JUMAPILI: 26 JULY 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:
Katika
maisha ya kila siku,tunapita katika vitu vigumu na vizito. Ulalapo usiku, huwa unamshukuru Mungu kwa sababu siku kama
ile maishani mwako haijirudii tena. Hata hivyo imeandikwa katika 2WAFALME
18:19 kwamba…[Yule amiri akawaambia, Haya, mwambieni Hezekia, kusema,
Mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia?]…
Hata sisi ndivyo ilivyo kwamba kuna nyakati tunajiona hatufai tena. Ujue kuwa tatizo
lako halipo kwenye ile shida uliyo nayo, bali lipo kwenye ‘tumaini’ ulilo nalo
maishani mwako. Jambo la kwanza ni kubadilisha mtizamo wako, bila kuhesabu
idadi ya miaka yako kwenye wakovu. Yesu Kristo alipoambiwa na Shetani ageuze
jiwe liwe mkate, alimjibu shetani kuwa “mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo kinywani
mwa Mungu”. Weka macho
yako kwenye tumaini lako.
Tatizo ulilonalo ni dogo mno bali tatizo lipo kwenye tumaini unalolitumainia. Musa hakuona Bahari ya Shamu kama kikwazo chake, kwa sababu ile bahari haikuwa pale kwa ajili ya kumuangamiza. Wana wa Israeli waliotoka Misri walikuwa ni wengi sana, lakini ni wawili tu waliofika nchi ya Ahadi, (Joshua na Kaleb). Siyo kwamba watu hawa wawili hawakuwaona wale manefili, lakini kilichowasaidia ni kuwa na tumaini kwa Mungu wa Israeli. Watu hawa wawili waliweza kwa sababu tumaini lao lilikuwa kwa Mungu. Tumaini lako umeliweka wapi? Je, unamwekea tumaini ndugu yako kwa sababu amesoma sana? Kumbuka kuwa, Mungu huyo huyo aliyewaokoa wana wa Israeli ndiye aliyewaangamiza pia wale Wamisri.
Tatizo ulilonalo ni dogo mno bali tatizo lipo kwenye tumaini unalolitumainia. Musa hakuona Bahari ya Shamu kama kikwazo chake, kwa sababu ile bahari haikuwa pale kwa ajili ya kumuangamiza. Wana wa Israeli waliotoka Misri walikuwa ni wengi sana, lakini ni wawili tu waliofika nchi ya Ahadi, (Joshua na Kaleb). Siyo kwamba watu hawa wawili hawakuwaona wale manefili, lakini kilichowasaidia ni kuwa na tumaini kwa Mungu wa Israeli. Watu hawa wawili waliweza kwa sababu tumaini lao lilikuwa kwa Mungu. Tumaini lako umeliweka wapi? Je, unamwekea tumaini ndugu yako kwa sababu amesoma sana? Kumbuka kuwa, Mungu huyo huyo aliyewaokoa wana wa Israeli ndiye aliyewaangamiza pia wale Wamisri.
Tumaini ni kama usukani ndani ya mwanadamu. Hivyo
bila tumaini huwezi kwenda. Wengi akili zetu zinakuwa zimetengeneza picha,
inaweza ikawa "picha za kushindwa au kushinda". Maisha ya mwanadamu ni kama
msafiri na dereva uliye naye ni tumaini ulilonalo je litakufikisha salama.
Unapokuwa na tumaiani ndani ya Yesu Kristo haijalishi tatizo ulilonalo. Angalia
maisha yako ni kwanini hofu na mashaka zimejaa ndani yako? Ni kwa sababu
umekosa tumaini katika maisha yako.Hata Yesu Kristo hakuwaponya wagonjwa
wote. Yesu alikuwa anaangalia tumaini la
mtu lipo wapi. Shetani hupenda sana
kuchenzea akili za watu kwenye eneo la tumaini.
Imeandikwa katika ISAYA 12:2…[Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa; Maana
Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.]… Isaya anasema Mungu ndiye
tumaini lake naye hataogopa. Anasema hivi kwa sababu hofu ndio kitu cha kwanza kinachoondoe
“tumaini”. Siri kubwa ya shetani ni kukuingiza hofu, ili zipeperushe kila tumiani la watu kwa
Mungu. Ili kushinda tatizo siyo
kulikimbia tatizo, bali ni kupita katikati ya hilo tatizo. Vita
vikiinuka kazini, suluhisho siyo kukimbia hiyo kazi, bali mtafute
aliyesababisha tatizo na kushughulika na ile roho ya hilo tatizo ndani
mwake. Kulikimbia tatizo siyo ushindi
dhidi ya hilo tatizo, bali ni sawa na kuahirisha hilo tatizo. Mungu
tunayemtumikia sisi anataka tupambane na adui zetu na siyo kuwakimbia.
Unapotaka kuitwa mpiganaji, lazima upigane. Ili uitwe shujaa ni lazima
upambane.
Mtu yule anayepigwa ngumi ndiye anayejua uzito wa
ngumi.Tunaona wana wa Israeli walipo uzunguka ukuta wa Yeriko bila wao kujua
kila siku walipozunguka walikuwa wanarusha ngumi, na siku ya saba ilipofika
ukuta ukaanguka. Na ulipoanguka Yoshua akasema na alaaniwe atakaye jenga tena huu
ukuta. Kumbe ukuta unapoanguka laana hutolewa palepale. Hivyo hata wewe rusha
ngumi juu ya adui zako. Kila unaporusha ngumi misuli yako inabadilika na inakuwa
si ya kawaida, ni kama Samson alivyowekwa gerezani na kuanza kusaga ngano, Kila
siku alipokuwa akisaga ngano kulimpa nguvu na uwezo misuli kukua. Tunaona siku
aliyoangusha nguzo aliweza kuuwa watu wengi mno kuliko kipindi cha nyuma.
Yesu Kristo aliliweka tumaini lake kwa Mungu, na
ndiyo maana akiwa pale msalabani alimwambia Yule mwizi kuwa “Hakika, leo hii tutakuwa wote
paradiso”. Imeandikwa katika YOHANA 14:1-3…[Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana
naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja
tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.]… Usiweke
tumaini lako kwa mwanadamu, bali kwa Yesu Kristo, ambaye alisema anaenda
mbinguni kuandaa makao, ili alipo yeye
na wewe uwepo. Ni Yesu
pekee aliyesema alipo yeye anataka na wewe uwepo, hivyo ndio mtu unayetakiwa
kumtumainia. Ukimtumainia Yesu atakupa unacho hitaji.
Kuna msemo unasema aliyeshiba hamwangalii mwenye
njaa. Hivyo usitegemee kusaidiwa hata na ndugu yako maana anaweza asikusaidie.
Acha kumtumainia mwanadamu maana inapotokea hatari atatafuta usalama wake
kwanza na baada ya hapo ndipo ataangalia kama kuna nafasi kwa ajili yako ili
akusaidie.
Siri ya mkristo wa kweli ni kupigana. Utaona Bwana
asema, Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndio jina lake. Pia anasema hiki ndio chuo
cha vita. Hivyo kama mkristo ni lazima uingie kwenye chuo cha vita na upigane.
Pale unapokuwa na shida ndipo mahali Mungu anajitokeza. Tunaona hata Musa
alipokuwa kwa Farao penye raha, Mungu hakuweza kusema naye lakini tunaona Mungu
aliweza kusema naye kwenye kichaka mahali ambapo hapakuonekana kama panafaa.
Hivyo inatakiwa tatizo ulilonalo ng’ang’ania hapo hapo pambana na upigane. Hilo
tatizo lililoko mbele yako ni la kupiga, haupaswi kuliogopa. Unapoiona dhahabu,
ujue upo mwamba mgumu ulipasuliwa hadi ikapatikana. Unapoona mtu amefanikiwa
ujue mtu huyo amepambana hadi amefanikiwa. Hivyo ili ufanikiwe ni lazima
upambane.
Kuna vitu viwili kwa mwandamu miaka na hatma.
imeandikwa katika YOHANA 17:1-4.. [Maneno hayo aliyasema Yesu;
akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika.
Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2 kama vile ulivyompa
mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu
Kristo uliyemtuma. 4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile
uliyonipa niifanye.]… Tunaona Yesu anasema Baba kazi yako uliyonipa
nimeimaliza. Ina maana alikamilisha ile hatma yake baada ya miaka ile kuisha.
Tunaona wana wa Israeli walikaa utumwani miaka 430 badala ya 400 ili kwenda
Kanaani, NCHI YA AHADI, kwa sababu hawakujua muda. Ila baada ya Mungu kusikia
kilio chao ndipo alipowatoa utumwani. Hivyo nawe ni lazima umlilie Bwana ili
asikie kilio chako.
Kazi kubwa ya shetani ni kukufanya uogope. ZABURI 20:7…[Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja
jina la Bwana, Mungu wetu.]…. Ukilitaja jina la Bwana Mungu wa
majeshi, utakuwa na ushindi katika safari ya maisha yako. Ukitaka kuwa mfalme
kama alivyokuwa Daudi, usitaje magari wala farasi bali taja jina la Yesu.Daudi
akasema toka ujana wake hadi uzee hajawahi kumuuona mwenye haki akitangatanga
na kuomba barabarani. Hivyo tumaini lako liweke kwa Yesu maana hata kuacha
uaibike.
Endapo Mtu hujaokoka, leo ni fursa nyingine kwa wewe kufanya maamuzi hayo, ili uweze kupata ushindi sawasawa na ahadi za
Mungu maishani mwako.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church inMorogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545