kwa Jina la Yesu. Amen
|
2. Sehemu
ya PILI ambayo shetani hufuatilia maisha ya watu ni katika MAFANIKIO.
Wapo watu wasiopendelea kuona mafanikio yako. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 4:40…[ Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru
leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi
katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele.]…. Ni mpango
wa Mungu ufanikiwe, wewe na uzao wako. Shetani kazi yake ni kuzuia mpango wa Mungu usifike. Leo ni siku
ya kudai chako, na vile vya kwao, pia
tunavidai view vyetu kwa Jina la Yesu‼‼ Wale walioiba kipato chako kwa muda wa
kutosha, leo ni siku ya kuwafanya kama walivyokufanya wewe. Leo
tunawagusa tu waliotugusa, ambao
hawajatugusa leo hatuwagusi kamwe kwa Jina la Yesu.
Mungu alisema
“Ahabu lazima afe”. Hata hivyo, Ahabu
aligoma akasema hatakufa. Walipoenda vitani, Ahabu alitumia ujanja/hila kwa kuyavua
mavazi yake ya ufalme, na kumvisha Yehoshafati.
Wakiwa vitani, askari walikuwa wameagizwa wamtafute mfalme Ahabu pekee na kumuua. Hata hivyo, Yehoshafati
hakujua kitendo cha kuvaa mavazi ya Ahabu kingemfanya awindwe na kufa vitani. Walipomfuata
Yehoshafati wamuue, ilibidi Yehoshafati apige kelele aseme yeye siye Ahabu. hata
hivyo, Kijana mrusha mshale, alifanikiwa kuurusha mshale angani, na ulipokuwa unarudi ili kutua ardhini ulienda
moja kwa moja kumtafuta Ahabu alipo na kumuua‼‼! Hii ni saa ya kurudishiwa
vilivyo vyetu. Tena Biblia inasema “mwizi akikamatwa, atarejesha mara saba”.
UKIRI
Ninakivunja kiwanda cha umaskini, Kwa Damu ya
Mwanakondoo. Leo najiondoa kwenye orodha ya maskini wa Taifa hili Kwa Damu
ya Mwanakondoo. Kwa Jina la Yesu, leo naushika mshale, maana imeandikwa Elisha alipokuwa anaumwa,
Yehoashi mfalme wa Israeli akamwendea, naye Elisha akamwambia “Rusha mshale, na
unapourusha sema hivi ‘Mshale wa Bwana, Mshale wa Kushinda” (2 Wafalme 13:14-19)…. na mimi leo natangaza mshale wa Bwana mshale wa kushinda. Na mimi leo naachia mshale wa
kuangamiza kila kiwanda cha umaskini, leo nakishambulia kiwanda cha umaskini
kwa Jina la Yesu. Ewe adui mwenye kiwanda nakutangazia kuwa sitakuwa maskini kamwe
Kwa Damu ya Mwanakondoo. Amen.
|
3. Eneo
la TATU la kushughulikia ni kwenye VIFUNGO, ambavyo kwavyo unakuwa unavipitia bila kujua. Maisha
yanakwenda kwa ugumu kwa sababu ya vifungo maishani mwako. Hata Lazaro baada ya
kufufuka, Biblia inasema alikuwa
amefungwa miguu yake na leso usoni mwake. Maana yake ni kuwa,
unaweza kweli kuwa umeokoka,
lakini kumbe umefungwa na hivyo
maisha unayopitia ni ya ugumu ugumu tu. Leo ni siku ya kuwafanya kama
walivyotufanya sisi. Kila aliyenifunga, nami
namfunga. Imeandikwa, “Nitakachounga hapa duniani na mbinguni kitakuwa kimefungwa”
UKIRI
Kwa Damu Ya Yesu, leo nafanya vita kukata kila kamba iliyonifunga
viungo vyangu vya mwili. Ewe adui uliyenifunga leo
nakuteketeza kwa moto wa Damu ya Mwanakondoo. Kuanzia sasa, nimetoka mautini
naingia uzimani kwa Jina la Yesu. Amen
|
Zipo sababu ambazo waganga wa kienyeji na wachawi
huzitumia ili kufanikisha mambo yao ya kuwatenda watu wengine kaatika maisha.
Mojawapo ni hizi sababu zilizoandikwa katika MALAKI 3:7…[Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala
hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami
nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa
namna gani? ]… Mtu yeyote anayeampenda Yesu lazima akimbilie kwa
Yesu. Huwezi kumtenda adui yako kama alivyokutenda kama hujamrudia Bwana Yesu. Leo tunataka tumrudie Bwana Yesu ili
tuweze kuwapiga wale waliotuonea.
Pia imeandikwa katika MALAKI 3:8-9….[Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini
ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi
mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
]… Kumbe kitendo cha kumuibia Mungu
kinaitwa ‘laana’. Sasa ili kuziepuka laana hizi, kila mmoja wetu
anatakiwa kulipa zaka na dhabihu zote
kwa Bwana.
Kumtolea Mungu zaka na dhabihu ni njia mojawapo ya
kumfanya shetani akose uthibitisho wa kukushtaki au kukulaani.
Imeandikwa katika MALAKI 3:10-12…[Leteni zaka kamili ghalani, ili
kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa
majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni
baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu
nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu
hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana
wa majeshi. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya
kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.]… Zaka ni kodi ya Mungu.
Chakula katika nyumba ya Bwana siyo ubwabwa, ila ni neno la Mungu. Hivyo kwa kutoa zaka, ni ili kuwezesha neno la Bwana liweze kuhubiriwa kila mahali.
Kwa wewe ambaye hujaokoka, leo ni fursa muhimu sana kufanya
maamuzi hayo ili uweze kuwatenda wale waliyotenda mabaya maishani mwako.
KWA
SIKU TANO ZOTE WIKI NZIMA TUTAFUNGA NA KUOMBA
ILI
KUWATENDA ADUI ZETU SAWASAWA NA WALIVYOTUTENDA SISI.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545