JUMAPILI: 23 AUGUST 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Na:
BRYSON LEMA (RP) &
Dr.
GODSON I. ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Paulo
alikuwa anamwamini Bwana Yesu kama na wewe unavyomuamini. Paulo alikuwa mwanadamu kama
wewe ulivyo. Hata hivyo iliifika wakati ambapo alijiuliza swali, kama ambavyo
imeandikwa katika 1KORINTHO 15:30…[Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?]…Ndani ya
maisha kuna hatari. Kama wewe hadi leo hujaweza kujua kwa nini unakuwa
hatarini, hutaweza kufanikiwa. Hayupo aliyeyaongea mambo ya maisha kama Paulo (Mfano aliongelea jela,
njaa, dhiki n.k.). Paulo anapoongelea
hatari ni kwa sababu yeye pia ni mtu wa hatari. Hauwezi kushinda kama haupo
tayari kupitia shida, hatari na magumu ya maisha.
Kwa macho tu ni mbaya sana kuangalia hatari za
maisha.Lakini baada ya hatari ujue yapo mafanikio. Yeremia naye aliliona
hili. Imeandikwa katika MAOMBOLEZO 5:9…[Twapata chakula kwa
kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani.]….
Hatari zipo kila siku kwa sababu hakuna aliye tayari kukuona wewe unafanikiwa
na kusonga mbele. Mafanikio ya mwanadamu wa leo ni ya yule aliye tayari kuingia
katika hatari. Hii ni kwa sababu kile ninachotaka kukipata, ni lazima
nijihatarishe.
Shetani anakuona wewe ni hatari pale unapoanza kudai
afya yako, watoto wako, uponyaji wako, mali zako n.k. Ni rahisi sana kumtia moyo "mtu anayetoa
uhshuhuda wake" kwa kumwambia hongera, lakini unasahau kumuuliza siri ya mafanikio
yake. Ndiyo maana Biblia inasema kuwa
Eliya alisema “mvua haitanyesha
ila kwa neno langu” na ikawa hivyo. Ukisoma katika Agano Jipya,
Biblia inasema “Eliya alikuwa
mwanadamu kama sisi akaomba kwa bidiii na mvua haikunyesha kwa muda wa miaka
mitatu na nusu”. Daudi hakuvumilia kumuona Goliath akilitukana
Jina la Bwana. Kwa siku moja tu, Daudi alimsikia Goliath akitukana na kuchukua
hatua kwenye ile hatari, wakati wale Israeli walimsikia Goliath akitukana kwa
siku zote 40 mfululizo bila wao kuchukua hatua yoyote, kwa kuogopa hatari.
Hatari zipo, lakini kuna baraka katika hizo hatari.
Kuna kujiingiza katika hatari ili uweze kutoka hapo ulipo. Kumbuka Samsoni
alimuua simba, Na baada ya siku ile Samsoni alijipatia asali ndani ya mzoga wa
simba yule yule.
KUTOKA
13:18-21…[ lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya
Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha. 19 Musa akaichukua ile mifupa ya Yusufu
pamoja naye; maana, alikuwa amewaapisha sana wana wa Israeli, akisema, Mungu
hana budi atawajilia ninyi; nanyi mtaichukua mfupa yangu kutoka hapa pamoja
nanyi. 20 Nao wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpaka wa
ile jangwa. 21 Bwana naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo,
ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru;
wapate kusafiri mchana na usiku; ]….
Hapo ulipo unatakiwa kutoka na kuufuata
ushindi wako pale ulipo. Nyakati zingine watu hawajui njia za kulibeba andiko
na kulifanya liwe lao. Wana wa Israeli
hawakupigana wakiwa Kanaani. Wana wa Israeli walipokuwa Kanaani, hawakupigana
na badala yake waliuzunguka ukuta wa Yeriko.Walipokuwa nyikani, Wana wa Israeli walipambana na
Mfalme Ogu, na baada ya kumuua waliweza kusonga mbele. Wakiwa nyikani walipambana na nyoka wa
jangwani na ili kupona, iliwabidi waingalie sanamu ya nyoka wa shaba‼‼
Unapojiona wewe ni mgonjwa, ujue una tatizo. Kila
ugonjwa una chanzo chake. Kila tatizo pia kwenye maisha yako lina mwanzilishi
aliyelileta hilo tatizo.
1
SAMWELI 14:1-10…[Basi ikatukia siku moja, ya kwamba Yonathani, mwana wa Sauli,
akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na tuwavukie Wafilisti
ngomeni, pale ng'ambo ya pili. Walakini hakumwarifu babaye. 2 Naye Sauli
alikuwa akikaa katika upande wa mwisho wa Giba, chini ya mkomamanga ulioko
kwenye uga; na hao watu waliokuwa pamoja naye walipata watu mia sita; 3 na
Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli,
kuhani wa Bwana huko Shilo, mwenye kuvaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya
kwamba Yonathani ameondoka. 4 Na katikati ya mianya, ambayo Yonathani alitaka
kuipitia ili kuifikilia hiyo ngome ya Wafilisti, palikuwa na genge la jabali
upande huu, na genge la jabali upande huu; jina la moja liliitwa Bosesi, na
jina la pili Sene. 5 Hilo genge moja limesimama upande wa kaskazini, mbele ya
Mikmashi, na hilo la pili upande wa kusini, mbele ya Geba. 6 Basi, Yonathani
akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie
ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la
kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache. 7 Naye
huyo mchukua silaha akamjibu, Fanya yote yaliyomo moyoni mwako; angalia, mimi
hapa ni pamoja nawe, moyo wangu ni kama moyo wako. 8 Ndipo Yonathani akasema, Tazama, sisi
tutawavukia watu hawa, na kujidhihirisha kwao. 9 Nao wakituambia hivi, Ngojeni,
hata sisi tuwafikilie; ndipo tusimame pale pale mahali petu, tusiwapandie. 10
Lakini wakisema hivi, Haya! Ninyi, tupandieni sisi; hapo ndipo tutakapopanda;
kwa maana Bwana amewatia mikononi mwetu; na hii itakuwa ndiyo ishara kwetu.]…
Yonathani anatukumbusha kuwa hakuna cha kumzuia Bwana kutenda; Iwe ni
kwa wengi au kwa wachache.
Yonathani alikuwa anaijua ishara na sauti ya watu waoga.
Kila anayeingia katika safari yangu lazima apigwe
nyundo. Haijalishi huyu mzuiaji ni nani!!!.
Yesu Kristo alikuwa na uhakika wa kufika ng’ambo ya Bahari, na ndiyo maana alilala usingizi wakati ule merikebu
inapigwa na mawimbi kona zote. Leo hii
tunamsoma Goliath kwa sababu ya Daudi. Mwisho wa Kitabu cha Samweli, Biblia
inawataja mashujaa 320 wa Daudi ambao ni wale watu waliokuwa na madeni, wenye
dhiki na kila aina ya adha.
UKIRI
Baba Mungu, leo
nakataa kurudi nyuma, nakataa vitisho vya adui zangu, kila mamlaka za giza
zinazokaa ili kunitisha, leo nazisambaratisha kwa Jina la Yesu. Ewe adui
uliyesababisha vita hii, nakufuata, wewe na wajumbe wako na kila mtu aliyekaa na wewe. Leo nafanya vita na kila
vuruugu, kila adui na ninaanza kuwapiga kwa Jina la Yesu, mliokaa ili
kuniletea vita leo nawasha moto kwa
Jina la Yesu. Amen.
|
Usioogope aliyekupiga
vita au kusimama mbele yako. Kama upo na hujaokoka kwa kumpokea Yesu Kristo
maishani mwako,leo ni fursa muhimu ya
kumwamini Yesu Kristo ili aweze
kukushindia yote.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545.