Monday, April 11, 2016

Somo: ROHO YA KUZAA MAPOOZA


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH

UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO

JUMAPILI – 10 APRIL 2016

Na: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)

 


Kuzaa mapooza ni kuzaa  vitu vilivyokufa kabla ya wakati wake. Ni hali ya kuzaa kitu kisicho kuwa  na uhai. Kwa hapa Tanzania, kwa mfano, wapo  akinamama  wakienda kujifungua watoto mahospitalini, baadae huambiwa na wale wazalishaji kwa  msemo maarufu kuwa “mtoto ni bahati mbaya”. Maana yake hapo mama wa aina hii amezaa mapooza.

 

SNP Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha somo la Kuzaa Mapooza Jumapili 9/4/2016
katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro.

 

Katika Biblia 2WAFALME 2:19-22 imeandikwa “Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. 20 Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. 21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena. ” Watu wa mji walimweleza ukweli Elisha kuhusu tatizo la mji wao. Alichokifanya Elisha ni kwenda kwenye chanzo cha yale maji (kwenye chanzo cha tatizo) na kutoa tamko kusitisha tatizo lile. Yamkini ipo ndoa unayoiona kuwa nzuri sana kwa nje kwa macho ya nyama,  lakini kwa ndani hiyo noda imeooza. Leo tunazifuta aina zote za mapooza maishani mwetu kwa Jina la Yesu.

 

 

UKIRI
Kwa Jina la Yesu ninakataa kuzaa mapooza. Ninakataa mapooza ya iana yoyote, nakataa mapooza kwenye maisha yangu. Amen
 

 

Nikweli umepata kazi nzuri, lakini ndani yake  kuna mapooza (rushwa za ngono). Wapo wawnaopata kazi nzuri lakini mwisho wake fedha ikipatikana haikai mfukoni,  kila mara misiba na magonjwa yanaambatana. Uchumba unaweza kuwepo, wa watu wazuri tu kanisani, lakini roho la kuzaa mapooza likiwemo, binti aweza kujikuta anapata ujauzito kabla ya ndoa na hata pengine magonjwa kama vile UKIMWI. Endapo  leo utaivunja roho  ya mapooza utafanikiwa katika Jina la  Yesu.

 

 

Kuzaa mapooza ni  sawa  na kupukutisha matunda kabla ya wakati wa kuvunwa. Katika MALAKI  3:11 imeandikwa hivi: “11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.” Endapo watu hawatamuibia Bwana, atakemea wale walao na mizabibu ya huyo  mtu  hayatapukutisha matunda yake.

 

Katika mji wa Naini, alikufa kijana mmoja,  mwana pekee wa mama mjane. Tukio hili liliwaleta watu wengi waliokuja kumtia faraja mama mjane kwa kifo cha ghafla cha mwanae. Misafara ya mauti ilianza, na watu wakajikusanya sana, ila ikaingiliwa kati na msafara wa uzima wa Bwana Yesu.

 

LUKA 7: 11-15Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. 12 Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. 13 Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.”  Kilio chako leo hii kigeuke na kuwa furaha  kwa Jina la Yesu. Hata kama ndoa yako  imekufa muda mrefu, ukikutana na Yesu ataifufua tena kwa kuwa yeye ni Ufufuo na Uzima.

 

Maelfu ya Watendakazi wakiwa kwenye ibada iliyoongozwa na SNP Dr. Godson Issa Zacharia tarehe 9/4/2016 (Jumapili) yenye Somo la  "Roho ya Kuzaa Mapooza."
 
 

KWELI ZINAHUSIANA NA KUZAA MAPOOZA KWENYE MAISHA YAKO

1.      Katik KUTOKA 23:25-26... “Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.” Kuharibu mimba ni sawasawa na mapooza. Hata Ayubu, mtumishi wa Bwana, mifugo yake ilitekwa nyara na watenda kazi wake kuuawa na Waseba, ambao kimsingi ni roho za mashetani walioruhusiwa kuingia ndani ya miili ya Waseba na kufanya walichofanya. Kwa nini? Roho ya mapooza ilikuwepo. Roho  ya kuzaa mapooza ni roho  la kuzalisha taabu. 

 

 

CHANZO CHA ROHO YA MAPOOZA

Kuzaa mapooza huanzia rohoni. Ni  roho la kishetani linalosababisha vitu kufa kabla ya wakati  wake.

 

MALAKI 3:7-12Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi,   nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani?   Mmeniibia zaka na dhabihu.9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo,   asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.”

 

Katika mstari wa 11 imeandikwa “yeye alaye”. Kimsingi shetani ndiye mwenye desturi ya kula vitu vya Mungu alivyovitoa kwa  watu wake. Shetani ndiye  mkurugenzi wa wizi, naye huiba furaha, mafanikio,  amani,  afya n.k. katika maisha ya watu. Shetani huitwa pia “Kerubi Afunikaye”, kwa sababu alikuwa na mafuta yafunikayo.

 

 

UKIRI
Ewe roho  ya kuzaa mapooza leo nakukemea kwa Jina la Yesu.
 

 

Platform ya Ufufuo na Uzima Morogoro wakimwimbia Bwana tarehe 9/4/2016

 

Imeandikwakatika YEREMIA 1:10angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Umwekwa juu ya mataifa, ofisi, falme, viongozi n.k  ili kuharibu nakuangamza roho  za kuzaa mapooza kwa Jina la Yesu. Fahamu leo kuwa Bwana amekuweka juu ya kazi, juu ya ndoa, juu ya biashara, juu ya familia n.k. ili kuharibu,  kung’oa na kubomoa roho za mapooza kwa Jina la Yesu. tukim,aliza kufanya hayo, tutaenda kujenga visivyoharibika kwa Jina la Yesu.

 

UKIRI
Bwana Yesu, niwezeshe leo nihamishe kwa Namna ya rohoni ili niwakamate wote na kuwang’oa, na kubomoa na kuwaharibu wote kwa Jina la Yesu. Naagiza kuanzia sasa, malaika wa kuzimu mliopanda kuzaa mapooza kwenye elimu, kazi na maisha,  leo nawasambaratisha kwa Jina la Yesu.
 
Bwana Yesu imeandikwa kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokolewa, leo naliitia  Jina lako, kwa kuwa katika Jina lako,  kila goti litapigwa. Nalazimisha magoti ya wale majini, wasoma nyota, waganga wa kienyeji, majoka na wachawi walioniopandia roho za mapooza yapigwe mbele ya Jina lako Yesu. Napokea uwezo wa kupiga vita na yeyote aliyenipandia mapando ya roho za mapooza leo ninampiga na kumshinda kwa Jina la Yesu. Amen.
 

 

 

Yapo mapooza ambayo  watu wameyasia ili  baadaye  yaote maishani mwa watu. Njia pekee ya kupata uwezo wa kuzing’oa roho za mapooza maishani mwetu ni kwa kumpokea Bwana Yesu kwa maana ya kuokoka.

 

 

 

 

©  MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH

 
Share:
Powered by Blogger.

Pages