SNP Dr. Godson Issa Zacharia, akihubiri Jumapili 02/05/2016
Bonde la Maono Mkundi - Morogoro.
|
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 01 MAY 2016
Na: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Somo: SABABU 20 ZA KWA NINI WAFU WAFUFULIWE
Wiki iliyopita nilikuahidi kuwa leo tutaendelea na sababu zile 20 za kwa nini wafu wafufuliwe. Tuliona sababu kama sita kati ya 20 za kwa nini wafu wafufuliwe, na zenyewe ni hizi zifuatazo:
- Sababu ya kwanza ni ili andiko litimie. Mathayo 10:8... Kwa sababu hili ni neno la Bwana kwamba lazima
- Mungu ni mwenye haki. Mungu siyo mwanadamu hata aseme uongo. Kwa hiyo watu wote lazima wahubiriwe kabla ule mwisho haujaja. Kwa hiyo, wale wafu walioibiwa kabla ya kumjua kristo lazima warudi
- Watu wengi wapo mashimoni. ISAYA 42:22, lazima hawa nao wafufuke
- Walio jehanamu ni wengi kuliko waliopo duniani.mfano mzuri ni ule wa Lazaro na tajiri, kwamba tajiri alikuwa kuzimu na Lazaro alikuwa paradise na Ibrahimu. Yule tajiri alikuwa na ndugu zake 5 waliokuwa watarajiwa wa kwenda kuishi huko motoni. Unapofufua, wale watarajiwa wa kwenda motoni hawataingia huko tena.
- Ishara ni kwa wasio amini. Ishara ya kufufua wafu ni mojawapo itakayofanya wale wasioamini bila ishara waweze kuamini.
- Ufufuo wa Wafu uliwahi kutabiriwa. Katika Isaya imeandikwa katika ISAYA 26:19-20. Nabii Isaya aliwahi kutabiri kuzaliwa kwa Yesu, nayo ikatokea. Alitabiri tena kuhusu mateso ya Yesu nayo ikawa hivyo. Kwa hiyo, anapotabiri kuhusu wafu kufufuka, ni lazima itokee vivyo hivyo kwa Jina la Yesu.
Wiki hii tunaendelea na sababu zingine zilizosalia ili kujua kwa nini wafu wafufuke:
- MAARIFA YAMEONGEZEKA
RP Steven (Kulia) akiwa pamoja na wachungaji waangalizi kutoka GCTC - DSM wakiwa safarini kuchunga makanisa mapya huko Ulanga, Turiani na Kilosa. |
Katika Daniel 12:1-4...( 1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. 2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. 3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele. 4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.).
Mungu ameweka watu duniani ili dunia iende mbele. Zamani zile za Yesu, ili kuondoka mji mmoja na kwenda mwingine, lazima umtume mtu apige mbio. Magari au treni au ndege zilikuwa hazipo. Hata barua kuituma ilikuwa inachukua miezi kadhaa kufika kule inakopaswa kwenda. Zipo nchi ambazo watu hawataki kumwamini Yesu kwasababu ya maendeleo ya teknoolojia waliyo nayo. Hata hivyo, saa inakuja ambapo watu wa aina hii jambo/tukio la ufufuo litokee katika nyumba zao ili wapate muda wa kuja na kuukimbilia Msalaba wa Yesu. Ni lazima sisi tufufue wafu ili wale waliojidai sana kwa elimu na teknolojia zao wakifa wafufuliwe na papo hapo waanze kusimulia ukuu wa Bwana.
- UOVU WA DUNIA HII UMEONGEZEKA SANA
Showers of Glory katika ubora wao, wakiimba na kumchezea Bwana Yesu, Jumapili 01/05/2016 ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Bonde la Maono Mkundi - Morogoro. |
Utaona kuwa watu wamefikia hatua ya kuchukua misukule wazi wazi. Hata Morogoro aliwahi kutokea mtu aliyemfungia mtoto wake kwenye boksi kwa zaidi ya miezi sita. Watu wamejaa uovu hata kufikia kutwanga wenzao kwenye kinu. Binti mmoja aliyerudishwa msukule wiki iliyopita hapa kanisani, alielezea kisa ambapo kabla ya kurudishwa alikuwa akikaa mlimani, na waarabu wanne na boss wao. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kutwanga watoto wachanga wanaoibiwa mahospitalini. Kule hospitalini wakifika huvalishwa nguo kama manesi, na boss wao huwagusa wale manesi wa ukweli na papo hapo hulala. Hawa manesi feki ndiyo huondoka na watoto hawa na kuacha midoli.
UKIRI
Kwa Jina la Yesu,ninaamuru watu wote waliochukuliwa msukule,waliofichwa mapangoni,mashimoni ninawaita leo njoo kwa jina la Yesu,rudisha wote uliowachukua kwa jina la Yesu.
|
- BWANA ANATAKA WAJUKUU WOTE WA IBRAHIMU WAMWAMINI YESU
Hawa wajukuu wa Ibrahimu ni akina nani? Kama utakumbuka, Sara alikuwa hazai, na hivyo akamsihi Ibrahimu aingie kwa mjakazi wake Hajiri, na baadae akampata mtoto aitwae Ishameli. Hata hivyo, baada ya muda kupita, Sara alimpata mwana aitwae Isaka.
MATHAYO 28:11-15...(Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi. 15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.)
Kwa Wayahudi, uongo huu ulioenezwa umefanya waendelee kuamini kuwa Yesu hajawahi kuwepo. Watakapofufuliwa wafu katika kizazi chao hawa, nguvu hii ya ufufuo itawafanya wamwamini Yesu.
- MAARIFA YA UTUKUFU WA MUNGU LAZIMA YAIJAZE DUNIA YOTE
AP Gideon Gasper akidhihirisha "maarifa ya utukufu wa Mungu kuijaza dunia yote", wakati akimuombea na kisha kumrudisha Dada aliyechukuliwa Msukule 01/05/2016. |
Kwa hapa duniani, kadiri mtu anavyokuwa na taaluma za kutosha, mtu wa aina hiyo hutukuka sana. HABAKUKI 2:14...(Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari. )... Dunia itajazwa maaraifa ya utukufu wa Bwana badala ya ule utukufu wa elimu za watu. Ifike mahali ambapo wale walioshawishika kusema “hakuna Mungu” kwa sababu ya elimu au fedha au maarifa ya hapa duniani wakose cha kusema‼
- UTUKUFU WA MWISHO WA KANISA UWE MKUBWA KULIKO WA KWANZA
Ufufuo wa Wafu utasababisha utukufu wa kanisa kwa kanisa uwe mkubwa kuliko wa kwanza.
HAGAI 2:3-9 ....(Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu? 4 Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi; 5 kama neno lile nililoagana nanyi mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope. 6 Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; 7 nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. 8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi. 9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi.).... Nyumba inayoongelewa hapa ni ile aliyojenga mfalme Sulemani. Ilikuja kubomolewa ikajengwa nyumba nyingine. Hata hivyo, kiunabii, nyumba hii ni Kanisa. Na kwa hiyo, wakati utafika kwa sababu ya wafu kufufuliwa, watakimbilia kanisani kupata msaada kwa sababu utukufu wa mwisho utakuwa mkuu kuliko wa mwanzo. Je,ni utukufu gani huu? Yesu alizungumzia utukufu wa ufufuo wa wafu.
- KAZI ALIZOFANYA BWANA YESU LAZIMA NIZIFANYE, NAAM KUBWA KULIKO HIZO.
Imeandikwa katika YOHANA 14:12....(Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.)... Yaani wewe ukimwamini Bwana Yesu, unao uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi ay yale aliyofanya Yesu.
Mamia ya Watendakazi wa ufufuo na Uzima Morogoro wakifuatilia kwa makini somo la "Sababu 20 kwa nini wafu wafufuliwe" siku ya Jumapili 01/05/2016 katika Bonde la Maono Mkundi - Morogoro. |
MATHAYO 14:15-21....(Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. 16 Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula. 17 Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. 18 Akasema, Nileteeni hapa. 19 Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. 20 Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. 21 Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.)... Kwa haraka,mkutano huu wa Yesu ulikuwa na watu 25,000 (kwa sababu wanamume ni 5,000 wanawake kwa kuwa ni wengi zaidi ya wanaume tuseme walikuwa nao ni 10,000 na watoto kwa sababu ni wengi kuliko wazazi tuseme nao ni 10,000).
Yesu aliwahi kufufua wafu wengi tu. Mmojawapo ni binti Yairo, mwingine ni aliyefufuliwa katika lango la Naini, na pia alimfufua Lazaro aliyekaa kaburini kwa siku 4 akiwa ananuka. Endapo watu watamwamini Bwana Yesu kwa dhati, mtu huyo lazima naye afufue wafu kwa Jina la Yesu.
- WATU WA MUNGU WAMEDHARAULIWA SANA NA DUNIA
Leo hii duniani hapa, wapo watu wanadharau sana watu waliookoka. Wengine hujisika vibaya wanaposemwa kwa maneno mabaya au machafu. Kanisa limedharauliwa. Mlokole kwa nyakati za zamani, hata kuwa na magari ilikuwa kitu nadra sana.
Imeandikwa katika ISAYA 61:7...(Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.)......
- SIYO LENGO LA MUNGU WATU WAENDE JEHANAMU
Jehanamu haikuandaliwa kwa ajili ya wanadamu, bali iliandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake. Imeandikwa katika MATHAYO 25:41....(Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;)... Ni lazima tufufue wafu kwa sababu wanadamu hawakuandaliwa huu moto kwa ajili yao. Wengi wa watu wanaoenda huku kuzimu au jehanamu ni kwa sababu wanaibiwa. Siyo kwamba Yesu amesahau. La hasha. Yesu alisaza hii hekima kwa wakati kama huu ili kusaidia kanisa lisonge mbele.
- HAPENDI HATA MTU MMMOJA APOTEE BALI WOTE WAIFIKILIE TOBA
Imeandikwa katika 1TIMOTHEO 2:3-4
Imeandikwa katika 2 PETRO 3:9....()... Bwana a Yesu hapendi hata mtu mmoja apotee. Wapo watu wengi leo hii ambao hawajaokoka. Hii ni kwa sababu Yesu ahapendi hata mtu mmoja apotee. Kwa kupitia Ufufuo wa wafu, wengi watakuja upande wa Yesu.
- SHETANI NA WACHAWI WAMEONGEZA UTAALAMU/MAARIFA YAO YA KUCHUKUA WATU MISUKULE
Wakristo wengi wamekuwa wakilitumia neno la Mungu katika MATHAYO 10:8 kwa kujikita katika kuponya wagonjwa, kupooza wenye mapepo na kutakasa wenye ukoma, lakini kwenye eneo la kufufua wafu hapana‼
UKIRI
Kwa Jina la Yesu, ewe mchawi, msoma nyota uliyeniibia maisha yangu,nyota yangu leo nakuamuru rudisha vyote kwa Jina la Yesu.
|
17. WATUMISHI WA MUNGU WAONGO WAMEONGEZEKA DUNIANI
Shetani amesajili watumishi ambao ni wajumbe wa shetani, kufanya kazi za Mungu kana kwamba wapo upande wa Mungu. Kwa nguvu ya Ufufuo na Uzima.
UKIRI
Kwa Jina la Yesu, yeyote aliyeniteka akanifungia mahali fulani na kuniweka kama msukule, leo nakupiga na kukuponda kwa jina la Yesu. kuanzia leo mimi ninatoroka kwa Jina la Yesu.
|
- YESU NI UFUFUO NA UZIMA
Imeandikwa katika YOHANA 11:25.....(Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;)... Ni lazima nifufue wafu kwa sababu mwasisi wa kufufua ni Bwana Yesu mwenyewe.
- HOFU YA MUNGU IRUDI KANISANI
Kanisa la leo limekosa hofu ya Mungu. Ndiyo maana hata leo wapo wanaodiriki kutenda dhambi kanisani. Hofu iliingia kanisani baada ya vifo vya Anania na mkewe Safira.
MATENDO 5:1-11...(Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, 2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. 7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. 8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. 11 Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.)
Mungu anataka wafu wafufuliwe ili hofu ya Mungu iingie kanisani tena. Kupitia ufufuo, wengi wataacha
- AKIWAENDEA MTU ALIYETOKA KWA WAFU WATATUBU
Hii ni ile habari ya tajiri mmoja aliyekufa na Lazaro maskini naye alipokufa pia. Huyu tajiri alizoea kumtuma Lazaro angali wakiwa hai, akadhani kuwa hata baada ya kufa ataendelea kumtumikisha tu bado.
Kufufua wafu kutasababisha lile jawabu la tajiri aliloomba litimie tena. Kwamba watu wakisikia habari za mtu aliyefufuka, itakuwa rahisi kwa wengine wasioamini waaanze kuamini katika Jina la Yesu.
Unaposikia mtu ameibwa, maana yake hata vile vitu vyake vinakuwa vimeibiwa (elimu, mali n.k. Wiki jana nilikufundisha kuhusu aina tatu za msukule. Ya kwanza ni ile ya gogo-style (ambapo mtu huugua ghafla na kufa kifo cha ghafla, na huzikwa haraka), aina ingine ni pale mtu wa ndani anachomolewa na kuwekwa roho ya kitu kingine, na ya mwisho ni ya mtu kupotea moja kwa moja.
Hata hivyo, Sababu kubwa ya watu kuchukuliwa msukule ni DHAMBI. Kwa wewe ambaye hujaokoka, leo ni siku muhimu kwako kumpa Yesu maisha yako ili usiwe miongoni mwa hao watu wanaochukuliwa msukule.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|