Na:
STEVEN NAMPUNJU (AP)
Utangulizi:
Wapo watu
wanaowinda maisha ya watu wengine katika hii dunia tunayoishi. Ukienda
nyikani utawaona wanyama walio hodari
wakiwinda wale walio dhaifu. Na kwa
wanadamu ndivyo ilivyo. Mwindaji ni mtu au mnyama anayetaka kunasa maisha ya
mwenzake kwa kutumia nyenzo zinazosaidia uwindaji wake.
Imeandikwa katika EZEKLIEL
13:18…..[useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi
katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili
wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai
roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi
kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili
kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao
haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi
Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa
hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa
nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.]…..
Hirizi ndizo silaha wanazotumia kuwindia vipawa vya mtuili wavikamate. Mungu
hakumuumba mwanadamu akawe mtawaliwa,
bali mtawala. Shetani anapofusha macho ya wengi ili wasifanikiwe kama alivyopanga Mungu. Hata shetani, katika
kuutega mtego wake, alimfuata mwanamke
kule bustanini na alipomkuta yu peke yake paophapo akafanikisha kumtegea mtego naye akanaswa!!!
Mara zote anayewinda huvaa mavazi au umbile lisilo la asili
yake, na kujificha ili usimgundue. Wanyama porini hubadilisha hata miondoko
yao, na kujifanya hajui wakijifanya hawajui kukimmbia. Hata hivyo, anapofanikiwa hudhihirisha
umbile lake la asili.
Kwa wanadamu
vivyo hivyo,wapo wanaotembea na mitego yao hadi makanisani ili kunasa wengine.
Pengine huko mtaani ameshakuona, lakini
ikawa ngumu kukupata. Njia rahisi
atakayotumia ni kuja kanisani, na baadae
atatumia silaha ya kuokoka. Mwishowe, akeshampata wa kumuoa, biashara ya wokovu
inaishia hapo hapo.
Upo wakati wa kuwinda. Katika kuutega, mwindaji hutengeneza namna za kupata mawindo
yake. WAGALATIA 4:4…[Hata ulipowadia utimilifu wa
wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya
sheria,]… Kumbe hata Mungu alipokuwa akiandaa wokovu wetu,
ulikuwepo wakati wa kusubiria ili ufike. Kwenye mawindo,utulivu hutawala. Mwindaji hutulia sana akiwa anawinda.
Mathalani, endapo ni mnyama wa porini, hata kupumua kwake hupungua.
UKIRI
Leo nauondoa utulivu wowote wa kishetani,
uliowekwa ili mimi ninaswe, Leo nauondoa kwa Jina la Yesu. Ninakataa leo,
utulivu wowote aliouweka adui yangu ili anase maisha yangu, niachie leo kwa
Jina laYesu. Amen.
|
KWA
NINI WANAWINDA?
Lengo kubwa la mwindaji kuwinda na kuweka mitego yake ni KUHAMISHA
mtu au kitu kutoka sehemu moja hadi nyingine. Anayewinda, anataka akutoe
kwenye ndoa/hatima/kazi/ biashara ili akupeleke sehemu nyingine. Mathalani yupo
atakayekushauri usiolewe na mtu fulani wakati yeye binafsi hajaolewa. Yupo
anayewinda maisha yako, siyo akakutunze,
bali akakuchinje na kukumaliza siku hiyo hiyo.
Mungu alivyowatoa wana wa Israeli kuiendea nchi ya
maziwa na asali, wale watu hawakujiuliza
maswali, je hao ng’ombe wa kutoa hayo
maziwa wapo wapi au wanafugwa na
nani?! Na hata walipoikaribia Bahari ya Shamu, Mungu alimwamuru Musa aigawanyishe Bahari kwa kuitumia fimbo
yake mkononi mwake
Mwindaji hulenga piakuchukua vitu kwa nguvu.
Imeadikwa katika EZEKIEL 22:23-25 [Neno la Bwana likanijia, kusema,
24 Mwanadamu, uiambie nchi, Wewe u nchi isiyosafika, wala kunyeshewa mvua siku
ya ghadhabu. 25 Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye
akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya
thamani; wameongeza hesabu ya wajane wake ndani yake.]….Biblia
pia inasema mtu mwenye nguvu
alindapo vitu vyake vinakuwa salama,lakini endapo
atatokea mwingine mwenye nguvu zaidi hutumia nguvu na kuviteka.
ISAYA
42:22…[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika
mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye;
wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]…. Mungu anawaona
watu walioibiwa na kutekwa. Ni watu ambao walipaswa wakae mahali fulani
waitumikie serikali, lakini kwa sasa
wapo sehemu tofauti.
UKIRI
Nakataa kwa Jina la Yesu, ewe shimo uliyeandaliwa
ili kuyakamata masiha yangu, ninakataa kwa Jina la Yesu. Kila gereza
lililoandaliwa ili kushika uzao wangu leo nakuagiza unikatae
kunishikilia, na uniachie kwa JIna la
Yesu. Amen
|
Ipo taarifa mbaya kwa kila aliyetega mtego kwa
maisha yako. Leo hii kila aliyeandaa mauti juu yako, tunawataarifu kuwa, kila
aliyetega mtego mtego utamnsas kwa Jina la Yesu. Mungu ndiye shujaa wa
kuokoa.Mwanadamu hawezi kukuokoa.
UKIRI
Kuanzia leo, nakuanzia sasa, enyi watu waovu
mliojipanga kuotea maisha yangu, leo ninawapiga kwa Damu ya Yesu. Mahali popote ambapo
iblisi ametegea mitego ili kuyanasa
maisha yangu, nakataa kwa Jina la Yesu. Amen.
|
Mwindaji mmoja,
Mfalme wa Misri asiyemjua Yusufu alipogundua kuwa wana wa Israeli
wanaongezeka kwa kasi, alibuni mpango mkakati wa kuwapunguza idadi yao kwa
kuwaendea wazalishaji ili kwamba
watakapokuwa wakiwazalisha wanawake wa Kiebrania, basi "wawatendee kwa akili" –
kwamba wawaue watoto wa kiume tu, lakini wale wa kike waachwe waishi. Kwa nini wawaue wa kiume tu? Ni kwa sababu wanaume baadae ndiyo washika
silaha na wapiganaji. Kwa hiyo wangeongezeka zaidi wangeungana na maadui wa Misri katika kufanya vita.
KWA NINI WAWINDE ROHO TU?
Ahadi yoyote ambayo Mungu aliwahi kumuahidi mwanadamu, ipo
katika roho. Mungu anaposema, “Ujapopita katika maji mengi hayatakugharakisha”, siyo kwa ajili ya mwili wako bali roho yako.
Wawindaji nao wanafahamu haya. Kwamba
hawawindi mwili, bali huwinda roho. Hata
silaha zeetu hazipo katika mwili, bali katika roho zetu. Mwindaji anafahamu kuwa akikamata roho, ameukamata na mwili pia. Ukiiteka roho
umeuteka na mwili pia. Silaha za Mungu
wetu hazipo mwilini, bali katika roho.
Imeandikwa “Roho ndiyo itiaayo
uzima, mwili haufai kitu”.
Roho ikiondoka mtu anakufa, roho ikirudi
mtu anafufuka na ndicho tunachokisoma katika (1WAFALME 17:17) na kuendelea kuhusiana na ufufuo wa yule kijana.
Roho inaweza ikasafiri na kwenda mahali ilikumfungua
mtu. Wakati Petro alikuwa maefungwa gerezani, penye ulinzi mkali sana, Petro
mwenyewe alijikatia tamaa. Hata hivyo kanisa lilipokuwa likiomba, wale waombaji
hawakuamini kuwa ingewezekana Petro kuwekwa huru. 1PETRO
3:18…[Kwa maana Kristo
naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio
haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19
ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu
wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu,
safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane,
waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia
siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele
za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu,
amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.]. Maandiko haya yanatuambia kuwa, Baada ya Yesu kufa msalabani, roho ya Yesu
ilisafiri hadi kuzimu kufanya
kazi. Yesu aliwaendea waliokufa zamani zile za enzi ya safina ya Nuhu
akawahamisha baada ya kuwahubiria. Kumbe roho
ina uwezo wa kuhubiri. Kama roho
inaweza kusafiri na kumtoa mtu
kwenye gereza/ au shida, vivyo hivyo roho za waovu zinaweza kusafiri na kuleta shida
na matatizo kwa watu wengine.
Hivi unafahamu kuwa Goliath ndiye aliyempa ufalme
Daudi? Bila Goliath, hakuna ufalme kwa Daudi. Shida au taabu iliyopo maishani
mwako ndiyo itakayokupa ufalme kwa Jina la Yesu. Daudi hakuwahi kupata mafunzo ya kijeshi. Daudi aliuliza
swali, akitaka kujua kwamba ni kitu gani ambacho mtu atapewa baada ya kumshinda Goliath? Baadae,
Daudi alilazimika kujitambulisha mbele ya Goliath kuwa “mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu
wa majeshi ya Israeli uliowatukana”. Ukilibeba Jina la Bwana wa Majeshi, utapata
ushindi wako dhidi ya adui zako wanaokuwinda.
Ili uupate
muujiza wako lazima uwe na kitu. Yule mama mjane vivyo hivyo,
alipoulizwa na Elisha ana nini nyumbani
mwake alisema ana mafuta kidogo sana yamebakia nyumbani mwake. Hicho kidogo ulicho nacho kitumie, na ukeshafanya hivyo utapokea muujiaza wako
kwa Jina la Yesu. Zipo roho zinazotokea mahali fulani, labda ni shimoni au
baharini ili kuikamata roho yako.
Silaha kubwa ya iblisi ni kukupiga
akitokea ndani. Pengine mtu alikuwa muombaji mzuri, lakini leo hii haombi tena, ni kwa sababu shetani ameingia ndani ya huyo mtu!!
UKIRI
Kwa Damu yaYesu, kuanzia leo, na kuanzia sasa, yeyote anayewinda
roho yangu aniachie, kila roho iliyo ndani yangu au nje yangu leo niachie kwa
Jina la Yesu. Ewe mwindaji unayewinda roho yangu, leo niachie kwa Damu ya
Yesu. Ninaikata kila kamba ya mtego iliyonifunga, Uliyetumwa ukae ndani yangu
ili uniwinde, leo kwa Jina la Yesu achia, kwa Jina la Yesu. Amen
|
Wapo waoteaji, wanatazama na kusema huyu mtu hana wa
kumsaidia. Ni heri leo ukamuamini Yesu, atakuwekea alama ya Damu yake na
kukusajili kuwa mmoja wa watu wake.
=== © Information Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Glory of Christ (Tanzania) Church in Morogoro.)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545