GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 14 AUGUST 2016
Na:
STEVEN NAMPUNJU – (RP MOROGORO)
Michoro ni nini? Neno “michoro” humaanisha
lugha ya mawasiliano. Michoro ni wazo la kiufundi. Endapo fundi-nyumba anataka
kujenga jengo fulani, huchora michoro na mtu yeyote mwenye uwezo wa kuisoma
michoro ataweza kujua mchoro wa aina ile umelenga kitu gani. Hata mafundi-umeme
vivyo hivyo, kwa kuitumia michoro iliyochorwa katika karatasi huweza kuitumia
na kujenga taswira halisi ya kile ambacho kinatakiwa kufanywa. Katika ulimwengu
wa roho ili mtu uweze kufanikiwa lazima uwepo mchoro. Na ili mtu aharibikiwe,
lazima pia uwepo mchoro.
Katika Kitabu
cha MWANZO 4 tunamuona Kaini na Habili wakitoa sadaka zao lakini ile ya
Kaini ikakosa kibali machoni pa Mungu bali
ile ya Habili ilikubalika. Kaini alimuinukia ndugu yake akamuua, na Mungu akamwekea Kaini alama (mchoro) ili popote atakapoonekana auawe. Hata hivyo Kaini
alimuomba Mungu na mchoro ule ukabatilishwa.
Imeandikwa katika KUTOKA 31:1-11... (Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2
Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa
kabila ya Yuda; 3 nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na
ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa
dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na
kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. 6 Tena, tazama,
nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani;
nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate
kufanya vyote nilivyokuagiza; 7 yaani, hema ya kukutania na sanduku la
ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;).
Mungu alimwambia Musa kuhusu watu aliowachagua ilikuifanya kazi ya kubuni wa
ufundi na ustadi. Kumbe upo uwezekano wa kutimiza kusudi la Mungu kwa kufuata
mchoro ambao Mungu ameukusudia maishani mwake.
Katika KUTOKA
35:30-35 Imeandikwa.....(Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni,
Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya
Yuda; 31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na
kazi ya ustadi kila aina; 32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya
dhahabu, na fedha, na shaba, 33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti,
atumike katika kazi za werevu kila aina.34 Naye amemtilia moyoni mwake ili
apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani. 35
Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya
mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi
za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na
ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi
za werevu. )... Mungu alimwekea Bezaleli
mwana wa Uri roho ya ubunifu na ujuzi.
Kupitia mtu huyu, kile ambacho Musa aliambiwa akifanye, aliweza kukifanya
kwa kuhamisha fikra zake Musa (kupitia mchoro) na kutengeneza kitu jinsi ile
ile ambayo Musa laitaka kifanyike.
Imeandikwa katika 2NYAKATI 2:1-7...(
1 Basi
Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, na kuujengea ufalme wake
nyumba. 2 Sulemani akahesabu watu sabini elfu wawe wachukuzi wa mizigo, na watu
themanini elfu wawe wachongaji milimani, na elfu tatu na mia sita wawe
wasimamizi wao. Sulemani akatuma watu kwa Hiramu a mfalme wa Tiro, akisema,
Kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi, ajijengee nyumba ya
kukaa, unitendee na mimi. 4 Angalia, najenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu
wangu, ili kumfanyia wakfu, ya kufukizia mbele zake fukizo la manukato, na ya
mkate wa wonyesho wa daima, na ya sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na
za siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa za Bwana, Mungu
wetu. Hili ni agizo la milele kwa Israeli. 5 Nayo nyumba nitakayoijenga ni
kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote. 6 Lakini ni nani
awezaye kumjengea nyumba, ikiwa mbingu hazimtoshi, wala mbingu za mbingu? Nami
ni nani basi, hata nimjengee nyumba, isipokuwa kwa ajili ya kufukizia fukizo
mbele zake? 7 Unipelekee basi mtu mstadi wa kazi ya dhahabu, na ya fedha, na ya
shaba, na ya chuma, na ya urujuani, na nyekundu, na samawi, mwenye kujua
kuchora machoro, pamoja na wastadi walioko Yuda na Yerusalemu pamoja nami,
aliowaweka baba yangu Daudi.). Kumbe mchoraji aweza kuwepo nchi moja na
akashirikiana na wachoraji wa taifa linguine. Na hapa tunamuona Selemani akitoa
picha ya jengo linaloenda kujengwa kuwa ni
kubwa mno kwa sababu Mungu wake ni Mkuu kuliko miungu yote. na kwamba
huyo Mungu wake,mbingu na mbingu hazimtoshi. Hadi sasa tumejifunza kuwa
- Ni Lazima uwepo mchoro ili kutimiza kile ambacho Mungu amekikusudia kwako.
- Mchoraji mmoja anaweza kuchora mchoro na wachoraji wengine wakautafsiri na kuutekeleza vile vile.
Katika YEREMIA
5:25-27 Imeandikwa....(Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu
zimewazuilia mema msiyapate. 26 Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu;
huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. 27 Kama
tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa
wakuu, wamepata mali. 28 Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa
matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui
haki ya mhitaji.). tunajifunza
kuwa kumbe hata katika watu wa Mungu, wanaweza kupatikana humo watu wachora
michoro wanaopelekea wengine kuharibikiwa. Wapo wanaoandaa mchoro kumzuia mtu
asiolewe, kwa kuandaa majini maalumu ya kuzuia mtu asiolewe au asizae n.k. na baadae kuwaweka wasimamizi wa
mchoro ambao ni majini. Chanzo cha yote haya ni
mtu mmoja katika ulimwengu wa roho ambaye alikaa na kubuni yote hayo.
Katika Kitabu
cha KUTOKA, Mfalme yule aliyetokea asiyemjjua Yusufu alitangenza mchoro wa
kuwadhibiti Israeli wasizaliane kwa kasi. Mchoro huu ulizuia watoto wa kiume
kuuawa wakati wa kuzaliwa.
Mfano mwingine wa mtu aliyewahi kuchorewa mchoro ni
Daniele. Imeandikwa katika DANIEI 6:1-9.....
(Ilimpendeza
Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; 2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli
alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora
ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote. 4 Basi
mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa
habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana
alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. 5 Ndipo wale
watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika
mambo ya sheria ya Mungu wake. 6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika
pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele. 7 Mawaziri
wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya
shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye
yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda
wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba. 8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi
maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza
kubadilika. 9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.) Katika maandiko haya
tunaona namna kikao cha mchoro kilivyoitishwa na kuhitimishwa kuwa lazima iwepo
sheria ya kumtenganisha Danieli na Mungu wake kwa sababu hakuwa na kosa la aina
yoyote katika maisha yake.
Imeandikwa katika MATENDO 23:12-16 ...(Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano,
wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. 13
Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. 14 Nao wakaenda kwa
wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata
tumwue Paulo. 15 Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari
amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi
tu tayari kumwua kabla hajakaribia. 16 Mjomba wake Paulo akasikia habari za
kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.).
Mipango yoyote inayofanywa huenda sambamba na maombi. Kumbe watu waovu wanaweza
kujifunga kwa viapo vya kufunga bila kula wala kunywa ili kutekeleza michoro
yao. Leo tunawatangazia wale waliojifunga kwa kipao wafe kwa njaa zao kwa Jina
la Yesu.
RP Steven Nampunju akifundisha kuhusu Michoro ya Uovu hapo Jumapili 14/8/2016 ndani ya Bonde la Maono - Ufufuo na Uzima Moorogoro. |
Wapo waliochorewa michoro ya kufukuzwa kazi,
michoro ya kupata ajali, michoro ya
mauti na wasimamizi wa michoro wapo tayari na pengine unatembea nao. WASIMAMIZI WA MICHORO hawa siyo wa kawaida
bali ni wale wanaoaminiwa na wachora michoro,
kwa sababu wanao uwezo wa kutekeleza kile kilichoamriwa na wachora
michoro jinsi ile ile.
UKIRI
Michoro ya kishetani na kichawi, naifuta
michoro yao kwa Jina la Yesu. leo kwa Jina la Yesu naoichoma michoro yote kwa
Jina la Yesu. wewe uliyepandwa ndani yangu nakulazimisha toka kwa Jina la
Yesu. Leo niachie kwa Jina la Yesu.
|
Wachoraji michoro katika ulimwengu wa roho huwa
wamesharatibu hatima ya maisha ya mtu, ingawa kimsingi unaweza kujiona uko mzima
kabisa. Maana yake wapo watu wanatembea na michoro ya uovu wanatembea nayo bila
wao kujua. Kinachosubiriwa hapo ni muda ulioratibiwa wa utekelezaji wa ujenzi wa michoro husika.
Ndiyo maana wapo watu wanapatwa
na tatizo laaina fulani na baadae tatizo
la aina nyingine liinafuatia.
RP Steven Nampunju na Watendakazi wengine wakiombea watu waliofika ibadani na ambao wenye matatizo ya Michoro ya Uovu maishani mwao ili kuwafungua wawe huru kwa Jina la Yesu. |
NAMNA YA KUKABILIANA NA MICHORO YA UOVU
1
Kumwamini Yesu.
Kwa mtu ambaye anaishi
maisha ya dhambi, kutampelekea mtu
kukosa Baraka zake ambazo Mungu alikusudia. Imeandikwa katika YEREMIA 5:25....(Maovu yenu yameyageuza haya, na
dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.). Kumbe maovu yanaweza kuzuia
mema yasimpate mtu. Siyo kila siku anayepatwa na matukio na mtenda Dhambi, lakini kwa mtenda dhambi kupatwa na mambaya
ni kawaida. Kwa mtu aliyemwamini Yesu anaongozwa na Roho wa Mungu. Dhambi ina
kinywa, inaweza kutafuna na kumeza kabisa kile
ambacho kilikusudiwa na Mungu. Dhambi zipo katika makundi mawili:-
Ø
Kufanya
kile ambacho Mungu amekataza usifanye.
Ø
Kufanya
kinyume na kile ambacho Mungu ameruhusu kufanya
2
Kuwachafulia usemi
au lugha zao:
Imeandikwa katika MWANZO 11:1-9...(Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi
mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare
katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali
tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya
chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike
mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate
kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara
waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa
moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa
hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko,
tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana
akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana
alipoichafua lugha ya dunia yote; na
kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.)
Katika maandiko haya, Mchoro wa Mungu
ulikusudia watu watawanyike duniani kote. Hata hivyo, mchoro wa wanadamu
ulikudia kuweka mnara ili hata
wakitawanyika warudi pale pale. Wapo
watu wanapitia shida fulani kwa sababu ya mnara uliochorwa kwa ajili yao. Zipo familia ambazo matatizo waliyo nayo
yanafanana, kiasi kwamba hata watu
wakitaka kuoa huzigopa familia za aina hii. Wachawi wanaweza kuchora michoro ya
kuifanya familia iwe ni ya kushindwa, familia inakuwa ndoa hazidumu, watu wa
familia korofi n.k.
Katika 1WAKORINTHO
3:9 Imeandikwa...(Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu;
ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.). Je wewe umepandiwa nini?
Mkulima aliyekupandia ni nani? Kama watendakazi wa ibilisi wakikupandia maovu
ndani mwako (majini mahaba) basi ujue unaweza kufanyika jengo la ibilisi.
Imeandikwa katika ISAYA 49:16...(Tazama, nimekuchora katika vitanga vya
mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.). Kumbe Mungu naye
ni mchoraji. Mungu anaweza kumchora mtu
katika vitanga vya mikono yake. Kama Mugu anaweza kuchora uwe na hakika kuwa
hata ibilisi naye anaweza kukuchora
katiika vitanga vya mikono yake katika ulimwengu wa roho.
UKIRI
Mchoro wowote uliochorwa na mashetani leo
nakabiliana nao kwa Jina la Yesu. Naamuru uniachie kwa Jina la Yesu. Wewe
uliyetawala maisha yangu, leo niachie kwa Jina la Yesu. Amen
|
3
Kuwa Mwaminifu mbele za Mungu unayemtumikia.
Tumeona kuwa Danieli pamoja na kwamba watu
walimchorea michoro ya uovu, hakubadilisha mahusiano yake na Mungu, na badala
yake aliendelea na ratiba yake ya kuomba mara tatu kwa siku, tena hadharani bila kujificha.
Leo tunaenda kuikabili michoro yote kwa Jina la
Yesu. ni kweli wametoa kafara za ng’ombe na za watu lakini leo kila aliyechimba
shimo atatumbukia mwenyewe kwa Jina la Yesu.
kwa wewe ambaye hujaokoka leo
fanya maamuzi binafsi ya kupokea Yesu maishani mwako na kuwa huru kwatika Jina
la Yesu.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T)
CHURCH
==GCTC==
Tel: +255765979866 / or +255713459545
MOROGORO CHURCH
|