GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH,
KANISA LA UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI -:- 04
DESEMBA 2016.
MHUBIRI: STEVEN NAMPUNJU (RP - MOROGORO).
Usingizi ni njia mojawapo ya mtu kupumzika. Kila
aliyealala anakuwa na sababu zake za kufanya hivyo. YONA 1:1-6…(Basi
neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, 2 Ondoka, uende Ninawi,
mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele
zangu. 3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa
Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi,
akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso
wa Bwana. 4 Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa
baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika. 5 Basi wale mabaharia
wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena
iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka
hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. 6 Basi nahodha
akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu
wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee). Kila anayelala anacho
kitu cha kumfanya alale. Nahodha aligundua jambo kutokana na Yona kulaa usingizi. Kumbe mtu anaweza kuwa amelala, na
kitendo hicho kinaweza kuleta maangamizo. Ukiwa umelala huwezi kumuomba Mungu jambo lolote. Yona
anamkimbia Mungu kwa sababu anaijua mioyo
ya watu wa Ninawi.
UKIRI
Ewe uliyelaza maisha yangu, kwa sababu yoyote ile iliyaofana unilaze usingizini,
leo nakataa kwa Jina la Yesu.
|
Siku moja Yesu akasema “ninyi ni watoto wa bab yenu ibilisi…..”
Na kama ilivyo kawaida, mzazi yeyote akitaka kufanya kazi na papo hapo mtoto
wake akawa anamsumbua, mzaazi humbembeleza mtoto huyo na kumwimbia nyimbo nzuri
ili alale usingizi. Kwa maana hiyo, hata ibilisi kwa kuwa anao watoto wake wa
kiroho, endapo atagundua yupo mtoto wake anayemsumbua, atambembeleza na
kusababisha mtoto huyu alale usingizi ili afanye yale matukio ambayo alitaka
kuyafanya. Endapo utakataa kulala, mzazi wa kiroho (ibilisi na wachawi wake)
watashindwa kufanya yale waliyokusudia katika
maisha yako kwa Jina la Yesu.
Ukikataa kulala, ajali hazitakuwepo tena. Ukikataa kulala misukule
hawatachukuliwa tena.
Yona alikuwa na siri ya bahari kuchafuka
wakati wanaenda Tarshishi. Nahodha hata baada ya kutumia mbinu zote, ikiwemo
kupunguza shehena ya meli, lakini kumbe
mwenye siri ya mambo yale alikuwa ni Yona. Hata katika familia zetu, wapo watu
wenye siri ya mambo yanayoendelea katika familia hizo. Ni hadi pale aliyelala
katika familia hizi atakapoamka na kuelezea siri ya Bahari kuchafuliwa.
Tunagundua siri kuwa Kila anayelala, anakuwa na zile siri za matatizo ya
familia au taifa lake.
MATHAYO
8:23-27…(Akapanda chomboni, wanafunzi wake
wakamfuata.24 Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na
mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakamwendea,
wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. 26 Akawaambia, Mbona mmekuwa
waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa
shwari kuu. 27 Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo
na bahari zamtii?). YESU alikuwa na siri ya bahari kuchafuka. Yesu
baada ya kuamka alikuja na majibu. Kumbe kila anayelala anazo siri za
changamoto katika maisha ya watu wengine. Inawezekana hata katika familia zetu
ni vyema kuwaamsha wale wanaolala usingizi
kwa sababu wanazo sababu na majibu ya mafanikio ya watu na uhuru wao. Wachawi
ndiyo maana huwalaza watu wale wanahatarisha shughuli zao za uharibifu.
WARUMI
13:11…..(Naam,
tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa
maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini). Ipo
saa ya mtu kuamka usingizini.
WAEFESO
3:14…(Hivyo husema, Amka, wewe
usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na
Kristo atakuangaza.). Aliyesinzia ni kama aliyejiingiza mwenyewe kuwa
miongoni mwa waliokufa.
DALILI
ZA MTU ALIYELAZWA USINGIZI WA KIROHO.
1.
Mtu hawezi kutambua thamani ya kitu hadi kitu hicho kiwe kimeondolewa
kwake
Katika Biblia wapo watu wa aina hii. MATHAYO 27:51-54…( Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande
viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi
yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;53 nao wakiisha kutoka
makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea
wengi.54 Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu,
walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema,
Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.). Hata baada ya Yesu kuhubiri kwa muda mrefu, lakini Akida anamgundua Yesu ni mwana wa Mungu mwihsoni kabisa. Kwa mtu
aliyelazwa usingizi wa kiroho, hawezi kugundua thamani ya kitu hadi kitu hicho
kiondolewe kwake.
YOHANA
4:39-40…..( Na
katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke,
aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. 40 Basi wale
Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili.
41 Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya
neno lake. 42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya
maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu
ndiye Mwokozi wa ulimwengu..). Watu wa mji huu walimuamini Yesu pale tu waliposikia wenyewe
kwa masikio yao.
YOHANA
6:14…(Basi watu wale, walipoiona ishara
aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.).
Mtu aliyelazwa usingizini anaweza kuidharau
kazi anayoifanya, na ni hadi kazi hii aikose ndipo atakapogundua umuhimu wa
kazi yake ya awali. Mtu akeshaikosa kazi yake, ndipo hugutuka na kuanza
kuitamani imrudie tena lakini inakuwa haiwezekani tena.
2.
Ni mzito
kufanya maamuzi ya kuchukua hatua
Likiwepo jambo lolote la kufanyia maamuzi, mtu
wa aina hii huwa mzito sana kwa mambo ya kumfanya apige hatua. Linapotokea
jambo lisilo na faida, anakuwa mwepesi.
3.
Aliyelewa usingizi hawezi kutumia akili yake kuvumbua mambo mabli mbali.
Mungu ametupatia akili ili tuzitumie kama
msaada wa maisha yetu. Imeandikwa katika 1YOHANA
5:20…(Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili
kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli,
yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa
milele.). Kumbe Mungu anampa mtu akili ya kujua mambo mbalimbali. Ili
uunasue mtego inahitajika akili.
Aliyelazwa usingizini atakuwa anatumia
akili za watu wengine: akiona
wenzake wanafanya biashara fulani naye ataifanya kwa sababu hatumii tena akili
zake binafsi. Imeandikwa katika MITHALI
9:10...(Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu).
Ni hadi pale mtu anapomcha Bwana ndipo atakapopata hekima ya kufanya mambo bila
kuiga wengine wanavyofanya.
4.
Mtu aliyelezwa usingizi huridhika na hali
aliyo nayo hata kama ni mbaya na
haipendi.
Endapo mtu wa aina hii hana kazi, ataridhika
na hali kama hiyo, na atajitetea kwamba kazi hamna. Kwa mtu yule aliyeamka
usingizi, ataamua kutafuta kazi popote
ilipo hata kama elimu yake ni ndogo. Mtu
mwingine pengine ni mgonjwa, na ukitaka kumwombea atajitetea kuwa
ameshaombewa sana kwenye makanisa mbalimbali, na kwa hiyo haoni dalili za kupata uponyaji.
Leo usikubali kuridhika na hali uliyo nayo.
Hata kwa mtendakazi wa hapa kanisani, endapo atakuwa karidhika kukaa tu
kanisani bila kuwa na washrika wapya aliowahubiria na kuwaleta nyumbani mwa Bwana,
ujue hiyo ni dalili kuwa mtendakazi wa
aina hiyo amelazwa usingizini.
5.
Mtu aliyelazwa usingizi hawezi kudai haki zake
za msingi.
Uwezo wa kuthubutu au kuzidai haki zake
anakuwa hana, kwa mtu aliyelazwa
usingizi. Kwa kuwa akili ya mtu wa aina hii inakuwa inamilikiwa na mtu
mwingine, matokeo yake hataweza kujitetea au kudai haki zake.
MITHALI
28:1…(Waovu hukimbia wasipofuatiwa na
mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. ). Mtu muoga anakimbia
hata bila kuwepo kwa mtu anayemfuatilia. Makanisani, wakiwepo watu waoga
hujitetea kuwa hawezi kuomba na kufunga kwa sababu eti wanaogopa kuvitibua
vidonda vya tumbo.
6.
Mtu hawezi kutambua kusudi la Mungu maishani
mwake.
Kila mtu aliyeumbwa ana makusudi maalumu ya
kufanya hapa duniani. Mungu anapomuangalia mtu huitazama ile hatima yake siyo
hali yake, na ndiyo maana Biblia inasema
“Mungu huuangalia mwisho kabla
mwanzo kuwepo”. Kwa mtu aliyelzawa usingizi wa kiroho, hawezi kutambua
kusudi la Mungu maishani mwake.
Imeandikwa katika YEREMIA 1:4-5…(Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni,
nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana
MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.). Sehemu hii inatuonesha kusudi la Mungu maishani mwa mtu kuwa linakuwepo kusudi hata kabla aya
mtu huyo kuzaliwa.
Katika YEREMIA 1:10 Imeandikwa…(angalia,
nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na
kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.).
Kumbe katika moyo wa Mungu, kusudi la Yeremia kuwepo ni kwa namna kuu 4: za kung’oa, kubomoa, kuharibu
na kuangamiza. Kusudi la Mungu ndilo linalobeba siri ya mafanio
ya Mungu. Kusudi hilo ndilo linalompa
mtu kibali cha kuishi. Kama kusudi la
Mungu kwako ni kuwa mfanyabiashara,
taraji
UKIRI
Ewe roho ya usingizi nanakulazimisha
leo uniachilie kwa Jina la Yesu. Kila
rohon iliyolazamaisha angu, naishambulia kwa Damu ya Yesu. Maana imeadnikwa kila silaha
itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa.
|
7.
Mtu hushindwa kutambua uzuri wa mtu au ubaya
wa mtu mwingine
Mtu aliyelazwa usingizi hana uwezo wa kumtambua Musa wa maisha yake, ambaye atakuja na kumtoa Misri kwenye nyyumba
ya Utumwa.
Imeandikwa katika KUTOKA 8:1-2...(Bwana akamwambia Musa, Ingia kwa Farao,
ukamwambie, Bwana asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia. 2
Tena kama ukikataa kuwapa ruhusa, tazama, nitaipiga mipaka yako yote kwa kuleta
vyura;). Wapo mafarao wengi leo hii
waliokamata maisha ya watu. Musa ndiye mwenye uwezo wa kuongea na Farao,
kwa sababu ndiye aliyepewa kibali hicho na Mungu. Shida uliyo nayo leo hii ni kwa sababu hujamjua Musa wa maisha
yako ni nani. Pengine huwa unapishana na Musa wa miasha yako, bila wewe
kumfahamu.
Mungu
humtuma Musa kwa ajili yako baada ya kukiona kilio chako. Mtu aliyelazwa
usingizini hawezi kugundua Musa wake. Mara zote atalalamika kuwa watu wote duniani sio wazuri. Mtu mmmoja aliwahi kusema kuwa wanaume wote
duniani siyo watu. Mtu huyu alijisahau kuwa anaye baba mzazi na kwa maneno hayo
amemfanya hata baba mzazi wake aonekane kuwa siyo mtu!!!!
Imeandikwa katika LUKA 19:41-44 …(Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42
akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini
sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako
watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44
watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya
jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.). Yesu aliulilia
Yerusalemu, kutokana na matukio yaliyokuwa karibu kutokea mle ingawa watu wake
hawakuyajua.
8.
Mtu aliyelazwa
usingizi hawezi kuthubutu kufanya jambo jipya.
Mtu wa aina hii huyafanya tu yale anayoona
wengine wakiafanya. Hawezi kuthubutu kuanza jambo jipya
9.
Hapendi utekeleza majukumu yanayomhusu.
Tuliposoma katika YONA 1:1-6 tuliona kuwa YONA hakutaka kutimiza majukumu yake
yanayomhusu, na badala yake anakimbilia Tarshishi. Kwa mtu uliyeokoka, mojawapo
ya makusudio ya Mungu kwako yanayokuhusu ni kuwashuhudia wengine habari za
Mungu ili wengi waokoke. Waliolazwa usingizi hawashuhudii.
10.
Mtu aliyelzwa usingizi bidii yake ya awali
inakuwa haipo tena.
Imeandikwa katika MHUBIRI 7:7-8…(Kweli jeuri
humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa
huuharibu ufahamu. 8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya
kiburi.). kama mwanzoni ulikuwa unaisoma Biblia lakini kwa sasa husomi
tena, ujue upo usingizini, na umekosa wa
kukuamsha. Endapo unasema zamani ulikuwa unawaleta watu wengi kanisani lakini kwa sasa hufanyi
tena ujue umelazwa usingizi.
Wachawi wataendelea kumpandia mtu magonjwa na
kila aina za mateso kwa sababu mtu huyo wamemlaza. Ni jukumu lako kukataa
kulazwa ili uweze kuwashughulikia wanaotaka kukuletea usingizi kwa Jina la
Yesu.
Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 15:5…(kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti ya
Bwana, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya.).
Ukeshaona bidii haipo kwenye kazi yako au katika jambo lingine lolote lile ujue
tayari mtu wa aina hii amelazwa usingizi. Kataa kutokuwa na bidii kwa Jina la
Yesu. Bidii ndiyo humfanya mtu ashinde, na ang’ang’ane na changamoto zote za
maisha. Shetani huleta ulegevu kwa kila jambo ili mtu asiwe na bidii ili mtu
huyo asifanikiwe kwa mambo ya mwilini na yale ya rohoni.
Dhambi ni chanzo mojawapo cha kumfanya shetani
na mawakala wake (wachawi, waganga wa kienyeji na wasoma nyota) kumlaza mtu
usingizini. Leo ni siku muhimu kwa mtu ambaye hujaokoka ufanye maamuzi ya
kumpkea Yesu maishani mwako ili kuondoka kwenye hatari ya kulazwa usingizini.
© Media and Information Ministry
Glory of Christ Tanzania Church,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +25571765979866 / +255713459545
|
KISWAHILI
ENGLISH