GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 24 JULY 2016
Na:
Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP - MOROGORO)
Askofu Dr.Godson Issa Zacharia (Kulia), akimhoji Mariamu (Katikati) jinsi Yesu alivyomponya na ugonjwa wa BP ya kupanda Jumapili 24/7/2016. Kushoto ni RP Steven Nampunju |
Adui wa maisha ya kila mmoja wetu hapa ni
shetani. Ijulikane kuwa hapo awali, shetani alikuwa MALAIKA huko mbinguni, ila pale
alipomuasi Mungu alitupwa nje duniani na kuwa SHETANI. Kwa kawaida, shetani ni ROHO na hufanya kazi kupitia
watendakazi wake ambao ni wachawi, wasoma nyota, waganga wa kienyeji, wasihiri
n.k. Shetani kupitia watendakazi wake hawa wanakuwa na uwezo wa kuzuia masomo
yako, elimu, kazi yako, maendeleo yako, kauli yako n.k.
Shetani huyu huyu kuna wakati alimzuia Paulo asiifanye kazi aliyotaka
kuifanya. Katika ITHESALONIKE 2:18 imeandikwa....(Kwa
hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na
Shetani akatuzuia). Inabidi ujue kuwa Paulo alikuwa mtumishi mkubwa
sana wa Bwana, lakini hata hivyo shetani alimzuia, yeye na wenzake. Shetani anaweza
kukuzuia kwa kuingia ndani ya mtu ili kufanya akuzuie kufanya jambo fulani. Kumbuka
shetani ni roho, na hivyo ili atende kazi lazima aingie katika kiumbe chenye mwili.
Wakati ule Yesu akiwa kwenye merikebu kuelekea
Mji wa Wagerasi, shetani akitambua ujio wa Yesu mjini humo na akasababisha
upepo mkubwa sana kiasi cha kutaka kuzamisha ile merikebu ila Bwana Yesu baadae aliutuliza ule upepo usiendelee kuvuma. Vipo vizuizi vya kishetani kabisa vyenye
kuzuia kule unapotaka kwenda ili usifike.
Imeandikwa katika ISAYA 43:4.....(Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu,
na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili
yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.). Mungu anasema
ataandaa watu kwa ajilli ya maisha yako. Kabila za watu humaainsha wale watu ambao siyo wa
faimilia yako. Swali la kujiuliza hapa ni hili: Mbona sijaona hao watu wa kunisaidia,
wawe ndani au nje ya kunisa? Jibu ni
kuwa wapo wanaozuia ili yale watu wanayokuahidi yasianze kutokea. Kuna watu
wameshaandaliwa na Bwana ili wakusaidie wewe lakini shetani amewazuia ili
wasikusaidie.
UKIRI
Watu wote
na makabila yote waliotumwa kwangu ili wanisaidie ninawita wote njoo kwa Jina
la Yesu. Amen.
|
ISAYA
43:6.....(nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.).
Kumbe kaskazi ilishapewa ruhusa ya kukusaidia wewe, lakini kusi imekaa na kujipanga ili kuzuia. Hawa
ndio tunaowaita "wazuiaji".
Imeandikwa katika MATHAYO 8:28.......(Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya
Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali
mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.). Hii ilikuwa ni njia pekee,
na Yesu alipoipita hii njia alikutana na
hawa watu wawili wakali sana na wenye pepo wanaozuia njia ya kuiendea Mji huu.
Kwa Maana nyingine ni: Unapotaka kutafuta bidii ya kusoma ili usonge mbele kimasomo, wapo wanaozuia njia hiyo isipitike. Unapokuwa unaelekea katika mambo mazuri, wapo wanaojitokeza kukuzuia usifanikiwe kufikia malengo yako.
Kwa Maana nyingine ni: Unapotaka kutafuta bidii ya kusoma ili usonge mbele kimasomo, wapo wanaozuia njia hiyo isipitike. Unapokuwa unaelekea katika mambo mazuri, wapo wanaojitokeza kukuzuia usifanikiwe kufikia malengo yako.
Hebu jiulize:
Ø
Mbona
wengine wakianza kulima mashamba wao hufanikiwa lakini mimi sifanikiwi?
Ø
Mbona
wengine wakiposwa hufikia kuolewa lakini
mimi sifanikiwi kuolewa?
Ø
Mbona
wengine wakianza biashara, mambo yao hukua lakini mimi hata mtaji wa biashara
huisha kabla sijafanikiwa?
Wapo wanaozuia, na Biblia inasema ni wakali mno
na hawaruhusu mtu kuipita hiyo njia ya mafanikio: Leo Bwana atawakomesha wote
kwa Jina la Yesu.
Yapo mambo
mengi umemuomba Mungu na ameshakupatia. Hata hivyo yupo anayekuzuia usiapate majibu ya maombi yako:
Ø
Ni
mkali mno hataki uanzishe biashara
Ø
Ni
mkali mno na hataki ndoa yako itokee
furaha na amani.
Inawezekana umefanya maombi sana. Wapo watu ambao
wanahama kanisa moja kwenda jingine kwa sababu hawajapata majibu ya maombi yao.
Ikitokea hivyo watu wa aina hii
huwalalamika wachungaji kuwa pengine hawana upako. Leo inabidi ufahamu
kuwa shida siyo wachungaji, bali ni wewe binfasi. Ni wajibu wako kushindana na
wale wanaozuia kwa Jina la Yesu.
Danieli alipewa kabisa jibu, lakini jibu lake likawa limezuiliwa. Hata wewe na mimi maombi yetu yaweza kuzuiliwa na ni wajibu wetu kushindana na hao wazuiaji. Kama Danieli asingeendelea na mfungo kwa siku zote zile 21, angeweza kukata tamaa, na hata lile jibu aliloletewa na Malaika Gabrieli asingepokea kamwe.
Danieli alipewa kabisa jibu, lakini jibu lake likawa limezuiliwa. Hata wewe na mimi maombi yetu yaweza kuzuiliwa na ni wajibu wetu kushindana na hao wazuiaji. Kama Danieli asingeendelea na mfungo kwa siku zote zile 21, angeweza kukata tamaa, na hata lile jibu aliloletewa na Malaika Gabrieli asingepokea kamwe.
Imeandikwa katika YOHANA 14:13....(Nanyi mkiomba lo lote kwa jina
langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.). Kwa neno
hili “lo lote” maana yake ni jambo lo lote utakaloliomba kwa Jina la Yesu. Shetani huwa
haondoki bila kupigwa. Ndiyo maana hata mbinguni
ilitokea vita kati ya Mungu na Shetani.
Showers of Glory Morogoro wakionesha umahiri wao wa kuimba na kumchezea Bwana Yesu hapo Jumapili tarehe 24/7/2016, katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro (Bonde la Maono) |
Imeandikwa katika UFUNUO 12:7-8...(Kulikuwa na vita mbinguni;
Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao
pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena
mbinguni.). Kama Mungu mwenyewe
aliamua kumpiga shetani, je siyo zaidi wewe na mimi kumpiga shetani? Hii ni kwa
sababu, tunaoshindana nao wapo. Imeandikwa katika WAEFESO 6:12....(Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya
damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.).
Bila kupigana hauwezi
kumiliki. Wana wa Israeli walimiliki Nchi ya Ahadi kwa kupigana. Wale waliojaribu
kuwazuia wana wa Israeli wasipite, walipigwa na kuangamizwa kabisa. Mikaeli
yule yule aliyepigana na Mkuu wa Uajemi, ndiye huyo huyo aliongoza vita ya
kupigana na shetani Kitabu cha Ufunuo 12:7-8.
Unapoona yale uliyoomba hujapokea, fahamu kuwa MUNGU
AMESHAKUPATIA, ILA WEWE HUJAPIGANA VITA KUDAI VITU VYAKO KUTOKA KWA SHETANI ANAYEKUZUIA.
Kwa kawaida shetani ana uwezo wa kugeuka na kuwa kitu chochote. Usipopigana huwezi
kumiliki.
UFUNUO
12:1-5...(Na
ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini
ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. 2 Naye
alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. 3 Ikaonekana
ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba
na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. 4 Na mkia wake wakokota
theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka
akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto
wake.). Unaona jinsi ambavyo shetani amekaa kujiandaa mtoto azaliwe ili
ammeze? Shetani anaweza kumeza. Anaweza kusubiria biashara yako ili aimeze. Anaweza kusubiria ajira au kazi au
masomo yako pale yanapotaka kutokea ili ayameze. Leo tutampiga yule aliyetaka
kumeza vitu vyako kwa Jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.
Shetani ni Joka. Anao uwezo wa kujua mambo ya
rohoni haraka sana kuliko hata wanadamu kwa kuwa yeye ni roho. Imeandikwa katika UFUNUO 12:4-6....(Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za
mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule
mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 5 Naye akazaa mtoto
mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake
akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. 6 Yule mwanamke
akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe
huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.).
Imeandikwa pia katika UFUNUO 12:14-16...(Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai
yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa
wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa
katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa
na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza
mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.). Shetani katika
maandiko haya anajigeuza kuwa mto mkubwa wa maji. Mito ya aina hii huweza
kuleta mafuriko na kuua watu wengi, na kwa akili za kibinadamu watu hufikiria kuwa ni
mafuriko tu ya kawaida. Hata hivyo Mungu alisababisha ardhi iyameze mafuriko ya maji ya ule mto wa kishetani.
Askofu Dr. Godson Issa Zacharia akiomba Baraka kwa Watendakazi wa Ufufuo na Uzima Morogoro (Bonde la Maono) Siku ya Jumapili 24/7/2016. |
UKIRI
Ewe unayezuia, msoma nyota, uwe mchawi uwe
mganga wa kienyeji, imeandikwa “Nao wakamshinda kwa Damu ya Mwanakondoo” nami kwa leo
ninawashinda wote kwa Jina la Yesu. Amen
|
Kama Paulo alizuiliwa, mtume mkubwa sana
aliyeandika zaidi ya nusu ya Biblia (Agano Jipya), wewe je umemzidi Paulo?
Danieli alikuwa Nabii aliyetafsiri ndoto, na aliyewekwa ndani ya tundu lenye simba
wakali na wenye njaa, yeye pia alizuiliwa maombi yake. Wewe je umemzidi Danieli?
Ni sharti upigane ili uweze kupata haja
zako mbele za Mungu.
WAEBRANIA
4:12....(Maana
Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote
ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta
yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na
kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.)... Kumbe vipo pia viumbe
vinavyotumika kuzuia maombi. Kama kiumbe kinakuja kwako kama mjusi, au kuku, au njiwa au
paka, ni maombi yetu leo kuwa wabaki
katika maumbile haya haya milele kwa Jina la Yesu, na watu wawatafute ila wasionekane tena kwa kuwa hawatarudi katika miili yao ya asili tena milele kwa Jina la Yesu.
Katika Biblia yupo mtu aitwae Samsoni, Mnadhiri Mkuu wa
Bwana ambaye alizuliwa na lango la mji. Hata hivyo Samsoni alipozuiliwa na lile
lango la mji aliamua kuling’oa na kulitupilia mbali. Watu waliokuzia kwa mageti
ili usifikie hatima yako, leo ni siku maalumu kuyang’oa mageti yao kama
alivyofanya Samsoni katika Jina la Yesu.
MATENDO 10:6-9...(Walipokwisha
kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa
uongo, Myahudi jina lake BarYesu; 7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio
Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake,
akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo
tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa
kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu,
akamkazia macho).
Huyu liwali alikuwa anataka kuokoka,
lakini mchawi aitwae Elima akaanza kumzuia. Wachawi wana uwezo wa kuingiza roho
za kuzuia mafanikio ya mtu yasitokee. Ni sawa na kwamba
Ø
Ulitaka
mkopo lakini yule aliyekuwa tayari kukusaidia akabadilisha mawazo
Ø
Ulitaka
kuoa au kuolewa lakini akatokea mama katika uo ukoo na kuzuia ndoa ile isitokee
Paulo alipogundua kuwa Elima Mchawi anataka
kuzuia, alimkemea kwa kumkazia macho. Hata sasa, wapo watu ambao hawataki
kuokoka
Watendakazi wakifuatilia kwa makini mahubiri ya Jumapili 24/7/2016 "VIZUIZI VYA KISHETANI" lililofundishwa na Askofu Dr. Godson Issa Zacharia. |
UKIRI
Kwa Jina la Yesu, leo Ninawakamata wachawi wote
waliojipanga, wachawi waliojipanga kunizuia, wasoma nyota wote waliojipanga
kunizuia, wasihiri wote waliojipanga kunizuia leo nawafyeka kwa Jina la Yesu.
Imeandikwa “ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome;” ewe ngome unayenizuia leo nakupasua kwa Jina la Yesu, ewe
ngome kizuizi cha maisha yangu leo nakuangusha kwa Jina la Yesu. Ewe ngome unayenizuia
kuanzia leo nakupasua kwa Jina la Yesu, ewe ngome kizuizi cha maisha yangu
leo nakuangusha kwa Jina la Yesu. Amen
|
NAMNA GANI WACHAWI NA MASHETANI HUMZUIA
MTU?
1. Kwa Kuingia Ndani ya mtu. Hapa shetani huingia ndani ya mtu na
kumzuia kabisa. Hata ukienda hospitalini
watatumia vigezo vya kitaalamu kama vile: huwezi kuzaa kwa sababu mayai
yako yanaharibika, au sperm count zako ni kidogo. Maana yake shetani amemuingia
mtu ndani ya mwili wake na kujigeuza. Shetani anaweza kuingia ndani ya mwili wa
mtu na kujigeuza uvimbe katika tumbo la uzazi.
Wapo waliotumwa kuzuia kwa kuingia ndani mwako. Shetani anaweza kumuingia mtu ndani hata aliyeokoka. Mbinguni kilikuwepo kikao, na shetani akapenyeza pale pale ili kutaka kufanya uharibifu. Yuda Iskariote aliyekuwa mtunza fedha wa Yesu, aliingiwa na mapepo, na kuanzia pale akawa wa tofauti. Imeandikwa katika LUKA 22:3 ...(Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5 Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. 6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.) Wanaozuia wanaweza kumuingia mtu na kuzuia. Shetani alimuingia Yuda Iskariote ili kazi ya Yesu ya kuhubiri Injili isiendelee.
Wapo waliotumwa kuzuia kwa kuingia ndani mwako. Shetani anaweza kumuingia mtu ndani hata aliyeokoka. Mbinguni kilikuwepo kikao, na shetani akapenyeza pale pale ili kutaka kufanya uharibifu. Yuda Iskariote aliyekuwa mtunza fedha wa Yesu, aliingiwa na mapepo, na kuanzia pale akawa wa tofauti. Imeandikwa katika LUKA 22:3 ...(Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5 Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. 6 Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.) Wanaozuia wanaweza kumuingia mtu na kuzuia. Shetani alimuingia Yuda Iskariote ili kazi ya Yesu ya kuhubiri Injili isiendelee.
Kumbe shetani anaweza kumuingia hata mtu wa
karibu na wewe, shangazi, au mjomba au
ndugu wa karibu sana. katika Biblia shetani pia aliwahi kuingia ndani ya Manabii.
Imeandikwa katika 2NYAKATI 18:20-21....(Akatoka
pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia,
Jinsi gani? 21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii
wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo.).
Hawa ni manabii 400 wa Mungu, lakini pepo waliingia vinywani mwao na wakaanza
kutabiri “maneno ya uongo”.
Yumkini Unaweza kutaka kuanzisha biashara
mahali fulani akatokea mtu au kiongozi wa mtaa na kukuzuia. Hata hivyo utaweza
kushangaa kuona kuwa, baada ya muda fulani, eneo lile lile akatokea mtu mwingine
na kufanya biashara ya aina ile ile
uliyotaka kuifanya.
2. Shetani anaweza kushindana na wewe akitokea nje. Hapa ni baada ya
shetani kuona kuwa, uwezo wa kuingia ndani mwako hana. Atakachofanya ni
kumuingia mtu mwingine na kumtumia ili kukuzuia wewe. Imeandikwa katika ZEKARIA 3:1...(Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani
mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa
kuume ili kushindana naye.).
UKIRI
Imeandikwa “mimi ni rungu la Bwana la vita,
na kwa mimi nitampiga farasi na mpanda farasi”, ewe Farao wa maisha
yangu uliyejipanga kunizuia, leo ninakuponda kwa Jina la Yesu. Amen
|
Wewe ambaye hujaokoka, leo ni nafasi yako kumpa
Yesu maisha yako na kuwa na uwezo wa kusindana na mashetani wanaozuia maisha
yako.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T)
CHURCH
==GCTC==
Tel: +255765979866 /
or +255713459545
MOROGORO CHURCH
|