JUMAPILI: 30 AUGUST 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Na:
BRYSON LEMA (RP) &
Dr.
GODSON I. ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Imeandikwakatika
2KORINTHO 2:14….[Ila Mungu ashukuriwe,
anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye
kila mahali kwa kazi yetu.]…Unaweza kumfahamu mtu lakini papo hapo
usimjue huyo mtu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumjua mtu na kumfahamu mtu.
Kumjua mtu ni zaidi ya kumfahamu mtu husika.
Paulo aliwahi kuwauliza watu katika MATENDO
17:23, kama ilivyoandikwa ..[Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada
yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi
mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. ]…
Pengine hata wewe umewahi kujiuliza kwa nini hawa watu walifanya hivyo kwa
kuyaandika maneno hayo?. Musa na wana wa Israeli walitofautiana katika kumjua
na kumfahamu Mungu. Wakati wana wa Israeli walimfahamu Mungu kuwa ndiye aliyewavusha Bahari ya
Shamu, Musa alimjua zaidi kwa namna alivyokuwaanawasiliana naye ana kwa ana.
Ukijua jinsi Mungu wako anavyofanya kazi hata tatizo
lako litaisha, kwa sababu unamjua Mungu
unayemtumika. Mtumishi wa Elisha alipotoka nje na kuona majeshi
yaliyomzunguka, alirudi ndani na
kumwambia Elisha, “Bwana wangu na
Mungu wangu.” Ndiposa Elisha akamuuliza kwani kuna nini
ulichokiona? Yule mtumishi akamwelezea vikosi
vya jeshi alivyoviona nje.
Ukimjua unayemtumikia wala hatatishika. Ungejua wapi tumaini lako lilipo utaishi maisha mazuri sana. Ni kama vile Tanzania leo
hii itangaze vita kupigana na Marekani leo hii, je unadhani Marekani itatishika
hata kidogo? Hapana, kwa sababu Marekani inajua ilicho nacho cha kuiteketeza
Tanzania. Tatizo la wakristo wengi hawamjui Mungu ila wanajua maandiko ya Mungu‼!
Ukimuuliza mkristo andiko fulanii
lipo wapi, atakutajia,lakini hajui Mungu
aliyeyasema hayo maneno.
MITHALI
2:5…[Ndipo utakapofahamu kumcha
Bwana, Na kupata kumjua Mungu.]…Kumbe kufunga,siyo kumjua Mungu.
Kumbe kuomba siyo kumjua Mungu. Kumbe kuja kanisani siyo kumjua Mungu. Yamkini
mtu anakuja kanisani kwa sababu zake binafsi, lakini kumjua Mungu anayemuamini
hakupo. Wakristo wengi ni bingwa wa kubeba Biblia lakini siyo wa kumjua Mungu. Kumjua Mungu huanza kwa
“kusikia”, kwani ndicho chanzo cha kumjua
Mungu. Kabla ya kumjua Mungu unaanza kumfahamu Mungu kwa njia ya kuzisikia habari zake.
Ndiyo maana katika Biblia kuna watu wanatajwa majina
na wengine hawatajwi kabisa. Mfano ni "Tajiri mmoja" na "maskini mmoja jina lake Lazaro".
Tajiri hajatajwa kwa sababu mbele za Mungu hakuwa na mahusiano yoyote. Lazaro
ametajwa kwa sababu alimjua Mungu na kuwa na mahusiano na Mungu. Maisha ya wokovu ni kukua kutoka hapo ulipo na kwenda hatua nyingine. Maisha
ya kila siku kama hayajabadilika ndiyo maana hata wewe hujabadilika‼
Mungu huangalia kile unachokihitaji wewe. Ndiyo
maana Mungu maeiweka siku ya
hukumu, kwa ajili ya kutuhukumu kwa
matendo yetu.
WAFILIPI
3:8..[Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu
mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu,
Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu
kuwa kama mavi ili nipate Kristo;]… Paulo aliyaacha yote ya
kumfanya asiwe na uhusiano na Mungu , na
kuyahesabu kama hasara / mavi kwake.
Paulo ndani yake alikuwa na shauku ya
kutengeneza uhsiano na Mungu wake. Wapo watu wanatengenza mahusiano na kanisa
au mchungaji kiongozi, na kuacha kuweka mahusiano na Mungu ambaye mwishowe kwake
watatolea hesabu mbele zao zake. Shida ya watu ni kusahau kuwa, tunawajibika
kwa Mungu mbinguni. Je, Mungu anakuona
wewe kama nani?
Uhusiano wako na Mungu kama una kasoro, amka
usingizini na kuweka mahsuaino mazuri na Mungu‼ Hivi mimi na Mungu
tunashauriana? Kanisa haliwezi kukua na watu wanafiki, bali na wale walioamua
ndani kuwa na Yesu Kristo. Siyo muda wa kufumbia macho dhambi.
Kanisa linaanzia nyumbani, na maisha ya kila siku yapaswa yakuelezee
jinsi ulivyo. Ili uweze kuwa wa thamani
kwa Mungu, tengeneza uhusiano wako na Mungu. Fanya mazoezi ya kuwa na Mungu
ndanimwako. Yesu Kristo akae ndani yako.Wokovu wako uwe wa kila saa na kila dakika.
Unajua kuna vitu
vingine vinatupata kwa sababu ya kutotengeneza mahusiano yetu naMungu?
Ukristo unakoelekea kwa sasa ni kubaya. Wokovu unakoelekea kwa sasa ni kwenye kuwa
“DINI”. Hii ni
kwa sababu hakuna mabadiliko ya ndani. Mtu alikuwa mwizi anaacha kuiba.
Mtu alikuwa kahaba anaacha ukahaba. Leo hii wote hawa na tabia zao wanakuja
kanisani nakutoa sadaka zao wakiwa na tabia zile zile. Hii ni kwa sababu watu
wanapenda kumfurahisha mchungaji kiongozi badala ya kumpendezesha Mungu.
Biblia inasema “Usimpe ibilisi nafasi.” Lakni je, hii nafasi tunampa je shetani? Ni kwa
sababu hatutaki kutengeneza mahusiano na Mungu. Kwani Mungu wako ni wa wakati wa kuumwa tu? Mungu wako ni wa ndani kwa ndani tu? Hapana. Ifike mahali watu wakikuona wamuone
Mungu unayemtumikia. Inafaa kila mahali tunapotembea Mungu wetu adhihirishwe. Ndiyo
maana Biblia ikasema, mtoto Yesu akakua
katika kummjua Mungu na kuwapendezesha
wanadamu.
2
PETRO 1:2-3…[Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana
wetu. 3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na
utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.]…
Nikianza mimi kumjua Mungu ananikirimia
ili kupata vyote. Kuna vitu
unavishikilia ambavyo kwa Mungu ni dhambi, na hivyo huwezi kusaidiwa na Mungu
kwa kujichanganya changanya. Kumbuka aliyewaokoa wana wa Israeli, ni huyo huyo aliyewaangamiza Wamisri.
Shetani ana uwezo wa kukujengea ukuta kiasi kwamba
kuomba kwako kukashindikana. Mtu wa aina hii, ni mzuri sana katika kusoma
magazeti ya udaku au 'kucheza games' katika simu lakini kuomba Mungu hayupo
tayari. Mchana wa leo, tunaenda kuvunja kila
uzio ambao adui amekuwekea ili kusababisha kukosekana kwa kiu ya maombi. Leo
tutamuomba Bwana atupe kiu ya kujifunza neno la Mungu, na kiu ya kusikiliza neno la Mungu.
Kila kitu ukifanyapo huanzia ndani. Endapo ndani
kukitaa, huwezi kufanya lolote. Shetani hupenda kuleta mawazo ya kukataa
kufanya maombi. Hii ni kufanya mahusiano
yako na Mungu yasiwepo. Tumejifunza kuwa, ukimjua Bwana unapata vyote. Maisha
yako yatabadilika pindi tu mtu akijenga mahusiano haya na Mungu.
Kama mtu uliyepo hapa hujaokoka, na kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako, leo ndiyo fursa ua kufanya hivyo. Na hata kama uliwahi
kuokoka na baadae kuacha wokovyi, leo pia ni vizuri kufanya maamuzi upya na kugeuka ili kuanza upya na Bwana Yesu.
UKIRI
Leo ninasambaratisha kila mashetani walionizuia, kila mashetani mliokaa ili
kunifunga, kila waliotumwa ili kunifunga ili nisitengeneze mahusiano ya kudumu na Mungu
leo nawasambaratisha Kwa Jina la Yesu Kristo. Amen
|
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545