GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH,
KANISA LA UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI -:-
02 OKTOBA 2016.
NA: BRUNO
(SNP IRINGA)
&
DR. GODSON
ISSA ZACHARIA (SNP - MOROGORO)
Dr. Godson Issa Zacharia (SNP - MOROGORO) katika maombi Jumapili 2/10/2016 Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bonde la Maono Mkundi - Morogoro |
Mungu alituumba kwa namna ya
kushangaza ili tuushangaze uilimwengu ili Yeye Mungu aonekane. Mungu
hakutuwekea mikono bure, Mungu hakutuwekea miguu bure, Mungu hakutuwekea macho
bure, Mungu hakutuwekea masikio bure bali vyote hivi tumewekewa ili kupitia
sisi tuushangaze ulimwengu kwa Jina la Yesu.
YOSHUA 1:3… (Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu
yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.). angani ni kila mahali,
baharini, darasani, ofisini n.k. ambapo nyayo za miguu yetu inakanyaga tayari tumepewa. Kuna
agaano au kiapo ambacho Mungu alimwapia Musa kwamba kila mahali nyayo zetu
zitakapokanyaga tayari tumepewa. Kama wewe ni maskini hizo ni akili zako
zinavyowaza. Mungu aliapa na mmoja. Mungu haapi na watu wote bali humtafuta mtu
mmoja kwa ajili ya watu wengine wote.
Hivi kwa nini ukanyage kwanza ndiyo upewe? Mungu alipotuumba
sisi, alituwekea viungo mbalimbali na vyote vina maana zake. Kila aliyeumbwa na
Mungu, kuna sehemu aliyobarikiwa nayo. Wengine kwenye mikono, miguu, kichwani, macho, usoni n.k.
Ipo nguvu ya Kimungu katika miguu na mikono yetu. Ukimuona mtu anaenda
kwenye udahili (interview) na mtu huyo akashindwa kuipata kazi aliyoiendea,
ujue tayari mtu huyu miguu yake imechukuliwa, na hivyo ile nguvu ya kutiisha,
kutawala na kumiliki haipo. Akienda interview mtu huyo anaenda bure na akirudi
anarudi bure.
Mungu alisema katika ISAYA
66:1…(Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa
kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa
kupumzikia ni mahali gani?). Kwamba Mungu anamiliki mbinguni aliko na
hata hapa duniani anamiliki. Imeandikwa katika UFUNUO 10:1-2 …(Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu
akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa
chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. 2 Na
katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa
kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.). Yohana anamwelezea
huyu malakia aliyeshuka toka mbinguni. Nguvu za huyu malaika zilikuwa katika
mguu wake wa kushoto, na hakuna chochote kitakachotoka baharini au nchi kavu
itakayomshinda.
Lazaro alipokufa, Yesu hakwenda nyumbani kwake hata zilipotimia
siku nne akiwa ameshazikwa kaburini na ananuka, ili kudhihirisha kuwa Yesu siyo
wa kuponya mafua na magonjwa madogo madgogo tu. Pamoja na kwamba Lazaro
alifufuliwa baada ya siku 4, Biblia inasema bado alikuwa amefungwa sanda katika
mikonno na miguu yake na leso
usoni, na Yesu akaamuru
afunguliwe aachwe aende zake. Hii kufungwa mikono na miguu lilikuwa tatizo
lingine kwa Lazaro. Kuokoka siyo tatizo, lakini tatizo ni pale unapookoka na
kuendelea na maisha huku miguu imefungwa, mikono na usoni kote kumefungwa. Je,
mtu wa aina hii ataziona lini hizo fursa? Mtu wa aina hii atatembea je
kuziendea fursa zilizopo? Ataenda je kwenye biashara? Ataziendea je kwenye
mafanikio yake? Lazaro alikaa katikati ya baraka tele, lakini mikono ya
kupokelea ilikuwa imefungwa. Hata leo hii watu wa aina hii wapo sana.
Askofu wa Iringa (SNP Bruno) akifundisha somo la "Kuifungua nguvu iliyoko kwenye mikono na miguu" katika Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro Jumapili 2/10/2016. |
Unamhitaji Kuhani wa
Bwana akutamkie nenoo ili upate haja za moyo wako. Yesu alitamka kwamba Lazaro
afunguliwe miguu, mikono na uso wake. Penina alikuwa na watoto lakini Hana
akiwa tasa. Hana alikuwa akienda Shilo kuabudu kila mwaka lakini hakupata mtoto
kipindi chote hicho. Hata hivyo, Mungu
alisababisha divine connections ya Eli
aingie hekaluni asubuhi ile ili amtamkie neno lenye kusababisha muujiza wake.
Hivi ulishajiuliza swali,
kwanini Petro alipokamatwa alifungwa mikono kwa minyororo lakini Paullo
na Sila walifungwa miguu kwa mikatale? Kwa kawaida, pale unapozaliwa kuna
wanaoweza kukuwahi kuikomesha nguvu yako. Uwezo wa Paulo na Sila ulikuwa
kwenye miguu kwa namna ya kuipeleka
Injili kwa Mataifa.
MATENDO 12:1-7 …(Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda
mabaya baadhi ya watu wa kanisa. 2 Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. 3 Na akiona ya
kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa
siku za mikate isiyochachwa. 4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia
mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na
kumweka mbele ya watu. 5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba
Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. 6 Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku
ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo
miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. 7 Mara malaika wa Bwana
akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni,
akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.). Ile nguvu ya Petro ya kutenda kazi
ilikuwa katika mikono, na alipokamatwa
mikono yake ikafungwa. Petro alikuwa
akiweka mikono yake juu ya wagonjwa nao wakapata afya tena.
MATENDO 16:16-24 ….(Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja
aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa
kuagua. 17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni
watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. 18 Akafanya
hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo,
Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 19 Basi
bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata
Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; 20 wakawachukua
kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi; 21
tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala
kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. 22 Makutano wote wakaondoka wakawaendea,
makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. 23 Na
walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa
gereza awalinde sana. 24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba
cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.). Paulo alipokamatwa
waliomkamata waliwahi miguu yake kwa kuwa kwenye iguu ya Paulo
ilikuwepo nguuv ya kuipeleka
Injili mataifa mabli mbali.
KUMBUKUMBU 8:15-18 ….(aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye
nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika
mwamba mgumu, 16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate
kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. 7 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono
wangu ndio ulionipatia utajiri huo. 18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye
nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama
hivi leo.). Mungu ndiye atupaye nguvu
yakupata utajiri, siyo nguvu ya kubeba zege, wala matofali n.k. na nguvu hi ni
ya rohoni. Endapo mtu hana nguvu hii, fedha haiwezi kuja kwako. Wapo wajanja
wenye uwezo wa kufunga nguvu hizi za rohoni kwa njia za kichawi. Na ndiyo maana
wapo wenye kutumainia nguvu za chuma ulete. Ukumbuke kwamba, toka enzi za
Yohana hadi sasa, ufalme wa mbinguni hutekwa na wenye nguvu na wenye nguvu ndio
huuteka.
Umati wa Watendakazi wakisikiliza kwa makini neno la Mungu, Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro Jumapili 2/10/2016. |
WAEFESO 3:20…(Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya
ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo
kazi ndani yetu;). Mungu alituumba na nguvu hii ya kimungu, na wachawi
ndiyo huiwahi na kuifunga. Kumbe kuna nguvu ya kumsaidia mtu kuwa tajiri, kuwa
na maendeleo, kuwa mhubiri n.k. na ndiyo nguvu walikuwa nayo akina Petro na
Paulo na Sila. Petro aliuchukua upanga wake na kumkata sikio mmoja wa wale
waliokuja kumkamata Yesu. Hata hivyo Yesu hakumwambia Petro autupe upanga wake
bali alisema aurudishe upanga alani
mwake kwa sababu yapo masikio mengi ambayo Petro angekuja kuyakata hata
baada ya Yesu kuondoka. Na hiki kiliwafanya Petro kufungwa mikono yake
alipokamawa kwa sababu ndani ya mikono yake ipo nguvu.
KUMBUKUMBU 28:6….(Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na
utokapo.). Unapoingia unatumia miguu na unapoondoka unatumia miguu hiyo
hiyo. Wapo watu ambao kutembea kwao ni bure na kurudi kwao pia ni bure. Wapo
watu ambao umuiliki wao wa pesa hauruhusu zizidi sh.50,000/= na ndiyo
maana wanapokuwa na pesa inayozidi hapo magonjwa mbalimbali hutokea na
kusababisha pesa hiyo isikae mikononi mwao.
Umaskini siyo kukosa magari au nyumba au pesa. Umaskini tafsiri
yake ni kuwa endapo una vitu kama vile
magari au nyumba au pesa lakini vyote hivyo haviwezi kuwasaidia wengine ujue wewe
bado ni maskini tena wa kutupwa. Mungu akikubariki anataka baraka zako
ziwasaidie na watu wengine. Mungu akikubariki ni kwa sababu uwalishe mayatima, wajane, ndugu na watu wengine.
Ukimuona Mfalme Suleimani, kila siku watu walikuja nyumbani kwake kula na
kunywa na kusaza. Kama unayo elimu na kwa elimu hiyo husaidii wengine wala
kulisaidia kanisa, ujue bado hujasoma. Msomi mzuri atatamani kusaidia wengine
nao wafikie hali aliyo nayo. Imeandikwa “Heri kutoa kuliko kupokea”. Siri kubwa ya kubarikiwa ni kutoa. Wengine
hawatoi fungu la kumi la viatu
vyao, nguo zao n.k.
KUMBUKUMBU 28:8…. (Bwana ataiamuru baraka ije juu
yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia
katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako). Maana yake, chochote
utakachotia mikono yako kitabarikiwa. Ukiandika mtihani, utafaulu huo mtihani. Ukiandika proposals za
miradi itafanikiwa. Hii ni kwa sababu ipo nguvu katika mikono iliyowekwa na
Mungu. Usidhani kiwango ulichobarikiwa
ni tayari, bado.
MARKO 16:15-18…(Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka;
asiyeamini, atahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa
jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata
wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya
wagonjwa, nao watapata afya.). Mikono ina kitu gani hata ukiiweka juu
ya mtu anapata afya? Je nini kitatokea endapo mkono wa kichawi utawekwa juu
yako? Kwenye mikono ipo nguvu, siyo ya kuponya magonjwa tu bali pia ya
kusababisha utajiri, nyumba, mali, n.k.
Kila utakayemkaribisha nyumbani kwako, kunakitu atakiacha
nyumbani kwako. Endapo ni mtumishi wa
Mungu umemkaribisha nyumbani kwako, kuna kitu atakiacha pale. Endapo utamkaribisha
mtumishi wa lusifa nyumbani kwako, ujue atakuachia nguvu za kichawi mahali hapo. Yule uliyemkaribisha
ndiyo chanzo cha matatizo kwenye nyumba
yako.
Endapo mtu hajaokoka, leo umeipata fursa nzuri ya kumwamini
Yesu na kuwa kiumbe kipya.
© Media and
Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|
Kwa Maelezo Zaidi ya Somo Hili au kuzipata CD zake wasiliana
nasi, au Bonyeza hapa chini kuingia katika
FACEBOOK yetu: