GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[UFUFUO NA UZIMA MOROGORO]
(SIKU YA 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA)
SOMO: KUOMBA KWA BIDII
– SIKU YA 1
JUMATATU: 30 JANUARI
2017
MHUBIRI: Dr. GODSON ISSA ZACHARIA
(SNP)
YAKOBO 5:6........(“Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii")
Kuomba kwa bidii ni hali ya kuomba kwa ufanisi (effectively)
- ni kuomba kwa kung'ang'ania
- ni kuomba kwa shauku
- ni kuomba kwa hisia ukitegemea kupata
- ni kuomba kwa ushupavu
- ni kuomba kwa nia,
- ni kuomba kwa kukereketwa na hamu.
Ukiomba kwa bidii, nikuhakikishie majibu yako yatakuwa makubwa sana. Siyo kila maombi ni maombi ya ufanisi/ya bidii. Utaona Hanna akaomba kwa bidii akamzaa Samuel ingawa alishabezwa na Penina na watu wengine kuwa yeye ni tasa. Eliya naye aliomba kwa bidii akapata majibu. Utaona Biblia inasema “Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita” (YAKOBO 5:17).
Kwakuwa kuomba kwa bidii kunaleta majibu ya uhakika, unawezaje kujua unaomba kwa bidii?
Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya kufunga na kuomba nitakuonyesha DALILI ZA MTU ANAYEOMBA KWA BIDII
1. DALILI #1: Mkao wako (Jinsi unavyokuwa wakati wa kuomba kwa
bidii) - The Posture. =Hii ni ile Staili ya Eliya ya kuomba kwa bidii=
Utaona Eliya alipoomba kwa bidii ili mvua inyeshe, kuna mkao wake aliokuwa nao wakati huo. Maandiko yanasema "..........Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini” (1 WAFALME 18:42). Akajitupa chini (he cast himself down), akainama uso mpaka magotini, akaanza kuomba kwa bidii mpaka mvua ikanyesha. Aliendelea kuomba na akamwambia mtumishi wake nenda hata mara saba kuangalia dalili ya mvua (1WAFALME 18:43).
Kuomba kwa bidii ni kuomba mpaka upate ishara au dalili ya majibu yaani kuomba kwa kung'ang'ana mpaka upate majibu ya unachokiomba, ni kuendelea kuomba mpaka kieleweke kwa Jina la Yesu. Ni maombi yangu Mungu akutie ujasiri wa kuomba kwa bidii mpaka upate majibu kwa Jina la Yesu.
2. DALILI#2: Kuomba kwa Kulia sana na machozi/ kwa sauti kuu
Hii ni style ya kuomba kwa bidii aliyotumia Bwana Yesu.
Yesu alipokuwa duniani aliomba kwa kulia
sauti kuu na machozi. Je wewe unaomba kwa sauti laini au sauti kuu na
machozi? Mimi ninachagua staili ya Bwana Yesu maana Yeye ni chanzo cha imani
yetu.Hii ni style ya kuomba kwa bidii aliyotumia Bwana Yesu.
Utaona maandiko matakatifu, "Yeye, siku hizo za mwili wake, *alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi*, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (WAEBRANIA 5:7)
“Who in the days of his flesh, when he had offered up prayers and supplications with *STRONG CRYING and TEARS* unto him that was able to save him from death, and was heard in that he feared;” HEBREWS 5:7 KJV
Staili hii ya kulia sana kwa sauti sio kilio kama kile cha watu wanacholia kwa kumkumbuka marehemu fulani, siyo kilio cha msiba, hapana hapana, hiki siyo kilio cha kuona matokeo ya kufeli, hapana, bali ni kilio ambacho unalia wakati unamtolea Mungu *maombi na dua vinavyoambatana na kulia sana na machozi*.
Ni kuomba kwa bidii, kwa mtu ambaye anaomba ili aokolewa na mauti (WAEBR 5:7). Yawezekana kuna mauti imetangazwa kwako, au kwenye kazi yako (unakaribia kufukuzwa), au ndoa yako, biashara yako, makazi yako, watoto wako, mauti imetangazwa kwenye ajira, mradi, uchumba, masomo n.k.
Maombi haya ni lazima yakupelekee kuyatoo na dua pamoja na kulia sana na machozi. Unaweza kuomba kwa bidii kwa staili hii ya Yesu kama ukitambua kuwa yuko anayeweza kukuokoa na mauti.
Utaona Bwana Yesu wakati anaelekea Gethsemane kuomba, aliwaambia wanafunzi wake maneno haya ".......Roho yangu ina *huzuni nyingi kiasi cha kufa* kaeni hapa, mkeshe pamoja nami"
Unaona alikuwa amekabiliwa na mauti, mauti ilikuwa mbele take ndipo akaamua kupanda mlimani na akaomba kwa bidii sana mpaka *hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini*.
Imeandikwa LUKA 22:44 "Naye kwa vile *alivyokuwa katika dhiki*, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini." Bwana Yesu aliomba maombi haya ya hisia kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba. Kumbe unavyokuwa katika dhiki, ni wakati wa kuomba sana, maombi, siyo wakati wa kulalama, au kutafuta suluhu mbadala mahali pengine, bali ni wakati wa kumtolea *maombi na dua pamoja na kulia sana* yule anayeweze kukuokoa na mauti “ya kazi yako (unakaribia kufukuzwa), mauti ndoa yako, biashara yako, makazi yako, watoto wako, mauti imetangazwa kwenye ajira, mradi, uchumba, masomo n.k”.
UKIRI
Ninaamuru katika jina la Yesu wiki hii ya
kufunga na kuomba upate upenyo wa kuomba kwa bidii na aliyekutega na mauti
mitego yake yote ifyatuke na kukuacha kwa JINA LA YESU, Amen. |
3. DALILI #3: Kuugua kimya kimya moyoni
Hii ni staili ya kuomba kwa bidii ambayo Hanna aliitumia.
Hii ni staili ya kuomba kwa bidii ambayo Hanna aliitumia.
Utaona imeeandikwa katika 1 Samweli 1:12-15 (Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za BWANA, Eli akamwangalia kinywa chake. 13. Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; MIDOMO YAKE TU ILIONEKANA KAMA ANENA, SAUTI YAKE ISISIKIWE; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. 14. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. 15. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA).
Huu ni mfano dhahiri wa staili ya kuomba kwa bidii ya mtu aliyeomba kwa hisia na shauku kwa ajili ya kumpata mtoto Samweli. Hapa haikuwepo kuomboleza kwa kulia wala kupiga kelele. Ndiyo maana utaona kuhani Eli hakuwa na sikia sauti yoyote kwa habari ya Hanna alichokuwa anaomba, na akadhani Hanna ni mlevi sasa, yaani amepata shida akaamua kunywa pombe na kuwa mlevi.
Mtoto wa Mungu, usilewe kwa pombe au divai kwa sababu umepata uchungu na dhiki; kimbilia msalabani kwa Yesu maana kuna msaada, yeye ni msaada upatikanao tele wakati wa shida. Usilewe kwa kileo bali ukiomba kwa bidii utajazwa na Roho Mtakatifu na ulewe Huyo.
Maombi haya ukiyaomba kwa staili hii ya kuugua kimya kimya moyoni mwako, yakiombwa kwa bidii yatawafanya watu wengi wasikuelewe. Hanna akaomba kwa staili hii na midomo yake ikawa inachezacheza lakini Eli hakusikia chochote akawa hamuelewi. Maana Hanna alikuwa katika shida kubwa ya kumpata mtoto, kwa hiyo kwa desturi alikuwa anaomba mno kwa staili nyingi tu bila majibu. Hata alikuwa anaomba hata kwa kulia, SAMWELI 1:10 "Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana AKALIA sana". Na Ndipo baadae akagundua siri "nibadilishe staili, niombe kwa bidii kwa kuugua kimya kimya moyoni", akakimbilia Shilo hekaluni na akaanza kuumimina moyo wake kwa Bwana.
Staili ya Hanna ni ya maombi ya kuugua moyoni kimya kimya kwa bidii, ni maombi ya mtu aliyechoka, aliyekata tamaa ya jambo fulani kutokea, aliyekataliwa na ndugu zake (akina Pennina hata leo wako wengi kwenye maisha yako). Ni maombi ambayo hayasubiri mtu akwambie njoo twende kwenye maombi, unajisikia na unasukumwa na hali ulinayo na haja moyo wako. Hanna hakuanza kushangaashangaa hekaluni mle bali alianza kuumimina moyo wake (Self motivated and DO IT by yourself prayers).
Siku ya leo hii AMKA ewe Hanna wa leo katika jina la Yesu ukaumimine moyo wako hekaluni, njoo hekaluni Bonde la Maono (Ufufuo na Uzima – Mkundi, Morogoro), kuhani naye yupo hekaluni, atalitamka neno hekaluni litakalokudhihirishia majibu yako ya ushindi ili uende na uso wako ukiwa haujakunjamana tena katika *SIKU HIZI 7 KUFUNGA NA KUOMBA* na furaha ya kudumu itakujilia kwa Jina la Yesu.
*Bwana wetu hakawii kuitimiza ahadi, bali huvumilia*
Pastor Godson Zacharia
Ufufuo na Uzima - Morogoro.
Ufufuo na Uzima - Morogoro.
===========================
Kwa msaada zaidi na maombezi wasiliana na nasi kipitia:
Facebook: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on Instagram: pastordrgodson
Follow
us on Youtube: pastor:dr.godson
Simu: 0719 798778 (Sms only)
blog: Ufufuo na Uzima Morogoro
http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/?m=0
© Media and Information Ministry
GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH,
(Kanisa la Ufufuo na Uzima)
Mkundi - Morogoro
Tel: +255719612874 / +255713459545
|