GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH,
KANISA LA UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI -:- 13
NOVEMBA 2016.
MHUBIRI: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP - MOROGORO)
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia (SNP Morogoro) akifundisha Neno la Mungu ibadani Jumapili 13/11/2016 Bonde la Maono. |
Katika ZABURI
91:1-3 imeandikwa maneno haya ya Mungu…(Aketiye mahali pa siri pake Aliye
juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na
ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa
mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.). Kumbe ni ahadi ya Mungu kwetu kutuokoa
dhidi ya mtego wa mwindaji. Kwa hiyo uwe na uhakika kuwa mtego upo. Maana yake tayari upo mtego uliotegwa ukunase au tayari pengine mtego huo umeshakunasa
tayari. Mungu hawezi kusema uongo kama ilivyoandikwa katika HESABU 23:19…(Mungu si mtu, aseme uongo; Wala
si mwanadamu, ajute;Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?). Tena imeandikwa tena katika 1SAMWELI 15:29 ….(Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli
hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.).
Tunajifunza kuwa Mungu hasemi uopngo lakini wanadamu wanaweza kusema uongo. Mwanadamu hata kama ni ndugu au mwanasisasa
anaweza kusema uongo. Wapo wanadamu wengine wanaweza kuweka ahadi za kuoa
lakini mwishowe wakaghairi, kumbe wote huo ulikuwa ni uongo.
Katika TITO
1:2 imeandikwa…( katika
tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu
milele;). Kwa hiyo Mungu huyu
huyu anaposema atatuokoa na mtego wa mwindaji anamaanisha juu ya neno lake. Pengine
ipo mitego ama kwenye ndoa yako, masomo
yako, au biashara yako. Mungu ameahidi kuutuokoa na aina hizi zote za mitego.
Mitego huwekwa kwa siri. Haiwezi kuwekwa
mahali peupe pa kuweza kuonekana. Lengo la kuuficha mtego ni ili uweze kumkamata yule aliyetegwa. Imeandikwa
katika MHUBIRI 9:12…(Maana
mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya,
na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati
mbaya, unapowaangukia kwa ghafula.). Kumbe hii ndiyo leseni namba
moja: Kwamba maadamu u MWANDAMU, ujue lazima utanaswa na wategaji. Kwa
kuwa wewe ni mwandamu, mtego unaweza kunasa maisha yako tena katika wakati
mbaya. Huu ni ule wakati unapojiona upo sawa, hakuna shida yoyote lakini kumbe
mtego wa mwoteaji (shetani) upo kwa ajili yako. Mambo ya aina hii hufanyika kwa
ghafla. Leo tutaitegua aina hii ya mitego kwa Jina la Yesu.
Umati wa Watendakazi wakifuatilia mahubiri, Jumapili 13/11/2016 katika Bonde la Maono Mkundi Morogoro. |
Imeandikwa katika ISAYA 24:17….(Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee
mwenye kukaa duniani.). Hii ni leseni namba mbili, kwa kuwa MWANADAMU
UPO DUNIANI. Ili mradi unakaa
Morogoro, Mkundi, n.k. ambapo kote huku ni duniani, vitu vyote hivi: hofu,
mashimo na mitego ipo kwa ajili yako vimewekwa kukuandama ili unaswe.
Mungu aliyeziumba mbingu na nchi anazungumzia
kukuokoa wewe na mtego wa mwindaji.
Mambo muhimu manne ya kuangalia katika somo hili la kuiteegua mitego ya
mwindaji ni haya yafuatayo:
1.
Mtego wenyewe:
Hiki chaweza kuwa ni kifaa, maneno, hirizi n.k chenye uwezo wa kunasa ndoa,
biashara, watoto, elimu, kazi, nyumba, afya n.k. Hili ni tegemeo la mtegaji. Kupitia
mtego kile kilichowindwa lazima kitanaswa tu.
2.
Mwindaji / Aliyetega Mtego
Huyu
ndiye mwenye kitengo cha kuratibu shughuli nzima ya kuwinda na kunasa
watu (mastermind). Kimsingi huyu awza kuwa ni mchawi, mwanadamu, pepo n.k. mwindaji
huyu anajua kila kitu kumhusu yule
anayetegwa, na anajua jinsi ya kutega na
mbnu zote za kufanya haddi kufanikiwa.
Mfano, mwindaji akijua huyu binti ni mlokole safi
na haingiliki ovyo ovyo, atatafuta mbinu
za kumnasa!!. Pengine atatafuta kukufahamu, na kugundua kumbe shida kubwa ya
huyu binti ni anatafuta mchumba, na atatumia mbinu ya kuigiza kuwa naye ni
mpendwa. Kumbuka kuwa hata Shetani katika kumjaribu Yesu (LUKA 4), alipoona ameshindwa kabisa mbinu zote, shetani
aligeuka kuwa mhubiri na kutumia neno la Mungu kumwambia Yesu kuwa, ajirushe
chini
“kwa kuwa imeandikwa Mungu atatuma malaika zake ili wakuokoe usijikwae mguu wako katika jiwe”!!!
Ndivyo afanyavyo hata mwindaji katika uwindaji wake, atajigeuza kuwa mwenye kulijua
neno la Mungu kumbe ni mbinu tu, siyo kweli.
Shetani Akipigwa kabisa na Mitego yake ikeshateguliwa, furaha tele hutokea kama unavyoona hapa pichani. |
UKIRI
Leo yeytoe anayekuja kwa ngozi ya kondoo
ilihali ni mbwa mwitu tutamponda kwa Jina la Yesu.
|
3.
Aliyetegwa
Huyu ni mwanadamu ambaye ametegwa mtego lakini
bado hajanaswa. Ili mradi mtu unaishi duniani, mwindaji mwenye mtego atakutega
tu. Utakuwa hujui utenaswa lini au wapi. Ndiyo maana imeandikwa katika MHUBIRI 9:12…(Maana mwanadamu naye hajui wakati
wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa
mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa
ghafula.). hawa watu wa aina hii hawakati tamaa hadi wanase.
UKIRI
Kwa Jina la Yesu,
leo ewe mtego ulioficaham ninakufayatua kwa Jina la Yesu. Ewe mtego uliyetega
ndoa yangu, watoto, biashara, juu ya masommo, juu ya afya ninakutegeua kwa
Jina la Yesu. Amen
|
Inategemea hali ya maisha uliyo nayo wewe
uliyetegwa iko je. Wewe ni silaha za Bwana? Wewe ni jeshi la Bwana? Je, wewe ni
mtoto wa Mungu kama Biblia inavyosema katika YOHANA 1:12 (Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;)? Je, wewe
ni mpiganaji au mtu wa dini tu unayekuja kanisani ili kuombewa na kuondoka?
Cha kufanya ni kufanya vita na kuwapiga wale walioitega
mitego maisha yako. Kwa kuwa mimi ni silaha za Bwana, nitalivunja gari la vita.inajalisha unafanya
je? Mungu siyo mwanadamu hata aseme uongo, maana yake ameshaona mitego ipo.
Yesu akasema hata mkila vitu vya kufisha havitawadhuru, maana yake alishaona
mitego inaweza kuwekwa hata kwenye vyakula na vinywaji. Usikae kama wafanyavyo
watu wa dini. Ninakuonya wewe unayekumbatia mambo ya dini, kwa kuwa kupitia
hiyo dini mitego itakunasa tu maadamu upo duniani. Anayeokoa ni Bwana Yesu, siyo elimu yako ya Masters, au
PhD, bali ni Bwana Yesu atakuokoa na mtego wa mwindaji. Kazi uliyo nayo
haitakuokoa. Miradi uliyo nayo
haitakuokoa, ni Bwana Yes utu wa kuweza kukuokoa na mitego ya mwindaji.
Mungu hajasema eti alishakuokoa na mitego ya
mwindaji. Mungu anasema atakuokoa. Itategemea jinsi wewe utakavyojitoa kwake,
kwenye mkesha unaomba, unatoa sadaka, unafanya kazi za Bwana n.k. na kwa
kupitia haya ahadi ya Mungu ya kukuokoa
nah ii mitego inafanyika urithi kwako. Kumbuka kuwa wanaokuwinda wewe ni wengi
kuliko nywele zako. Hao ndiyo wategaji sasa: kwenye afya yako, sura yako, biashara yako, n.k na hata kukunasa.
4.
Walionaswa tayari na mitego
Baada ya kusdhindwa katika hatua ya tatu,
unaingia katika hatua hii ya nne ambapo tayari unakuwa umenaswa. Kwa wapumbavu
watafia kwenye aina hii ya mitego, pengine ni mimba lakini imeandamana na
Ukimwi. Hata hivyo kwa mwenye hekima atagundua kuwa amefanya dhambi, pengine
ana mimba tayari na ataitubu dhambi yake. Mtu wa aina hii atamuomba Bwana Yesu
amsaidie na kumukoa tena, atmwambia Bwana “Kwa kupigwa kwako nimepona”
nisaidi Bwana. Ni kweli umenaswa lakini
kaa ndani ya Bwana, naye atakuokoa na
huo mtego kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Leo ninatoroka kwenye mtego wa mwindaji kwa Jina la Yesu.
|
Mwindaji ni shetani mwenyewe. Imeandikwa katika 2TIMOTHEO 2:26…. (wapate tena
fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata
kuyafanya mapenzi yake.). Mtego ukeshanasa, utajikuta unaishi maisha
kama yao. Kwa wavualana hata mavazi yao yatakuwa ya kubana na kujiita ni modal.
Wengine watafanya kama wao, kwa kuiga unywaji wa vinywaji ambavyo ni zero
alcohol. Mwisho wa yote haya mtu hugeukia kunywa kidogo kidogo hata kilevi
na kunywa hadi kufanana nao na kuwa mmoja wao.
Imeandikwa katika 1TIMOTHEO 3:7 (Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio
nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi). Wategaji hawa
hutumia wanadamu, na ukeshanaswa utakuwa
hujui cha kufanya tena ili utoke. Ndiyo
maana tumekatazwa “wala tusifuatishe namna ya dunia hii”!!!
Imeandikwa katika EZEKIEL 13:18 na 20-21 ..(18 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao
wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu
ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu
wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?... 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi
ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege,
nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile
mnazoziwinda kama ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu
wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa;
nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.). Ina maana Mungu asipokuja kinyume na hizo hirizi tayari
utakuwa umenaswa tu. Leo tunamkabili yeyote aliyekuwinda kwa Jina la Yesu. Wawindaji
hutega mitego lakini leo tunaenda kuitegua yote kwa Jina la Yesu. Kuna mitego iliyokamata ndoa yako, afya yako,
bisahara n.k. na tutaipasua yote kwa Jina la Yesu.
Tunataka kuomba leo na kuipasua hiyo mitego popote pale ilipotegwa. Njia pekee ya
wewe kutoka kwenye hiyo mitego ni kukimbilia
kwa Yesu, na kama hujaokoka au hata kama tayari upo ndani ya mtego uje na
kumfanya Bwana Yesu kuwa tegemo pekee la kukusaidia kupata ukombozi.
© Media and Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255765979866 / +255713459545
|