Monday, July 18, 2016

Somo: Mihuri ya Kichawi

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI:  17 JULY 2016

Na: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP - MOROGORO)


Mihuri au chapa ni alama zinazowekwa mahali, kwa mtu, ofisi au kitu kinginecho kile ili kiwe kitambulisho cha kuhalalisha uhalali wa kitu fulani kilichokusudiwa. Mihuri mahali pengine hujulikana kama chapa au "Charter",  kiasi kwamba kitu hicho kinapoonekana watu hufahamu kwamba hii ni kitu gani. Mfano: Unapoona basi la kampuni fulani,  alama zake ni rahisi kukujulisha kwamba uonapo chapa (charter) ya aina hii  ni basi la kampuni fulani. Duniani hapa zipo aina nyingi  sana za utambulisho. Mihuri ya kichawi ipo ya aina mbili: Ile ya rohoni na ile ya mwilini. Wachawi humjua mtu  mwenye mihuri hii kupitia alama hizi, hata kama ungekimbilia mji tofauti na hapo ulipo sasa hivi.


Imeandikwa katika UFUNUO 13:16-18.... “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Hili andiko linazungumzia habari za Mpinga Kristo. Hata hivyo, zipo shida mtu aweza kupitia kwa  sababu mahali fulani kuna muhuri  au chapa inayokutambulisha kwenye hiyo shida. Katika andiko hili, chapa inawekwa kwenye MKONO WA KUUME kwa sababu ndiyo mkono wa nguvu na mamlaka. Alama pia inawekwa kwenye PAJI LA USO kwa sababu ni sehemu ya utambulisho.


Biblia inasema ni “hesabu za kibinadamu” kumaanisha kuwa ni kitu cha kidunia na cha kishetani. Unapoona mtu yeyote anakuambia tuongee kibinadamu, maana yake anataka ufanye mambo kwa jinsi ya kidunia na kama shetani anavyotaka. Hii ni lugha nyepesi nyepesi inayotumika. Bwana Yesu alisema sisi ni roho, kwa hiyo hatupaswi kufanya mambo ya kimwili. Mimi nimeumbwa kwa mfano wa mungu ambaye ni ROHO,  kwa hiyo usikubali kufanya mambo kwa jinsi ya kimwili (Kibinadamu).


TUNAJUA JE HAYA?

Imeandikwa katika YAKOBO 3: 15 .... “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.” Kumbe tabia ya kibinadamu ndiyo pia ya kishetani, na wala haitoki juu.

 
UKIRI
Kuanzia leo, naamuru uwe mbali na mihuri ya kichawi, katika Jina la Yesu. Amen


Mihuri au alama hizi zina hatari zake.  Ukisoma UFUNUO 14:11 utagundua haya:Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.”.... Wenye huu muhuri wanapata shida, hawana raha mchana wala usiku. UFUNUO 16:2... “Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.” Kumbe ule muhuri umesababisha jipu baya (matatizo) kumpata kila mwenye huu muhuri.


Mpinga Kristo ni nani?  Huyu ni shetani kabisa atatokea kuitawala dunia akiingia ndani  ya mtu, na nyakati hizo alama ya 666 itaanza rasmi kutumika. 1YOHANA 2:18 .... “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.” Kwa upande mwingine mchawi ni binadamu kabisa aliyefanya mapatano na kuzimu kumsaidia shetani afanye


Mihuri hii ipo ya aina mbili. Ile ya kuonekana (Kimwili), na ile isiyoonekana (Kiroho). Siku ya leo tutaingalia zaidi mihuri au alama za kuonekana:


MIHURI INAYOONEKANA

·        Mfano wake ni ina au kitambaa anachowekewa mtoto mdogo na wazazi wake ili kumkinga na macho ya watu wabaya.
 
·        Wengine huwafungia watoto wao uzi mweusi ambayo kimsingi ni HIRIZI lakini wanaokuwekea huiita ULINZI. Alama hizi pengine haunazo  hadi sasa lakini katika ulimwengu wa roho, ile  alama haifutiki.
 
·        Wengine ni alama ya kichawi amabzo wamemchanja mtu kwenye mwili kwa kuchukua damu kama alama ya utambulisho. Wengine huchanjwa mgongoni, kwenye ulimi, kifuani na maeneo mbalimbali ya mwili. Kwa njia ya hizi chale, wachawi wanaendelea kukufuatilia popote ulipo.
 
·        Unyoaji wa nywele (kiduku), mara zote ni alama ya kutambulisha. Hata uvaaji wa nguo huwa ni aina ya utambulisho fulani. Mfano: pale mtu anapova  suruali kwa mtindo  wa “Kata K” humtambulisha jinsi mtu huyo alivyo,  na popote pale mtu wa aina hii hata akienda kuomba kazi kwa mazingira kama hayo hawezi kufanikwa.


UKIRI
Kwa Jina la Yesu, ewe uliyewkwa kwenue kiuno changu, au kwenye mkono, niachie. Kuamnzia leo alama yeyote niliyowekewa na bibi au babu, naifuta kwa Jina la Yesu. Ewe alama kwenye uso, ewe alama kwenye ulimi leo nakufuta kwa Damu ya Yesu. Muhuri uliowekwa kwenye mwili wangu ili nikataliwe,  leo futika kwa Jina la Yesu.  Amen



Kuna watu wanapoenda kwa waganga wa klienyeji huagizwa kuleta kucha za mwili wake, au kuagizwa kuleta nywele za kila mahali za mwili wake, maana yake nguvu zako  zote unakuwa umempelekea.  Samsoni aliponyolewa nywele za kichwa chake, tazama nguvu za mwili wake zilimuishia. Hicho ndicho kinachotokea hata kwa mtu anayeenda kwenye nyumba za waganga wa kienyeji na kunyolewa nywele, kwamba nguvu ya mwili wake huicha kwa huyo mganga wa kienyeji.


Wapo watu wengine huamua kuvaa mkufu (chain) kwenye miguu au viunoni. Watu wa aina hii  ukiwauliza kwa nini wanafanya  hivyo husema ni kwa sababu waliona waigizaji wa tamthilia fulani. Kumbe badala yake, hizi hugeuka kuwa utambulisho wa kishetani wa kusabbaisha kukataliwa na kuonewa milele yote.


Katika DANIELI 6: 17-19 imeandikwa... (Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli. 18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa. 19 Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.)..... Mfalme mwenyewe anaonekana kwamba ameweka muhuri ili lisibadilike neno lolote. Maana yake, Danieli aliwe na simba. Yumkini walikuwepo watu waliofurahia jambo hili, wakidhani ndiyo fursa yao kupata cheo. Hata hivyo mfalme alipokuja kesho yake alimkuta Daniel akiwa mzima kabisa. Kinyume chake, wale waliomshtaki Danieli, mbiu ilipigwa wakaingizwa kwenye lile  tundu wao na wake zao, watoto wao na hata kabla ya kuingizwa mle shimoni, samba wale waliwararua na kuwala kwa Jina la Yesu.


Kuna watu wameweka alama /mihuri ili  kwamba usifanikiwe  kabisa.  Ni mihuri inawekwa ili  mtu asipatae kazi, asizae watoto,  asifanikwe n.k. Ingawa alama hizi hazionekani kwa macho, lakini zipo na zinamfuatilia mtu maisha yake yote.  Ingawa ipo mihuri mingi sana, lakini yupo Mfalme wa wafalme YESU KRISTO ambaye atakutoa kwenye dhiki za hiyo mihuri kwa Jina la Yesu.


UKIRI
Ewe shimo uliyewekewa mihuri leo ninaifuta mihuri yote kwa Jina la Yesu. Amen


WAGALATI 6:17.... (Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.). Paulo alibaini kuwa alikuwa na alama za kumsababishia yeye awe muuaji. Kumbe kuna mihuri ya kutaabika. Usipokuwa na chapa za Yesu maana yake unazo zile zingine. Kuna chapa za wachawi za kutaabisha watu: Unaanza mradi lakini unashindwa, unaanza masomo lakini unafeli mitihani. MWANZO 4:15...... (Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.) Kwa hiyo Mungu aliamua kumwekea Kaini alama ili yeyote atakayemuona asimuue. Paulo aliamua kuchukua mwilini  mwake alama / chapa za Yesu. Na Paulo anasema mtu (siyo jinni, siyo shetani n.k.) kumaanisha kuwa wataabishaji ni hao hao wanadamu, waliopo maofisini, kazini, kwenye biashara zako n.k.


CHAPA ZA YESU NI ZIPI  HIZO?

2WAKORINTHO 1:21...(Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,).


WAEFESO 4:30.... (Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.). Muhuri wako na wangu ni Roho Mtakatifu.


WAEFESO 1:13.....(Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.)...


Yupo Yesu awezaye kuifuta hii mihuri. Imeandikwa katika UFUNUO 5:1-5 ....(Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. 2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.). Leo kila muhuri au charter uliyowekewa ya upata ajali, au hasara  Bwana yupo  kwa ajili ya kuifuta hiyo mihuri kwa Jina la Yesu.


Leo wewe ambaye hujaokoka,  unaalikwa kufanya hivyo na kumpokea Roho Mtakatifu ndani mwako kwa Jina la Yesu. Ni sharti kwanza uwe msafi (mtakatifu) ili uwe na kibali cha kuomba na kuifuta mihuri hii ya kichawi maishani mwako.



©  MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH






Share:
Powered by Blogger.

Pages