JUMAPILI: 09 AUGUST 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Na:
BRYSON LEMA (RP) &
Dr. GODSON I. ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Imeandikwa
katika YEREMIA 17.18…[Na waaibike watu
wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione
hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.]
..Katika maisha ya kila siku kuna vitu
huwa vinaibuka maana kuna watu wanataka wewe uaibike. Kuna watu wamekaa vikao
na wanataka wewe uangamie na uende kuzimu, lakini leo hayo maangamizi na hiyo
aibu inarudi kwao. Bwana anasema hiyo aibu itapiga kona na kurudi kwao
walioituma, maana unaye dereva Yesu Kristo anayeendesha maisha yako. Jehova
anasema yeye ndiye dereva anayeendesha maisha yako haijalishi aibu waliyokuwekea
maana yeye alikujua toka tumboni mwa mama yako na akakutakasa. Usihofu maana
dereva uliyenaye yupo macho halali anazunguka kuangalia adui zako naye anafanya
njia mahali pasipo na njia katika maisha yako. Haijalishi tatizo lako limekaa muda gani na nani aliyelitengeneza
maana ninachojua sitaaibika maana imeandikwa “achimbaye shimo atatumbukia
mwenyewe na ategaye mtego utamnasa mwenyewe”. Tunaona Goliathi alipoyatukana
majeshi ya BWANA, Daudi alipoenda hakuangalia ni nani, ndipo akasema ni “nani
anayeyatukna majeshi ya Bwana”. Ndivyo Bwana anavyosema kwako pia ni
nani anayekutukana, ni nani anayekuletea aibu‼.
Mungu tunayemtumikia hawezi kukuacha uangamie,
lakini mwanadamu anataka uangamie maana anachora michoro ili uangamie na
uaibike, lakini tunaye dereva Yesu ambaye atakuongoza. Umefika
mahali unaona kila mtu anakupinga na kukuambia kwa nini unaenda kusali mbali,
wasichokijua ulikuwa na dereva Yesu aliyekuongoza kuja katika Bonde la Maono,
Ufufuo na Uzima. Adui amekaa ili uaibike lakini Bwana anasema hiyo aibu
haitakupata. Pamoja nao wamekesha usiku kucha lakini kila wanachokifanya hakitakupata bali
kitawarudia wao na uzao wao, maana maandiko yanasema “Bwana asipolinda mji waulindao
waulinda bure”. Umesahau yupo wapi Yule Siseri aliyekuwa na magari ya
chuma na yupo wapi mfalme Ogu ambaye
alikuwa ni mtu hodari kuliko wafalme wote lakini wana Waisraeli walimshinda kwa
kuwa Ogu alitumainia nguvu zake mwenyewe , wakati wana Waisraeli walimtumainia
Mungu, na hivyo wote walishindwa kusimama mbele ya wana Waisraeli. Hivyo usimwogope
yule aendaye kwa waganga bali mwogope Mungu (ZABURI 35:1-4).
Wakati Daudi hana kitu hakuna aliyemwinukia hata
mmoja, lakini baada ya kupakwa mafuta ndipo watu waliinuka juu yake ili
kumpinga. Kumbe adui wanainuka juu yako baada ya kuona kitu ndani yako cha
thamani kama vile Daudi. Vita ni vingi duniani kwa sababu hakuna mwanadamu
anayetaka mwenzake afanikiwe, na ni furaha kwao wanapokuona unaangamia. Wote
waliomwita Bwana , Bwana aliwaponya wote, hivyo unapomtumainia Bwana ndipo
anapokuponya na aibu walizokuandalia adui zako. Kama vile Modekai alivyowekewa
aibu na Naamani lakini Bwana alimtetea na hakuipata aibu hiyo bali ilimrudia
Naamani mwenyewe.
Ipo vita iliyotengenezwa mbele yako, lakini wakati
wao wanasherekea kwa ajili ya aibu yako
ndipo aibu itawarudia wenyewe. Leo kila
aliyeinua aibu juu yako tunamwambia Bwana geuza hiyo aibu iwarudie wenyewe na
tunaomba Bwana aigawe vipande vipande kwa kiwango walichokutendea.
Unatakiwa ujue yale unayokutana nayo yupo
aliyoyaandaa, maana kabla ya kuzaliwaBwana alishakuandalia baraka zako. Lakini
adui wameinuka na kukuondelea yale ambayo ulikusudiwa uyapate. Sara alichelewa
kupata mtoto hadi katika umri wa miaka
90 maana huo ndio ulikuwa wakati wake ingawa alishakata tamaa. Hivyo nawe
inawezekana sasa ndio wakati wako ingawa umeona umechelewa kupata.
Ili aibu isikupate unatakiwa kufanya yafuatayo:-
1. Cha kwanza ni kubadilisha mtazamo wako kwanza.
Kila mtu ana mtazamo wake kwa sababu ya ile imani au
jinsi unavyo muona Mungu, jinsi unavyo muona Mungu ndivyo unaweza kupata
matokeo. Kama tunavyo muona Shedrack, Meshack na Abgenego walipokaa kwenye moto
maana walikuwa wanamjua Mungu wanayemtumikia na kwamba atawaokoa na ni kweli
akawaokoa.
Uwezo wako wa kumfahamu Mungu ndiyo uwezo wako wa
kushinda. Lakini wewe unaliangalia tatizo na unalipima na uwezo wako na kujiona
kama sisimizi mbele ya hilo tatizo. Maana unaliona hilo tatizo kama ni kubwa na
limezidi na ndio maana miaka yote uko hapo hapo na tatizo halitoki, hivyo ni
lazima ubadili mtazamo wako na umwangalie Mungu unayemtumikia. Tunamwona Gideon
anapokutana na malaika, malaika anamwambia wewe ni shujaa wakati Gideon alikuwa
akijificha kwenye ngano akiwaogopa Wamidiani. Ndivyo ilivyo kwako umekuwa ukijificha
kwa ajili ya adui zako na kujiona udhaifu wakati ni shujaa. Gideon hakuombewa
bali alibadili mtazamo wake na kujua yeye ni shujaa.
Utakapobadilisha mtazamo wako ndipo utaona uwezo
wako na kuweza kushinda na pia utaona muujiza wako. Ibrahim hakuamini Mungu
alipomwambia atapata mtoto Isaka katika uzee wake, ndipo Mungu akamtoa nje na
kumwonesha nyota na kumwabia azihesabu ila akasema ni nyingi mno, ndipoMungu
akamwambia huo ndio uzao wako. Kila alipokuwa akiangalia nyota za angani
alimwona Isaka na ndio maana hata alipoambiwa amtoe Isaka hakuogopa.
Historia ni historia, hivyo usiangalie historia ya
nyuma kama kuna makosa uliyafanya, bali iangalie kesho yako kwa kufuta makosa
ya nyuma na kusonga mbele ili kuitengeneza kesho ya maisha yako. Ukifanikiwa
kugeuza mtazamo ulionao juu ya tatizo ulilo nalo, muelekee Mungu aliye jibu la
maisha yako. Usiogope watu kukuongelea
vibaya, bali wanapofanya hivyo na wewe jisifu kwa sababu una nguvu. Ukiona watu
wanakusemasema ujue wameisha kuchungulia ndani, wanaona hapo ulipo sio pako
wanataka uende sehemu nyingine, lakini hiyo aibu haitakupata maana ni lazima
uivuke ng’ambo.
Saa imefika yakufanya ile aibu iwarudie wenyewe na
saa yenyewe ndio sasa.Unatakiwa usiweke macho yako kumwangalia adui bali
mwangalie Mungu maana amesema hata kuacha hadi mwisho wa dahari. Haijalishi ni nani anaye kushambulia maana
wamekaa katika njia yako ili kukuzuia na kukupinga lakini sisi tunaye Mungu
mkuu kuliko miungu yote ambaye atawavua mavazi yao ili waaibike maana wanajifanya
kama kondoo lakini ndani mwao ni mbwa mwitu.
2.
Baada
ya kugeuza mtazamo, cha pili usikate tamaa.
Usikate tamaa maana Shetani huwa anacheza na macho
yako akipima ukubwa wa tatizo na ukaliona ni kubwa kwa mapana yake. Biblia
inasema Shetani ni kama Simba angurumaye, kumbe ni kama Simba lakini siyo Simba,
hivyo hutakiwi kumuogopa. Lazima ifike mahali upambane kama kuku wa kienyeji
maana kuku wa kienyeji huwa anakufa kishujaa. Inatakiwa uamke usikubali kutishwa,
ile aibu waliyokutengezea kwa ajli yako ikawarudie wao wenyewe.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church inMorogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545