GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 05 JUNE
2016
Na: Dr. GODSON
ISSA ZACHARIA (SNP)
Kufa maana
yake ni nini? Kufa ni "Utengano kati ya
Roho na Mwili". Twajua ya kuwa mwanadamu ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa
mwili. Mwanadamu siyo mwili kwa sababu ingekuwa hivyo mtu asingekufa nasi
tukasema kuwa ‘fulani ametutoka au
fulani amekufa’ wakati mwili wake huyo mtu bado tunauona.
Katika YOHANA 6:63 imeandikwa “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima”. Kwa hiyo kufa ni pale utengano wa hii roho na mwili unapotokea. Je, Kufufua maana yake ni ipi? Kufufua ni kuirejesha ile roho iliyoondoka katika ule mwili (yaani nyumba au hekalu lake). Zipo Shahidi takribani 13 hivi za KIBIBLIA kuthibitisha kuwa, watu waliokufa wanaweza kufufuka:
Katika YOHANA 6:63 imeandikwa “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima”. Kwa hiyo kufa ni pale utengano wa hii roho na mwili unapotokea. Je, Kufufua maana yake ni ipi? Kufufua ni kuirejesha ile roho iliyoondoka katika ule mwili (yaani nyumba au hekalu lake). Zipo Shahidi takribani 13 hivi za KIBIBLIA kuthibitisha kuwa, watu waliokufa wanaweza kufufuka:
1. ELISHA ALIMFUFUA KIJANA ALIYEKUWA TAYARI AMESHAKUFA.
Imeandikwa
katika 2WAFALME 4:18-19......(Hata yule mtoto alipokua, ikawa siku moja alitoka kwenda kwa baba yake kwenye
wavunao. 19 Akamwambia baba yake, Kichwa changu! Kichwa changu! Naye akamwambia
mtumishi wake, Mchukue kwa mama yake. )....Kumbe unapofikia wakati wa
kuvuna wapo wengine ambao hawafurahii kuona mavuno yako, na hivyo husababisha
hali za vifo kutokea ili wewe usifurahie mavuno ya kazi zako.
Imeandikwa
katika 2WAFALME 4:22-23 ....(Kisha akamwita mumewe, akasema, Tafadhali,
uniletee mtu mmoja wa watumishi, na punda mmoja, ili nimwendee yule mtu wa Mungu kwa haraka,
nikarudi tena. 23 Akasema, Kwa nini kumwendea leo? Sio mwandamo wa mwezi, wala
sabato. Akasema, Si neno. 24 Akatandika punda, akamwambia mtumishi wake,
Mwendeshe, twendelee mbele. Usinipunguzie mwendo, nisipokuambia. 25 Basi
akaenda, akafika kwa yule mtu wa Mungu, katika mlima wa Karmeli. Ikawa, yule mtu wa Mungu alipomwona kwa
mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, Tazama, Mshunami yule kule. 26
Tafadhali piga mbio sasa kwenda kumlaki, ukamwambie, Hujambo? Mume wako
hajambo? Mtoto hajambo? Akajibu, Hawajambo. 27 Naye alipofika kwa yule mtu wa
Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake
ndani yake ina uchungu; na Bwana amenificha, wala hakuniambia.)....
Wenye shida wanapomkimbilia Yesu, wapo wengine ambao hutokea kuwazuia. Hata Bartmayo
yalimkuta mambo kama haya. Ni maombi yangu leo kuwa, asiwepo hata mmoja wa kuwazuia watumishi wa Bwana
kumkimbilia Yesu katika Jina la Yesu.
Imeandikwa
katika 2WAFALME 4:28-30...(Yule
mwanamke akasema, Je! Naliomba mwana kwa bwana wangu? Mimi sikusema,
Usinidanganye? 29 Ndipo Elisha
akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende
zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na
mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.)....
Kwa nini Elisha atoe masharti kama haya? Ni kwa sababu katika wafu kufufuliwa,
wapo watu wengine na hasa wasioamini, hujitokeza na kuwa wazuiaji. Hawa hujaribu kuzuia kile walichokiua kisipate uhai tena.
Imeandikwa
katika 2WAFALME 4:30.... (Na
mama yake yule mtoto akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo,
sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata. 31 Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile
fimbo juu ya uso wa mtoto; lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema,
Mtoto hakuamka. 32 Basi Elisha alipofika
nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. 33 Basi
akaingia ndani, akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba
Bwana. 34 Akapanda juu ya kitanda, akajilaza juu ya mtoto, akaweka kinywa chake
juu ya kinywa chake, na macho yake juu ya macho yake, na mikono yake juu ya mikono
yake; akajinyosha juu yake; mwili wake
yule mtoto ukaanza kupata moto. 35 Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko na
huko mara moja; akapanda, akajinyosha juu yake;
na yule mtoto akapiga chafya mara saba, na mtoto akafumbua macho yake. 36 Akamwita Gehazi, akasema, Mwite yule
Mshunami. Basi akamwita. Na alipofika kwake, Elisha akasema, Haya! Mchukue
mwanao)... Kumbe yawezekana mtu akafa na mtumishi wa Bwana akaitwa na
kuomba na baadae mtu huyo aliyekufa akafufuka (maana yake kurudiwa na uhai tena).
2. ELIYA ALIMFUFUA MTOTO.
Imeandikwa
katika 1WAFALME 17:17-20....(Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule
mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana
pumzi tena. 18 Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia
ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu? 19 Akamwambia, Nipe mwanao.
Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe,
akamlaza kitandani pake. 20 Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu,
je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe)...
.... Unaona kuwa, kifo kinaanzia katika ugonjwa. Na kwamba, kufufua lazima
kuandamane na kumuomba Mungu, na si vinginevyo.
Imeandikwa
katika 1WAFALME 17:21-22...(Akajinyosha
juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu,
nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena. 22 Bwana akaisikia sauti
ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka. 23 Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka
orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.).. Tunaona kuwa roho ya mtoto inaurudia mwili
ule ambao ilitengana nao. Hii ndiyo tumesema kuwa kifo ni utengano wa roho na mwili. Imeandikwa katika YOHANA 5:25....(Amin, amin, nawaambia, Saa
inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale
waisikiao watakuwa hai.).... Eliya aliomba maombi na Bwana akairejesha
roho ya yule mtoto aliyekuwa amekwisha kufa. Hii ndiyo maana ya wafu kuisikia sauti ya Mwana wa Mungu.
3. MIFUPA YA ELISHA INAMFUFUA MTU ALIYEKUWA AMEKUFA
Imeandikwa
katika 2WAFALME 13:20-21...(Elisha
akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa
mwaka. 21 Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa
yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha,
alifufuka, akasimama kwa miguu.)... Kama mifupa ya mtumishi wa Bwana Elisha,
iliweza kumfufua mtu, je, siyo Zaidi wewe mtendakazi katika Nyumba ya Bwana, hili huwezi?
Thamani yako ni kuu kuliko mifupa ya Elisha. Watu wasikutishe, wanaokuambia
kuwa utamfufua mtu, wewe ni nani?
4. YESU ALIMFUFUA BINTI YAIRO
Yairo
alikuwa mkuu wa Sinagogi, na mwanae alipougua alipewa taarifa kuwa kuna
mtu mmoja aitwae Yesu anayeponya
magonjwa. Hata hivyo alisahau kuwa Yesu siyo wa kuponya magonjwa peke yake,
bali hata kufufa watu waliokufa. Ndiyo maana watu wale “WAVUNJA MOYO” walijitokeza na kumwambia Yairo, "Msismsumbue Mwalimu
kwa sababu binti yako ameshakufa".
Imeandikwa
katika LUKA 8:49-56...(Alipokuwa akinena hayo, alikuja
mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha
kufa; usimsumbue mwalimu. 50 Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na
hofu, amini tu, naye ataponywa. 51 Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia
pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye. 52
Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali
amelala usingizi tu. 53 Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.
54 Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka. 55 Roho yake
ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula. 56 Wazazi wake
wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia..)...
Bwana Yesu anasema usiogope, hatra kama nyumba yako imelegalega imeshakufa,
USIOGOPE, pengine biashara yako imeshakufa au kazi yako, Yesu anasema USIOGOPE
maana atayafufua hayo yote tena. Hii nayo ni
kanuni ingine ya kufufua wafu. Inabidi uangalie sana watu unaoambatana
nao kwa kazi ya kuufufua wafu, maana yake yamkini wewe unaomba
kurudisha, lakini wale ulioambtatana nao, wale wasioamini wapo kinyume na maombi yako wewe.
5. YESU AKAMFUFUA KIJANA KATIKA LANGO LA NAINI
Imeandikwa
katika LUKA 7:11-13...(Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja
uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. 12
Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni
mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja
naye. 13 Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie)....
Huyu mama ni mjane na ana mtoto mmoja
tu. Maana yake ni kuwa, huyu kijana ndiye msaada pekee alio nao huyu mama.
Imeandikwa
katika LUKA 7:14-15 ...(Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa
wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15 Yule maiti
akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.)... Simamisha msafara
wa mauti. Naagiza waliopanga muda wa kuzika masomo, kibali, biashara yako,
Bwana Yesu akaviguse vyote hivyo kuanzia sasa.
UKIRI
Ewe
masomo uliyekufa naamuru inuka. Ewe biashara uliyekufa, nasema inuka tena
katika Jina la Yesu. Yupo Bwana Yesu anayeturudishia vyote vilivyokufa katika
Jina la Yesu. Amen.
|
6. YESU AKAMFUFUA LAZARO
Imeandikwa
katika YOHANA 11:1-41 kwamba, Lazaro
alikuwa hawezi,maanfa yake alikuwa mgonjwa. Kuanzia mstari wa 9-13, mauti ya Lazaro inazungumziwa.(Yesu
akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa
sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu
nuru haimo ndani yake. 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia,
Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale
wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa
amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala
usingizi.)....
YOHANA 11:25-27....... (Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo
ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye
kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? 27
Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa
Mungu, yule ajaye ulimwenguni.)... Yesu ndoye huo ufufuo na uzima.
Hakuwa na wasiwasi wowote alipoingia ndani ya nyumba hii ya Martaha na Mariamu
kwa sababu, pamoja na idadi ya siku kuwa nne (4).
Imeandikwa
katika YOHANA 11:38-44.. (Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake,
akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39
Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia,
Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi
sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa
lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa
umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili
ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe
uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo
huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi,
na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende
zake).
7. PETRO AKAMFUFUFA DORKAS
Imeandikwa
katika MATENDO 9:36-39....(Na
mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi
(yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.37
Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba
Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja
kwetu.. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu
orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu
na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa
nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena,
Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua,
akaketi. 41 Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na
wajane akamweka mbele yao, hali yu hai.)....
Kuna sababu
zilizomfaanya Petro amfufue Dorkas. Yamkini kuna nguo alizowagawaia watu wa
Mungu ili kuwabariki. Kanuni ile ile ya
kuwatoa watu nje anaitumia Petro mahali hapa pia. Kwa nini? Kwa sababu zipo
nguzo mbili (2) ambazo shetani anapenda sana kuzitumia:
(a)
Nguzo
ya Mauti, na
(b)
nguzo ya kuzimu.
Dorkas
alikufa, lakini amejaaa matendo na sadaka njema anazozitoa. Petro aliomba, kwa
sababu kikanuni, lazima kufufua wafu kuendane na maombi.
8. PAULO ALIMFUFUA KIJANA JINA LAKE YUTIKO
Imeandikwa
katika MATENDO 20:7-12.....(Hata
siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo
akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake
hata usiku wa manane. 8 Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa
tumekusanyika. 9 Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani,
akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na
usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa. 10 Paulo
akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima
wake ungalimo ndani yake. 11 Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi
kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake. 12 Wakamleta yule kijana, yu
mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.).... Biblia haisemi maombi aliyofanya Paulo, lakini bila shaka alimuombe a Yetiko.
9. YESU ALIPOFUFUKA WALE WALIOKUWA
WAMEKUFA MIAKA MINGI WALIFUFUKA NAYE
Imeandikwa
katika MATHAYO 27:50-54.....(Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa
nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama,
pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi
ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya
watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka
kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. 54 Basi yule akida, na hao
waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo
yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.)....
10. MAANA KAMA WAFU HAWAFUFULIWI, KRISTO NAYE HAKUFUFUKA
Imeandikwa
katika 1WAKORITHO 15:12-17...... (Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba
amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama
Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Naam,
na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia
Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye
hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo
naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo
katika dhambi zenu.)..... Akiwepo mtu yeyeote mwenye cheo cha utume,
uaskofu, mchungaji n.k. anaye endelea kukataa kuwa wafu hasawafufuliwi, basi
maana yake mtu huyo angali kwenye dhambi kwa sababu dhambi zetu ziliondolewa
pale mnsalabani na kwa njia ya ufufuo wa Bwan wetu Yesu Kristo.
11. KUFUFUKA KWA WAFU KULITABIRIWA
Imeandikwa
katika ISAYA 26:19..... (Wafu
wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa
mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa
waliokufa.).....Ardhi ni
mahali au makazi ya mwisho wanapowekwa watu wanapokufa. Utabiri wa watu kufufuliwa
ulitolewa na Mungu, kuonesha kuwa ipo siku wafu watafufuliwa kutokea ardhini.
Imeandikwa
katika HOSEA 6:2... (Baada
ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.)...
Ni ushahidi tosha hapa kwamba baada ya siku mbili zilizonenwa na Nabii Hosea, maana yake ni baada
ya miaka 2,000 kupita, na kwa sababu imeandikwa katika 2PETRO (Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili,
kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.)....
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Dunia tumeanza siku ya tatu baada ya mwaka 2,000 kuanza, kudhirisha zilke nyakati za 'baada ya siku mbili' ndizo hizi, na zimeshaanza, kama alivyonena Nabii Hosea.
12. YESU MWENYEWE ALIFUFUKA
Kaburi
lilimwachia Yesu, mauti ikashindwa. Yesu ni limbuko la wale
waliolala katika wafu.
13. KUFUFUA WAFU NI AGIZO LA BWANA YESU
Imeandikwa
katika MATHAYO 10:7-8.....( Na
katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure,
toeni bure.)..... Yesu anawaagiza wanafunzi kuhusu Ufalme wa Mbinguni. Umekuwa nani wewe
unayekataa agizo la Mungu? Kwa nini katika kuponya wagonjwa, kupooza wafu na
kutoa mapepo upo tayari sana, LAKINI katika KUFUFUA WAFU unakwepa?
KWA NINI YESU ALISISITIZA HAYO YOTE
YA KUFUFUA WAFU?
(a)
Imeandikwa
1 WAKORINTHO 2:4-5....(Na
neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi
akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, 5 ili imani yenu isiwe
katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.).....
(b)
Imeandikwa 1 WAKORINTHO 4:20....(Maana
ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.)... Inatakiwa
iwepo nguvu ya kutia changamoto teknolojia na akili za wandamu wa leo hii
wasipenda kuamini kuhusu ufufuo. Wengi wao ni wale wanaokimbilia kuzika tu
baada ya mtu kufariki dunia, badala ya
kutii sauti ya Bwana Yesu ya kufufua wafu.
(c) Imeandikwa 1WATHESALIONIKE 1:5.....(ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika
maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu
mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.).....
(d) Imeandikwa katika 2TIMOTHEO 1: ....(Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya
moyo wa kiasi.)
Maneno ya
Mungu katika maandiko yote manne hapo juu (vifungu
a-d) yanazungumza kuhusu NGUVU.
Tunaihitaji hii nguvu ya ufufuo na uzima ili irudishe kila kitu kilichokufa
katika maisha yetu.
Imeandikwa
katika WAEFESO 3:20....(Basi
atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au
tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;).... Ipo nguvu itendayo kazi ndani
yetu. Hii ndiyo ya kufufua wafu kwa Jina la Yesu.
Imeandikwa
katika MATENDO 1:8 ....(Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi.)... Ukimpokea
Roho Mtakatifu, utapokea pia nguvu hizi kwa Jina la Yesu.
Kifo
ni kitu kinachoogopwa sana na watu leo hii duniani kote.
Biblia inasema, adui wa mwisho ni Mauti. Wewe ambaye hujaokoka, leo hii unapewa nafasi hii ili umpokee Yesu
maishani mwako. Hii ni kwa sababu DHAMBI humfanya mtu awe mfu kiroho, bali pale
mtu unapokubali kuokoka unafanyika tena kiumbe kipya, na ya kale yote yanakwisha.
© MEDIA &
INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|