Na:
BRYSON LEMA (RP) &
Dr.
GODSON I. ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Imeandikwa
katika MITHALI 13:23…[Chakula kingi
chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali
viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.]..
Biblia inasema chakula kipo kingi kwa mkulima lakini vipo viharibuvyo. Leo
unafanya kazi zako kwa nguvu kubwa lakini matokeo ya kile ulichofanya hayaji
kama ulivyotegemea kwa sababu wapo wanaokudhulumu. Adui zako kila kukicha
wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kukudhulumu, na ndio maana maisha yako
hayawezi kwenda vizuri na kile unachokitegema huwezi kukipata kwa sababu adui
ambaye ni “roho ya dhuluma” anataka uharibiwe.
MWANZO
6:11…[Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.]…Biblia inasema kuwa “Dunia ikaharibika, na
dunia ikajaa dhuluma” na kila mwenye mwili amejiharibia njia yake. Hapa Mungu
aliona dunia imeharibika maana binadamu wamejaa dhuluma na hawawazi kujitafutia
vya kwao bali wamekaa ili wakuharibie na kukudhulumu, lakini leo tutawapiga kwa
Jina la Yesu.
Maisha tunayoishi leo si kama tunavyofanya kazi, kwa
sababu hiyo maisha yetu yanakuwa magumu kila siku.Tumefanya mambo mengi kwa
bidii lakini tumepokea tofauti maana matokeo yamekuwa madogo maana yupo adui
anayefanana na mchwa maana anasubiri uwekeze yeye aharibu.
Inawezekana umeomba Mungu uongezewe mshahara, lakini baada ya kipato kuongezeka ndipo unaona matatizo mapya yanakuja maana yupo adui wa kukudhulumu ambaye anaamka maskini na jioni anakuwa tajiri. Hii dunia imejazwa na dhuluma maana msingi wa Shetani katika dunia amejenga katika kudhulumu, maana yeye Shetani yupo kwa ajili ya kuharibu, kuchinja na kuiba.
Inawezekana umeomba Mungu uongezewe mshahara, lakini baada ya kipato kuongezeka ndipo unaona matatizo mapya yanakuja maana yupo adui wa kukudhulumu ambaye anaamka maskini na jioni anakuwa tajiri. Hii dunia imejazwa na dhuluma maana msingi wa Shetani katika dunia amejenga katika kudhulumu, maana yeye Shetani yupo kwa ajili ya kuharibu, kuchinja na kuiba.
ZABURI
55:1-8…[Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche
nikuombapo rehema.2 Unisikilize na kunijibu, Nimetanga-tanga nikilalama na
kuugua.3 Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu.
Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.4 Moyo wangu unaumia
ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia.5 Hofu na tetemeko limenijia, Na
hofu kubwa imenifunikiza.6 Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia
mbali na kustarehe.7 Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani.8 Ningefanya
haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.]… Tunaona Daudi anamwendea Mungu kwa
kuomba maana aliiona dunia kwa wakati wake imejaa dhuluma. Kwa sababu ya
dhuluma hii Daudi akasema hofu ya mauti imemzunguka maana yake wako tayari
kumwua. Daudi kutokana na kudhulumiwa akaona kama angekuwa na mabawa angeruka
kama tai aende mbali ili asikae karibu na wale wanaotaka kumdhulumu.
Tunaona tatizo la Daudi lilianza pale alipopakwa
mafuta. Na matatizo hayo yalianza kwa kasi, na yalianza mara alipomwua Goliathi
na hapo ndipo mfalme akataka kumwua Daudi, badala ya kumsifia Daudi kwa kitendo
chake cha kumsaidia mfalme kumwua Goliathi. Inawezekana hata wewe kwenye maisha
yako kutokana na bidii yako kazini, bosi wako badala ya kukusifu kwa uchapakazi
wako lakini badala yake atainua vita juu yako maana anakuwa anahisi labda
utachukua nafasi yake. Unapoonekana una bidii tayari wanaanza kukufuatilia na
vita inaanza maana wameona kitu ndani yako. Lakini mtu aliye mvivu hutaona akifuatiliwa
wala kuinuliwa vita. Huu ni mwaka wa kumiliki, kutiisha na kutawala, hivyo ni
lazima kuwapiga wanaokudhulumu na lazima warudishe vitu vyote walivyo viiba. Inawezekana umeibiwa
afya, kazi, ndoa n.k, vitu hivi unaweza kudhulumiwa kwa sababu wanaweza
kukuwekea afya, kazi au ndoa bandia.
Kwa kadiri dunia inavyoongeza maarifa na Shetani
naye anaongeza maarifa. Na hivyo dunia hii inahitaji wapambanaji wanaosema
hapana sikubali. Saa imefika ukakatae hayo magonjwa na matatizo ya kwamba
hapana mimi sikuumbwa hivyo. Wapo walioibiwa akili na watoto wamekuwa wa kifeli
mitihani.
ZABURI
55:9-14…[Ee Bwana, uwaangamize, uzichafue ndimi zao, Maana nimeona
dhuluma na fitina katika mji.10 Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na
taabu zimo ndani yake;11 Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila
haziondoki mitaani mwake.12 Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo,
ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo,
ningejificha asinione.13 Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana
nawe sana.14 Tulipeana shauri tamu; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na
mkutano.]… Daudi hakuachia pale akasema anayeniletea dhuluma
ni rafiki yangu sana ambaye tulipeana ushauri na tuliingia nyumbani mwa Mungu
pamoja. Ina maana kwamba hadi kanisani wapo wanaodhulumu. Kanisani pamefika
mahala kuwa si mahali pa watu kujengwa bali watu kulalamika.
Saa ndio hii kanisa la kweli lionekane nalo
litaonekana kama wewe utasimama na kumpiga adhulumuye. Kanisani hatuji kwa
ajili ya kuombewa bali ili Mungu atusaidie. Unapoenda kanisani ni lazima kanisa
likufanye ubadilike. Kanisa linaanza na wewe mwenyewe na si mtu mwingine hivyo
ni lazima umpige yule akudhulumuye. Wapo watu waliodhulumiwa kwenye akili,
unaweza ukamwona kama mtu lakini ndani amewekewa akili ya mnyama. Ni afadhali
ukutane na Simba usiku unaweza ukamkwepa, lakini si kukutana na binadamu wakati
wa usiku. Ndio maana tuona watu wameweka
mbwa katika nyumba zao ili kujilinda na wanadamu. Utaona wapo watu wanaoweza
kujilipua wenyewe ili kuwadhuru wengine, uwe na uhakika watu hao ndani yao si
watu bali ni kitu kingine.
Jambo lolote unaloliona limetokea ujue ipo nguvu ya
rohoni iliyosababisha jambo hilo kutokea. Dunia inapoelekea ni kwenye hatari na
hivyo ni lazima uamke usingizini maana Shetani anataka kuleta madhara makubwa
katika kudhulumu. Mfano tunaona ipo ndege ambayo ilianguka na hata unywele
mmoja haukoonekana,” HII HAIWEZEKANI”. Shetani hapa alipofika hatuwezi
kumwondoa kwa ibada ya siku moja bali inatupasa kuingia ndani sana na kuweza
kumpiga. Ni muhimu uwe mtu wa kufanya ibada si kanisani tu bali hadi nyumbani.
Na hii ni Saa ya Ufufuo na Uzima duniani ni saa ya kupeleka msingi mwingine
katika dunia hii, ni saa ya kuvunja vunja nguvu za Shetani. Saa imefika na saa
ndio hii kanisa limeinuka na misingi imeiunuka, ni saa yako ya kuinuka na ni
saa ya waganga wa kienyiji kuondoka Tanzania. Ni saa ya kila kilichoibiwa
kurudishwa. Acha kupewa moyo na amani tuliyonayo, amani hii ni utumwa na hivyo
ni lazima tupigane safari hii. Ni saa ya kuangusha misingi ya uovu. Hatuikubali hiyo amani maana wanakula wengine.
Je! Amani hiyo ipo wapi?
Unapookoka ndiyo kazi inaanza maana ndipo watu
wanainuka kukupinga. Lakini ukiokoka na kustarehe hutaona ukipingwa.Unapoona
nyumba imejengwa ujue umechimbwa msingi na nyumba ndio ikasimama. Ukitaka
usimame hapo ulipo ni lazima uchimbe umpige Shetani na baada ya hapo hakuna
atakaye kupinga nawe utasimama juu. Unapochimba dhahabu kuna jiwe ambalo lazima
ulipasue kwa baruti vingenevyo huwezi kupata dhahabu. Hivyo nawe ni lazima
umpige Shetani, na usikubali kufarijiwa kwa kuambiwa Bwana atatenda, bali utake
Bwana atende.
ZABURI
55:21…[Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni
vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Bali hayo ni panga wazi.]…Mdhulumaji haji kwa ghafla bali anakuotea. Ni
saa ya kupambana sikubaliani na vitu vinavyoendelea katika maisha yangu, nataka mabadiliko, na mabadiliko hayo si ya
Taifa nataka mabadiliko yangu.
ZABURI
10:15…[Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma
yake, hata usiione.]…Anasema
aneyekudhulumu mkono wake uvunjwe. Kila mkono ulionyooshwa mahali popote
uvunjwe kwa jina la Yesu. Wakuvunja mkono huo ulionyooshwa si mwingine bali ni
wewe.
ZABURI
55:15…[Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali
hai, Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.]..Daudi anasema wanaokudhulumu mauti iwapate, maana biblia
inasema usimwache mwanamke mchawi aishi.
Ni lazima uokoke ili uweze kupata kibali cha kuvunja
mkono ulionyooshwa juu yako na vitu vyako.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545.