GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 24 APRIL
2016
Na: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Baba (SNP) Dr.Godson Issa Zacharia akifundisha sababu 20 za kwa nini wafu lazima wafufuliwe
Jumapili 24/04/2016 katika Bonde la Maono - Morogoro
|
1. Wafu wanatakiwa wafufuliwe ili andiko litimie
Imeandikwa katika MATHAYO 10:8… (Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni
wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.). Kila aaminiye
inampasa pia kuamini kuwa kwa Jina la Yesu anaweza kuwafufua watu waliokwisha kufa kwa kuwani mojawapo ya mamlaka ambayo Yesu alitupatia.
Tena imeandikwa katika YoHANA 5:25….(Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.). Hili ni agizo alilotoa Bwana Yesu, ya kuwa wafu wataisikia sauti ya Bwana na kufufuka. Kumbe hata wafu wanaweza kuisikia sauti ya Yesu na baada ya hapo wakafufuka.
Tena imeandikwa katika YoHANA 5:25….(Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.). Hili ni agizo alilotoa Bwana Yesu, ya kuwa wafu wataisikia sauti ya Bwana na kufufuka. Kumbe hata wafu wanaweza kuisikia sauti ya Yesu na baada ya hapo wakafufuka.
2. Mungu ni mwenye haki.
Mungu hawezi kuhukumu kwa upendeleo. kwa kuwa ni mwenye kutenda haki.
Bwana Yesu alisema hatarudi mara ya pili hadi
habari ya injili ihubiriwe duniani kote. Haimaanishi hiyo habari ihubiriwe kwa watu wa Morogoro tu, la
hasha. Injili ihubiriwe Kenya, India, Uabuni na kwingine kote. Ni lazima tufufue wafu ili wote walioibiwa katika haya mataifa na wakafichwa mashimoni watoke huko
waliko waje kumfuata Yesu.
MATHAYO 27:51-53
(Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi).... Kuna watu ambao walikufa kabla ya Yesu hajazaliwa. Hawa ina maana hawakuhubiriwa kabisa habari za wokovu upatikanao kwa kumwmini Yesu Kristo. Je, itakuwa je kwa watu kama hao? Utawahukumu je wakati hawakuisikia injili ya Yesu. Biblia inasema Yesu akiwa msalabani, roho yake ilienda kuzimu na kwenda kuwahubiria watu waliokuwa kuzimu na ndiyo hao waliofufuka siku ile ya kufa kwa Yesu msalabani.
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi).... Kuna watu ambao walikufa kabla ya Yesu hajazaliwa. Hawa ina maana hawakuhubiriwa kabisa habari za wokovu upatikanao kwa kumwmini Yesu Kristo. Je, itakuwa je kwa watu kama hao? Utawahukumu je wakati hawakuisikia injili ya Yesu. Biblia inasema Yesu akiwa msalabani, roho yake ilienda kuzimu na kwenda kuwahubiria watu waliokuwa kuzimu na ndiyo hao waliofufuka siku ile ya kufa kwa Yesu msalabani.
3. Ni kwa sababu watu wengi wapo
mashimoni.
Hatumainishi kuna handaki limechimbwa mahali, hapana.
Hili ni shimo la rohoni, ambapo mashetani na wachawi huingiza watu humo, na
kuwahiadhi humo.
ISAYA
42:22 (Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha).
Isaya alioneshwa na Mungu watu wakiwa
wamenaswa katika mashimo. Shimo hili kwa jina lingine linaitwa KUZIMU. Leo kila
aliyeibiwa lazima arudshwe. Wapo watu tayari mashimoni, wanateswa na kuumizwa.
Zipo aina kama
3 hivi za misukule:
(a) Mtu
kuugua ghafla, bila dalili za ugonjwa wowote na hata akipelekwa hospitalini, anafia njiani au afikapo hospitalini. Hii ni sawa na
kuiita gogo style. Ndugu zake huanza kulia na kuomboleza wakisema Bwana alitoa na Bwana
ametwaa!! Ni kweli Bwana alitoa lakini katika kutwaa, siyo Bwana. Hii staili ni
ya kmazingaumbwe zaidi. Na kwa sababu hiyo, hata mkimzika mtu kama huyu siyo
yeye mliyemzika bali ni kama gogo tu, na yule mtu mzima hupelekwa shimoni na
kufanya kazi huko.
(b) Mtu
anapotea (ndugu, mtoto, rafiki n.k). Mtu wa aina hii, akipotea kwa staili hii,
hata mkienda polisi watakwambia ni hadi saa 24 ziishe.
(c) Mtu
anaibiwa kimazingara. Mtu wa ndani (roho yake) hutolewa na kuacha mwili wake.
AYUBU 33:29-30 ....(Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai). Kumbe roho ya mtu huweza kuibiwa na kupelekwa shimoni.
Ndiyo maana katika 2WAKORINTHO 12:2-3 imeandikwa hivi:…(Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);)... "Roho" ndiyo "mtu mwenyewe". Ni kwa sababu mtu ndiyo roho yenyewe. Kumbe mtu huyu aweza kukaa ndani ya mwili au nje ya mwili.
30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai). Kumbe roho ya mtu huweza kuibiwa na kupelekwa shimoni.
Ndiyo maana katika 2WAKORINTHO 12:2-3 imeandikwa hivi:…(Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);)... "Roho" ndiyo "mtu mwenyewe". Ni kwa sababu mtu ndiyo roho yenyewe. Kumbe mtu huyu aweza kukaa ndani ya mwili au nje ya mwili.
Biblia inasema YOHANA 6:63
maneno haya: (Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima). Ili mtu akiibiwa asiweze kufa, wachawi huweka roho ya kitu kingine ndani yao ili kumpa uzima.
Hawa misukule wa aina hii ni wengi sana hapa duniani na hata Tanzania.
Mtu wa aina hii, hubadilika
kitabia. Ni mtu alikuwa mzuri, lakini ghafla anafanya matendo ya ajabu ajabu.
Mtu mathalani ni mkurugenzi lakini anakamatwa kwa kosa la kubaka mtoto mdogo.
Media & Information Ministry wakishuhudia kwa makini maelezo ya binti aitwae Theresia ambaye
wakati wa maombi haya alijiona akiwa anabebwa na joka na ndipo akaanguka chini kwa mshtuko.
|
4. Walioko Jehanamu ni wengi
kuliko walioko duniani.
Jambo hili ni dhahiri kabisa. Imeandikwa katika
MITHALI 27:20 (Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi). Kuzimu haishibi ingawa Waliopo
ndani ya hiyo kuzimu ni wengi zaidi ya waliopo duniani, na jambo hili linathibitishwa na
takwimu za Kibiblia.
LUKA
16:20-28 imeandikwa (Na maskini mmoja, jina
lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 1 naye alikuwa akitamani
kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa
wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na
malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi,
kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu
kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu,
nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi
wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu,
kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro
vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26
Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi umewekwa shimo kubwa, ili wale
watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja
kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa
kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa
pa mateso.).
Lazaro akiwa kifuani mwa Ibrahimu na tajiri akiwa
kuzimu. Na takwimu zinaonesha, tajiri anao ndugu watano watarajiwa wa kuja
kuingia kuzimu. Kwa hiyo waliopo paradise ni mmoja wakatai watu sita watakuwa
raia wa kuzimu.
ISAYA
5:14….(Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa
yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na
ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.)
Kinywa cha kuzimu kimemeza watu wengi, lakini leo lazima kiwaachie hawa watu
kwa Jina la Yesu. Kwa takwimu za 2006 zilizofanywa na Mmarekani mmoja kujua idadi ya walokole duniani, ni kwamba watu waliokoka ni
takribani 1billioni. Dunia kwa sasa ina watu bilioni 7, na kwa maana hiyo
endapo Yesu atarudi ghafla duniani, wale watakaokolewa ni 1 bilioni na shetani atabaki na
bilioni 6.
Mama (RP Happiness Godson), hakubaki nyuma, alikuwa makini kabisa kuandika na kufuatilia maandiko. |
5. Ishara ni kwa ajili ya wale
wasioamini.
Kwa mimi niliyeokoka, hata
kama kiwete hatakuwa mzima, bado mbinguni nitaenda tu. Kwa wale ambao
hawajaokoka, ishara huwafanya waamini. Na zisipokuwepo ishara, watu wasioamini
hujjitenga au kuahamia makanisa mengine.
Imeandikwa katika YOHANA
11:40 – 43….
(Yesu
akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41
Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba,
nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia
sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili
wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia
kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.). Yesu anathibitisha ukweli kwamba ishara hazijakuwepo kwa ajili ya wanaoamini bali ni kwa ajili ya wale wasioamini.
6. Ufufuo wa Wafu ulitabiriwa
ISAYA
26:19 ….(Wafu wako wataishi, maiti zangu
zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni
kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.)
Watu waaweza kusema, Isaya
alitabiri tu mambo ambayo ni kwa kipindi kile cha Wana wa Israeli. Lakini
ikumbukwe pia kuwa Isaya huyo huyo ndiye alitabiri habari za Yesu kuzaliwa katika ISAYA 7:14…(Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba,
atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.). Na jambo hili lilitokea kama lilivyotabiriwa na Nabii Isaya.
Tena akatabiri tena katika ISAYA
9:6
…(Maana
kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani
mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. ), na yote haya yakatokea vile vile.
Isaya huyo huyo alitabiri
habari za Yesu kuteswa na kuuawa kwake kwa ajili ya wokovu wa dunia nzima. Na ikatokea vivyo hivyo kwa jinsi
ilivyotabiriwa. ISAYA 53:1-5 ….. (Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na
mkono wa Bwana amefunuliwa nani? 2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo,
Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana
uzuri hata tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni
nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 4 Hakika ameyachukua masikitiko
yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na
Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu
yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.)
Imeandikwa pia katika HOSEA
14:7….(Na wao wakaao chini ya uvuli wake
watarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufu yake
itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni..)…
Maana yake wafu watamea kama ngano imeavyo na kuchipua katika udongo.
HOSEA
6:2 .... (Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi
mbele zake.). Kwa hiyo baada ya siku 2 inakuja sikua ya tatu. Ni wakati wa kufufua wafu
kwa sababu katika kizazi chetu hiki Bwana atatuinua.
2
PETRO 3:8…. (Lakini, wapenzi, msilisahau
neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama
siku moja.) ….Kumbe katika kizazi chetu hiki
wafu lazima wafufuke, kwa sababu hata Hosea alishaitabiria hiyo hali kutokea LAKINI baada ya siku ya pili (maana yake kwa sasa tumeianza siku ya tatu, kwa maana ya miaka yote baada mwaka 2,000 (sawa na siku ya 2 kwa Bwana) na kwa kuwa tumeshaanza kuelekea mwaka 3,000 Baada ya Kristo).
Sababu kubwa ya watu
kuchukuliwa msukule, ni DHAMBI. Kwa wewe ambaye hujaokoka, leo ni siku muhimu
kwako kumpa Yesu maisha yako ili usiwe miongoni mwa hao watu wanaochukuliwa
msukule.
========== ITAENDELEA TENA JUMAPILI IJAYO ==========
© MEDIA &
INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|