GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 08 MAY
2016
RP Steven Nampunju akifundisha somo la "Kufufua ni Kurudisha Uhai" Jumapili ya tarehe 8/5/2016 katika Bonde la Maono - Mkundi Morogoro |
Na: MCH. STEVEN NAMPUNJU (RP)
Kurudisha Uhai ina maana kurudisha uhai uliochukliwa na shetani na wachawi wake, wako watu waliouwawa ambao hawakumaliza kazi yao hapa duniani, Mungu aliweka vipawa ndani yao wakauwawa. Hivyo ni kurudisha vipawa alivyo weka Mungu ndani ya mtu.
Zaburi 31:13
Maana nimesikia
masingizio ya wengi; Hofu ziko pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
Wako
watu ambao wanaweza kushauriana na wengine ili kuondoa hai wa mtu.
Zaburi 38:12
Nao wanaoutafuta
uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri
hila mchana kutwa.
Wako
wanaotafta uhai wa mtu kwa kutega mitego. Utaona iko Jamii, au watu ambao nia
yao ni kuweka mitego ili kuondoa uhai wako.
Maombolezo 3:53
Wameukatilia mbali
uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu.
Ukiri
Aliyepanga
kutoa uhai wangu nakataa kwa jina la Yesu.
RP Steven pamoja na Watenda kazi wa Bonde la Maono Mkundi - Morogoro wakiwasaidia mamia ya watu waliohudhuria ibada, wenye vifungo mbalimbali ili warudishwe tena hapo 8/5/2016 |
Uhai
kitoka ndani ya mtu, ndio mwisho wa maisha ya mtu, uhai ukitoka mtu anakufa, na
ni lazima kuwe na sababu ya hai kutoka, na uhai ukirudi maisha yanaendelea.
Yohana 10:15
kama vile Baba
anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Yesu
anatoa uhai kwa ajili ya kondoo.
Yohana 13:37
Petro akamwambia,
Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa
ajili yako.
Mungu
aliweka hatima njema ndani ya kila mtu. Wachawi wanandaa mpango wa kuondoa
uhai. Kondoa uhai ni kupoteza. Lengo la kurudisha uhai ni kuregesha yale
yaliyokufa maishani mwako. Inawezekana udhaifu ulionao wanataka kutoa uhai
wako, lakini imeandikwa yeye alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
Mifano ya waliowahi
kurudisha uhai;
1. Elisha
1Wafalme 17:17-24
17
Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua;
ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena.
18
Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi
yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?
19
Akamwambia, Nipe mwanao. Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani
mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake.
20
Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane
huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe.
21
Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu
wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.
22
Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.
2. Elisha alimfufua
mtoto, pia maiti inarudishiwa uhai ilipogusa mifupa kaburini
2Wafalme
2:4-18-37
3.
Luka 7:15
Yule
maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16 Hofu ikawashika
wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu
amewaangalia watu wake.
RP Steven akitaja maandiko mbalimbali ya Biblia yenye kuonesha Waliowahi kufa na kufufuliwa |
4.
Luka 8:49
Alipokuwa
akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi,
akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu.
50
Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.
51
Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na
Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
52 Na
watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali
amelala usingizi tu.
53
Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.
54
Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka.
55
Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.
56
Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.
5.
Matendo 9:36
Na
mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi
(yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
37
Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
38 Na
kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba
Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja
kwetu.
39
Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote
wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona
Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
40
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti,
akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro
akajiinua, akaketi.
41
Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane
akamweka mbele yao, hali yu hai.
6.
Matendo 20:7-22
Hata
siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo
akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake
hata usiku wa manane.
8 Palikuwa
na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.
9
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na
usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi
wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
10
Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana
uzima wake ungalimo ndani yake.
11
Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri,
ndipo akaenda zake.
12
Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.
13
Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia
kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu
kwenda kwa miguu.
14
Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene.
15
Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku
ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto.
16
Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika
Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya
Pentekoste, kama ikiwezekana.
17
Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa.
18
Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga
hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote,
19
nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu
yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;
20 ya
kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali
naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,
21
nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu
Yesu Kristo.
22
Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni,
nisiyajue mambo yatakayonikuta huko;
Lengo
la kukupa mifano hii ni kukupa ufahamu ili ufufue kila kilichokufa katika
maisha yako.
RP Steven akiwaandaa watu kwa Maombi ya Kujifungua kutoka kwenye 'vifungo vya rohoni'. |
Ezekiel 37:1
1 Mkono wa Bwana
ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini,
katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
2 akanipitisha
karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda!
Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
3 Akaniambia,
Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua
wewe.
4 Akaniambia tena,
Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la
Bwana.
5 Bwana MUNGU
aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi
mtaishi.
6 Nami nitatia
mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na
kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
7 Basi nikatoa
unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo
mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa
mwenziwe.
8 Nikatazama,
kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika
juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake.
9 Ndipo akaniambia,
Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi;
Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate
kuishi.
10 Basi nikatabiri
kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi
kubwa mno.
11 Kisha
akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao
husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali
kabisa.
12 Basi tabiri,
uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na
kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni
katika nchi ya Israeli.
13 Nanyi mtajua ya
kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika
makaburi yenu, enyi watu wangu..
Ezekiel
alipitishwa katikati ya mifupa mikavu, ambayo uhai haukuwepo. Mungu akamuliza
Ezekiel mifupa hii yaweza kuwa hai, akasema wewe Bwana wajua. Ili uhai
upatikane ni lazima kwe na ushirikiano na Mungu, ukatoe unabii kama
ulivyoamriwa na Bwana, na matokeo yake yataonekana.
MP Alphonse akimuombea mmoja wa watu waliokuwa na vifungo vya rohoni kumrudisha sawa. |
Ili
Uhai urudi lazima apatikane mtu wa kurudisha na pi ili uhai utoke lazima
apatikane mt wa kuutoa. Hakuna awezae
kurudisha uhai isipokuwa ni Mungu. Wewe ukirudisha uhai ni Mungu amerudisha,
pia wewe ukidai uhai ni Mungu amedai.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|