PRESHA HATARI KWA MARIAMU
YATOWEKA
NDANI YA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
USHUHUDA WA TAREHE 24-07-2016
USHUHUDA WA TAREHE 24-07-2016
Mariamu ni mama aliyeolewa na kulelewa katika Imani ya Kiislamu. Anaishi Morogoro na mumewe, na wanamlea mtoto wao mdogo ambaye bado ananyonya.
Hata hivyo, lipo Tatizo la BP
ya juu lililokuwa linamsumbua Mariamu. Kila mara, BP ilifikia kiwango cha juu cha hadi 180/110 na ikafanya madakatari wamwambie kwa hali ilivyofikia BP ya aina hiyo itamletea "stroke" (kiharusi) wakati wowote.
Dawa za kutumia mara kwa mara zikawa hazikosekani nyumbani kwa Mariamu. Watu wa kumshauri pia wakaja kwake kumwambia hili na lile. Ipo siku akashauriwa
akamuone daktari bingwa (specialist) wa magonjwa kama moyo yasiyoambukiza na kufanya hivyo. Alihojiwa na daktari kujua kama kuna ugomvi wa muda mrefu na mumewe au kazini zipo changamoto zo zote zinazomsibu lakini yeye akasema hakuna!!!
Hatimaye kwa upendo wa Mumewe kumsaidia akamshauri aache kazi. Hata hivyo, boss wake
Mariamu ni Mtendakazi wa Ufufuo na Uzima Morogoro (Jina Kapuni), ambaye ngazi yake ni Potential Shepherd. Huyu tokea awali alimkazania sana Mariamu akubali kuombewa kwa JIna la Yesu lakini akakataa kwa kuwa anayo DINI yake, na amekuwa akijitahidi kuswali mara tano na kuzisoma aya mbali mbali za kitabu cha dini yake hiyo. Kila akimkumbushia kumuombea, Mariamu hakuwa tayari kwa sababu ya DINI yake.
Siku moja Mariamu
alitoka nyumbani kwake kwenda kuomba ruhusa kwa boss wake kutokana na ile hali kumrudia na kumsumbua.
Badala ya kumpa ruhusa, POTENTIAL SHEPHERD huyu
alimuuliza Mariamu kama yupo tayari kuombewa. Kwa hali ilivyokuwa imefikia, kwa shingo upande Mariamu aliazimia kumruhusu
Boss wake huyu amuombee ili kuondoa maswali ya mara kwa mara‼
Kwa takribani dakika 45 maombi yalifanyika na Mariamu akaanza kujiona mwepesi, na hali ile ya uzito ikawa imetoweka. Kwa maneno ya kinywa chake, Mariamu anasema "Wakati wa maombi nikawa naona mwili unasisimka na kama vile moyo umewekwa barafu na kujiona mwepesi kabisa". Siku ile alipofika nyumbani alichukua kipimo cha BP ambacho mumewe alimnunulia ili kumsaidia kujua hali ya afya yake. Hakuweza kuamini majibu ya kipimo hiki, kwani kipimo kilisoma BP ni 130/92.
Baadae alimfuata Daktari aliyekuwa anamtibu mara kwa mara na alipompima pale hospitalini alikuta presha ikiwa 120/86 na kubaki mdomo wazi. Ilibidi daktari ashangae na kumuuliza mara mbili mbili siri ya muujiza huu na kuambiwa ni MAOMBI YALIYOFANYWA KWA JINA LA YESU. Mumewe Mariamu (ambaye bado ni muislamu) amemruhusu mkewe kuja Kanisani na kwamba atampa ushirikiano wote maadamu ndipo penye uponyaji.
Mariamu kwa hiari yake amemau kuokoka tarehe 24/07/2016, kwa kumpa Yesu Kristo maisha yake yote. SIFA HESHIMA NA UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.