GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 07 AUGUST 2016
Na:
STEVEN NAMPUNJU – (RP MOROGORO)
&
&
Dr. GODSON ISSA ZACHARIA –
(SNP MOROGORO)
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 07 AUGUST 2016
Na:
STEVEN NAMPUNJU – (RP MOROGORO)
Dr. GODSON ISSA ZACHARIA –
(SNP MOROGORO)
Somo: MWENYE NGUVU WA MAISHA YANGU
Mwenye nguvu wa maisha yako ni viumbe vya rohoni ambavyo vina uwezo wa
kuzuia mtu asipate kitu fulani anachokitafuta. Mathalani washirikina wanapotaka
kumtia mtu utasa, hutafuta katika ulimwengu wa roho na kulipata jini lenye
uwezo wa kuzuia mtoto asikae tumboni mwa mama.
Mwenye nguvu “ni aliye na uwezo wa kufanya jambo fulani”. Hii haimaainishi kwa wandamu peke yake. Lahasha. Ndiyo maana
hata wanyamakazi huchaguliwa wale wenye nguvu na kujaribishwa kama wanaweza
kulima au la. Maana ingine ya “mwenye
nguvu”, ni mtu yeyote ambaye anatumia nguvu zake kupata haki fulani
ijapokuwa siyo mara zote hiyo haki ni haki yake. Mathalani, majambazi hutumia
nguvu zao kupora, na hivyo anachopora siyo halali yake. Katika LUKA 11:21-22 Imeandikwa...(Mtu
mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi
salama; 22 lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda,
amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka
yake.). Tunajifunza kumbe yupo mwenye nguvu ambaye ameyatesa maisha
yako (wachawi, majini, waganga wa kienyeji, n.k). Mwenye nguvu anakuwa amevaa
silaha na hataki mchezo. Ili uweze kuchukua chochote ndani mwake sharti
umfunge kwanza.
RP Steven Nampunju akifundisha somo la Mwenye Nguvu wa Maisha Yangu, katika ibada ya Jumapili 7/8/2016 Bonde la Maono - Mkundi, Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Imeandikwa katika 2SAMWELI 22:17-20... (Alipeleka kutoka juu, akanishika; Akanitoa
katika maji mengi; 18 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale
walionichukia; Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. 19 Walinikabili siku ya msiba wangu; Lakini
Bwana alikuwa tegemeo langu. 20 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya
kwa kuwa alipendezwa nami.). Daudi aligundua kuwa adui zake walikuwa na
nguvu kuliko yeye. Daudi alijua kuwa nguvu za adui zake kama akina Goliathi na
Mfalme Sauli zilikuwa kubwa kumzidi lakini hata hivyo Bwana alimsaidia
kuwashinda. Nataka nikuambie siku ya leo kuwa yupo Yesu aliyewashinda wenye
nguvu naye atakushindia katika jaribu lako kwa Jina la Yesu. Wenye nguvu
walinikabili nisiolewe, Wenye nguvu walinikabili nisifanikiwe, Wenye nguvu
walinikabili nisisome n.k. lakini Yesu anazo nguvu kuwashinda hawa wote.
UKIRI
Bwana yesu naomba ukanisaidie, ukaniokoe
na adui yangu mwenye nguvu. Amen
|
MIFANO YA KIBLIA YA WALIOKABILINA NA WENYE NGUVU
Imeandikwa katika DANIELI 3:8-17....(Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia,
wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi. 9 Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza,
Ee mfalme, uishi milele. 10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu
atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na
zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya
dhahabu; 11 na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto
uwakao. 12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya
Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme,
hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya
dhahabu uliyoisimamisha. 13 Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na
ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu
hao mbele ya mfalme. 14 Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na
Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala
kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? 15 Basi sasa, kama mkiwa tayari
wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na
santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu
niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru
iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
16 Ndipo Shadraka, na
Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja
kukujibu katika neno hili. 17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza
kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.) Meshaki, Shedraki na
Abednego waliwahi kukabiliana na mfalme mwenye nguvu ambaye alitaka watu wote
katika ufalme wake waisujudu sanamu ya dhahabu aliyoitengeneza. Na kwa sababu ni mwenye nguvu alitoa tishio
la kuwatupa wasioabudu sanamu yake. Wenye nguvu walikuzuia usipate ajira. Wenye
nguvu walikuzuia usisome lakini hata baada ya kusoma wamekuhamisha kutoka
gereza lile na kukupeleka uhamishoni (gereza la kukosa ajira). Hata hivyo Mfalme Nebukadreza pamoja na
vitisho vyake akina Meshaki, Shedraki na Abednego hawakumjibu. Hata wewe usijibizane na hao wenye nguvu, bali mwachie Bwana Yesu awashughulikie.
Katika ISAYA
1:18-20 Imeandikwa...(Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi
zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa
nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. 19 Kama mkikubali na kutii mtakula
mema ya nchi; 20 bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana
kinywa cha Bwana kimenena haya.). Mwenye mamlaka ana uwezo wa kuamuru
nini kifanyike. Kumbe hata Mungu wetu ambaye ni mwenye nguvu sana kuppita wote anaweza kuwanagamiza kwa upanga wale wasiotii kwa kuwa Yeye ni Mwenye Nguvu.
Imeandikwa katika 1WAFALME 20:16-22... (Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe
usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana? 17 Akasema, Naliwaona
Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. Bwana
akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. 18
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema,
ila mabaya? 19 Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana
ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande
wa mkono wake wa kuume na wa kushoto. 20 Bwana akasema, Ni nani
atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema
hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi
nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa
pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na
kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa
uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako.
24 Ndipo akakaribia Zedekia, mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu,
akasema, Roho ya Bwana alitokaje kwangu ili aseme na wewe? 25 Mikaya
akamwambia, Angalia, utaona siku ile utakapoingia katika chumba cha ndani ili
ujifiche. 26 Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya, mkamrudishe kwa Amoni
mkuu wa mji na kwa Yoashi mwana wa mfalme; 27 mkaseme, Mfalme asema hivi,
Mtieni mtu huyu gerezani, mkamlishe kwa chakula cha shida, na maji ya shida,
hata nitakaporudi kwa amani. 28 Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana
hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.). Mungu alikusudia
kumwangamiza Ahabu na familia yake. Mfalme Ahabu ambaye ni mwenye nguvu wa
nchi, anaamuru Mikaya akamatwe na kulishwa chakula cha shida. Chanzo cha haya
yote ni mwenye nguvu.
Je, maisha unayoishi ni ya shida? Ukiona hivyo,
yupo mwenye nguvu aliyeamuru uishi jinsi unavyoishi. Leo kataa huyo mwenye
nguvu wa maisha yako, amuru mwenye nguvu wako akafie huko huko vitani alikoelekea na asikusumbue
tena kwa Jina la Yesu.
Wenye nguvu wamekuamulia usile vitu vya sukari. Chanzo cha Mikaya kukaa gerezani ni mwenye nguvu aliyeamuru hivyo. Mfalme anatumia jeshi lake kumsweka Mikaya ndani. Kumbe mwenye nguvu analo jeshi. Wanaopandwa kuzuia shida ya mtu siyo raia, ni majeshi ya pepo wachafu. Katika WAEFESO 6:12 Imeandikwa... (Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.). Hata wewe, chanzo cha taabu uliyo nayo ni mwenye nguvu wa maisha yako, na leo tutamshughulikia pamoja kwa maombi kwa Jina la Yesu.
Wenye nguvu wamekuamulia usile vitu vya sukari. Chanzo cha Mikaya kukaa gerezani ni mwenye nguvu aliyeamuru hivyo. Mfalme anatumia jeshi lake kumsweka Mikaya ndani. Kumbe mwenye nguvu analo jeshi. Wanaopandwa kuzuia shida ya mtu siyo raia, ni majeshi ya pepo wachafu. Katika WAEFESO 6:12 Imeandikwa... (Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.). Hata wewe, chanzo cha taabu uliyo nayo ni mwenye nguvu wa maisha yako, na leo tutamshughulikia pamoja kwa maombi kwa Jina la Yesu.
Katika kitabu cha KUTOKA, alitokea mfalme
asiyemjua Yusufu, na huyu aliamuru watoto wa kiume wa Kiebrania wanapozaliwa
wauawe. Farao aliwatumikisha Israeli kwa
kutumia uwezo wake nguvu za giza zikifanywa na mawakala wa shetani, yaani wachawi. Hata hivyo, pamoja na mambo yote hayo, Nyoka wa Musa ndiye aliyemeza nyoka wa wachawi
wa Farao.
Imeandikwa katika LUKA 11:21...( 21 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo
nyumba yake, vitu vyake vi salama; 22 lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye
atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa
akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake). Huwezi kulinda nyumba yako
kama hujavaa silaha. Kama hauna silaha maana yake utaonewa siku zote. Umepata
mchumba lakini siku si nyingi uchumba
unaisha. Umeanza biashara lakini baadae mtaji unakwisha ghafla. Hapo ujue tu
kuwa yupo mwenye nguvu amevamia maisha yako. Ili mwenye nguvu aweze kusafiri na
silaha zake na kuweza kumfunga mtu, lazima kuna kitu anataka aibe kil;ichoko
ndani mwako. Katika YOHANA 10:10 Imeandikwa... (Mwivi haji ila aibe na kuchinja
na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.).
Hayupo jambazi anayevunja nyumba ya mtu na kuondoka bila kuchukua chochote.
Mwenye nguvu mwingine akija ili kumzidi
mwenzake ataanza kwa kumfunga. Kufungwa
ni hatua ya kwanza. Je, wewe umefungwa? Hatua ya pili kukunyang’anya silaha zako. Mathalani ukiona huna amani kabisa kuomba.
Ukiona huna amani kabisa kwenda Kanisa
la Ufufuo na Uzima kwa visingizio mbalimbali, ujue tayari yupo mwenye nguvu
ambaye amekufunga na kukunyang’anyua silaha. Mwenye nguvu na mwenye silaha zake
anafungwa kwa magonjwa na baada ya hapo silaha ya maombi inakuwa haipo tena.
Kama leo umekuwa ni mzito wa kuomba ujue tayari silaha ya maombi
umeshanyang’anywa.
Mwenye nguvu akeshavamia maisha ya familia na
kuwanyang’anya mateka, atasababisha wanandoa kuanza kuuza vitega uchumi vyao
kama ardhi na kadhalika na kugawana pesa zake badala ya kuwekeza.
Katika MARKO
5:1-3 Imeandikwa....(Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya
Wagerasi. 2 Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye
ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini;
wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;)..
Huyu kijana aliingiliwa ndani na mwenye nguvu. Hata ukimletea nguo ili avae, atakachofanya ni kuzitoboa toboa ili
kuviharibu. Kijana huyu alikuwa akilala makaburini ingiawa nyuumba zilikuwepo. Mungu hakumuumba
asivae nguo. Mungu hakumuumba alale makaburini.
Imeandikwa katika 2NYAKATI 16:7-9 ...(Wakati ule Hanani mwonaji akamwendea Asa
mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala
hukumtegemea Bwana, Mungu wako, kwa hiyo limeokoka jeshi la mfalme wa Shamu
mkononi mwako. 8 Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye
magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea Bwana,
aliwatia mkononi mwako. 9 Kwa maana macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani
mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo
kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.).
Hanani mwonaji anampa mifano Mfalme Asa kwamba walipokuwepo wenye nguvu
lakini Mungu akamsaidia. Hata hivyo
mwishowe alikengeuka kwa kufanya makosa ya kutomtegemea Bwana.
Kuna mwanzo wa vita uiliyo nayo. Kama
ilivyokuwa kwa Asa, vivyo hivyo hata wewe ukimwacha Bwana katika maisha yako,
vita itainuka kwa sababu wenye nguvu wapo saa zote kukukabili.
Katika MARKO
5:5 Imeandikwa...( Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na
milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa
mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina
nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. 8
Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako
nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, a kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi sana
asiwapeleke nje ya nchi ile. 11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la
nguruwe, wakilisha. 12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe,
tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa.
Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote
likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa
baharini. 14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani.
Watu wakatoka walione lililotokea. 15
Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili
zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.). Jeshi la wenye nguvu
lipo ndani ya mwili wa mtu mmoja. Kijana huyu alipaswa kuwa mhubiri wa
Injili, lakini badala yake mfumo wa
maisha yake ukabadilishwa kabisa na mwenye nguvu. Mji wa wagerasi unaelekea
kuwa ni wa kibishara zaidi. Kiasili Wayahudi walikuwa siyo wala-nguruwe, na kwa
sababu hiyo ule mji watu wa mataifa
mbalimbali walikuwa wakikaa humo.
Wapo wenye nguvu wanaozuia mtu asifanikiwe
kabisa. Wanaweza kukaa ndani ya mtu fualni kukuzuia. Kama yule kijana
alivyozuia watu wasipite ile njia, ujue hata kwako, wapo wenye nguvu
wanaokuzuia usifanikiwe katika njia fulani ya maisha yako. Leo tunalazmisha
wenye kukuzuia wakuachie haraka kwa Jina la Yesu.
Wapo watu leo hii mmedanganywa na wenye nguvu.
Katika 2WAFALME 22 tunakiona kikao cha mbinguni kikifanyika na pepo alijigeuza
kuwa pepo la uongo na kusababisha manabii zaidi ya 400 kutamka uongo. Yumkini
ugonjwa ulio nao ni matokeo ya pepo kuwaingia madaktari na wakatoa maelekezo ya
ugonjwa huo, kumbe siyo kweli. Kama adui zako wameizika talanta yako, Ufufuo na
Uzima m=tunaamni kuwa tunaye Bwana Yesu
wa kutmegemea ili kwenda kufukua hazina hizo kwa Jina la Yesu.
Mwenye nguvu huondolewa na mwenye nguvu. Imeandikwa
katika 1PETRO 3:8...(Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa
ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu;
mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea
roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;). Tunaona kuwa, mwenye nguvu
shetani alipondwa kichwa chake na Bwana Yesu.
UKIRI
Bwana Yesu naomba unisaidie kuanzia leo na
kuanzia sasa naomba unipake mafuta ili nishindane na wenye nguvu wa maisha
yangu. Naomba uwezo na nguvu ya kuwashinda kwa JIna la Yesu. naomba unitie
alama ya ushindi lwa Damu ya Yesu. Amen
|
Imeandikwa katika DANIEL 7:7....(Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na
tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye
alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na
kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale
wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.). Wenye nguvu wana uwezo wa kutafuna. Mwenye nguvu
akiingia katika afya ya mtu, ataitafuna afya yake na kukanyaga mabaki ya hiyo
afya. Mwenye nguvu aweza kula biashara
yako, na mwishowe kuharibu hata mabaki
ya mtaji ulio nao.
ZIPO HATUA
SITA ZA KUMKABILI MWENYE NGUVU
1. Kumwendea: Akiwepo mwenye nguvu mahali popote, unatakiwa
umfuate. Endapo umeingia katika familia fulani, cha kufanya ni kumwendea mwenye
nguvu. Daudi alipoona watoto, wakeze na
mifugo imetekwa nyara na adui, alimu
2. Kumfunga: Hapa ni kuhakikisha kuwa hafurukuti wakati
akiwa chini ya mamlaka na uweza wako.
3. Kumnyang'anya silaha zote anazotegemea yeye: (wengine silaha za ni
majini, mahiriizi, uongo n.k)
4. Kutwaa mateka: Aliyekuwa na kazi nzuri ikaibiwa, aliyekuwa
na afya njema akaugua au kufa ghafla, unatakiwa sasa urudishe mateka yote.
5. Kumfyeka na kumwangamiza:
Hii ni kwa sababu atakuwa hana nguvu tena, wala hana chochote tena ni mtupu.
6. Kutapanya nyara
Kama wewe hujaokoka kwa maana ya kumwamini Yesu maishani mwako leo pokea uwezo
wa kumpinga mwenye nguvu wa maisha yako
kwa Jina la Yesu.
© MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T)
CHURCH
==GCTC==
Tel: +255765979866 / or +255713459545
MOROGORO CHURCH
|