NA RP; ADRIAN
LUKA 6: 17-19 “Akashuka pamoja nao, akasimama mahali
tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu
waliotoka Uyahudi wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni waliokuja
kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Na wale waliosumbuliwa na pepo
wachafu waliponywa. Na makutano yote
walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.
Hapa tunaona jinsi
ambavyo watu walikuwa wakienda kwa Bwana Yesu ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa
yao. Watu huwa wanapenda kuja kusikiliza na wanapokuwa wanasikiliza, Roho
Mtakatifu huwa anakutana nao na kuwaponya magonjwa yao. Unaweza ukawa umekuja
kusikiliza tu, umefanya vema sana name nakushauri sikiliza kwa nguvu zako zote
maana muujiza wako upo ndani ya kusikiliza. Maana biblia inasema watu walikuwa
wanatoka sehemu mbalimbali kwenda kumsikiliza Yesu na walipokuwa katika
kusikiliza ndipo wakawa wanaponywa magonjwa yao.
MITHALI 2:2 “Hata ukatege sikio lako kusikia hekima,
ukauelekeze moyo wako upate ufahamu.”
Ili mtu aweze kusikiliza ni lazima awe na sikio la
kusikiliza. Lakini ulimwengu wa leo umeingilia systems ya kusikiliza ili kwamba
watu washindwe kupokea kile ambacho BWANA anataka kuwapa kupitia neon lake.
KUMBUKUMBU 31:12-13 “Wakusanye watu wanaume na wanawake na
watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na
kumcha Bwana Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii. Na
watoto wao wasiojua , wapate kusikia na kujifunza kumcha Bwana Mungu wenu siku
zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.”
Angalia wewe ambae umemwacha mwanao nyumbani tena hajaokoka,
lakini unasema nikimchukua motto huwa nitachelewa. Ni muhimu ufahamu kuwa
ulimwengu unahitaji mtu mwenye uwezo wa kumwongoza mtu ili apate kumfikisha
salama anakokwenda. Mungu anataka tufanye
jukumu la kuwakusanya watu wote waende kwake. Lakini kuna wengine wapo
hapa leo huku watoto wao wamewaacha nyumbani, wamemwachia Farao, maana Farao
alimwambia Musa na Haruni kuwa nimewapa ruhusa ya kwenda lakini watoto
mtawaacha. Lakini Musa akasema kuwa hatutaacha chochote tutakwenda na kila kitu
maana hatujajua Mungu atataka tumwabudu tukitumia nini. Hawakuacha hata ukwato.
Shida ni kwamba tumekuwa wavivu wabinafsi na wachoyo, ndo
maana hatutaki kuwaleta wengine kwa Yesu huku ukisema “si unajua tena, wale
watu ni wajanja sana” mbona hata wewe ulikuwa mjanja kama wao lakini sasa
umeokoka?
LUKA 8:18 “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo, kwa kuwa mwenye
kitu atapewa, na Yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa
kuwa anacho”
Hapa unatakiwa kuwa makini sana, maana kupitia kusikia
shetani anaweza kukuwekea mtego, yaani usikie taarifa mbaya tu kuhusu mkeo,
mchungaji wako, mfanyakazi wako. Watu wengi sana maisha yao yameharibika
kupitia kusikia. Ni muhimu sana kuyachuja yale maneno unayoyasikia.
Na pia unatakiwa uwe makini sana maana kupitia kuongea ongea
umepoteza muujiza wako ungali mchanga. Mungu akisema na wewe kitu au akifanya
kitu kwa ajili yako wewe unakuwa wa kwanza kusemasema mpaka muujiza wako
unapotea maana kupitia yule unaemwambia shetani anaanza kuweka mitego ili kuua
muujiza wako ungali mchanga ni kama vile Herode alivyotaka kumuua Yesu angali
mchanga.
Lakini pia na kwa sababu watu huwa wanaenenda kwa mazoea,
wanakuwa wamezoea neno la Mungu, wamezoea siku ya BWANA, wamemzoea Roho
Mtakatifu, wamezoea watumishi wa Mungu. Kwa kufanya hivyo hauwezi kupokea
muujiza wako maana Mungu si wa mazoea ukitaka kupokea kutoka kwa BWANA inabidi
uondoe mazoea kabisa kwenye maisha yako.
Kwa mfano, mama aliyekuwa akitokwa na damu kwa muda wa miaka
12 aliposikia habari za Yesu, akasema moyoni mwake “nikimgusa vazi lake tu,
nitapona”. Na akaenda alipogusa vazi la Yesu Yule mama akapona palepale. Lakini
pale Bwana Yesu alikuwa katikati ya kusanyiko watu wengi walikuwa wanamgusa
Yesu lakini walikuwa wanamgusa kwa mazoea.
Na kuna watu wengine ni wataalamu wa kufanya dhambi,
wanafanya dhambi pasipo mtu yeyote kujua hawajui kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa
na kufunika moto kwa karatasi ya nailoni. Biblia inasema, kila kinachofanyika
uvunguni kitawekwa juu ya paa. Kila uovu unaoufanyani lazima ipo siku utakuja
kuonekana wazi na watu wote watashangaa.
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH-(UFUFUO NA UZIMA)
MOROGORO BRANCH