GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI – 03 APRIL 2016
Na: STEVEN NAMPUNJU (RP)
Somo: KUHAMA KUTOKA KATIKA UFALME WA GIZA
Kuhama
ni kutoka eneo moja na kuelekea sehemu nyingine, sasa ninapo sema ufalme nina
maana ya utawala na utawala huu umegawanyika katika pande mbili, utawala wa
Nuru na utawala wa giza, na ninapo sema
giza nina maana ya kukosa uelekeo au matumaini au faraja, mfano tunasoma kwenye Wakolosai
1:13 "Naye alituokoa katika nguvu za
giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake";
Ufalme huu giza una nguvu kabisa ambazo watu
wanakuwa wameshikiliwa nazo na kufungwa lakini jambo jema hapa ni kwamba leo hii utakombolewa na
kufunguliwa vifungo vyako kwa Jina la Yesu.
Ukiwa
ndani ya ufalme wa Mungu vitu vyote vinashikana katika Mungu, natangaza leo
Mungu akukutanishe na biashara, kazi n.k kwa Jina la Yesu. Wakolosai 1:14- 17 “ambaye
katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu
asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,
vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana;
ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa
kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako
kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye”.
Hata
mwanadamu alipoumbwa na Mungu alipewa kazi ya kufanya mfano, Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu
kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu
ya nchi”.
Imeandikwa
katika 2WAKORITHO 4:16-18 “Kwa hiyo
hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani
unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa
kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie
vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu;
bali visivyoonekana ni vya milele”.
Mungu
ni Mungu wa kuhamisha, aliwahi kuhamisha watu wengi, alimhamisha shetani kutoka
mbinguni, aliwai kuhamisha taifa la Israeli kutoka utumwani, na leo Mungu atakuhamisha tena, atakutoa, kutoka
katika vifungo vyako na kukupeleka katika furaha yako tena kwa Jina la Yesu.
Ili Mungu
akuhamishe ni lazima asikie kilio chako: mfano alisikia kilio cha wana wa
Israel naye akashuka na kuwatoa utumwani na leo paaza sauti yako na Mungu
ataisikia na matokeo yake atashuka na kukusaidia tena kwa Jina la Yesu.
Kila
ufalme una mikakati ya ufalme na malengo yake mfano Imeandikwa katika 1Yohana 3:8 “atendaye dhambi ni wa Ibilisi;
kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu
alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi”. Ibilisi
anawatawala wake, na ili uonekane wewe ni raia wa ufalme unatambulika kwa
matendo unayoya fanya, katika utawala wa giza kuna mipango ya giza inaendelea
ya kuua, ya kuchinja. Imeandikwa katika Yohana
10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na
uzima, kisha wawe nao tele”.
DALILI YA WANA
WA GIZA AU WA IBILISI
Imeandikwa
katika Matendo 13:6-11 “Walipokwisha
kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa
uongo, Myahudi jina lake BarYesu; mtu
huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali
akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini
Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka
kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo,
akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa
haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa
Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi
kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na
kumwongoza”.
-Wana wa ibilisi
wamejaa hila
-Wana wa ibilisi
wamejaa uovu
-Wana wa ibilisi ni
adui wa haki yote
-Wana wa ibilisi huwa
hawaachi kuzipotosha njia za Bwana.
Kumbe
utagundua ufalme huu na mipango yake ambayo ni ya uovu, lakini leo nakutangazia
leo mwana wa uovu hatakushinda tena kwa Jina la Yesu.
Shetani
anapo fanya kazi anafanya kazi kwa mipango na anaanza kuweka kitu fulani ndani
yako kidogo ambacho kitamsaidia yeye kukufuatilia lakini leo tunafuta yote na
kuhama kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Kwa
jina la Yesu, leo nina hama mimi na familia yangu, na biashara yangu, na ndugu
zangu wote kwa jina la Yesu. Amen
|
Shetani
ana mipango, lakini Mungu pia ana mipango ndiyo maana Imeandikwa katika Kutoka 11:1 “Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao
na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa
ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa”. Usife moyo Bwana ameendaa
pigo kwa watesi wako wote kwa Jina la Yesu.
Katika
Yohana 8:12-20 imeandikwa “Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa
na nuru ya uzima. Basi Mafarisayo
wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli. Yesu akajibu,
akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli;
kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala
niendako. Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. Nami
nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi
na yeye aliyenipeleka. Tena katika
torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. Mimi ndimi
ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia. Basi
wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu
hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu. Maneno hayo aliyasema
alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu
aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado”.
Kumbe
kila mtu anayo saa yake mwenyewe. Imeandikwa katika Yohana 7:25-30 “Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu
siye wanayemtafuta ili wamwue? Na kumbe!
Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa
huyu ndiye Kristo? Lakini huyu twamjua
atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. Basi Yesu akapaza sauti
yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua;
wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua
ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. Basi
wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika,
kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado”.
Ipo saa ambayo
watu wameandaa kabisa ili wakuangamize, walitaka kmkamata Yesu lakini
ikashindikana maana saa yake ilikuwa bado saa haijafika, na mimi nakutangazia
kila saa za wachawi na waganga juu yako nazifuta zote kwa Jina la Yesu.
Imeandikwa
katika Luka 22:47-53 “Alipoondoka katika
kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni. Akawaambia,
Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni. Basi
alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye
ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu
kwa kumbusu? Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema,
Bwana, tuwapige kwa upanga? Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata
sikio la kuume. Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio,
akamponya. Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee,
waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata
mnyang'anyi? Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono,
lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza”.
Utaona
kumbe ufalme wa giza una saa zao wa kutenda kazi, sasa wewe uliyempokea Yesu
unatakiwa utende kazi bila kuchoka maana shetani yeye naye anatenda kazi gizani
ili kuyafunga maisha yako.
Pale
ambapo umeketishwa na tarajiwa kuhamishwa leo kwa Jina la Yesu. Imeandikwa
katika Isaya 14:17 “Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Ufalme wa giza ndio unao leta ukiwa, leo
utahamishwa kutoka katika ukiwa wa ndoa, ukiwa wa kazi, ukiwa wa biashara na kuingizwa
katika furaha tena kwa Jina la YESU.
SABABU ZINAZO
MFANYA MTU AWE RAIA WA GIZA
Katika
Waefeso 2:1- 5 imeandikwa “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa
na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu,
na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika
wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote
nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya
mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao
wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni
mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya
makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema”.
Sababu
kubwa inayo mfanya mtu awe raia wa giza ni DHAMBI
na MAKOSA, pale mtu anapo fanya
kinyume na mapenzi ya Mungu anakuwa ameingia katika ufalme wa giza,
Imeandikwa
katika Wakolosai 2:13-14 “Na ninyi
mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu,
aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani”; Unapo kuwa unatenda dhambi unakuwa na uhalali wa
kuingia katika ufalme wa giza.
Katika Zaburi 50:15-21 imeandikwa “Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na
wewe utanitukuza. Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza
sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa
maneno yangu nyuma yako. Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na
wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.
Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo
ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini
nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya
macho yako”. Kinywa pia ni sababu ya kuingia katika ufalme wa giza
Lakina
leo Mungu anataka akufanye upya tena kwa jina la Yesu, ili kila ukitamka Baraka,
Baraka iwepo, ukipiga wachawi nao wapigwe.
Utu
wa ndani ndio shetani anaoushika na kuufunga, lakini Mungu kama nilivyo sema ni
Mungu wa kuhamisha, leo Mungu anataka ayahamishe maisha yako na historia yako
anataka aibadilishe tena kwa Jina la Yesu.
Maisha
ya dhambi ni maisha ambayo Mungu hayafurahii kabisa, sasa kabla hujaanza
kuomba, chukua muda mchache na sema maneno haya
SALA YA TOBA
KATIKA
JINA LA YESU, KWA DAMU YA YESU, KUANZIA LEO,NA KUANZIA SASA, NAMKATAA SHETANI
NA KAZI ZAKE ZOTE KWA JINA LA YESU, BWANA YESU UNISAMEE MAKOSA YANGU YOTE
NILIYO KUTENDA KWA DAMU YA YESU. NA ULIFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA
MAUTI NA ULIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA MBINGUNI.
|
Sasa
upo huru kuomba.
MAOMBI KUHAMA KUTOKA KATIKA UFALME WA GIZA
UKIRI
Kwa
Jina la Yesu, na kuanzia sasa ninakataa kazi zote za ufalme wa giza zilizo
fanywa ndani yangu, utu wangu wa ndani ulioharibiwa na kuibiwa nina urejesha
tena na walio nikamata leo nina wateketeza kwa Jina la Yesu.
Saa
ambayo nimeandikiwa na wafalme wa giza, Saa ya mauti, saa ya ajali, saa ya
kuharibu mimba, saa ya kuharibikiwa leo nina ziharibu na kuzivunja saa zao kwa Jina
la Yesu,
Leo
achilia maisha yangu, hatma yangu, kazi yangu, ajira yangu, ndoa yangu
achilia kwa Jina la YESU.
Nina
hama kwenye kambi zao, kambi za wakuu wa giza, kambi za wachawi, kambi za
waganga, nina zihama leo na kuzipiga kambi zao zote na kuzichoma moto kwa Jina la Yesu.
|
Sifa
ya kuhamishwa kutoka kwenye Ufalme wa Giza ni
kwa kumpokea Bwana Yesu maishani
mwako. Kitendo cha kumkiri Yesu kuwa
Bwana na Mwokozi wa Maisha yako kitakufanya ukose zile sifa za kuendelea kuwa raia wa 'ufalme wa giza'
na kuhamia katika "Ufalme wa Bwana Yesu".
©
MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|