GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH,
KANISA LA UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI -:- 20
NOVEMBA 2016.
MHUBIRI: Dr.
GODSON ISSA ZACHARIA (SNP - MOROGORO)
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia akiwa anaomba kwa ajili ya ibada ya tarehe 20/11/2016. |
Imeandikwa katika 2 WAFALME 2:19-21…(Watu
wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri,
kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akasema,
Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda
mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema
hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza).
Kuzaa mapooza maana yake ni kuzaa kitu kilichokufa , au inalinganishwa na kuzaa kitu ambacho hakina uhai,au kwa maana nyingine ni kutokuzaa kabisa,au kwa maana nyingine ni kupukutisha matunda maana yake kuzaa kitu ambacho hakijakomaa .Unaweza ukaanzisha vitu vyako vizuri kabla havijakomaa vinakufa ,kwahiyo maana nyingine ya kuzaa mapooza ni kufa kabla ya wakati.Watu wa mji ule walipouangalia mji wakagundua mji ule ni mzuri lakini huzaa mapooza.
Imeandikwa katika MALAKI 3:11…(Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia
mimi, naam, taifa hili lote.Kwahiyo kupukutisha majani kabla ya wakati )…
Hii maana yake ni kuzaa mapooza.
Elisha alipoona mji ule una matatizo kwanza aliwauliza shida hii imeanzia wapi ,ni vizuri kujua chanzo cha tatizo ukishakijua chanzo cha tatizo ukakishughulikia utakua umemaliza tatizo,Elisha akaagiza aletewe chumvi akaagiza apelekwe kwenye ile chemchemi ya maji akatamka neno juu ya yale maji,ni vizuri kila unapokuja kanisani utamkiwe neno juu ya maisha yako,ni kweli wamepanda mapooza kwenye ndoa yako ,kwenye kazi yako,elimu yako lakini leo Bwana anakwenda kuweka chumvi kwenye chanzo cha tatizo lako na chumvi hiyo ni neno la kristo,neno la kristo ni uhai likaondoe mapooza kwenye shida yako,kile unachokiamini ndicho utakachokipokea ,wana wa Israeli walipofika jangwani wakaanza kumlalamikia musa na kumwambia ni bora ungetuacha misri kuliko kutuleta mahali hapa ,lakini Biblia inatuambia walifia wote jangwani walibaki watu wawili tu ,ushindi wako unategemea unatamka nini ,jifunze kutamka maneno ya ushindi hata kama unaona hamna kitu kinachoendelea wewe tamka maneno ya ushindi,
Ni kweli yamepandwa mapooza, jamii, kazi,
familia, katika maisha yako, lakini mimi leo nakuja kwako kama neno la Kristo.
Usihangaike na chumvi zinazotolewa na wahubiri mbalimbali nyakati hizi. Wengi
wao wanawaza kwa kuwa Elisha alitumia
chumvi basin a wao wautumie ufunuo huo huo. Ni kawaida endapo mtu utanyweshwa
chumvi nyingi kutapika lazima utatapika. Cha kufanya siyo kutumia chumvi bali
neno la Kristo kaw kuwa neno la Kristo ni kila kitu maishani mwetu.
Watu wa dunia hii ni wa ajabu sana. Endapo mhubiri ukiwa tajiri
sana watu hao watasema huyu ni free mason. Endapo mhubiri wa Bwana ukiwa
maskini na maisha yamekupiga sana na hata viatu huna, watu hao hao wataanza
maneno kuwa hawawezi kumfuata Mungu wa aina hiyo. Usiwe unakiri mambo hasi kwa
sababuukifanya hivyo maneno ya kinywa chako yatatimizwa vivyo hivyo kwa sababu
Mungu huyaangalia maneno yako ili ayatimize. Cha kufanya ni kukiri kuwa wewe ni
mshindi. Unppaswa kukiri kuwa utaishi na hautakufa, na kila siku hata kama upo
kwenye nyumba ya kupanga, anza kukiri kwa kinywa chako kuwa utajenga nyumba
tena ya ghorofa na utaishi, na wewe na watoto wako mtafanikiwa. Yapo mashetani
yanayofuatilia maneno unaotamka kinywani mwako. Endapo maneno yako ni negative
utapkea vivyo hivyo na kama maneno yako ni positive viyo hviyo utayapokea kwa
Jina la Yesu.
UKIRI
Leo
ninang’oa kila roho ya kuzaa mapooza kwa Jina la Yesu. Natangaza
kuanzia leo, mapooza yaliyotengenezwa kwenye kazi, elimu, ndoa na maishani
mwako, ninayang’oa yote kwa JIna la Yesu.
|
Katika kitabu cha 2WAFALME 2:19…(Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia,
twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji
yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.). Ukiisoma ayah ii vizuri
utagundua kuwa ni kweli mji huu ulikuwa
mzuri kw akila hali. Ni kama ambavyo hata leo hii mji wetu wa Morogoro watu
wanausifia kuwa ni mzuri, wakiupa Jina
la “Mji kasoro bahari”. Lakini pamoja na uzuri wote huu, mji huu huu watu
wanachukuliwa msukule. Mji unazaa mapooza: Watu hawajengi nyumba zao, na
wakijenga ujenzi haumaliziki;
Kazi yangu
ni nzuri lakini inazaa mapooza. Ndo yangu ni nzuri lakini inazaa
mapooza. Leo tunayang’oa kila mapando ya mapooza kwa Jina la Yesu. Pengine
una mume wako ulimpenda sana katika uchumba wako, lakini kwa kuwa hukufuata
taratibu za kanisa ukaanza kuishi naye bila ndoa. Yamkini mume huyo huyo
alikudanganya kuwa hata yeye anampenda Bwana Yesu ingawa siyo wa kanisani
mwako. Leo hii maisha yako yamekuwa magumu na ajabu kwa sababu mume huyo ni
mlevi na amekuwa akikuletea akina mama wengine ndani ya nyumba hiyo hiyo. Cha kufahamu hapo ni kuwa, ndoa yako
ilikuwa nzuri lakini imezaa mapooza.
UKWELI
KUHUSU KUZAA MAPOOZA KATIKA BIBLIA
Kwanza
jua kwamba Kuzaa mapooza na kufa ni jambo linaloanzia rohoni.
KUTOKA
23:26…(Hapatakuwa na mwenye kuharibu
mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.)
UFUNUO
6:8…(Nikaona, na tazama, farasi wa
rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu
akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na
kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.). Mauti inauvaa mwili na
kuanza kutembea. Vita yoyote uionayo maishani mwako inaanzia rohoni, na hata
ushindi pia huanzia rohoni.
WAEFESO
6:12…(Kwa maana kushindana kwetu sisi
si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza
hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.). Kwa
hiyo hata mapooza yanashughulikiwa
rohoni kwa panga za rohoni siyo za mwilini. Mapooza yanaanzia rohoni, yakiletwa
na shetnai ambaye naye ni roho.
Ndiyo maana unaona kuwa kama ni uchumba au
kazi mambo yanaanza viruri lakini nyuma yake yanakuwepo mapooza yamepandwa
ili kuharibu hatima yake.
YOHANA
10:10…(Mwivi haji ila aibe na kuchinja
na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.).
hapa wanaongelewa watu wa aina mbili: mmoja
(SHETANI) amekuja kwenye familia yako aibe mali, fedha, akili, watoto na
vingnievyo ili aviibe, aviharibu na avichinje. Wa pili ni YESU ambaye amekuja ili upate uzima
kwenye masomo, kwenye familia, ndoa, biashara na vinginevyo.
MALAKI
3:7..(Tokea
siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika.
Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,
asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?).
Biblia inasema kwa kitendo cha wababu walichofanya enzi hizo miaka hiyo kwa
sasa ipo vita inayokuandama ingawa wewe hukuhusika na kosa hilo.
UKIRI
Ninag’goa kwa Jina la Yesu. Ninnagiza vitu
vyangu vilivyoibiwa NJOO, Ninaagiza kazi yangu ilivyoibiwa NJOO, Ninnagiza
afya iliyoibiwa NJOO kwa Jina la Yesu.
|
MALAKI
3:8-11…(Je! Mwanadamu atamwibia Mungu?
Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani?
Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi,
naam, taifa hili lote.10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika
nyumba yangu, kanijaribu kwa njia hiyo,
asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni,
na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa
ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala
mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,
asema Bwana wa majeshi. 12
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema
Bwana wa majeshi.). Mungu anahesabu kitendo cha wewe kutokutoa kwako zaka na dhabihu
kuwa ni wizi wa kumwibia Mungu mwenyewe. Kumbe ukitaka anayekula maisha yako,
ni wewe kuleta zaka kamili nyumbani kwa
Bwana. Anayekula na kupanda mapooza katika familia yako ni shetani. Kupukutisha
ni hali ambayo unaanza vizuri lakini unashindwa kumaliza: Mfano unaanza masomo
lakini hhaufikii mwisho wake; unaanza kilimo lakini mwishowe ukame unaingia na
kusababisha usivune chochote; unashika fedha lakini zinaishia kwa matumizi
yasyoleta maendeleo kwako. Ni ahadi ya Mungu kwetu kuwa Bwana atachilia baraka
zake juu yetu endapo tutamtumikia, na kila atakayetuona aseme sisi ni heri.
Tunatangaza kuanzi leo uwe heri kwa Jina la Yesu. Wale waliokudharau waanze kukutafuta na kukuona wewe ni heri kwa
Jina la Yesu.
TUNANG’OA
JE ROHO ZA MAPOOZA?
YEREMIA
1:10…(angalia, nimekuweka leo juu ya
mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.).
Kwa maneno haya Mungu aliyeumba mbingu
na nchi, anasema hata wewe umewekwa juu ya falme, ukoo, nyumba
nilizokutega na kusababisha uzae mapooza, ili kungooa mapooza, kuibomoa nyumba
iliyobeba mapooza. Hata hivyo, ni wajibu
wako kuweka mambo yako vizuri na Bwana. Huwezi kung’oa mapooza kabla hujampokea
Yesu Kristo maishani mwako. Leo ni fursa pekee kwako kuweka sawa mahusiano yako
na Yesu ili uipate neema hii ya kung’oa mapooza maishani mwako.
© Media and Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|
ENGLISH